Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hatua Za Kufikia Upako
Hatua Za Kufikia Upako
Hatua Za Kufikia Upako
Ebook181 pages4 hours

Hatua Za Kufikia Upako

Rating: 4.5 out of 5 stars

4.5/5

()

Read preview

About this ebook

Unatamani kuwa mpakwa mafuta? Katika kitabu hiki cha kihistoria, Dkt Dag Heward-Mills anagawa hatua kadhaa za hadi kupokea upako. Kitabu hiki kwa hakika kitakuwa cha baraka kwako na utumishi wako. Gundua hatua unazohitaji kuchukua ili uwe mpakwa mafuta.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613953709
Hatua Za Kufikia Upako
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Hatua Za Kufikia Upako

Related ebooks

Reviews for Hatua Za Kufikia Upako

Rating: 4.666666666666667 out of 5 stars
4.5/5

6 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hatua Za Kufikia Upako - Dag Heward-Mills

    Kimetafsiriwa na Rev. Jackson Daniel Kusenha

    Maandiko yote yamechukuliwa kutoka katika Biblia ya Union Version inayotolewa na vyama vya Biblia vya Tanzania na Kenya

    Copyright © 2008

    1ST Printing 2008 

    Barua pepe Dag Heward-Mills:

    bishop@daghewardmills.org

    Tafuta zaidi kuhusu Dag Heward-Mills katika:

    www.daghewardmills.org

    Andika kwa:

    Dag Heward-Mills

    P.O.Box 114

    Korle-Bu

    Accra

    Ghana 

    ISBN: 978-1-61395-370-9

     Haki zote zimehifadhiwa katika sheria ya kimataifa. Ukitaka kutumia au kuchapa sehemu yoyote ya kitabu hiki unahitaji ruhusa ya maandishi kutoka kwa mtoaji, isipokuwa kwa kuchukua kwa ufupi sehemu ya maandiko hayo kwa ajili ya mafundisho.

    Yaliyomo

    Sura ya 1: Sababu Saba Kwa Nini Ni Lazima Upakwe Mafuta

    Sura ya 2: Matokeo Kumi na Tano Yanayotokana na Upako katika Huduma Yako

    Sura ya 3: Hatua Moja ya Kuelekea Kwenye Upako

    Sura ya 4: Hatua Saba za Upako wa Yordani

    Sura ya 5: Hatua Saba za Upako Jangwani

    Sura ya 6: Hatua za Upako Katika Nyumba ya Kornelio Vi

    Sura ya 7: Jinsi ya Kushikilia Upako Mpaka Unapoanza Kutumika

    Sura ya 8: Hatua za Upako Katika Chumba cha Juu

    Sura ya 9: Hatua Saba za Upako kwako Mwenyewe Unapokuwa Pamoja na Wengine

    Sura ya 10: Hatua za Upako Katika Mlima Mtakatifu

    Sura ya 11: Hatua Saba za Upako Unaoweza Kuuhisi

    Sura ya 12: Upako wa Manabii na Wenye Haki

    Sura ya 13: Masharti kwa Waliopakwa Mafuta

    Sura ya 14: Upako wa Kifalme

    Sura ya 15: Upako wa Nabii Isaya

    Sura ya 16: Nini Maana ya Kuwa Mpakwa Mafuta wa Bwana

    Sura ya 17: Hatua za Kuelekea Kupoteza Upako

    Sura ya 18: Njia ya Kuufikia Upako

    Sura ya 19: Mapambano Kwa Ajili ya Upako Maradufu

    Sura ya 20: Maisha ya Mpakwa Mafuta

    Sura ya 21: Nitajuaje Nitakapokuwa Nimepekwa Mafuta?

    Sura ya 22: Timiliza Huduma Yako

    72 544x376

    Sura ya 1

    Sababu Saba Kwa Nini Ni Lazima Upakwe Mafuta

    1. Ni lazima upakwe mafuta kwa sababu hakuna anayeweza kutimiza huduma yake kwa nguvu zake za asili au kwa nguvu za kibinadamu isipokuwa ni kwa Roho Mtakatifu tu.

    Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la Bwana kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema Bwana wa majeshi.

    Zekaria 4:6

    Huduma ya kweli itakuwa na mafanikio kwa kupitia nguvu za Roho Mtakatifu peke yake. Huduma isiyo sahihi ni ile inayofanya kazi kwa kutegemea mafundisho ya mwalimu wa chuo, Mhadhili wa chuo kikuu au ushawishi wa mhubiri. Lakini amua kuwa mtu aliyepakwa mafuta na kuingia katika huduma.

    2. Ni lazima upakwe mafuta kwa sababu hata Yesu Kristo alisubiri apakwe mafuta kabla ya kuanza huduma yake.

    Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;

    Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.

    Na Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa amepata umri wake kama miaka thelathini, akidhaniwa kuwa ni mwana wa Yusufu …

                                                                                  Luka 3:21-23

    Tukio hili linaonesha mwanzo wa huduma ya Kristo. Hatusikii jambo lolote kuhusu Yesu mpaka alipokuwa amefikia umri wa miaka thelathini. Tangu wakati huu baada ya Roho Mtakatifu (Upako) kutumwa juu yake, Yesu alianza kuhubiri, kufundisha na kuponya watu.

    3. Ni lazima upakwe mafuta kwa sababu hata mitume waliambiwa wasubiri Roho Mtakatifu (Upako) kabla ya kuanza huduma yao.

    Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mliisikia habari yake kwangu. 

    Matendo ya Mitume 1:4

    Je unadhani utakuwa na huduma ya namna gani bila Roho Mtakatifu? Hata mitume wakuu waliotembea na Kristo walihitaji kupokea upako ili kwamba wautumie katika huduma.

    4. Ni lazima upakwe mafuta kwa sababu manabii wakuu kama Elisha alipopata fursa ya kuomba jambo analotaka, aliomba upako.

    Elisha aligundua kuwa huduma ilikamilishwa kupitia kupakwa mafuta peke yake. Eliya alipomwuliza ni kitu gani alichotaka, alisema alitamani upako mara dufu kutoka kwake.

    Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, omba kwangu lolote nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu mara dufu ya roho yako na iwe juu yangu.

    Wafalme 2:9

    Elisha angeweza kuomba mambo mengine mengi kutoka kwa Eliya. Angeweza kuomba jina zuri la Eliya, fedha zake, rasilimali zake, gari lake au hata mke wake. Lakini kwa miaka ile aliyotembea na Eliya, Elisha alifahamu siri ya huduma ilikuwa imeegemea wapi.

    Elisha alifahamu kuwa mambo hayo yote yalitokana na upako, ndiyo maana aliomba upako mara dufu kwa ajili ya huduma. Kwa nini wewe unatafuta mambo mengine wakati manabii wakuu kama hao wanatafuta upako?

    5. Ni lazima upakwe mafuta kwa sababu Mfalme Sauli hakuweza kubadilika kuwa mtu tofauti mpaka alipopakwa mafuta.

    Sauli alibadilishwa kutoka mtu wa kawaida kuwa mfalme baada ya kupakwa mafuta. Kwa jinsi iyo hiyo, hata wewe utafanyika kuwa mtu mwenye mamlaka (mfalme) katika ufalme wa Mungu mara baada ya kupakwa mafuta.

    Unaweza kutumia njia nyingine za kuwakandamiza na kuwaamuru watu wafanye unayotaka, lakini huwezi kuwa mtu mwenye mamlaka bila ya kupakwa mafuta. Upako wa Roho Mtakatifu utakubadilisha uwe mtu mwingine.

    Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta uwe mkuu juu ya urithi wake.

    1 Samweli 10:1

    Na roho ya BWANA itakujilia kwa nguvu, nawe utatatabiri pamoja nao, nawe UTAGEUZWA KUWA MTU MWINGINE.

    1 Samweli 10:6

    6. Ni lazima upakwe mafuta kwa sababu Mfalme Daudi, Mtunga Zaburi aliyepakwa mafuta na mwandishi wa maandiko, alidhani kuwa baraka zake zote zilitokana na upako mtakatifu.

    Daudi anaona kuwa karibu kila kipengele cha maisha yake kilitokana na upako. Watu wakuu wa kiroho wanatambua matokeo ya nguvu ya upako katika maeneo mbalimbali ya maisha yao.

    Katika Zaburi ya themanini na tisa, tunamwona Mfalme Daudi akiimba moja ya Zaburi nzuri kuliko zote. Katika Zaburi hii, anaelezea matokeo ya nguvu ya upako katika maisha yake.

    Ikiwa Mtunga Zaburi alipata mambo haya yote kutokana na upako, ni kwa jinsi gani wewe unategemea mambo hayo hayo yaje kwako bila upako? Je, unaweza kumshutumu Mfalme Daudi alipomlilia Bwana, Usiniondolee Roho wako Mtakatifu?                                                                                                                                                                                                                                                           Zaburi 51:11

    Roho Mtakatifu (upako) alikuwa ni wa thamani sana kwake.

    7. Upako ni wa lazima kwa sababu Musa alikataa kuendelea na huduma bila upako.

    Ikiwa Musa hakuchukua hata hatua moja ya huduma bila kuwa na upako, inakuwaje wewe una ujasiri wa kuendelea katika huduma bila ya kuwa na upako huo?

    Katika kitabu cha Kutoka, tunaona jinsi Musa alivyokataa kuendelea na huduma kama Mungu angemwondolea Nguvu Zake pamoja na upako. Wakati Musa aliporejea katika uwepo wa Bwana, alirejea akiwa na upako na nguvu za Mungu juu yake.

    Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa. Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepeta neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi?

    BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako.

    Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.

    Kutoka 33:15-19

    72 544x376

    Sura ya 2

    Matokeo Kumi na Tano Yenye Nguvu Yanayotokana na Upako Katika Huduma Yako

    Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.

    Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

    Zaburi 89:19-21

    Katika Zaburi moja nzuri sana ya Agano la Kale, Mfalme Daudi aliimba kuhusu baraka alizopokea kwa sababu tu alikuwa amepakwa mafuta.

    Kutokana na uzoefu wangu, nimegundua ni watu wachache sana wanaoweza kuhusisha baraka zao na chanzo halisi cha baraka hizo. Hawajui ni wapi na jinsi gani walivyofika hapo walipo na kuwa na vitu hivyo vyote. Mara zote huo huwa ndio msingi wa uasi na kukosa shukurani. Nadhani ni sifa muhimu mtu kuweza kufikiri kwa kina na kutambua chanzo cha baraka zote.

    Ni jambo la ajabu kusoma jinsi Daudi alivyodhani kuwa kila aina ya manufaa aliyoyapata yaliyotokana na upako. Kwa hiyo aliutunza upako kwa makini na mara zote upako huo ulimrejesha kujiona kama aliyepakwa mafuta na Bwana.

    Ikiwezekana Mungu afungue macho yako ili uone thamani ya upako wake katika maisha yako pamoja na huduma!

    Naamini kwamba kama watumishi wengi zaidi wangeona jinsi upako unavyofanya, wangeutamani na kuutafuta juu ya kila kitu. Kama upako ulikuwa na baadhi ya matokeo katika maisha ya Daudi, lazima utegeemee kuwa upako huo uwe na matokeo katika maisha yako na katika huduma pia!

    1. Upako utaleta majibu katika kupokea msaada wa ki-Mungu katika maisha yako na huduma.

     Daudi alihisi kwamba huduma yake kama mfalme ilisaidiwa kwa sababu ya upako. Alisema,  … Nimempa aliye hodari msaada…

    Zaburi 89:19b

    2. Upako utasababisha uinuliwe juu zaidi katika huduma.

    Daudi aliona kuinuliwa kwake kama jibu la kupakwa kwake mafuta.

    Nimekutuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.                                                                                                                                                                               Zaburi 89:19c

    3. Upako utakuimarisha katika huduma.

    Unaweza kuona tofauti ya wazi kati ya huduma inayoimarishwa na Mungu na ile ambayo haiimarishwi na Mungu. Mfalme Daudi aliimarishwa kwa ajili ya upako.

    Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. AMbaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

    Zaburi 89:20-21

    4. Upako utadhihirisha nguvu katika huduma yako.

    Mara nyingi watumishi ni wadhaifu katika kuhubiri na katika huduma. Nguvu ya kutoa ujumbe na nguvu ya kubadilisha maisha ya watu kwa ujumla haimo ndani yao. Upako utaondoa kila aina ya udhaifu katika maisha yako na huduma. Mfalme Daudi alihisi alikuwa na nguvu zaidi kwa sababu ya upako.

    Daudi alisema, … Mkono wangu utamtia nguvu. 

    Zaburi 89:21

    5. Upako utakulinda na udanganyifu.

    Udanganyifu ni uovu ambao huwafunga watumishi wengi. Udanganyifu huanzishwa na upofu wa kiroho na unafiki katika huduma. Watumishi

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1