Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Wale Wanaokuacha
Wale Wanaokuacha
Wale Wanaokuacha
Ebook201 pages2 hours

Wale Wanaokuacha

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Watu wanaokuacha wanaweza kukuharibu. hakuna kitu kinachoweza kuelezea hisia ya mfadhaiko, kuchangayikiwa na mhangaiko ambazo hushuka wakati watu wanakuacha. Kitabu hiki kimeandikwa kukusaidia kupambana na uharibifu ambao unaachiliwa wakati watu wanapokuacha. Usidanganye. Kutelekezwa au kuachwa sio la kipekee kwako na utumishi wako. Wengine wengi wameteseka na mambo sawia. Shetani alikuwa muasi wa

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613953914
Wale Wanaokuacha
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Wale Wanaokuacha

Related ebooks

Reviews for Wale Wanaokuacha

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Wale Wanaokuacha - Dag Heward-Mills

    Sababu 15 Zinazoweza Kumfanya Mungu Awaruhusu  Watu  Kukuacha Wewe

    Zifuatazo ni sababu kadhaa kwa nini Bwana anaweza kuruhusu watu kukuacha na kuondoka kwako akijua kuwa jambo hilo linaweza likakuumiza sana.

    1. Bwana anaweza akawaruhusu watu kuondoka kwako na kukuacha ili makosa ya kimsingi katika huduma yako yaweze kusahihishwa.

    Mwanzoni mwa huduma, mara nyingi tunakuwa tumejawa na  hofu ya kutokuweza kufanya vizuri au kutokuendelea kabisa. Hofu hizi za kutokuweza zinaweza kutusababisha sisi  kupokea msaada wowote unaopatikana kwetu bila ya kuutafakari kwa undani.  Katika hatua za kunyosha mkono ili tuupokee msaada ule, watumishi wengi wanajikuta wameshikamana na  watu wasiowafaa.

    Katika jambo hili tunamwona Abramu kama mfano halisi. Mungu alikuwa amemwambia kuwa, atoke katika jamaa yake ili aende safari ndefu na kwenye nchi asiyoijua na ni nchi ya ahadi. Badala ya kuondoka  yeye peke yake toka katika jamaa yake,  kama vile Bwana alivyokuwa amemwambia, aliondoka pamoja na baadhi ya jamaa zake na mmoja wao aliyejulikana ni Lutu.

    Bwana akamwambia Abramu, toka wewe katika nchi yako, NA JAMAA ZAKO,  na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi  nitakayokuonyesha.

    Mwanzo 12:1

    ... Abramu akapanda kutoka Misri, yeye na mkewe, na kila alichokuwa nacho, NA LUTU PAMOJA NAYE, mpaka kusini.

    Mwanzo 13:1

    Matatizo yote  ambayo Abramu aliyapata katika safari yake yanaweza kuwa ni sababu ya kuwa na Lutu maishani mwake.  Taarifa ama kumbukumbu za matatizo  ambayo Abramu aliyapata  kwa sababu ya kuwa na Lutu pamoja naye ni kama zifuatazo.

    1. Abramu alipata tatizo la (magomvi ya kila mara) kugombana hasa baina ya wafanyakazi wake na wale wa Lutu, na hata kutoelewana. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu ya kuwapamoja  na Lutu. Hatimaye Abramu alifikia hatua ya kutengana na jamaa zake kwa ajili ya Lutu.  (Mwanzo 13:7-8).

    2. Abramu alipigana vita kitu ambacho kama asingelikuwa pamoja na Lutu basi asingelipigana vita hivyo. Abramu alimsaidia au kumwokoa Lutu  kutoka kwa mfalme Kedorlaoma (Mwanzo 14:1-16)

    3. Abramu alihitaji kuomba maombi maalumu kwa ajili ya Lutu. Abramu alihitaji kumwokoa binamu yake kutokana na maangamizo makubwa yaliyokuwa yakiijia Sodoma na Gomora (mwanzo 18:23-33).

    Jambo hili ndilo ninaloliita makosa ya kimsingi katika huduma. Ni kosa unalolifanya mwanzoni mwa huduma yako,  kawaida  ya kosa hili ni kwamba hufanyika bila ya kuwa na hofu yoyote. Makosa haya yanaweza kuhusishwa na mtu asiyehusika kabisa, inakuwa kama ndege  mkubwa wa baharini mwenye mabawa marefu aitwaye albatross kwa yale yote unayoyafanya.  Wakati mwingine watu wengine huoana na watu wale ambao hawakuwa wamepangiwa na Mungu,  mara tu wanapoanza huduma.  Hata hivyo Mungu anaweza kabisa kumwondoa duniani mtu huyo ili uweze kuwa huru  kutokana na  albatross shingoni mwako. Mungu asipomwondoa mtu huyu maishani mwako basi utaendelea na huduma yako yote  pamoja na albatross shingoni mwako.

    Watu fulani  waliokuwa nami mwanzoni kabisa mwa huduma yangu kwa sasa hawaendelei nami.  Pengine sababu yaweza kuwa   niliwachukua baadhi  ya watu hao wawe pamoja nami kwa sababu ya kuogopa  kuwa nisingeweza kuendelea mbele  bila ya kufanya huduma pamoja nao. Uwepo wao pamoja nami  ilikuwa inanipa uhakika kuwa  nitafanikiwa.  Mungu kwa Rehema zake alisababisha watu hao  kuniacha na kuondoka zao.  Pamoja na kwamba ninawakumbuka na ningelipenda waendelee kuwa nami kihuduma,  niligundua kuwa Mungu aliwaruhusu kuondoka kwangu  kwa sababu ilikuwa ni makosa katika sehemu ya kwanza  kuwa pamoja nao katika maono yangu mapya ya kujenga kanisa.

    2. Mungu anaweza kabisa kuruhusu watu wakuache  ili akutweze  (kukunyenyekeza).

    Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako, aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ILI AKUTWEZE, kukujaribu, kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.

    Kumbukumbu la Torati  8:2

    Ni jambo la kutweza watu wanapotelekeza au kujiuzuru kutoka kwenye shirika lako.  Kila tukio la kuondoka kwa mtu, kunaacha radha ya ukakasi fulani mdomoni mwako.  Kila wakati mtu anapoondoka kwa kimyakimya, nyuma yake huacha alama ya maswali yasiyojibika.   Mashaka hayo yaliyosababishwa na watu walioondoka huvuruga na kutia wasiwasi kitu ambacho humtweza mtu ama kumnyenyekeza.

    Baada ya kuanzisha makanisa kwa miaka mingi , nilikuwa nimebarikiwa  sana kwa kuwa na mamia ya Wachungaji waaminifu na watiifu, vijana kwa mabinti.  Pia nilikuwa nimebarikiwa sana kwani miongoni mwao kulikuwa na ndugu zangu kabisa waliokuwa wachungaji makanisani.

    Hata hivyo, siku moja baadhi ya ndugu zangu waliniacha katika huduma yangu na wakafanya yaliyo kinyume kabisa na yale ambayo nilikuwa nimeshafundisha.  Ilikuwa ni aibu kubwa kwangu kwani ndugu katika familia yangu  walitokea  kuwa kiini cha ukaidi na uasi kanisani. Hivyo nikapaswa kupambana na ndugu zangu. Hali hii imeshatokea kwangu mara nyingi kuwa nimeshawashawishi watu kuwa waaminifu na watiifu lakini  kumbe nilikuwa sijawahi kufanya hivyo kwenye familia yangu.

    Nilihisi kuwa Mungu alikuwa akinitweza (akininyenyekeza)  kupitia tukio hili. Alitaka kunionyesha kuwa   haikuwa kwauwezo wala nguvuha sio kwa mafundisho  au sheria na maelekezo yoyote bali ni kwa ajili ya neema yake pekee.  Pengine umeshawahi kuwapata watu waliowahi kukuacha wewe.  Mruhusu Mungu afanye kazi yake ya kiroho ili akutweze (akunyenyekeze)  kwa ajili ya huduma yake.

    3. Mungu anaweza kuruhusu watu waondoke na kukuacha kwa sababu wewe mwenyewe umekwisha ruhusu watu wako wawe wajinga kwa kutokuwafundisha  juu ya uaminifu na  madhara ya kutokuwa waaminifu.

    Na watu mia mbili walioalikwa  wakatoka Yerusalemu pamoja na Absalomu, WAKAENDA KWA UJINGA WAO wasijue neno lolote.

    2 Samweli 15:11 

    Mwovu huwatia  watu ujinga. Udanganyifu huongezeka kila siku wakati ambapo  watu hawajaelekezwa vema  kwenye ukweli wa  neno. Uwezo wa Absalomu ulikuwa ni kuongoza watu mia mbili tu ambao walienda kwa ujinga wa akili zao.  Huuujinga wa akili wakati mwingine inaeleweka kama hali ya kurahisisha mambo.

    Kanuni za kuwa mwaminifu na kutokuwa mwaminifu, misingi yake na kumbukumbu zake mara nyingi hazifundishwi makanisani. siyo ajabu kuwa washirika wanaweza kusumbuliwa sana kiurahisi na mapepo ya udanganyifu yanayowajaza katika ujinga wao. Kutokana na masomo haya pengine umegundua kuwa ulisharuhusu ujinga kuenea ndani ya washirika wako. Shetani ameshatumia faida ya ujinga wao na hivyo kuweza kuwavuruga na kuleta maangamizo  miongoni mwao.

    Ndiyo ni kweli kabisa kuwa pengine usharika wako unaweza kuwa umebarikiwa kabisa na  ujume wa mafanikio, ndoa na uponyaji, lakini kati ya haya yote hakuna linaloweza kufaa ili kuulinda usharika  kutokana na mapepo ya kutokuwa mwaminifu na hata vitendo vya udanganyifu.

    Siku moja mchungaji mmoja aliniuliza kwa nini nilikuwa ninayafundisha mafundisho hayo. Alinifanyia mzaha,uaminifu si kitu ambacho mtu anatakiwa akifundishe, ni kitu ambacho kinaamuriwa.

    Kisha akaendelea tena kwa tabia yako nzuri, unawaamuru wale waaminifu kwa asili ambao wako karibu nawe

    Muda mfupi tu baada ya haya, alikumbana na tukio zito la vitendo vya udanganyifu wa washirika kanisani kwake.  Hakuweza kuamini kile kilichomtokea.  Baada ya tukio hili, kwa zile dharau zake kwa vitabu vyangu na mafundisho yangu, alibadilika na kupendezwa au kuvutiwa navyo.  Akawa mshabiki mkubwa wa somo la uaminifu na kuanza kuvipigia debe vitabu vyangu yeye mwenyewe.  Pengine huwezi kujua umuhimu wa mafundisho  mpaka pale  utakapokutwa na shida ya ujinga.

    4. Bwana anaweza kuwaruhusu watu waondoke kwako kwa sababu  ulimdharau mhudumu mwenzako  kanisa lake lilipogawanyika.

    ... naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.

    Mithali 17:5

    Mara nyingi, tunawadharau watu wanapopatwa na shida na matatizo.  Kama marafiki wa Ayubu,  tunaonekana kuwa kama vile tunajua sababu ya  mabaya yote yaliyowatokea watu.  Tunawadharau watu wale walio na  shida kwa kuwa tunafikiri kuwa wamejisababishia shida zile wao wenyewe. Mwelekeo huu unaweza kumfungulia mlango shetani akaingia maishani mwetu na hata katika huduma zetu.

    Siku moja, nilikutana na wachungaji watatu  kutoka kwenye kanisa zuri  lenye mafanikio ya hali ya juu. Timu yao ilikuwa ikiundwa kwa watu watatu, yaani washirika wawili wenye nguvu na mchungaji mkuu,  kwa msaada huo wa watu wale wawili, mchungaji yule alifanikiwa kujenga kanisa kubwa kwenye mji ule. Ilionekana kama vile kila mtu pale alikuwa mshirika wa kanisa lile. Kanisa lao jipya lilikuwa likijivunia  kule kuongezeka kwa ibada na kujaa kwa watu kiasi kwamba wengine walihitaji kukaa nje.  Wakiwa wamechangamka sana kwa ajili ya mafanikio yao yaliyokuwa yamepatikana katika kipindi kilichokuwa kimepita, walianza kuonyesha kwa vitendo na kujiuliza kwa nini kanisa lao lingine la mijini halikui! 

    Walisema maneno ya dharau na kejeli juu ya Mchungaji wa kanisa lile,watu wanaondoka kanisani wanapokuwa na kiongozi mbaya.

    „Ni kwa sababu ya  uongozi wake mbaya ndiyo maana watu  wameiacha huduma yake na  kujiunga kwetu".

    Na kwa wakati huo sikuwa nimejua kuwa watu wengine walikuwa  wakiondoka katika kanisa lile jingine na kujiunga katika kanisa lao.  Ni kwa mara ya kwanza niliposikia kuwa kanisa lile lingine lilikuwa na kiongozimbaya. Ilikuwa rahisi kutambua kejeli na mizaha jinsi walivyoongea vibaya kuhusu kanisa hili na kiongozi wake mbaya".

    Ndiyo, sitii  shaka kuwa  watu wanaweza kabisa kuacha huduma kwa sababu  kwa ajili ya uongozi mbaya.  Lakini unatakiwa kuwa  mwangalifu sana  jinsi unavyoamua na utakavyomaliza naye kihuduma.

    Miaka kadhaa baadaye, viongozi hawa watatu walianza hatua nyingine ya huduma. Kila hatua mpya inaweza kuleta mabadiliko katika uwezo kiutendaji.  Katika awamu hii mpya, washirika hawa wawili waliondoka na kumwacha mchungaji mkuu peke yake huku wakimsema vibaya hata kumlaani!  Mambo yale yale ya kumdharau  yule mchungaji sasa yalikuwa zikiwatokea wao maradufu.

    Mara niliposikia mgogoro huo,  kitu cha kwanza  nilichokiona ni hiki, kile walichokisema juu ya kanisa lile kubwa na kanisa lake dogo, na yale yote mabaya waliyokuwa wameongea kuhusu yule mchungaji, watu wanaondoka kwako unapokuwa kiongozi mbaya. Je, tuseme kuwa mchungaji wao mkuu aligeuka na kuwa kiongozi mbaya?  Hiyo haina ukweli kwa lazima.  Kuna sababu nyingi ambazo watu wanaweza wakakuacha. Lakini hakikisha kuwa usimdhihaki yeyote yule atakapopatwa na shida.

    Katika taifa langu,  kuna mithali inayosema hivi, unapoona kidevu cha rafiki yako kinaungua moto usimcheke usimuulize kwa nini aliruhusu kidevu chake kushikwa na motom nenda ukachote maji na kuyatunza kwako kwa tahadhari kuwa huenda ikawa kidevu chako pia kikashikwa na moto!. Biblia inayaweka mambo haya kama hivi...  naye aufurahiaye msiba hatakosa adhabu.  (Mithali 17:5)

    5. MUNGU ANAWEZA KUWARUHUSU WATU WAKUACHE KWA KUWA MAKUSUDIO/MALENGO/MATAZAMIO YAKO HAYAWAHUSU.

    Watoto ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo.  Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. WALITOKA KWETU, LAKINI HAWAKUWA WA KWETU. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio  wa kwetu.

    1 Yohana 2:18-19

    Sio kila mtu ameitwa kuwa sehemu ya timu yako.  Kwa kawaida tunatumia akili tunapowachagua watu ambao tungelipenda wawe pamoja nasi kihuduma.  Lakini Mungu mwenyewe ameshawachagu watu ambao wanatakiwa wawe sehemu katika matazamio yako.

    Kwa miaka sasa,  nimeshapitia kipindi chenye huzuni  kwa kuweza kuwaruhusu  watu ambao nilifikiri kuwa wangeliweza kuwa nami maisha yote kihuduma.  Lakini baadhi yao nilipokutana nao baada ya kuondoka kwao kwangu nilishikwa na mshangao mkubwa kwa mabadiliko waliyopata. Kwa kusema kweli nisingelikuwa nimewachagua wengi wa wale nilio nao sasa.  Lakini Mungu aliwaita ili waweze kunisaidia kupambana katika huduma.  Usipate shida watu wanapoondolewa ili waondoke kwako.  Wakati mwingine ni kwa ajili ya malengo yako ya milele kwamba waondolewe na kupatiwa wengine.

    6. Mungu anaweza kuruhusu  watu wakuache ili kwamba uweze kuelewa jinsi ambavyo Baba wa mbinguni anahisi wakati watoto wake wamwachapo.

    Akasema, mtu mmoja alikuwa na wana wawili; yule mdogo akamwambia babaye, baba nipe sehemu ya mali inayoniangukia. Akawagawia vitu vyake. Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali;  akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.

    Luka 15:11-13

    Kuwa baba inahusisha kuwa mwangalizi wa aina zote za watoto. Wakati mwingine, Mungu anaweza akakuruhu kupitia mambo fulani ili kwamba wewe uweze kukomaa na kuwa baba. Huwezi kuwa baba kwa sababu tu ya umri wako mkubwa. Unakuwa baba kwa sababu una watoto. Unakuwa baba kwa sababu  unaweza kushughulikia aina zote za watoto  na mambo wanayoyafanya.

    Mkumbuke Yakobo ambaye alikuwa na watoto wengi.  Kila mtoto alikuwa na tabia tofauti na mwingine.  Watoto wengine huondoka  kimya kimya kama vile mwana mpotevu alivyofanya. Mambo haya humtokea mungu kwani yeye ni baba yetu sisi sote.  Katika hatu za kukufikisha kwenye ubaba, watu wengine watakuacha pia. Kutenda wema na kuonyesha kukomaa au kukua kukabiliana na watu waliokufikisha ghafla mahali pasipostahili, kukuacha na kukutelekeza wakikuacha na maumivu makubwa, nap engine  kugeuka na kuwa kinyume nawe, ni sehemu ya maendeleo ya kukufanya wewe kuwa baba. Hii ndiyo sababu ambayo Mungu anaweza kuwaruhusu watu wengine waweze kuondoka na kukuacha  - ili kwamba uweze kuwa baba wa ukweli.

    7. Mungu anaweza  kuwaruhusu watu wengine waondoke na kukuacha ili aweze kukupata wewe na kukuongoza kwake.

    Basi  BWANA akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1