Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu
Ebook364 pages7 hours

Roho Mtakatifu

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Mfariji si kitabu tu kingine cha theolojia, bali ni mwongozo unaofaa sana na muhimu wa kuingia katika njia ya maisha yenye kujaa na kuongozwa na Roho. Wale walio na shauku ya kumjua Roho Mtakatifu kwa undani na kupata uzoefu Wake watabarikiwa watakapousoma uchanganuzi wa Dkt. Bailey wa mambo saba yanayomhusu Roho Mtakatifu:

  • Nafsi Hai ya Roho Mtakatifu
  • Huduma ya Roho Mtakatifu
  • Roho Saba za Bwana
  • Ubatizo wa Roho Mtakatifu
  • Karama Tisa za Roho Mtakatifu
  • Matunda Tisa ya Roho Mtakatifu
  • Maisha Yaliyojaa na Kuongozwa na Roho Mtakatifu
LanguageKiswahili
Release dateJun 1, 2021
ISBN9781596658998
Roho Mtakatifu

Related to Roho Mtakatifu

Related ebooks

Reviews for Roho Mtakatifu

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Roho Mtakatifu - Dr. Brian J. Bailey

    ROHO MTAKATIFU

    Mfariji

    Toleo 1.0 - Kimetafsiriwa kutoka Toleo

    la 1.0 la Kiingereza

    na

    Brian J. Bailey

    Roho Mtakatifu – Mfariji

    Toleo 1.0 kwa Kiswahili

    Kazi hii ni tafsiri ya Kiswahili ya kitabu:

    "The Holy Spirit – The Comforter"

    Toleo 1.0 kwa Kiingereza

    Kimetafsiriwa kutoka Kiingereza na Asubisye Mejala

    © 1995 na Brian J. Bailey

    Ubunifu wa Jalada la Mbele:

    ©  na Zion Fellowship, Inc.

    Haki Zote Zimehifadhi Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoweza kutolewa tena kwa njia yoyote au kwa njia yoyote ya kielektroniki au njia ya kiufundi bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mchapishaji, isipokuwa kwa nukuu fupi katika nakala au hakiki.wa

    Nukuu zote za Maandiko zilizotumika katika kitabu hiki zinatoka katika toleo la Biblia ya Kiswahili la Union Version isipokuwa itakapotajwa tofauti.

    Iliyochapishwa kama e-kitabu mnamo  2021

    huko Merika

    Kitabu cha E-ISBN 1-59665-899-1

    Kwa habari zaidi juu ya e-vitabu, tafadhali wasiliana na:

    Wachapishaji wa Kikristo wa Sayuni

    Ushirika wa Sayuni Ushirika ®

    P.O. Sanduku 70

    Waverly, New York 14892

    Simu: (607) 565 2801

    Faksi: 607-565-3329

    www.zcpublishers.com

    Kwa maswali juu ya vitabu vilivyochapishwa, tafadhali wasiliana na:

    Kimechapishwa Tanzania

    Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na:

    Zion Fellowship Incorporated

    S.L.P 2148

    Mbeya, Tanzania

    Simu: +255 (0) 686-170157

    Barua Pepe: blviola@gmail.com

    Wakfu

    Kitabu hiki kwa heshima kinatolewa wakfu kwa Utatu Mtakatifu, nikiamini kwamba kwa namna kidogo kinaonyesha kwa uaminifu maisha, kazi na huduma ya Roho Mtakatifu aliyebarikiwa.

    Kwa kufanya hivyo, maombi yangu ni kwamba Baba, Mwana, Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo, na Mfariji ambaye ni Roho Mtakatifu, atapokea utukufu.

    Shukrani

    Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watu wafuatao ambao wamefanya kazi ya toleo la Kiingereza la kitabu hiki: Brian Alarid, Carla Borges, Joe Cilluffo, Sandra Higman, Mary Humphreys, Justin Kropf, Lois Kropf, Sharon Miller, Claudia, Rebeca and Raquel Molina, Leslie Sigsby, Jessica Sparger, Caroline Tham, Joyce Walcott na Suzanne Ying.

    Na kwa watu waliofanya kazi ya toleo la Kiswahili: Stan Da, Justin Kropf, Joshua Silomba, Jerome Tonde, Benjamin Viola na Richard Yalonde.

    DIBAJI

    Tumechagua jina la kitabu chetu kuwa Roho Mtakatifu – Mfariji, kwa sababu hii ndiyo huduma ya msingi ya Roho Mtakatifu. Yesu alipofanya safari yake ya mwisho duniani kutoka Chumba cha Juu hadi Gethsemane, aliwaambia wanafunzi wake, Yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu, (Yn. 16:7).

    Msaidizi huyu mpendwa daima huwa nasi kwa ajili ya kututia moyo na nguvu katika safari yetu ya Maisha kutoka duniani kwenda mbinguni. Atatuongoza katika kweli yote na atatuonyesha mambo yajayo katika maisha yetu, na pia yale mambo yatakayotokea kwa mataifa na Kanisa.

    Kitabu hiki kinatolewa kwa matumaini kwamba utakuwa na uzoefu na kumjua Roho Mtakatifu kama ambaye anakuwezesha kuzaliwa mara ya pili, Yeye anayekuwezesha na nguvu kutoka juu unapobatizwa/jazwa na Roho Mtakatifu, na ambaye anakupaka mafuta kwa ajili ya huduma.

    Brian J. Bailey

    Nafsi Hai ya Roho Mtakatifu

    UTATU MTAKATIFU

    Mungu wa ulimwengu wote, Mungu pekee tunayemtumikia, ana nafsi tatu zinazotambulika, zilizo tofauti. Nafsi hizi tatu ni Mungu Baba, Mungu Mwana (Bwana Yesu Kristo), na Mungu Roho Mtakatifu. Japokuwa ni nafsi tatu, tunapaswa kuelewa kwamba Zote hizi ni Mungu mmoja tu, si miungu mitatu katika nafsi moja.

    Uungu unadhihirishwa kama nafsi zaidi ya moja katika Mwanzo 1:26, ambapo Bwana alisema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu. Kutoka mwanzoni kabisa kwenye Neno la Mungu, katika sura ya kwanza ya Biblia, Mungu anaweka wazi kwamba kuna nafsi tatu katika Uungu.

    Mungu Baba anaitwa Mzee wa Siku (Dan. 7:9, 13), na Mtukufu Aliye Juu (Ebr. 1:3). Daima anaonekana kama aliyeketi juu enzini (Dan. 7:9, Uf. 5:6-7). Yeye ndiye chanzo na asili ya kila kitu. Kutokana na Yeye zilitokea nafsi mbili nyingine ambazo daima zilipatikana katika Yeye. Baba ana sura na mwonekano kama wa Mwana, lakini ni roho (tazama Yn. 5:37, 4:24). Mungu Baba, Bwana Yesu Kristo, na Yehova wa Agano la Kale. Ndiye, na si Mungu Baba aliyemtokea Abraham. Musa, na manabii wengine. Anafanana kabisa na Baba, ila Yeye ni kijana.

    Bwana Yesu alithubutu kumwambia Filipo katika Yohana 14:9, Aliyeniona mimi amemwona Baba. Baba na Mwana wanafanana. Mwana ni ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake (Ebr. 1:3), lakini Baba anaonekana mkubwa zaidi. Mwana ana mwili wa kibinadamu unaoonekana, kwa kuwa ni sura ya Mungu inayoonekana, na Ndiye anayemiliki na kutawala Ufalme wa Baba yeke.

    Roho Mtakatifu pia ni nafsi. Ni nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu. Ni nafsi tofauti aliyetoka kwa Mungu, japokuwa ni sawa na Mungu (tazama Yn. 15:26). Ni roho, lakini pia ana mfano wa Baba na Mwana. Mara nyingi Roho Mtakatifu hutajwa katika Maandiko kama Yeye – He na si Kile – it. Yeye si nguvu fulani, bali ni nafsi. Huchukua amri za Baba na Mwana, na kusudi Lake la msingi ni kumtukuza Mwana.

    Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wako sawa. Kimsingi wanafanana kitabia, na ni wamoja katika maono, mawazo, na kusudi. Wafilipi 2:6 inamzungumza Yesu, Hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho. Katika Yohana 5:17 Yesu alisema, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi. Matokeo ya mstari huu yanaweza kuonekana kwenye mstari wa 18. Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Hivyo, Baba na Mwana ni wazi kwamba wako sawa.

    Kabla Bwana Yesu hajaenda msalabani, aliahidi kwamba atamtuma Msaidizi mwingine badala Yake, tunayemfahamu kwamba ndiye Roho Mtakatifu (Yh. 14:16, 16:7). (Hili neno mwingine kwa tafsiri ya moja kwa moja ya Kiyunani linamaanisha mwingine mwenye sifa zinazofanana.) Aliye sawa ndiye anayeweza kutumwa kwa niaba ya mwingine. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa uwazi kutoka kwenye Maandiko kwamba Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni wamoja.

    Hata Hivyo, kuna digrii tofauti za mamlaka katika Uungu. Baba ndiye mkuu. Ndiye mkuu katika nafasi na mamlaka. Mwana aliliweka wazi hili katika Yohana 14:28, aliposema, Baba ni mkuu kuliko mimi, Mwana na Roho Mtakatifu wananyenyekea kwenye mapenzi ya Baba. Yesu alimwambia Baba Yake, Si mapenzi yangu, bali mapenzi yako yatimizwe. Mwana ni mrithi wa mali ya Baba Yake, na Baba amempa vitu vyote mikononi Mwake (tazama Ebr. 1:2, Yn. 3:35, 13:3). Hamu yake ni kutufanya warithi pamoja Naye.

    Bwana Yesu atarithi falme zote za ulimwengu huu (Uf. 11:15). Anatawala Ufalme wa Baba Yake kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Katika Milenia (Miaka 1000), Mwana atatawala duniani katika mwili na utu wake. Hata hivyo, bado atatiishwa chini ya Baba yake. Wakorintho wa kwanza 15:28 inaweka hili wazi sana: Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote. Roho Mtakatifu, vilevile hufanya tu kile Baba anachomwambia kufanya (Yn. 16:13). Utatu Mtakatifu hufanya kazi pamoja katika umoja mkamilifu na kupatana katika kuuongoza ulimwengu.

    Roho Mtakatifu ni nafsi hai, na sio ushawishi. Yupo sawa na Mungu Baba na Mwana, lakini yupo chini yao.

    Utatu Unaodhihirishwa Katika Maandiko

    Utatu Mtakatifu unaweza kuonekana sehemu nyingi katika Maandiko. Kwa sasa tutayaangalia machache. Katika uumbaji, Mungu baba alitoa amri ulimwengu kuumbwa na kuwa na sura yake. Alilifanya hili kupitia Mwana, aliyetamka maneno ya Baba Yake (Ebr. 1:2, Ef. 3:9, Kol. 1:16). Lakini alikuwa ni Roho Mtakatifu aliyetembea juu ya uso wa dunia, na kusababisha kila kitu kutokea na kuwa katika mpangilio. (Mwa. 1:2-3).

    Washirika hawa watatu wa Uungu wanaweza pia kuonekana katika Kristo kufanyika mwanadamu. Baba aliuandaa mwili wa kibinadamu katika tumbo la Mariamu kwa ajili ya Mwana Wake Yesu Kristo kupitia Roho Mtakatifu (tazama Ebr. 10:5). Luka 1:32-35 inasema: Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi…Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.

    Hapa Baba anatajwa kama Aliye Juu na pia Bwana Mungu. Yesu anaitwa Mwana wa Aliye Juu, na Roho wa Mungu anatajwa kama Roho Mtakatifu (Holy Ghost). Hivyo, tunaona kwa uwazi katika Maandiko matakatifu Ushahidi usiopingika wa washirika watatu wa Uungu.

    Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wanaonekana tena katika ubatizo wa Yesu katika Mto Yordani. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye (Math. 3:16-17). Wakati Mwana akiwa amesimama kwenye mto akiwa anabatizwa, Roho Mtakatifu alimshukia kama hua, and Baba alizungumza kutoka mbinguni akisema kwamba alikuwa amependezwa na Mwanaye.

    Utatu Mtakatifu pia unaonyeshwa katika mwongozo wa ubatizo wa maji uliotolewa na Bwana Yesu katika Mathayo 28:19: Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Paulo aliliweka hili wazi sana pale alipowauliza Wakorintho swali ambalo hakuhitaji kujibiwa kama alimbatiza yeyote kati yao kwa jina lake (angalia 1 Wakorintho 1:12-15). Hakika, Paulo hakubatiza yeyote kwa jina lake! Wote walibatizwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

    Utatu Mtakatifu unadhihirishwa kupitia mateso ya Yesu pia. Paulo alisema katika Waebrania 9:14, basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Mwana wa Mungu alienda msalabani kwa nuvu ya uwezesho wa Roho Mtakatifu aliyekuwa pamoja Naye, akijitoa pasipo doa kwa Baba Yake.

    Baba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu kupitia nguvu za Roho Mtakatifu. Warumi 8:11 inatuma Ushahidi wa kimaandiko kuhusiana na ukweli huu: Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Paulo anarudia ukweli huu katika Warumi 6:4: "Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima." Ni Roho yuleyule ambaye atawafufua watakatifu katika siku ya ufufuo.

    Mwonekano mzuri wa Utatu Mtakatifu ulionekana wakati Stefano akiuawa. Matendo 7:55-56 inazungumza kuhusu Stefano, Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Hapa Stephano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, aliyafungua macho yake ili kumtazama Mwana akiwa amesimama katika mkono wa kuume wa Baba. Alikuwa akisubiri kumpokea mbinguni. Kwa kawaida, Kristo ameketi katika mkono wa kuume wa Mungu, lakini hapa anasimama kumpokea mmoja wa watakatifu wake wapendwa.

    Washirika watatu wa Uungu pia wanaonekana mbinguni: Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi (Uf. 5:6-7).

    Yohana Aliyependwa na Mungu alipoona kitabu mbinguni kilichotiwa muhuri, alilia kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kukifungua kitabu hiki. Hata hivyo, Mwanakondoo wa Mungu, Bwana Yesu, aliweza kukifungua kitabu hivyo akakichukua kitabu kutoka katika mkono wa kuume wa Mungu Baba aliyekuwa ameketi enzini Pake. Mwanakondoo amedhihirishwa kuwa na macho saba, ambayo ni roho saba za Mungu. Huyu ndiye Roho Mtakatifu aliyetulia juu ya Yesu. Hivyo, Utatu Mtakatifu unadhihirishwa vizuri katika maandiko.

    cover.jpg

    Katika 2 Wakorintho 13:14 kuna maombi ya kitume yanayotolewa na Mtume Paulo yanayotusaidia kuuona Utatu Mtakatifu: "Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amen."

    Paulo anazungumza kuhusu neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu. Tunawezaje kuwa na ushirika na nguvu? Ni wazi kwamba hatuwezi. Hivyo, Roho Mtakatifu ni nafsi iliyo hai, na anawatamani wale anaoweza kuwa na ushirika nao, na ambao anaweza kuwashirikisha hisia zake na matakwa yake ya ndani kabisa.

    Kama ambavyo tumetaja, Mwana anafanana na Baba. Tofauti ya pekee ni kwamba mwonekano wa Baba ni wa ukubwa kidogo. Kwa namna hiyo hiyo, Roho Mtakatifu anao mwonekano (Umbo). Inaweza kuwa vigumu hata hivyo mtu kuwa na maono ya Roho Mtakatifu, au kumuona. Licha ya hivyo, tunaweza kuwa na ushirika naye kwa sababu tumeumbwa katika mfano wake, na pia Yeye ni Mungu. Zaburi 103:13 inazungumza kuhusu Mungu Baba ambaye anatuonea huruma (au anatupapasa na kutugusa) kama baba anavyofanya kwa watoto wake.

    Miaka mingi iliyopita, nilipata maono ya Mungu Baba kutokea mgongoni, na katika maono haya, Alikuwa akiwagusa kwa upole Watoto mbinguni. Ziko nyakati ambazo tunaweza kuhisi hata mkono wa Bwana Yesu Kristo juu yetu. Nimekuwa nikihisi mkono wa Bwana ukiwa juu yangu kwenye matukio kadhaa. Kwa namna hiyo hiyo, tunaweza kumhisi Roho Mtakatifu akitufunika na kutupaka mafuta, na tunaweza kuwa na ushirika naye. Huu ni upendeleo mkubwa na heshima. Tusilichukulie jambo hili kwa wepesi.

    Tunapaswa kuomba kwa Roho Mtakatifu kama ambavyo tunaomba kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu. Kwa nini? Kwa kuwa Yeye ni nafsi ya tatu ya Uungu. Roho Mtakatifu anapaswa kuwa halisi kwetu. Tunapaswa kumtegemea na kuutambua uwepo wake katika nyakati zote. Kila mwamini aliyezaliwa mara ya pili na kujazwa Roho Mtakatifu anapaswa kusikia uhitaji wa kusogea karibu kwa Roho Mtakatifu. Kwa umuhimu wake, hilo ndilo kusudi la kitabu hiki.

    VIPENGELE SABA VYA UTU WA ROHO MTAKATIFU

    Roho Mtakatifu kimsingi si nguvu au uwezo fulani, lakini badala yake ni mtu (nafsi) ambaye ana sifa na tabia zinazohusiana na utu unaotambulika. Kama tunataka tuelewe umuhimu wa mshirika wa tatu katika Uungu, lazima tuchambue sifa au tabia hizi.

    1. Ana utashi au akili

    Mtume Paulo alitaaja katika Warumi 8:27 kwamba na yeye Aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu. Kutoka katika andiko hili tunaelewa kwamba Roho Mtakatifu ana utashi (akili). Utashi hauhusiani na nguvu. Bali ni moja ya sifa za mtu.

    Mitume walitamka katika Matendo 15:28, Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima. Katika hali hii katika Matendo 15, Roho Mtakatifu alikuwa kiweka wazi utashi wake na mawazo Yake ili yafahamike na mitume kuhusiana na mambo ya kiibada ambayo Wamataifa walipaswa kuyafuata. Hivyo, tuna mfano mzuri hapa kuhusu utashi wa Roho Mtakatifu.

    2. Ana kipawa cha hiari

    Tunaporejea kwenye ugawaji wa karama tisa za Roho Mtakatifu katika 1 Wakorintho 12:11, Mtume Paulo anasema, lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Kwa hiyo, Roho Mtakatifu pia ana kipawa cha hiari. Ni Roho Mtakatifu anayeamua karama zipi tunapaswa kuwa nazo, na hugawa karama kadhaa kwa kila mwamini sawasawa na anavyopenda.

    3. Ana hisia

    Roho Mtakatifu ana hisia pia. Paulo aliwaandikia waamini wa Efeso, "Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi" (Ef. 4:30). Isaya 63:10 inazungumza kuhusu Waisraeli waasi ambao walimhuzunisha Roho Mtakatifu. Tunapomkaidi Roho Mtakatifu na kufanya mambo yasiyompendeza, tunaleta huzuni kwa Roho Mtakatifu.

    Kuna nyakati tunaweza kuhisi huzuni tuliyomsababishia, kwa kuwa Roho Mtakatifu anao uwezo wa kuwasiliana nasi kuhusu hisia zake mioyoni mwetu. Pia, Roho Mtakatifu ana huruma sana, hivyo hutafuta kuumba upendo na matunda yake yote katika maisha yetu (tazama Gal. 5:22-23).

    4. Anaweza kudanganywa

    Akiwa kama mtu (nafsi iliyo hai), Roho Mtakatifu anaweza kudanganywa. Petro alimwambia Anania kwenye Matendo 5:3, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Hatuwezi kuidanganya nguvu; tunaweza tu kumdanganya mtu. Katika Yohana 16:7-15, Roho Mtakatifu anatajwa kama He au Him mara 12 – Huyu/Yeye. Kamwe hatajwi kama it – hiki/kile katika Maandiko ya asili.

    5. Inawezekana kumkufuru

    Bwana Yesu alitamka katika Mathayo 12:31-32: Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao. Katika kifungu hiki, Kristo alimweka Roho Mtakatifu katika kiwango sawa na Yeye. Alisema kwamba wale wanaomkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa. Hivyo, Roho Mtakatifu, kama nafsi aliye hai, inawezekana kumkufuru kama ambavyo inawezekana kumkufuru Mwana wa Mungu. Kumkufuru Roho Mtakatifu hutokea pale mtu anapotoa sifa kwa Shetani kuhusu kazi alizozifanya Roho Mtakatifu huku akijua moyoni mwake kwamba kazi hizi kimsingi ni za Roho Mtakatifu.

    6. Anaweza kuzungumza

    Roho Mtakatifu ana uwezo wa kuzungumza; nguvu au uwezo fulani hauwezi. Kama ilivyoandikwa katika Matendo sura ya 10, Patro alipokea maono ambayo yalimdhihirishia kwa uwazi kwamba Wamataifa walikuwa wanakubalika na Mungu. Alipokuwa akitafakari kuhusu maono haya, alisikia mtu akizungumza naye: Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta. Basi ondoka ushuke ufuatane nao, usione tashwishi, kwa maana ni mimi niliyewatuma (Matendo 10:19-20). Kuzungumza ni kitendo kinachofanywa na mtu. Nataka nirudie hili – Roho Mtakatifu siyo it – hiki/kile bali ni He – Huyu/Yule.

    Ukweli kuhusu uwezo wa kuzungumza wa Roho Mtakatifu unafunuliwa pia katika kitabu cha Ufunuo. Yohana alihitimisha kila ujumbe kwa makanisa saba ya Asia kwa maneno haya: "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa" (Rejea. Uf. 2:7, 2:11, 2:17, 2:29, 3:6, 3:13, 3:22). Tunaweza kumsikia Roho Mtakatifu akizungumza nasi kama tuna masikio yanayosikia, na kama tuna masikio yaliyo na umakini kwake. Kwa hiyo, tunahitaji masikio yetu ya kiroho yafunguliwe zaidi na zaidi.

    7. Anaweza kutukanwa na kuzimishwa

    Roho Mtakatifu anaweza kufanyiwa jeuri na kutukanwa, kama ambavyo Bwana Yesu anaweza kufanyiwa jeuri na kutukanwa. Katika Waebrania 10:29 tunasoma, Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

    Roho Mtakatifu anaweza kufanyiwa jeuri kwa matendo na maneno yetu. Kama tukirudi nyuma kwenye njia zetu za zamani baada ya kumjua Bwana kama Mwokozi wetu, tunakuwa tunamfanyia jeuri Roho Mtakatifu. Zaidi ya hayo, Paulo anatuambia katika 1 Wathessalonike 5:19, Msimzimishe Roho. Mambo haya saba kuhusu utu wa Roho Mtakatifu yanatoa ushahidi thabiti na uthibitisho kwamba Roho Mtakatifu kweli ni nafsi iliyo hai, na si nguvu fulani.

    img1.png

    NI MSHIRIKA WA UUNGU

    Kama tulivyosema awali, Roho Mtakatifu ni mshirika wa Uungu. Kwa namna hiyo, anazo sifa na tabia zote za washirika wengine wa Utatu Mtakatifi – Baba na Mwana. Kuna uthibitisho mkubwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Roho Mtakatifu ni mshirika wa Uungu, lakini tunakwenda kuangalia mambo sita tu yanayothibitisha hilo.

    1. Ni wa Milele

    Moja ya sifa ya Uungu ni kwamba ni wa milele (angalia Zab. 90:2, 1 Tim 1:17). Hawakuwa na mwanzo, na hawana mwisho. Yesu alikuwako, yuko, na ndiye atakayekuja (Uf. 1:4). Katika Waebrania 9:14 Mtume Paulo anaandika, basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? Kwa hiyo, Maandiko kwa uwazi yanasema kwamba Roho Mtakatifu ni wa milele. Pia ni wazi kwamba ana sifa zinazofanana za washirika wengine wa Uuungu.

    2. Yuko kila Mahali kwa Wakati Mmoja

    Sifa nyingine ya Uungu ni kwamba ni wa milele. Wanaweza kuwa kila mahali kwa wakati mmoja (mara moja). Katika Yeremia 23:24 Bwana anauliza: Je, mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana. Bwana ameijaza mbingu na dunia. Yesu ataonwa na kila mtu ulimwenguni kote katika ujio wake wa pili (Uf. 1:7, Math. 24:30). Roho Mtakaifu pia yuko kila mahali kwa wakati mmoja. Anao uwezo wa kuwa kila mahali kwa wakati mmoja.

    Katika Zaburi 139:7 Mfalme Daudi anauliza swali hili: Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? Kisha anaendea: Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika (Zab. 139:8-10). Mungu anaongoza mambo ya kuzimu, vilevile na mambo ya mbinguni. Watu ambao wamewahi kuwa na maono ya kuzimu wanathibitisha hili. Mfalme Daudi alikuwa anafahamu kwamba haijalishi alikoenda kwa sababu Roho Mtakatifu alikuwa kila mahali. Alihisi uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake kila wakati. Kwa hiyo, kama tunatembea nuruni, tunahakikishiwa kwamba Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nasi bila kujali tunakoenda.

    3. Ana Nguvu Zote

    Kama washirika wengine wawili wa Uungu, Roho Mtakatifu ana nguvu zote, au uweza wote. Malaika wa Bwana alimwambia Mariamu katika Luka 1:35, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Roho Mtakatifu anaitwa nguvu za Aliye juu, kwa kuwa ana nguvu zote.

    Bwana Yesu alitamka katika Mathayo 28:18, kabla tu hajapaa kwenda mbinguni, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kutoka kwenye maandiko haya tunaona kwamba Kristo alipakwa mafuta,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1