Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kuanzisha Kanisa
Kuanzisha Kanisa
Kuanzisha Kanisa
Ebook203 pages2 hours

Kuanzisha Kanisa

Rating: 3.5 out of 5 stars

3.5/5

()

Read preview

About this ebook

Upandaji makanisa ni jambo la kiajabu ambalo limeenea kati ya watumishi wenye haiba. Ilikuwa shughuli kuu ya wafuasi wa kale. Upandaji kanisa uliofaulu, hata hivyo, unadai ujuzi na unakumbatia sababu nyingi. Dag Heward-Mills anachambua vipengeleze mbalimbali vya upandaji kanisa katika kitabu hiki. Ni mwongozo wa mafunzo kwa kila mtumishi ambaye anataka kufanya upandaji kanisa ono lake la kimaisha.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613953679
Kuanzisha Kanisa
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Kuanzisha Kanisa

Related ebooks

Reviews for Kuanzisha Kanisa

Rating: 3.6666666666666665 out of 5 stars
3.5/5

3 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kuanzisha Kanisa - Dag Heward-Mills

    Kuendelea

    Kuna nyakati ambapo mtu hujiuliza kama kanisa linasonga mbele au hapana. Zipo shughuli nyingi sana kanisani na mipango mingi inaendelea. Lakini je, Ufalme Mungu unasonga mbele kweli au unazunguka hapo hapo?

    Kuna nyakati utaona katika miji mikubwa makanisa mapya yanazuka. Mara nyingi, hayo makanisa yanakuwa gumzo la mji mzima, na inaonekana kana kwamba Mungu anafanya jambo jipya. Kila mtu anakwenda huko na kila mtu anaonekana kulipenda hili jambo jipya. Lakini ukitazama hayo makanisa mapya kwa ukaribu zaidi, utagundua kwamba ni kundi la watu waliohamia kutoka kanisa la hapo jirani tu. 

    Ufalme wa Mungu umejaa Wakristo wa kimwili ambao siku zote wanatafuta kitu kipya chenye msisimko. Wachungaji wengi wanafurahi kwa sababu ya kudhania kwamba makanisa yao yanakua, na kuna uamsho. Ukweli ni kwamba kwa ujumla ukuaji ni mdogo sana katika Ufalme wa Mungu. Hapo ni kwamba, watu wanazunguka tu kutoka kanisa moja hadi jingine. Ufalme wa Mungu unahitaji kuendelea kwa uhalisi.

    Zamani, Wazungu walituma wamishenari Afrika na Asia. Kupitia tendo hilo la kujitolea, kuna nchi nzima zilizofanyika Wakristo. Watu waliokuwa wapagani hapo kwanza wameokolewa na kumfuata Kristo. Lakini, tusijidanganye: Watu ni wengi zaidi siku hizi katika dunia kuliko wakati ule. Pia, kuna watu wengi sana ambao hawana kanisa lililo hai au mchungaji. Kuna hitaji kubwa zaidi siku hizi kwa habari ya kusonga mbele kwa kanisa katika maeneo ambayo bado hayajajua Ukristo.

    Wazungu walipotuma wamishenari miaka kama mia mbili iliyopita, walikuwepo watu kiasi cha bilioni moja tu duniani kote. Leo hii kuna watu bilioni 6 na nusu duniani. Utasikia malalamiko kutoka duniani juu ya madaktari, kwamba si wengi kulingana na idadi ya watu.

    Je, kuna anayelalamika kuhusu idadi ya wachungaji kulingana na watu? Kuna wainjilisti wangapi siku hizi, kulinganishwa na mamilioni ya watu wanaoishi siku hizi?  

    Jinsi Ya Kuendeleza Ufalme

    Ufalme wa Mungu utapata maendeleo ya kweli tutakapofuata maagizo ya Kristo. Amri ya mwisho ya Yesu ilikuwa twende duniani kote na kuwafanya watu kuwa wanafunzi!

    Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. BASI, ENENDENI, MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI, mkiwabatiza katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu; mkiwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Na tazama, mimi niko pamoja nanyi siku zote, mpaka ukamilifu wa dahari. Amina.

    Mathayo 28:18-20

    Katika andiko hili, Yesu anatuambia sisi wote tuwafundishe Neno la Mungu. Huwezi kuwafundisha watu bila kuwakusanya pamoja.

    Kanisa Hasa Ni Nini?

    Mkusanyiko wa Wakristo mara kwa mara kwa kusudi la kujifunza huitwa kanisa. Yaani, Bwana wetu alikuwa anatuambia twende duniani kote na kuwakusanya watu mara kwa mara ili kuwafundisha Neno. Mungu anashughulika na kukusanya watu wanaoweza kufundishwa. Kwa Roho Wake, Mungu anawainua watu watakaokwenda katika semu zote za dunia ili kukusanya watu mara kwa mara na kuwafundisha Neno Lake.

    Kadiri mikusanyiko na makundi yanavyozidi kuongezeka, ndivyo Agizo Kuu linavyozidi kutimizwa. Makundi mengi zaidi yakifundishwa, ndivyo Agizo Kuu linavyozidi kutimizwa. Hayo makundi ni makanisa ambayo yanapandwa na watumishi wa Bwana ambao ni watiifu.

    Tunapenda Sana Watu Watuone

    Kwa bahati mbaya sana, kwa kuwa wachungaji wengi wanajali zaidi mawazo ya watu, hawawezi kufanikisha kutimiza Agizo hilo Kuu. Tunataka tuwe na kundi moja kubwa sana, ili watu wakione waseme basi! Tunataka watu wadhanie sisi ndiyo wenyewe! Kwa sababu, kadiri watu walivyo wengi katika kusanyiko, ndivyo mchungaji anavyoonekana wa maana.

    Katika WINGI WA WATU, ndipo heshima ya mfalme ilipo (au kukubalika) …

    Mithali 14:28, TLR

    Kuna haja ya kuanzisha mikusanyiko mingi ya watu katika kila eneo linalowezekana, ili tutimize Agizo Kuu. Ukubwa wa dunia na mgawanyo wa watu unadai kwamba wachungaji na watu waondoke kwenye mfumo wa kanisa moja na kuwa na mikusanyiko mingi katika maeneo mbalimbali. Kama kweli tunamaanisha kutii Agizo la Bwana wetu, hatuna uchaguzi isipokuwa kutii hilo.  

    Viongozi lazima wafundishwe. Wachungaji lazima wafundishwe. Watendaji lazima wafundishwe. Ile hali ya watu kuwa nyota makanisani lazima ife. Hiyo hali inataka tuwe na mchungaji mmoja mkuu ambaye kila mtu anamtambua na kumsifu.  

    Tumedanganyika mara nyingi kufikiri kwamba mchungaji mwenye kanisa kubwa kuliko wote ndiye atakayekuwa mkuu huko Mbinguni. Haitakuwa hivyo. Mchungaji atakayekuwa mkuu Mbinguni ni yule myenyekevu zaidi, kama mtoto.

    Wakati huo huo wanafunzi wakamjia Yesu na kumwuliza, NI NANI ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MUNGU? Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao, na kusema, Hakika nawaambia, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, hamtaingia katika ufalme wa mbinguni. Basi, yeyote atakayejinyenyekeza kama mtoto huyu mdogo, NDIYE ALIYE MKUU KATIKA UFALME WA MBINGUNI.

    Mathayo 18:1-4, TLR

    Yesu aliweka wazi kabisa nani atakayekuwa mkuu katika ufalme. Hakuna mtu awezaye kutambua unyenyekevu wako kwa ukubwa wa kanisa unalochunga. Ukweli halisi ni kwamba, wachungaji wenye makanisa madogo wanaweza kuwa wanyenyekevu zaidi (na kuwa wakuu Mbinguni) kuliko wachungaji wenye makanisa makubwa.

    Tunachohitaji ni sharika zaidi, makanisa zaidi na matunda zaidi kwa ajili ya Bwana wetu. Hebu tupande makanisa! Lengo la kila mtumishi wa kweli wa Mungu lazima liwe kanisa kwenye kila mlango na katika kila lugha. Mkusanyiko chini ya kila nguzo ya umeme au chini ya kila mti utafanya ufalme kusonga mbele.

    Hebu tuache kujaribu kuwafurahisha watu, au kujipendekeza kwa watu. Hebu tuache kuthamini huduma zetu kwa ukubwa wa makanisa tuliyo nayo. Hebu tuwe na mikusanyiko. Wapendwa viongozi wa kanisa: Tusitafute heshima ya wanadamu bali kuheshimiwa (au kukubalika na kuungwa mkono) na Mungu.

    Ninyi mtaaminije, wenye kupeana heshima (kukubalika na kuungwa mkono) wenyewe kwa wenyewe, wala hamtafuti heshima (kukubalika na kuungwa mkono) itokayo kwa Mungu peke yake?

    Yohana 5:44, TLR

    Je, Uinjilisti Ndiyo Kutimiza Agizo Kuu?

    Uinjilisti na mikutano ni vitu vizuri, kwa sababu ni vyanzo vya mafundisho hayo. Ni lazima wainjilisti watoke na kwenda. Lakini je, kweli wanatimiza Agizo Kuu? Ndiyo na Hapana! NDIYO kwa sababu wameanzisha mchakato. HAPANA kwa sababu, bila mafundisho, ambayo yanatokana na makanisa kuanza, Agizo Kuu halitatimizwa.

    Kwa lugha rahisi ni hivi: AGIZO KUU NI UINJILISTI UKIFUATWA NA KUPANDWA MAKANISA. Makanisa hayo ni mikusanyiko, na mikusanyiko hii inafundishwa Neno la Mungu.

    Panda Makanisa Katika Maeneo Mapya Kabisa

    Zaidi ya yote, makanisa lazima yapandwe mahali ambapo Bwana atatuongoza. Makanisa ni lazima yapandwe mijini na vijijini.

    Mimi naona hitaji kwa makanisa kupandwa katika maeneo mapya kabisa. Wengi wetu huelekeza nguvu zetu katika maeneo ambapo mambo yamekwisha anza kutokea. Lakini nikwambie? Kuna maeneo mengi ambayo hayajaguswa na chochote, ambako Mungu ametuita huko pia. Shauku na kujitolea kuvuna roho na kupanda kanisa lazima irudi kanisani, nasi ni lazima tuwatoe vijana wetu kwa ajili ya hilo.

    Wachungaji lazima wajali kwamba Uislamu unateka maeneo makubwa sana ya Afrika na duniani, huku kanisa likitazama tu bila ya kujali. Waislamu wanajitolea, na hawajali kuingia miji iliyoko ndani sana na hata vijiji vya ndani sana katika nchi nyingi.

    Wakati huo, Wakristo, ambao wameagizwa kwenda mpaka mwisho wa nchi, wameketi katika miji ya karibu, yenye starehe za kila aina! 

    Basi mtapokea nguvu, baada ya Roho Mtakatifu kuja juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Uyahudi wote, Na Samaria, MPAKA MIJI ILIYO KARIBU, YENYE STAREHE NA MAFANIKIO SANA, KATIKA DUNIA! (Hiyo ni Biblia gani?!)

    Tena mwanangu, kwa kurasa hizi chache, pata maonyo na ushauri, kwa sababu hakuna kikomo cha kutunga vitabu vingi.

    Sura Ya 2

    Akili Za Wapanda Makanisa

    Iweni na nia hiyo hiyo ndani yenu …

    Wafilipi 2:5

    Kristo alikuwa na jinsi alivyofikiri, iliyomfanya atende aliyotenda. Mstari huu unatufundisha kufikiri kama Kristo alivyofikiri. Ndiyo maana ya Iweni na nia hiyo hiyo ndani yenu.

    Akili yako inapofanya kazi kwa namna Fulani, ndipo utakapoweza ufanikisha mapenzi ya Mungu.

    Naandika jinsi akili yako inavyotakiwa kufanya kazi kama unataka kuwa mpanda makanisa. Bila msingi huu, hakuna atakayepiga hatua kuingia katika kazi hiyo ngumu sana ya kupanda makanisa.

    Sura zinazofuata zinakuelimisha tu juu ya umuhimu wa itikadi ya kupanda makanisa. Utahamasishwa na huduma yako itatiwa nguvu ili kuingia katika vuguvugu hili kuu la mwisho la kitume, la upandaji wa makanisa.

    1. Elewa kwamba Mungu anatazama matendo yako.

    Wapendwa: Matendo yako hapa duniani yanatazamwa na Mungu. Mungu atakudai jibu kwa ajili ya kile alichoweka ndani yako. Atakuuliza ulifanya nini na vipawa Vyake. Mungu atakudai vitu alivyokupa. Ataulizia kuhusu matendo au kazi zako!

    Inapendeza kwamba katika zile barua saba zilizoandikwa kwa yale makanisa saba, maneno Fulani yanarudiwa tena na tena – Nayajua maendo yako. Ni matendo gani hayo? Vyovyote vile, ni muhimu kwa kila kanisa kuwa na matendo hayo yamekamilika katika nafasi yake. Hebu tazama mistari ifuatayo:

    NAYAJUA MATENDO YAKO, na taabu yako, na subira yako, na jinsi usivoweza kuchukuliana na walio waovu, na kwamba umewajaribu wale wajiitao mitume, na siyo, ukagundua ni waongo

    Ufunuo 2:2, TLR

    NAYAJUA MATENDO YAKO, na dhiki yako, na umaskini wako (japo wewe ni tajiri), na ninajua makufuru yao wasemao ni Wayahudi, na siyo, bali ni sinagogi la Shetani.

    Ufunuo 2:9, TLR

    NAYAJUA MATENDO YAKO, na mahali ukaapo, kilipo kiti cha enzi cha Shetani. Wewe unalishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika zile siku za Antipa, shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa miongoni mwenu, mahali Shetani akaapo.

    Ufunuo 2:13, TLR

    NAYAJUA MATENDO YAKO, na upendo wako, na huduma, na imani, na uvumilivu wako, na kazi zako, na kwamba, za mwisho zimekuwa nyingi kuliko zile za kwanza.

    Ufunuo 2:19, TLR

    Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi, andika hivi: Haya mambo anayasema Yeye aliye na zile Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. NAYAJUA MATENDO YAKO, ya kuwa unalo jina kwamba uko hai, lakini umekufa.

    Ufunuo 3:1, TLR

    NAYAJUA MATENDO YAKO. Tazama, nimekuwekea mbele yako mlango ulio wazi, wala hakuna mwanadamu anayeweza kuufunga. Kwa sababu, unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza Neno langu, wala hukulikana jina langu.

    Ufunuo 3:8, TLR

    Mungu hakusema, ‘Nazijua nyumba zako na magari yako. Hakusema, ‘Naijua Benzi uliyo nayo. Alisema, Nayajua matendo yako! Hakusema, Nazijua shahada zako. Hakusema, Namjua baba na mama yako. Alisema, Nayajua matendo yako!"

    2. Kupanda Kanisa ndiyo siri ya kwenda na Mungu mpaka mwisho.

    Kwa kuwa kila atakayeokoa maisha yake atayapoteza; bali yeyote atakayekubali kupoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, atayaokoa.

    Marko 8:35, TLR

    Mwaka wa 1985 nilifanya uamuzi wa kwenda na kusimama na Mungu mpaka mwisho. Nilikuwa nimemaliza mtihani mgumu sana wa shule ya Utabibu. Kwa mtazamo na maoni yangu, mimi nilikuwa nimeponea chupuchupu katika huo mtihani. Nilipowaza kuhusu juhudi yote niliyotia kwenye mtihani huo, na kazi ya ziada niliyofanya, nilijisikia moyoni mwangu kwamba haikuwa stahili kabisa. Kwa nini niteseke hivyo kwa ajili ya matibabu tu? Kwa nini nitoe maisha yangu kwa ajili hiyo? Nikaapa kwamba tangu hapo na kuendelea, kipaumbele katika maisha yangu kitakuwa kazi ya Mungu. Kabla ya hapo nilikuwa nadhania kwamba Mungu ndiye wa kwanza katika maisha yangu. Nilikuwa kiongozi wa Kikristo mwenye kumaanisha sana, lakini sikutambua kwamba kazi ya Mungu haikuwa kipaumbele namba moja maishani mwangu. Tangu wakati ule niliazimia kwamba nitakuwa na kusudi moja tu, nalo ni kuifanya kazi ya Mungu! Maswala mengine yote yakawa vitu vya pembeni. Hapo, maisha yangu yakabadilika kweli kweli.

    Kuanzia hapo, kipaumbele namba moja kwangu akawa Mungu na huduma. Shule ya Utabibu ikapata nafasi yake stahili, namba mbili au tatu katika moyo wangu. Pengine naweza kusema kwamba wakati huo ndiyo niliingia katika huduma moja kwa moja.

    Cha ajabu ni kwamba, baada ya kufanya uamuzi

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1