Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Wale Wanaojifanyisha
Wale Wanaojifanyisha
Wale Wanaojifanyisha
Ebook108 pages1 hour

Wale Wanaojifanyisha

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kanisa zimejazwa na wanafiki ambao huwa wakosa ushikamanifu. Ufunguo mkuu wa shetani kwa kila wakati umekuwa udanganyifu na unafiki. Kiongozi ambaye hawezi ona ndani ya barakoa ya mnafiki atateseka kwa upofu wake. Vitisho, kufahamiana na mkanganyiko ni roho mbaya ambazo kupambana na watumishi. Wakati mwingi, watu hata hawajui nini kinachopambana nao. Kitabu hiki kitakusaidia kutambua na kupambana

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613958599
Wale Wanaojifanyisha
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Wale Wanaojifanyisha

Related ebooks

Reviews for Wale Wanaojifanyisha

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Wale Wanaojifanyisha - Dag Heward-Mills

    Vitisho ni namna ya KUMZUIA au kummiliki mtu KWA NJIA YA HOFU.

    1. Vitisho ni nguvu kubwa inayowatawala au kuwazuia watumishi wa Mungu kwa kuwafanya waogope kitu fulani halisi au cha kufikirika tu.

    Vitisho ni upinzani halisi usioonekana na usioelezeka kirahisi kwa huduma. Watumishi wengi hawaendelei kufanya kile alichowaambia Mungu kufanya kwa sababu wametishwa na jambo linalofanya ukweli kuonekana kama umepitwa na wakati na vile vile kukosa umuhimu wake.

    Kwenye Maandiko hapo chini, tunaona jinsi ambavyo Nehemia alikataa kutishwa na watu wanaotumwa na shetani. Usiruhusu huduma yako iyumbishwe au kutwaliwa na vitisho vya aina yoyote.

    "Ndipo Sanbalati akamtuma kwangu mtumwa wake vile vile mara ya tano, na barua wazi asema neno lilo hilo, ya kwamba wewe na Wayahudi mwakusudi kuasi; ndiyo sababu waujenga huo ukuta; nawe wataka kuwamiliki, ndivyo wasemavyo.

    Nawe umewaweka manabii ili wakuhubirie huko Yerusalemu, kusema, yuko mfalme katika Yuda; basi sasa ataarifiwa mfalme sawasawa na maneno haya. Njoo sasa basi, na tufanye shauri pamoja.

    Ndipo mimi nikatuma kwake wajumbe, kusema, Hakukufanyika mambo kama hayo uyasemayo, lakini kwa moyo wako wewe mwenyewe umeyabuni.

    KWANI HAO WOTE WALITAKA KUTUOGOFISHA, wakisema, italegea mikono yao katika kazi, isifanyike. Lakini sasa nitaitia mikono yangu nguvu. Nikaingia nyumbani kwa Shemaya, mwana wa Delaya, mwana wa Mehetabeli, aliyekuwa amefungwa; naye akasema, tukutane nyumbani mwa Mungu, ndani ya hekalu, tukaifunge milango ya hekalu; kwa maana watakuja kukuua; naam, wakati wa usiku watakuja kukuua. Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia. Nikatambua, na tazama, siye Mungu aliyemtuma; lakini amefanya unabii huu kinyume changu; nao Tobia na Sanbalati ndio waliomwajiri. KWA SABABU HII ALIAJIRIWA, ILI MIMI NIOGOPE, NIKAFANYE HIVYO NA KUTENDA DHAMBI, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie" (Nehemia 6:5-13).

    Miaka michache iliyopita nilikaribishwa kwenda kuhubiri katika kanisa fulani lililokuwa na maelfu ya waumini. Sijawahi kufika pale na wala sikujua nitarajie nini. Rafiki yangu mmoja alisikia nimekaribishwa kwenye kanisa hili kubwa, alinionya nihubiri ujumbe mzuri na kama nisingefanya hivyo nisingepata zawadi nzuri.

    Aliniambia yeye alihubiri katika kanisa hilo hilo na aliambiwa na Mchungaji kwamba mahubiri yake hayakuwa mazuri. Mchungaji alimwambia kwamba waumini hawakufurahia jumbe zake na kwa hiyo zawadi yake ilipunguzwa sana.

    Nilistushwa na taarifa hii, nikajiuliza kama naweza kuhubiri ujumbe mzuri. Nilijiuliza, Ujumbe mzuri ni upi? Nihubiri juu ya nini? Je, nihubiri kuhusu upendo au mafanikio? Nihubiri kuhusu pesa au jinsi ya kufanikiwa? Nilijua watu wanapenda kama hizo.

    Nilijisikia shauku na pia kutishwa na wazo kwamba ujumbe wangu utapimwa namna hiyo na Wachungaji na pia waumini. Nahitaji ujumbe utakaonifanya nipendwe na pia niwe maarufu ili niweze kupokea sadaka nzuri!

    Ndipo Roho Mtakatifu akaniambia, Hubiri ninachokwambia, hubiri ujumbe niliokupatia.

    Pale pale nikawekwa huru kutoka kwenye uhitaji wa kumpendeza mtu yeyote. Kile alichoniambia Roho Mtakatifu kikawa ndio nguzo yangu na nikamwomba Mungu anipe ujasiri kutamka ujumbe ambao alinipa. Bila kujali wengine wangeuonaje, nikahubiri kile Bwana alichoniambia. Na mwishowe nilifurahi kwamba sikutishwa na vitisho kwamba ujumbe wangu utakosolewa sana. Niliwekwa huru na uhitaji wa kuhubiri juu ya upendo au mafanikio. Nilihubiri Injili na uwepo wa Mungu ukadhihirishwa.

    2. Vitisho ni kumyumbisha mtu asifanye jambo fulani kwa kumtishia kufichua siri fulani uliyonayo juu yake. Roho ya vitisho husema Nakujua, najua mambo yako yote.

    Mtu asiyekujua vizuri hawezi kukutisha. Vitisho huja kutoka kwa watu wanaotumia vibaya kibali walichopewa juu ya mambo ya mtu. Ni watu wanaokufahamu ndio wanaoweza kukutisha. Roho ya kuzoeana na roho ya vitisho hufanya kazi pamoja.                                                 

    Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti,

    akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?

    NAKUTAMBUA U NANI, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke.

    Marko 1:23-25

    Najua Huna Miujiza

    Namkumbuka kijana mmoja aliyenidharau halafu akahama kanisa. Alimwambia kila mtu, Huyu jamaa hana miujiza yoyote. Hakuna nguvu ya Mungu katika kanisa.

    Nilijisikia kufedheheka kuhusu hilo. Nilijiona dhaifu na kujisikia sina maana. Wakosoaji wakaendelea, Yeye ni kiongozi tu. ‘Ni mzungu’ asiye na nguvu ya Mungu bali anatumia mbinu za kiuongozi kulisaidia kanisa. Nilijisikia kuwa Mchungaji mtupu na asiye na nguvu ya Mungu. Nilijiambia, Sifanani na watumishi wa kweli wa Injili duniani."

    Miaka michache baadaye, Mungu alinibariki na nikaanza kuwa na ibada za miujiza. Kila wakati kulikuwa na miujiza, ningelimkumbuka yule mtu na jinsi alivyonibeza kwa sababu ya kukosa miujiza katika huduma yangu.

    3. Chanzo cha Vitisho ni mapepo: Ni mapepo yanayotishia kutumia habari fulani ili kukuyumbisha au kukutawala. Yesu na Paulo wote walishambuliwa waziwazi na mapepo yaliyotaka kuwatisha.

    Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.

    Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.

    Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

    Matendo 16:16-18

    Usiku mmoja, katika nchi ya kigeni, nilikuwa peke yangu nikiwa nimelala kitandani kwangu nikaona jitu kubwa lililokuwa uchi lenye urefu wa futi nane au tisa likisimama pembeni mwa kitanda changu. Pale pale nikatambua ninaona katika Roho na kwamba ninayemtazama ni Ibilisi. Niliogopa.

    Ghafula, akaanza kunicheka ndipo nilitambua kitu kisicho cha kawaida. Lile jitu kubwa jeusi lilikuwa na sura ya mtu ninayemfahamu.

    Mtu huyu alikuwa kanisani kwangu lakini alinibeza na kudharau juhudi zangu za kufanya kazi ya Mungu.

    Wakati huo nilikuwa nimeshakatishwa tamaa na kutishwa kwa mambo aliyosema.

    Yalikuwa ni maono ya kutisha

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1