Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Waitwao ni Wengi
Waitwao ni Wengi
Waitwao ni Wengi
Ebook171 pages2 hours

Waitwao ni Wengi

Rating: 4 out of 5 stars

4/5

()

Read preview

About this ebook

Kwa kweli Mungu amewaita watu wengi. Maisha yetu duniani ni fursa ya kumtumikia, na Mungu anaangalia vitu unavyofanya kwa ajili ya Ufalme wake. Kitabu hiki kinachagamsha usomaji. Ukihifadhi akilini mawazo ya ukweli yaliyoandikwa na mwandishi, utapokea hekima kutumia fursa ya maisha yako kwa njia sahihi.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781613954065
Waitwao ni Wengi
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Waitwao ni Wengi

Related ebooks

Reviews for Waitwao ni Wengi

Rating: 4 out of 5 stars
4/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Waitwao ni Wengi - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Kwa Nini Bado Uko Hai

    Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

    Waefeso 2:10

    Wakati   mmoja   nilizungumza   na   dereva   Mwingereza aliyekuwa  akiendesha  teksi  nyeusi,  ambaye  alikuwa akinipeleka  katikati  mwa  jiji  la  London.  Nilimuuliza  kama alikuwa anamwamini Mungu. Alisema, "La hasha. Simwamini Mungu!

    Kisha nikamuuliza, Unaamini kuwa kuna Kuzimu La hasha! Alijibu kwa hamaki.

    Niliendelea, Je, unaamini juu ya Mbingu? Siamini kuhusu jambo lolote kama hilo?

    Kisha dereva huyo wa teksi aliniambia, Hebu nikuulize swali. Ndiyo, jisikie huru. Uliza swali lolote unalotaka, Nilimjibu. Aliniuliza, Unaamini juu ya Mbingu?

    Ndiyo ninaamini, Nilijibu.

    Basi nikuulize swali lingine , Aliuliza, Kama unaamini utaenda mbinguni, kwa nini basi usijiue na kwenda mbinguni sasa. Hata hivyo, ungeepukana na gharama za maisha, madeni na matatizo mengine ya dunia hii."

    Nilishtuka. Sikutarajia swali kama hilo. Lakini lilionekana kama linaleta maana. Kama Mbingu ilikuwa nzuri sana, nilikuwa bado nafanya nini duniani? Kwa nini nisijiue na kuondoka sasa hivi kwenye dunia hii isiyo na raha.

    Nilifikiria, Hilo ni swali zuri. Lakini kabla ya kupata nafasi ya kumjibu, tuliwasili tulipokuwa tukielekea.

    Tangu mazungumzo yale na dereva huyo wa teksi, nimekuwa nikilijibu swali lake kwenye mikusanyiko tofauti tofauti: Kwa nini hatuendi mbinguni mara tu baada ya kuokoka!

    Japokuwa Mungu ameyagusa maisha yetu na kutuahidi kwenda  mbinguni,  kuna  kazi  inayotakiwa  ifanyike  duniani. Kuna mambo ya kutimiza kwa ajili ya Mungu. Mungu anatarajia tuuitikie upendo wake mkuu kwa kujitoa kwenye kazi yake.

    Tunapokuja   kwa  Yesu,  Yeye   hututua   mzigo   wetu   wa dhambi  na  giza  na  kutupatia  mzigo  wake.  Njooni  kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. JIFUNGENI NIRA YANGU, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi  mtapata  raha  nafsini  mwenu.  (Mathayo  11:28-29). Mzigo wa Kristo ni upi? Ni mzigo wa nafsi zilizopotea katika ulimwengu huu.

    Inashangaza kuwa Wakristo wengi wanaishi maisha yao pasipo kutambua kuwa, bado wako hai ili wafanye kitu kwa ajili ya Mungu. Hawaishi ili wajenge nyumba na kupata vitu vizuri vya dunia hii. Hawaishi ili wapate pesa zaidi na kujiwekea hazina hapa duniani. Tuna sababu moja tu ya kuishi na hii ni kumtumikia Mwokozi aliyeacha kila kitu kwa ajili yetu. Ni ukweli unaosikitisha kwamba mafundisho mengi katika mwili wa Kristo huwaondoa Wakristo kwenye kusudi lao halisi la kuendelea kuishi.

    Hebu  tufikirie kuhusu Mungu wetu, Mwokozi na  Mfalme wetu. Yeye aliyetoa vyote. Aliacha kila kitu … ili kwamba tuwe rafiki zake.1  Najua kwamba tunafikiri mara chache kuhusu Mwokozi na Mfalme wetu. Tunafikiri mara chache kuhusu Yeye aliyejitoa kila kitu. Hii ndiyo sababu ni mara chache sana huwa tayari kuacha vyote. Hii ndiyo sababu hatuzai na hatuna matunda kwenye Ufalme.

    .1 Maneno ya Let’s Think about Our God na Tommy Walker (Wimbaji)

    Sura ya 2

    Wakristo Wengi Wameitwa

    Kama ungekuwa Mungu na ungekuwa na watu bilioni sita wa kuwaokoa, ungefanya nini? Je! Ungemtuma mtu mmoja au wawili kuwaokoa au ungetuma watu wengi? Kwa kweli, ungewatuma watu wengi kwenye mashamba ya mavuno. Na hivyo ndivyo hasa alivyofanya Mungu. Amewaita watu wengi! Usidanganywe na Wachungaji wachache unaowaona wakikaa kwenye  mistari  ya  mbele  kwenye  makanisa.  Hilo  siku  zote hutoa hisia kwamba walioitwa ni wachache, au kwamba wengi wao  katika  kusanyiko  hawajaitwa.  Kwa  kweli,  ni  kinyume chake kabisa. Wengi wameitwa kwa ajili ya kazi ya kuuokoa ulimwengu, na si Wachungaji wachache tu.

    Kweli Tano kuhusu Wito wa Mungu

    1. Waitwao ni wengi.

    Kwa   maana   waitwao   ni   wengi,   bali   wateule   ni wachache.

    Mathayo 22:14

    Nini maana ya Waitwao ni Wengi?

    Waitwao ni wengi inamaanisha idadi kubwa ya watu wameitwa. Waitwao ni wengi inamaanisha watu wengi sana wameitwa. Waitwao ni wengi inamaanisha idadi kubwa mno ya watu wameitwa.

    Waitwao ni wengi inamaanisha watu tele wameitwa Waitwao ni wengi inamaanisha walioitwa hawahesabiki. Waitwao ni wengi inamaanisha kuwa walioitwa ni wengi mno.

    Waitwao ni wengi inamaanisha watu walio wengi wameitwa.

    Waitwao ni wengi inamaanisha kuwa walioitwa ni wengi zaidi.

    Kwa  huzuni,  Wachungaji  wengi  huwachukulia  waumini wao kama watu wasio na wito. Wanahusiana nao kama watu ambao hawawezi kufanya sana kwa ajili ya Mungu. Wachungaji wengi huwafundisha washirika wao namna ya kuwa na Maisha mazuri. Mahubiri mengi ni kuhusu sisi wenyewe, maisha yetu, ndoa zetu, nyumba zetu, uchumi wetu, n.k. Mahubiri ya namna hii ndiyo yamesababisha kuwepo na kundi kubwa la waamini wabinafsi na wasiozaa matunda siku hizi.

    Wachungaji, Mitume, Wainjilisti na waalimu wapo kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu ili kwamba watakatifu hao wafanye kazi ya huduma. Hata mwinjilisti anayetarajiwa sana kuvuna roho za watu ana kazi ya msingi ya kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma. Naye alitoa wengine kuwa Mitume, na wengine kuwa Manabii; na wengine kuwa Wainjilisti na wengine kuwa Wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe (Waefeso 4:11-12).

    2.   Kuna Wito wa Kuzaa Matunda.

    Hauhitaji kusikia wito; umekishaitwa tayari.

    Keith Green

    Tumeitwa ili tufanye nini? Je, Wote tumeitwa ili tuwe Mitume, Manabii, Wainjilisti na Walimu? Jibu ni rahisi, Hapana. Wengi wetu hatuna wito mkuu wa namna hiyo. Kwa lugha rahisi, sote tumeitwa tukazae matunda.

    Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

    Yohana 15:16

    Kama  tungefuata  mantiki  halisi  ya  mafundisho  yetu  ya Kikristo, Wakristo wengi wangekuwa ni watu wa kujitoa na

    kufanya kitu kwa ajili ya Mungu. Cha kusikitisha zaidi, na pengine, sifa mbaya zaidi ya Wakristo wengi wa leo ni jinsi tunavyofanya kidogo kwa ajili ya Kristo. Tumeokolewa kwa tendo la ajabu la upendo na neema, lakini hatuko tayari kuacha chochote kwa ajili ya kuwaokoa wengine. Inasikitisha sana kuwaona Wakristo wanapoteza muda na maisha yao, pasipo kufanya lolote kwa ajili ya Bwana.

    3.   Wengine wameitwa kwa namna ya kipekee.

    Hata alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.

    Matendo 9:3-6

    Mtume Paulo aliitwa kwa namna ya ajabu na ya kipekee. Aliona nuru ikimwangaza kutoka mbinguni na alisikia sauti ikisema naye. Alianguka chini na akawa kipofu kwa siku kadhaa. Kwa bahati mbaya, mtu   anaposimulia kile alichokipitia, kila mtu hutaka apitie uzoefu ule ule. Kila mtu anataka aone nuru na kusikia sauti; la sivyo, hawataamini kuwa wameitwa. Lakini Mungu hawezi kuwekwa kwenye sanduku na hawezi kutarajiwa kujirudia katika njia ile ile inayoweza kubashiriwa tena na tena.

    Nakumbuka niliposoma jinsi Kenneth Hagin alivyoponywa ugonjwa wa moyo na jinsi alivyoinuka kutoka kwenye kitanda akiwa mahututi. Siku moja, nilikuwa naumwa na nikajaribu kuiga uzoefu ule ule. Nakuambia, rafiki yangu mpendwa, karibu nipoteze uhai wangu kwa kujaribu kulazimisha kupata uzoefu ambao Kenneth Hagin alipitia. Ninaamini, Mungu ana njia tofauti za uponyaji kwa watu tofauti.

    4.   Wengine wameitwa kwa namna ya kawaida.

    Akasema, toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima,  ukaivunjavunja  miamba  mbele  za  BWANA;  lakini BWANA hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi lakini BWANA hakuwamo katika lile tetemeko la nchi, na baada ya tetemeko la nchi; kukawa na moto lakini BWANA hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.   (1 Wafalme 19:11-12).

    Ni  vizuri  kumhisi  Mungu  katika  namna  ya  ajabu.  Wote tuna shauku ya uzoefu wa kipekee na Mungu. Kama mhubiri, nimekuwa na shauku ya kupata uzoefu wa mguso wa kipekee wa Mungu ili nije niwaambie washirika jinsi nilivyoguswa. Mara nyingi nilidhani kuwa hiyo ingenifanya nionekane mwenye nguvu zaidi. Rehema!

    Kwa makadirio yangu, watu wengi huitwa kwa jinsi ya kawaida na hili huwafanya wapuuzie wito wao. Ninapohubiri kuhusu watu kuitwa, ninatambua namna ambavyo huamsha kile kilichomo ndani yao. Watu wengi wameitwa lakini hawalijui hilo. Wanatazamia kuitwa kwa namna ya kipekee. Lakini wito mara nyingi huja kwa namna ya kawaida. Manabii wakuu kama Eliya walifanya kosa la kutazamia wito wa Mungu kwa namna ya ajabu na ya kipekee. Kama utaendelea kutazamia wito wa Mungu kwa namna hiyo, utazikosa baraka yako. …Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja- vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto SAUTI NDOGO, YA UTULIVU. Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. NA TAZAMA, SAUTI IKAMJIA, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya? (1 Wafalme 19:11-13).

    5.   Wengine wameitwa kupitia shauku zao.

    Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.

    1 Timotheo 3:1

    Hii ndiyo namna nilivyopokea wito wangu. Sikuwa na miguso ya ajabu ambayo watu wanaizungumzia. Mara zote hushangaa ninaposikia jinsi watu wanavyopokea wito wao kwa ajili ya huduma.

    Sikukutana na Mungu kwa namna hiyo ya ajabu lakini naamini kwamba nimeitwa na Mungu kwa kweli. Sikuona nuru wala kusikia sauti zozote. Yesu hajawahi kunitokea na kuniagiza kwenda kwenye ulimwengu wa utumishi. Lakini bado naamini kuwa nimeagizwa kihalisi kuingia kwenye huduma.

    Nakumbuka wakati mmoja alipokuja kaka mmoja nyumbani kwangu kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa wiki. Miezi michache baadaye aliniambia jinsi alivyokutana na Bwana nyumbani kwangu. Alikuwa mgeni wangu na alikuwa anakaa kwenye vyumba vya juu ghorofani pamoja na wanafamilia wengine. Alieleza jinsi mlango ulivyofunguka ghafla usiku mmoja na ghafla Bwana Yesu aliingia chumbani. Aliniambia jinsi Bwana Yesu alivyoweka kitu mkononi mwake na kumwambia kwamba alikuwa amemwagiza kwa ajili ya kazi kuu.

    Sikuweza kuamini nilichokuwa nasikia - Yesu kumtokea mgeni nyumbani kwangu! Kaka huyu alipoendelea kueleza alivyokutana na Bwana, nilipata hasira zaidi na zaidi lakini sikuweza kuionyesha dhahiri. Nililazimika kujifanya kuwa nilifurahia habari hiyo ya kukutana kwake na Yesu.

    Hili ndilo nimekuwa nikiomba, nilijiwazia mwenyewe. Nilikuwa na hasira na Bwana kwa sababu nilifikiri, Ni kwa nini Yesu aje nyumbani kwangu, na kunipita mimi mmiliki, mwenyeji na mwenye nyumba na kumtembelea mtu aliyekuwa analala usiku tu kama mgeni.

    Hakika Mungu hakunitendea haki, nilifikiri.

    Nimekuwa nikiomba kwa miaka na miaka kwamba Yesu anitokee. Nilikuwa na shauku ya kuwa kama Kenneth Hagin, ambaye alielezea jinsi alivyokutana kibinafsi na

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1