Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mpakwa Mafuta na Upako Wake
Mpakwa Mafuta na Upako Wake
Mpakwa Mafuta na Upako Wake
Ebook123 pages5 hours

Mpakwa Mafuta na Upako Wake

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345507
Mpakwa Mafuta na Upako Wake
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Mpakwa Mafuta na Upako Wake

Related ebooks

Reviews for Mpakwa Mafuta na Upako Wake

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mpakwa Mafuta na Upako Wake - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Upako Ni Nini Hasa?

    Habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huku na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.

    Matendo 10:38

    Upako ni Roho Mtakatifu. Kila fundisho unalolisikia kuhusu Roho Mtakatifu ni fundisho kuhusu upako.

    Neno upako ni kitenzi na nomino. Upako unaweza kumaanisha kitu ambacho kimetumiwa kumtia mtu mafuta; kwa mfano mafuta ya kumtia mtu.

    Upako pia unaweza kumaanisha tendo la kummiminia mtu mafuta.

    Ninapozungumzia kuhusu upako, nazungumzia kuhusu mtu Roho Mtakatifu ambaye unapewa wewe kutenda kazi ya Mungu. Ni muhimu kwenda zaidi ya mpakwa mafuta ili kuona huo upako. Mpakwa mafuta amefunikwa na huo upako wa Roho Mtakatifu.

    Yesu Kristo wa Nazareti alizunguka akitenda mema kwa sababu alikuwa amepakwa mafuta na Roho Mtakatifu na nguvu. Yesu angeweza kupakwa mafuta na mafuta ya mzeituni, mafuta ya gari, mafuta ya nazi au na Vaseline. Iwapo angepakwa mafuta na yoyote kati ya mafuta hayo tungesema kwa uhakika kwamba kitu cha upako ni mafuta ya mzeituni, mafuta ya gari, mafuta ya nazi au Vaseline. Lakini Yesu Kristo alipakwa mafuta na Roho Mtakatifu na nguvu. Kwa hiyo tunaweza kusema kwamba kitu cha upako ambacho Yesu alipakwa mafuta nacho ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu wa ajabu huja kukaa ndani ya mtu ambaye amepakwa mafuta na Mungu.

    Mtu anapopakwa mafuta, Mungu Mwenyezi huenda kukaa juu ya mtu huyo, ndani ya mtu huyo au kuwa pamoja na mtu huyo kwa njia maalum. Hili ndilo linalomfanya mtu awe amepakwa mafuta na mwenye nguvu. Unapojihusisha na mtu aliyepakwa mafuta kwa kweli unajihusisha na Mungu. Unapojihusisha na mtu aliyepakwa mafuta unajihusisha na Roho Mtakatifu.

    Hiyo ndiyo sababu kuna matokeo mabaya sana kwa watu wanaoshughulikia vibaya mpakwa mafuta na upako wake. Kwa kweli hawamtendei vibaya mwanadamu bali wanamtendea vibaya Mungu. Wakati Anania na Safira walipomdanganya Petro, ambaye alikuwa amepakwa mafuta kuwa mtume, walikufa mara moja. Haya yalikuwa matokeo mabaya sana ambayo yaliwaogopesha washirika wengine wa kanisa. Lakini Petro alielezea kosa ambalo Anania na Safira walifanya. Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako KUMWAMBIA UONGO ROHO MTAKATIFU, na kuhifadhi kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. (Matendo 5:3-5).

    Unaona kwamba kwa kweli Anania na Safira walimwambia uongo Roho Mtakatifu. Hawakuwa wakimwambia uongo Petro bali Roho Mtakatifu na hilo huleta matokeo mabaya na yanayoonekana kuwa makali sana. Kuwa muangalifu unapojihusisha na watu waliopakwa mafuta. Huenda ukafupisha maisha yako na huduma kwa sababu ya kukadiria visivyo na kuchukulia vibaya ukuu wa upako wanaobeba.

    Unaweza kujiuliza, Kwa nini leo hii watu wengi huwambia uongo wachungaji na hawaonekani wakifa mara moja? Je, ni kusema kwamba wachungaji hawa hawana upako? Jibu ni rahisi. Kuna aina tofauti ya udhihirisho wa Roho nyakati tofauti. Hata katika huduma ya Petro, hakuna mwingine yeyote aliyekufa kwa sababu ya kusema uongo. Huwezi kujua kamwe wakati ambapo nguvu za Mungu zitadhihirika kwa njia fulani. Nina hakika kuna watu wengine wengi waliokufa kwa sababu ya kumwambia uongo Roho Mtakatifu. Huenda ikawa si kifo cha ghafla lakini bado kifo ni kifo.

    Sura ya 2

    Upako Uko Wapi Hasa?

    Hazina ya upako inapatikana ikihusishwa na mpakwa mafuta. Upako hauwezi kutenganishwa na mtu mwenyewe. Mtu wa Mungu anao upako ndani yake, pamoja nae, na juu yake.

    Leo hii, mimi na wewe tunatafuta kile kinacholeta uponyaji, upenyo, ukombozi na maendeleo katika maisha haya. Huo ni upako! Upako ndio unaovunja nira.

    Kwa hiyo upako uko wapi hasa? Je, tunaweza kuupata upako katika Maduka ya West Hills? Je, tunaweza kuupata upako katika Maduka ya West Gate? Je, tunaweza kuupata upako katika ofisi? Je, tunaweza kuupata upako katika uwanja wa ndege? Je, upako unaweza kupatikana dukani? La, upako haupo katika sehemu yoyote kati ya hizi.

    Upako unapatikana NDANI ya mpakwa mafuta!

    Upako unapatikana NA mpakwa mafuta!

    Upako unapatikana JUU ya mpakwa mafuta!

    Upako hauwezi kutenganishwa na mtu ambaye Mungu amempaka mafuta.

    Ni Kipi Chenye Nguvu; Upako au Mpakwa Mafuta?

    Kwa vile upako ndio unaovunja nira hasa, ni muhimu kutafuta ulipo upako. Miaka kadhaa iliyopita, watu waligundua kwamba machungwa yanaweza kuponya magonjwa. Baada ya muda, sayansi ilienda mbele zaidi na kugundua elementi ndani ya machungwa ambayo hasa huleta huo uponyaji. Waligundua vitamini C! Leo hii, watu wengi huzingatia tu kula tembe zenye Vitamini C. Wana ufunuo wa siri ambayo huleta huo uponyaji.

    Vivyo hivyo, kuna elementi ndani ya watu waliopakwa mafuta ambayo hufanya maajabu na elementi hiyo ni upako. Kwa bahati mbaya, hakuna utaratibu wa kikemikali wa kutenganisha upako kutoka kwa mtu aliyepakwa mafuta kama vile Vitamini C ilivyotengwa kutoka kwa machungwa. Itakubidi ujihusishe na mtu aliyepakwa mafuta ikiwa unataka kuufikia huo upako. Hakuna maabara au kiwanda ambacho kinazalisha upako halisi katika chupa ambazo unaweza kuwa nazo bila kumuona kamwe huyo mtu aliyepakwa mafuta.

    Mungu amechagua mtu mweusi, mtu mweupe, mtu mwenye elimu au hata mpumbavu ampatie upako wake juu yake. Itakubidi uende kwa mtu huyo kwa sababu ana huo upako na anaubeba. Ni ukosefu huu wa kutofautisha baina ya mpakwa mafuta na huo upako ambavyo vinawamaliza Wakristo wenye kiburi. Nataka Mungu anitumie lakini sitaki kujihusisha na mpakwa mafuta wake ili niweze kupata upako huo.

    Upako Sehemu Tatu

    1. Upako uko na mtu aliyepakwa mafuta.

    Ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, MAANA ANAKAA KWENU, naye atakuwa ndani yenu.

    Yohana 14:17

    2. Mpakwa mafuta anabeba Roho juu yake.

    Roho wa Bwana YU JUU YANGU, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,

    Luka 4:18

    3. Mpakwa mafuta anabeba Roho ndani yake.

    Nanyi, MAFUTA yale mliyoyapata kwake YANAKAA NDANI YENU, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.

    1 Yohana 2:27

    Upako wa Roho Mtakatifu ama uko ndani ya mtu, pamoja na mtu au juu ya mtu. Hapo ndipo mahali halisi pa upako. Hii ndiyo sababu mtu aliyepakwa mafuta huwa muhimu kwako. Yeye ni mbebaji wa kitu unachohitaji. Yeye mwenyewe ni mudhaifu, hana nguvu, hana maana na ni binadamu. Lakini ameteuliwa kubeba sehemu ya Roho pamoja na yeye, ndani yake au juu yake. Upako umeshikanishwa sana na huyo mtu na ni sehemu ya huyo mtu sana kiasi cha kwamba mara nyingi tunadanganyika na kufikiria kwamba huyo mtu mwenyewe ana aina fulani ya nguvu.

    Uwezo wako wa kujihusisha na mpakwa mafuta na kuingiliana na mtu aliyepakwa mafuta utaamua kuufikia kwako huo upako. Kumbuka kwamba ni upako ambao unahitaji. Hebu chukulia kwamba unatamani juisi kidogo ya machungwa katika jagi. Ni juisi ya machungwa ambayo unahitaji lakini unapaswa kuishughulikia hiyo jagi kwa uangalifu kwa sababu jagi ndiyo iliyo na hiyo juisi ya machungwa.

    Watu wengi hufanya makosa ya kiroho inapofikia mambo ya mpakwa mafuta na upako wake. Wanataka huo upako lakini hawataki kufanya lolote linalohusiana na huyo mpakwa mafuta. Hawajui kwamba mtazamo wao kwa huyo binadamu aliyepakwa mafuta unawatenganisha na huo upako na kuwaelekeza kwa anguko lao. Mungu mara nyingi hupaka mafuta watu wa ajabu na uwezo wako wa kuingiliana na watu wa ajabu, wasiokuwa wa kawaida au hata watu wasiokuwa na maana huenda ndio tu wanaoweza kukuunganisha wewe na huo

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1