Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika
Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika
Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika
Ebook67 pages38 minutes

Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Saa yako kufika haimaanishi saa katika damu na nyama, kama vile saa saba mchana au saa ya kula chakula bali inamaanisha saa katika ulimwengu wa roho. Saa ni kipimo cha muda, katika ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho pia, lakini katika ulimwengu wa roho saa inasomwa kutokana na matukio. Kwa mfano, watu wanaweza kusema huyu amepona ajali mbaya kwa sababu saa yake haijafika.

Na ninaposema mambo ya kufanya saa yako ikifika siyo lazima iwe saa ya kufa kwako lakini saa au siku ya kufikwa na jambo fulani ambalo limekuwa likisubiriwa katika ulimwengu wa roho. Saa yako ikifika katika ulimwengu wa roho huwa ni kama mtihani pia. Ukivuka kwa ufaulu unaenda kiwango kingine cha juu zaidi na ngazi njema zaidi katika Kristo Yesu. Katika kitabu hiki utajifunza mambo ya kufanya ili uweze kufaulu mtihani wako saa yako ikifika.

LanguageKiswahili
Release dateFeb 24, 2023
ISBN9798215127223
Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika
Author

Msafiri J. Mwaikusa

MSAFIRI J. MWAIKUSA is an assistant pastor at a local Assemblies of God church in Dar es Salaam, Tanzania, where he lives with his wife, Tracy, and their children. He also hosts a weekly podcast named Biblia Inasema Usiogope which can be listened to through Radio Public, Google Podcast, Apple Podcast and other platforms. He holds a bachelor degree in Bible and Theology from the Global University of Springfield MO, U.S.A; Msafiri has an MBA and business experience in food industry and publication. He also has a teaching experience from the University of Dar es Salaam where he obtained his Bachelor of Science in Molecular Biology and Biotechnology.

Read more from Msafiri J. Mwaikusa

Related to Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika

Related ebooks

Related categories

Reviews for Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika - Msafiri J. Mwaikusa

    DIBAJI

    Mara nyingi katika maisha huwa kuna mambo yanatokea ambapo inakuwa ni kama saa yako imefika. Hii saa yako kufika haimaanishi saa katika damu na nyama, kama vile saa saba mchana au saa ya kula chakula bali inamaanisha saa katika ulimwengu wa roho. Saa ni kipimo cha muda, katika ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho pia, lakini katika ulimwengu wa roho tunaweza kusema saa pia tukimaanisha siku. kwa mfano watu wanaweza kusema huyu amepona ajali mbaya kwa sababu siku yake haijafika lakini maana hiyo hiyo inaweza kufikishwa kwa kusema saa yake haijafika.

    Kwa hiyo ninaposema mambo ya kufanya saa yako ikifika siyo lazima iwe saa ya kufa kwako lakini saa au siku ya kufikiwa na jambo fulani ambalo limekuwa likisubiriwa katika ulimwengu wa roho. Pengine huweza kuitwa saa ya kujiliwa au siku ya kujiliwa au hata majira yako. Naongelea jambo ambalo linaweza kuwa kama mwisho au hitimisho wa mtiririko wa matukio fulani ambayo yamekuwa kama yakikuandaa kufika hapo mahali au saa hiyo. Kwa mfano, katika ulimwengu wa mwili mwanafunzi aliyeanza darasa la kwanza mpaka darasa la saba unaweza kusema siku yake ni ile siku ya mtihani wa mwisho kabisa wa darasa la saba. Yaani kama vile kuhangaika kote kwa miaka saba ya kusoma sasa kunafika tamati kwa tukio la kufanyika mitihani ya darasa la saba. Nadhani hapo utaweza kuelewa vizuri nini ambacho nalenga katika somo hili.

    Majira haya au siku au saa yako ikifika katika ulimwengu wa roho huwa ni kama mtihani pia. Ukivuka kwa ufaulu unaenda kiwango kingine cha juu zaidi na ngazi njema zaidi kwa kadiri kiongozi wetu Kristo Yesu anavyoona inafaa kwa utukufu wa Mungu Baba.

    Sasa basi tuangalie mambo ya kufanya saa yako ikifika.

    UTANGULIZI

    Kitabu hiki cha Mambo ya Kufanya Saa Yako Ikifika kimetokana na somo la Kibiblia. Ingawa tutakuwa tunaangalia mistari mbalimbali katika Biblia, msingi hasa wa somo lenyewe umetoka kwenye Kitabu cha Injili kama ilivyoandikwa na Yohana sura ya 12 mstari wa 20-30

    20 Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.

    21 Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu.

    22 Filipo akenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.

    23 Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.

    24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.

    25 Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.

    26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

    27 Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.

    28 Baba, ulitukuze Jina Lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

    29 Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.

    30 Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.

    (Yohana 12:20-30)

    Kwa hiyo mara kwa mara tutakuwa tunarejea kwenye kipande hiki cha Injili na kutoa jambo muhimu la kuangalia. Mambo ya kujifunza kutoka kwenye sehemu hiyo ya Injili ni mengi lakini kwa sasa ni haya tu ambayo Roho wa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1