Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Waambie
Waambie
Waambie
Ebook146 pages10 hours

Waambie

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Mashamba ni meupe na mavuno ya roho yameiva, lakini je, wako wapi wahubiri? Kitabu kipya cha Dag Heward-Mills kinachovutia ni mwito wa ddharura kwa Wakristo ike wawe washinda roho.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613958520
Waambie
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Waambie

Related ebooks

Reviews for Waambie

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Waambie - Dag Heward-Mills

    Kuokoa roho ni kazi muhimu ya kuwaleta watu ambao hawajaokoka kwa Yesu Kristo.

    Roho zinaweza kuokolewa kwa kupitia uinjilishaji binafsi wa Injili, mkutano mikubwa ya Injili, mafunzo na maandiko ya Kikristo. Kazi za kimisionari, matamasha ya Injili, nyimbo za Kikristo hizo ni baadhi tu.

    Njia ya zamani ya kuokoa (kuvuta) roho zilizopotea ilikuwa ni kupitia maisha ya kujitoa ya wamisionari ambao walijitoa nafsi zao kwa ajili ya ukombozi wa mataifa, makabila na watu wote.

    Njia nyingine iliyozoeleka ya kuokoa roho ni kupitia mikutano mikubwa na uinjilishaji kupitia shuhuda za watu mbalimbali.

    Kitabu hiki kinaelezea kuhusu kuokoa roho (kuokoa nafsi) kupitia njia yoyote ile inayowezekana. Inahusisha uinjilishaji binafsi, mikutano mikubwa, vitabu, wamisionari. Kwa njia yoyote ile inatupasa kuokoa/ kuvuta roho.

    Unaweza kuuliza, Kwa nini sababu nyingi hivyo?

    Rafiki yangu mpendwa, nimekupa sababu mia moja na ishirini tu za kwa nini unapaswa kuokoa roho na ninakuhakikishia kwamba kuna sababu nyingi zaidi ambazo nimeshindwa kuwashirikisha.

    Zisome na kuziamini na upate roho ya Kristo, ambayo ni roho ya muokoa nafsi.

    Sura ya Kwanza

    Sababu mia moja na ishirini kwa nini unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi.

    1. Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu huu ndio wajibu mkuu, amri kuu, mamlaka kuu, agizo kuu, mpango mkuu tuliopewa na Bwana na Mkombozi wetu Yesu Kristo.

    Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

    Mathayo 28:18-20

    2.Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu wote tumeitwa kwa ajili ya kazi hiyo kuu.

    Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache; Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.

    Mathayo 22:14; 20:16

    Kile William Booth Alikisema Kuhusu Wito

    "Ulisema haukuitwa? Nadhani ulitakiwa kusema haukusikia wito."

    Elekeza masikio yako kwenye Biblia umsikilize (BWANA) anapokutaka uende kuwavuta wenye dhambi kutoka katika moto wa dhambi! Elekeza masikio yako kwa moyo wa binadamu wenye kupata mateso makali na wenye mizigo na usikilize kilio chake, cha kuomba msaada.

    Nenda kasimame kwenye milango ya jehanum, usikilize hukumu za kwenda motoni zinavyokusihi uende kwenye nyumba za baba zao na kuwaambia kaka na dada zao na watumishi na mabwana zao ili wasiende huko.

    Kisha mwangalie Yesu usoni - ambaye huruma yake umeikiri kuitii - na umwambie kama utaunganisha moyo na roho na mwili na hali yoyote katika kutangaza rehema yake kwa ulimwengu.

    William Booth, mwanzilishi wa Jeshi la Wokovu

    Ninaamini kwamba katika kila kizazi Mungu amewaita wanaume na wanawake wa kutosha kutangaza Injili kwa makabila yote ambayo hayajafikiwa na Injili. Siyo kama Mungu Haiti watu, ila ni binadamu ambao hawaitikii wito.

    Isobel Kuhn, mmisionari wa China na Thailand

    3. Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu uliumbwa ili kufanya kazi njema ya kuokoa roho.

    Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

    Waefeso 2:10

    Niliwahi kuzungumza na dereva mmoja huko Uingereza nilimwambia kuwa mimi ni Mkristo na kuanza kushirikiana naye habazi za Kristo. Nilimwambia pia kuhusu uhalisi wa mbingu na kuzimu. Alicheka na kuniuliza kama ni kweli nakiamini kile nilichokiongea.

    Alisema, Kama hakika mbingu ni halisi, kwa nini Wakristo wasijiue wenyewe ili waende huko?

    Alichokuwa akijaribu kusema ni kwamba kwa sababu mbinguni ni mahali pazuri zaidi, Wakristo hawana haja ya kuishi duniani, wajihamishie wenyewe mbinguni kwa kujiua.

    Kama kwa hakika Wakristo hawana kitu cha kufanya hapa duniani basi mtu huyu alikuwa sahihi kusema yale aliyoyasema. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Wakristo wana mambo mengi ya kufanya kabla hawajafika mbinguni. Tunatakiwa kushuhudia na kutangaza Injili ya Yesu Kristo. Tunapaswa kuokoa waliopotea kwa gharama yoyote ile.

    Wokovu wa mamilioni ya watu unatutegemea sisi. Ninasikitika kusema kwamba Wakristo wengi hawajajua sababu zilizofanya waokolewe.

    Biblia inasema kwamba tumeokolewa ili kutenda yaliyo mema.

    Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.

    Waefeso 2:10

    Wakristo huteleza kila siku kwa sababu hawana kusudi la kukaa ndani ya kanisa, watu huhudhuria kanisani na baada ya muda mfupi huanguka, wakiona hakuna maana ya kuwa na kanisani. Mtu yeyote anayefanya kazi ya kuokoa roho ataanza kugundua sababu ya wokovu wake. Kuokoa roho huongeza utukufu wa Mkristo.

    4. Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu kuokoa roho huwapa furaha kuu Wakristo na kuwatia nguvu.

    Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.  Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu. Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.

    Luka 10:1-3, 17

    Wakati wowote unapoenda kuhubiri utarudi ukiwa mwenye furaha. Kuna furaha roho zinapookolewa, siwezi kuelezea. Ni mama pekee anayeweza kuelezea jinsi gani anavyojisikia baada ya mtoto kuzaliwa. Nimewaona hata hivyo matesohayo ni juhudi zote haziwazuii wao kutofurahia.

    Unapowaleta watu mbele ya Mungu, utagundua furaha ya Mungu juu ya jambo hilo. Siwezi kuwaelezea, unapaswa kugundua wewe mwenyewe. Nimegundua kwamba washarika katika kanisa langu wanapata nguvu wanapojihusisha na kuokoa roho za watu. Kuokoa roho kunatupa furaha itokayo kwa Mungu ndani ya kanisa.

    5. Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu ukubwa/ ukuu wa kanisa lolote hautokani na idadi ya watu waketio ndani yake bali idadi ya wale wanaotumwa kwenda nje.

    6.  Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu kuokoka roho ni uhai wa Yesu (mapigo ya moyo wa Yesu).

    Miaka iliyopita, nilipata maono katika maono haya, niliona moyo wa binadamu ukiwa umefunikwa na damu. Moyo huo ulikuwa hai. Mungu alionionyesha moyoni mwangu siku ile kwamba kilio cha moyo wa Yesu Kristo ni mavuno yaliyoko shambani. Yesu hakuacha kiti chake cha ufalme bure! Alikuja duniani kuokoa wenye dhambi.

    Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

    Luka 19:10

    7.  Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu kuokoa roho huepusha kanisa kutengana.

    Washarika wanapojihusisha na matendo yenye kuzaa matunda, hukosa muda wa kugombana na kujijengea matabaka. Wachungaji wanapaswa kuwafundisha waumini kwamba roho ni roho na ni kitu cha thamani kwa Mungu.

    8. Unapaswa kuwa muokoa roho/nafsi kwa sababu kuokoa roho huleta ulinzi na msaada wa kiroho.

    Hatuchagui sisi kuitangaza Injili au la. Tusipofanya hivyo tutakutwa na mauti.

    Peter Tayler Feisyth

    Unapookoa roho unakuza msaada wa kiroho katika kile kitu unachokifanya.

    Unaposoma Biblia utagundua kwamba wokovu wa kiroho huzalisha furaha ya mbinguni kuna majibu ya mbinguni kwa kila roho inayookolewa kwa Mungu.

    Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu, Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.

    Luka 15:7, 10

    Makanisa yanapaswa kujua umuhimu wa uwepo wao, kuokoa roho ili ziende mbinguni. Ubalozi huwepo ili kuwakilisha serikali ya nchi fulani mahali ulipo. Vivyo hivyo makanisa huwakilisha mbingu.

    Watu wengi huomba Mungu awaepushe katika dhambi. Je ulifahamu kwamba ulinzi wa kiroho upo, unapatikana kwa wale wote waliopo katika mapenzi ya Mungu.

    Zaburi ya 91 inasema Mungu atawalinda na kudumu ndani yake kwa sababu umeweka upendo wako juu yake.

    Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

    Zaburi 91:14-16

    Unapoweka mapenzi yako kwa Mungu ili umpendeze Mungu anasema kwamba atakuokoa. Mimi naamini nafanya mapenzi ya Mungu. Labda hiyo ndiyo sababu ya mimi kuwa hai hadi leo. Kama ilivyo kwa Paulo, nilikutana na vitu vichache vilivyo hatarisha maisha yangu, ikiwemo ajali ya ndege na gari.

    Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini.

    2 Korintho 11:23-25

    Katika matukio yote haya ninaweza kusema kama alivyosema Paulo kwamba Mungu aliniokoa katika haya.

    Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

    Warumi 8:38-39

    Namuona Mungu akikuokoa sasa! Namuona Mungu akikusaidia wakati wa shida zako! Namuona Mungu akiwa pamoja nawe kwa sababu ya upendo wako kwake!

    Je, unataka kuishi katika mapenzi ya Mungu? Je unataka kanisa lako likue? Okoa roho za watu leo, utaona tofauti ndani ya kanisa.

    Ninaona kazi

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1