Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kitabu cha Sherehe
Kitabu cha Sherehe
Kitabu cha Sherehe
Ebook100 pages2 hours

Kitabu cha Sherehe

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Usiku mmoja, wakati akiwa ni mwanafunzi wa utabibu katika mji mmoja huko Ghana, katika hali ya mwujiza Mungu alimpaka mafuta Dag Heward-Mills wakati alipokuwa akimsubiri Bwana. Alipakwa mafuta kwa namna isiyo ya kawaida na kusikia maneno, “Tangu sasa na kuendelea unaweza kufundisha...” Wito huu usio wa kawaida ndio uliomwongoza kwenye huduma iliyosambaa duniani kote.

LanguageKiswahili
Release dateMay 16, 2018
ISBN9781641353748
Kitabu cha Sherehe
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Kitabu cha Sherehe

Related ebooks

Reviews for Kitabu cha Sherehe

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kitabu cha Sherehe - Dag Heward-Mills

    SURA YA 1

    Sherehe ya Kumpa MtotoJina

    Sherehe ya Kumpa Mtoto Jina nisherehe ya kitamaduni ambalo hufanyika baada ya mtoto kuzaliwa. Baadhi ya familia huzingatia utamadunisana na hufuata desturi zote zinazohusiana na tarehe na wakati wa sherehe hiyo.Kimsingi, wajibu wa mchungaji ni kuingizamtazamo wa kibiblia na kiroho katika sherehe hiyo. Bila shaka hilo linawezekana tu kulingana na kile ambacho familia husika inataka ama au inaruhusu.

    1. MAOMBI YA UFUNGUZI

    2. WIMBO : Njooni Tumuabudu

    Njooni tumuabudu

    Njooni tumuabudu

    Njoonitumuabudu

    Kristo Bwana

    Yeye astahili

    Yeye astahili

    Yeye astahili

    Kristo Bwana

    John Francis Wade

    3. SABABU YA SHEREHE

    Tumekusanyika hapa leo tukiwa na ndugu yetu na dada yetu, Bwana na Bi…. (Jina la mwisho la wazazi)…kwa sababu mbili:

    i. Kufurahia kile ambacho Mungu amewatendeana

    ii. Kumpatia jina mtoto wao aliyezaliwa.

    Biblia ndio chanzo cha yote tuyafanyayo, kwahivyo, andiko letu la leo ni:

    Luka Mtakatifu 1:57-64

    Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia, alizaa mtoto mwanamume. Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye. Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamaye akajibu akasema La, sivyo; bali, ataitwa Yohana. Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwaye jina hilo. Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita. Akataka kibao, akaandika ya kwamba, Jina lake ni Yohana. Wakastaajabu wote. Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kunena akimsifu Mungu.

    Kama ilivyokuwa desturi ya nyakati hizo, tungependa kumuita baba yake motto ili atuambie jina/majina anayotaka kumpa mtoto na maana ya jina au majina hayo.

    4. BABA ANATAJA JINA [Baba anasimama na kutaja jina kamili la mtoto huyo na maana ya jina hilo au majina hayo.].

    5. TANGAZO, UTAKASO NA UTHIBITISHO WA JINA JUU YA MTOTO

    i. Mchungaji anachukua mtoto na anawaambiawatu wote wasimame na washiriki katika kumuombeamtoto.

    ii. Mchungaji anaomba huku akimwekea mtoto mikono, kishaanampaka mtoto mafuta.

    6. MAOMBI

    MCHUNGAJI: Baba katika jina la Yesu, aliye Mwanaowa pekee, tunakushukuru kwa ajili ya jina/majina yaliyopeanwa siku ya leo. Tunatakasa jina/majina haya na tunatangaza ya kuwa mtoto huyu ataitwa … [Jina au majina ya mtoto]… Kuanzia leo ninaomba ya kuwa ataishi kulingana na maana ya jina hili (majina haya),

    Mchungaji anataja maana ya jina/majinana anamuombea mtoto aweze kutimiza kusudio la jina hilo. (k.m., Yohana inamaanisha ‘Yehova ni wa neema’, Yehova Mungu na amuonyeshe mtoto huyu neema daima.)

    MCHUNGAJI: Ninampaka mtoto huyu mafuta kama ishara ya Roho Mtakatifu, ili aishi chini ya ushawishi na nguvu za Roho Mtakatifu, siku zote za maisha yake . Amina.

    7. WIMBO: Kutakuwa na Baraka

    Kibwagizo

    Kutakuwa na baraka;

    Hilo ni neno lake

    Kutakuwa na faraja,

    Bwana hutoa kwake

    Baraka nyingi

    Baraka twahitaji

    Tumepokea kiasi

    Bali twataka nyingi

    Daniel W. Whittle

    8. TAMKO LA BARAKA KWA MTOTO

    MCHUNGAJI: Baba, kwa kweli tunakushukuru kwa ajili ya zawadi yauzima iliyo nzuri na kamilifu. Asante kwakubariki familia hii na mtoto huyu. Nafuta na na nakataa kila laana na matarajio yote ya adui kuhusu maisha ya... [jina/majina ya mtoto]...

    Naangusha kuta za upinzanina fadhaaambazo zimeinuliwa kinyume na maisha ya mtoto huyu. Nainua mapenzi ya Mungu juu na dhidi ya kila mpango, tarajio na kila utabiri wa adui dhidi ya maisha yako.

    Natamkabaraka ya Mungu juu ya maisha yako.

    Wacha wema na kibali cha Mungu kiwesehemu yako siku zote za maisha yako.

    Ishi uwebaraka kwa wazazi wako.

    Ishi uwe baraka kwa kizazi chako.

    Kuwa kile ambacho Mungu alipanga uwe.Katika jina kuu la Yesu.Amina.

    9. AGIZO KWA WAZAZI

    MCHUNGAJI: Je, mnahidi kumlea mtoto huyu katika njia za Bwana ili asiweze kuziacha wakati atakapokua?

    Kulingana na kitabu cha Kumbukumbu la Torati 6:7, Je, unaahidi …kumfundisha mtoto wako Neno la Mungu uketipo katika nyumbayako, nautembeapo njiani, naulalapo, na uondokapo?

    BABA: Ndio

    MAMA: Ndio

    WAZAZI WOTE KWA PAMOJA: Ndio.

    MCHUNGAJI: Amina! Hebu tuwapigie makofi. (Mchungaji anamrudisha mtoto kwa wazazi wake.)

    10. WIMBO: Mungu Mtukufu aliye Bwana

    Kibwagizo

    Mungu Mtukufu aliye Bwana, 

    Amtoa Yesu Mpendwa Mwana

    Akawa dhabihu kwa dhambi zote,

    Kufungua njia kwa watu wote.

    Bwana mshangilie

    Njoni kwake Baba

    Kwa Yesu Mwana,

    Mpeni heshima

    Aliye Bwana

    Msifuni! Msifuni!

    Nchi Imsikie

    Msifuni! Msifuni!

    Fanny Crossby (1875)

    11. KUTOLEWA KWA ZAWADI

    MCHUNGAJI: Sasa, kama ilivyofanyika wakati Yesu alipozaliwa, mamajusi walikuja kutoka mashariki wakiwa na zawadi za za thamani ya juu.

    Sasa tutapokea zawadi ambazo zimeletwakwa ajili ya mtoto.

    12. MAOMBI YA KUFUNGA

    SURA YA 2

    Sherehe ya Kuweka Mtoto Wakfu

    Sherehe ya kuweka mtotowakfu inafanana na Sherehe ya Kumpa Mtoto Jina.Hii huwa inafanyika katika ibada kanisani.

    Kuwekwa wakfu kunafanyika baada ya kuzaliwa kwa mtoto.Jukumu la mchungaji katika Sherehe ya Kuweka Mtoto Wakfuni kumuombea mtoto na kumweka wakfu mbele za Bwana.Jambo hilo hutekelezwa katika matumaini ya kwamba mtoto atakapokuwa mtu mzima, yeye mwenyewe atakuja kumjua Bwana Yesu Kristo.

    Mchungaji anamuweka mtoto chini ya ulinzi wa Bwana na anataja majina yake na maana ya majina hayo kwa washirika.

    1. KARIBISHA FAMILIA MADHABAHUNI (Mchungaji Anayeongoza sherehe hiyo anatambulisha familia kwa washirika).

    2. SABABU YA SHEREHE

    MCHUNGAJI: Tumekusanyika hapa leotukiwa na ndugu na dada yetu, Bw. na bi..... (Jina la mwisho la wazazi)... kwa sababu tatu:

    i. Kufurahia juu ya yale Mungu amewafanyia,

    ii. Kumpa mtoto wao aliyezaliwa jina na

    iii. Kumweka wakfu mtoto huyu mbele za Bwana.

    MCHUNGAJI: Kama Biblia inavyofundisha, tutamuita Baba ya mtoto

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1