Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi
Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi
Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi
Ebook450 pages16 hours

Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345354
Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi

Related ebooks

Reviews for Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Jemedari Mwema Sayansi ya Uongozi - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Jemedari Mwema Hujifunza Kuhusu Vita

    ... kwa haki ahukumu na kufanya vita.

    Ufunuo 19:11

    Vita vinahusu mauaji ya wengi, majonzi, huzuni na kifo. Vita ni mojawapo ya vitu vibaya zaidi vinavyoweza kutokea katika maisha ya wanadamu. Kwa hivyo ni nadra kusikia Mungu akihusishwa na vita. Itawezekanaje Mungu kuhusishwa na vita? Itawezekanaje Mungu atake watu wafe? Je, Mungu anataka kuua watu? Je, Mungu anataka kuwadhuru watu? La hasha!

    Mungu hana mipango miovu kama hiyo. Kuinuka kwa adui anayehitaji kuangamizwa ndiko husababisha vita. Mungu hupigana vita kwa njia ya haki na huangamiza maadui wake. Sisi kama Wakristo, tuna adui ambaye anahitaji kuangamizwa na kushindwa. Sisi kama wahubiri wa injili tuna maadui wengi zaidi na tunahitaji kufahamu jinsi ya kuwashinda, kuwaangamiza na kuwamaliza kabisa. Maandiko yanasema, Kwa haki ahukumu na kufanya vita. Kuna njia ya kupigana vita inayomcha Mungu. Kuna njia ya hekima ya kupigana vita. Mungu anataka upigane vita kwa njia yake na kwa hekima yake.

    Kitabu hiki kinazungumzia jinsi ya kupigana vita kwa njia inayomcha Mungu, kwa njia ya kiroho na kwa njia ya hekima. Yeyote anayefikiri kwamba hatuko vitani hana ufahamu. Shetani angependa uwe na wazo la kwamba tunaishi katika amani chini ya Mfalme wa Amani. Shetani angependa ufikirie kwamba hakuna shida yoyote. Lakini Neno la Mungu linasema wazi kabisa kwamba tuko katika vita. Neno la Mungu linasema wazi kabisa kwamba tunapaswa kupigana vita vizuri na tupigane vita vilivyo vizuri!

    Sababu Kumi za Kujifunza Vita

    1. Yesu Kristo anaongoza majeshi ya Mbinguni na anapigana vita kwa njia ya haki.

    Watu wengi hawafani katika huduma kwa sababu hawataki kupigana vita. Ikiwa unataka kumfuata Yesu, ni sharti ujiunge na jeshi lake na ni lazima upigane.

    Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, NAYE KWA HAKI AHUKUMU NA KUFANYA VITA.

    Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.

    Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.

    Na MAJESHI YALIYO MBINGUNI wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi.

    Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.

    Ufunuo 19:11-15

    2. Yesu Kristo ni Mwana-Kondoo anayepigana vita.

    Mwana-Kondoo alipigana dhidi ya wale wafalme kumi walioungana pamoja dhidi yake na akawashinda. Yesu Kristo ni Mwana-Kondoo anayepigana vita. Je, unataka kuwa kama Yesu? Ikiwa unataka kuwa kama Yesu, ni sharti ujifunze jinsi ya kupigana vita!

    Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.

    Hawa WATAFANYA VITA NA MWANA-KONDOO, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.

    ufunuo 17:12-14

    3. Mungu hufundisha mikono yetu kupigana vita.

    Mungu anataka kukufundisha jinsi ya kupigana vita. Ukiamini, utawezeshwa na kuongozwa kwa njia ya kiungu katika jinsi ya kupigana vita.

    ANANIFUNDISHA MIKONO YANGU VITA, Mikono yangu ikaupinda upinde wa shaba.

    Zaburi 139:23-24.

    4. Tumeagizwa tupigane vita vilivyo vizuri.

    Kuna andiko lililo wazi katika Biblia linalosema kwamba ni sharti upigane. Mungu anakuhimiza upigane! Vita vilivyo vizuri ni vita vilivyo vizuri kwa sababu unashinda. Vita vilivyo vizuri ni vita vilivyo na kusudi nzuri.

    PIGA VITA VILE VIZURI vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.

    1 Timotheo 6:12

    5. Tumeagizwa tupigane vita vizuri.

    Tumeambiwa tuwe na ujuzi wa kupigana vita. Hilo ni agizo kwa kila mhubiri wa injili. Timotheo alikuwa mmojawapo wa wachungaji wa kwanza kabisa katika historia ya kanisa. Na aliambiwa awe hodari katika kupigana vita.

    Mwanangu Timotheo, nakukabidhi agizo hilo liwe akiba, kwa ajili ya maneno ya unabii yaliyotangulia juu yako, ili katika hayo UVIPIGE VILE VITA VIZURI;

    1 Timotheo 1:18

    6. Huduma ya Bwana Yesu inaelezwa kama vita.

    Mtume Paulo alichukulia huduma yake kuwa kama vita na aliuliza swali muhimu. Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe?

    Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?

    1 Wakorintho 9:7

    7. Paulo alisema kwamba maisha yake na huduma yake ni kama vita.

    Paulo daima alikuwa anapigana. Ikiwa uko katika huduma, unapigana! Ikiwa unamfanyia Mungu kazi, wewe ni mpiganaji! Upende usipende, unapigania maisha yako. Daima nimekuwa nikihisi kwamba napigania maisha yangu.

    Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; NAPIGANA ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;

    1 Wakorintho 9:26

    Nimevipiga VITA VILIVYO VIZURI, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda:

    2 Timotheo 4:7

    8. Tumeamriwa tuwe na silaha za vita.

    Paulo, mtumishi wa Mungu, alikuwa na silaha za kupigana vita vyake vilivyo vizuri. Ikiwa Paulo alihitaji silaha, wewe pia utazihitaji.

    Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.

    2 Wakorintho 10:3-4

    9. Tumeagizwa tuwe hodari na tujihami kwa silaha.

    Kuna haja gani ya kujihami ikiwa hatutapigana vita? Tuko katika vita dhidi ya falme na mamlaka ya pepo wabaya katika ulimwengu wa kiroho. Simama imara na ujitayarishe kwa vita vilivyo vizuri, vya muda mrefu na vilivyo vigumu!

    Hatimaye, mzidi kuwa HODARI katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni SILAHA ZOTE ZA MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

    KUSHINDANA kwetu sisi si juu ya damu na nyama bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Waefeso 6:10-12

    10. Kuna vita dhidi ya joka na sisi tunahusika katika vita hivyo.

    Joka huyo hupigana vita dhidi ya watu wanaozifuata amri za Mungu. je, wewe huzifuata amri za Mungu? Ikiwa wewe huzifuata, basi tarajia kwamba kuna joka atakayekukabili na atapigana nawe.

    JOKA akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye VITA JUU ya wazao wake waliosalia, WAZISHIKAO AMRI ZA MUNGU, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

    Ufunuo 12:17

    Sura ya 2

    Jemedari Mwema Atajiepusha na Vita Vya Kipumbavu

    Pigana vita vilivyo vizuri vya imani....

    1 Timotheo 6:12

    Jemedari mwema ni mpiganaji aliyefundishwa kupigana lakini hatapigana vita vya kipumbavu. Biblia inatufundisha kupigana vita vilivyo vizuri. Ni jambo la busara kupigana vita vilivyo vizuri vya imani. Kupigana kunamaanisha kung'ang'ania kitu kwa dhati. Licha ya hiyo, kuna vita vingi vya kipumbavu ambavyo mtu anaweza kupigana. Je, uko katika vita vya kipumbavu au uko katika vita vilivyo vizuri?

    Jemedari Paulus na Vita Vya Kipumbavu

    Mnamo mwaka wa 1942, Adolf Hitler, kiongozi wa Ujerumani, alishambulia Muungano wa Kisovieti kwa mara ya pili na alijaribu kuteka mji muhimu unaoitwa Stalingrad. Adolf Hitler na Stalin (Kiongozi wa Urusi) walikuwa ni makamanda hodari na ilionekana ni kana kwamba walikuwa wametoshana nguvu mjini Stalingrad. Majeshi ya Ujerumani yalikuwa chini ya ukamanda wa Jemedari Paulus.

    Stalin alitoa amri kwa majeshi yake, ambayo ilikuwa ni: Hakuna kurudi nyuma hata hatua moja! Kila mtu alihitajika kupigana hadi kufa. Amri hiyo iliagiza kwamba kamanda yeyote atakayekubali wanajeshi wake warudi nyuma bila ruhusa ya wakubwa wake, atafikishwa katika mahakama ya kijeshi. Amri hiyo pia iliagiza kwamba wanajeshi watakaopatikana na hatia ya kurudi nyuma watalazimishwa kujiunga na vikosi vya adhabu. Hiyo inamaanisha watapelekwa sehemu hatari zaidi katika msitari wa mbele wa vita. Amri hiyo pia iliagiza wanajeshi wa Kirusi wawapige risasi wanajeshi wowote walio katika msitari wa nyuma ambao watajaribu kutoroka kwa ajili ya hofu. Miezi miwili ya kwanza baada ya amri hiyo kutolewa, zaidi ya wanajeshi 1,000 walipigwa risasi na vikosi vya wanajeshi wa kuzuia wenzao wasitoroke. Pia, zaidi ya wanajeshi 130,000 walipelekwa katika vikosi vya adhabu.

    Lakini Hitler pia alikuwa ametoa amri kwamba wanajeshi wake wasirudi nyuma hata iweje. Kwa ajili ya hiyo, mapigano yalitekelezwa katika barabara moja baada ya nyingine na katika jengo moja baada ya jingine mpaka mji wote ukabaki mahame. Wajerumani walitekeleza mashambulizi ya anga mara kwa mara wakitumia zaidi ya ndege 1,000 kwa wakati mmoja. Wanajeshi wa pande zote mbili walijificha ndani ya majengo yaliokuwa yamebomolewa kwa mabomu huku wanajeshi wadunguzi wa Urusi na Ujerumani wakiwapiga risasi wanajeshi adui kutoka kwa maficho yao ndani ya vifusi.

    Mnamo Januari tarehe 24, Jemedari Paulus aliomba ruhusa ya kusalimu amri. Alimtumia Adolf Hitler barua akisema, Wanajeshi hawana risasi wala chakula. Siwezi kuwaamrisha kwa ufanisi tena. 18,000 wamejeruhiwa na hakuna rasilimali zozote, dawa wala bendeji. Hakuna haja ya kuendelea kupigana. Hatuwezi kujizuia kushindwa. Jeshi linaomba ruhusa ya kusalimu amri mara moja ili kuokoa maisha ya wanajeshi waliosalia.

    Hitler alikataa kulipatia jeshi la Ujerumani ruhusa ya kusalimu amri akisema kwamba wapigane mpaka mtu wa mwisho atakapofariki. Kukataa kwa Adolf Hitler kumpa Jemedari Paulus ruhusa ya kusalimu amri kimsingi kulikuwa ni kama kutoa agizo la kupigana vita vya kipumbavu.

    Lakini Jemedari Paulus hakukubaliana na Hitler. Licha ya kwamba Hitler alimpandisha cheo na akawa Jemedari Mkuu, alikataa kuendelea kupigana vita hivyo visivyo na maana. Mnamo Januari tarehe 31 mwaka wa 1943, Jemedari Paulus alisalimu amri licha ya agizo la Hitler kwamba aendelee kupigana vita hivyo vya kipumbavu. Mwanajeshi mmoja wa Urusi alienda katika makao makuu ya jeshi la Ujerumani. Makao makuu hayo yalikuwa katika chumba cha chini ya ardhi cha duka moja lililokuwa limeharibika vibaya. Jemedari Mkuu Paulus na maofisa wake waliokuwa bado wangali hai walitoka nje na wakajisalimisha kwa utulivu. Walipuuza kabisa agizo la Hitler kwamba wapigane vita vya kipumbavu mpaka mtu wa mwisho atakapofariki.

    Basi Vita vya Stalingrad viliisha wakati Jemedari Paulus alikataa kuendelea kupigana vita vya kipumbavu visivyo na maana. Baada ya kushindwa katika vita hivyo, Jemedari Paulus, ambaye alikuwa na machungu, aligeuka na akawa adui ya Hitler. Alishirikiana na Warusi na wakaunda Kamati ya Kitaifa ya Kuweka Ujerumani Huru. Walipeperusha matangazo ya redio kutoka mjini Moscow wakiwahamasisha wanajeshi wa Ujerumani waache kumpigania Hitler.

    Pigano Langu la Kipumbavu

    Miaka mingi iliopita nilipokuwa shuleni, nilipigana na mwanafunzi fulani ambaye alipenda kuwachokoza wenzake. Vitu viwili vilitendeka baada ya pigano hilo. Kwanza, nilidhani nimeshinda pigano hilo au tumetoshana nguvu na adui yangu. Lakini kila mtu aliyeshuhudia pigano hilo alinicheka na walisema kwamba nilishindwa.

    Pili, ingawa nilitia juhudu za dhati katika pigano hilo, sehemu iliyo karibu na jicho langu moja ilikuwa nyeusi. Sehemu yote karibu na jicho langu moja iligeuka na ikawa nyeusi na ilisalia hivyo kwa takriban wiki moja. Baada ya pigano hilo, nilifikia hitimisho ya kwamba hakuna haja ya kupigana vita visivyo na maana dhidi ya watu wasiyo na maana, mbele ya watazamaji wasiyo na maana ambao hawawezi kuvutiwa na ujuzi wangu katika ubondia na kupigana!

    Kuanzia siku hiyo, niliamua kwamba nitapigana vita vilivyo vizuri ambavyo vinastahili kupiganwa peke yake. Niliamua nitapigania maswala mema peke yake na nitapigania maswala yenye matokeo mema peke yake. Ndio maana leo sijihusishi na vita vya kisiasa au hata vita vya kutafuta fedha. Nilijifunza kujiepusha na vita vya kipumbavu miaka mingi iliopita nikiwa shuleni. Leo, nimegundua mambo mengi mema ya kupigania. Neno la Mungu limenionesha mambo mengi yanayostahili kupiganiwa. Haya ni mambo ambayo yanastahili kung'ang'aniwa na yanastahili juhudi zetu. Unaweza kupigania kitu chema au upiganie kitu cha kipumbavu. Watu wengi wanapigana katika vita vya kipumbavu.

    Sura ya 3

    Jemedari Mwema Atapigana Vita Vilivyo Vizuri

    Pigana vita vilivyo vizuri vya imani....

    1 Timotheo 6:12

    Ni muhimu kutambua vita vilivyo vizuri ili usivitoroke wakati ukifika ambapo utatakiwa kuvipigana. Orodha iliyo hapa chini ni ya vita ambavyo unahitaji kuwa tayari kuvipigana. Jitayarishe kupigana kwa sababu wewe ni Mkristo. Jitayarishe kupigana hata zaidi ikiwa wewe ni mhubiri wa injili.

    Vita Kumi na Nane Vilivyo Vizuri

    1. Pigana ili uwe Mkristo mwenye nguvu.

    Wakristo wengi hawana nguvu katika Bwana. Inahitaji juhudi za dhati ili uwe muumini mwenye nguvu.

    Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.

    Waefeso 6:10

    2. Pigana ili uongozwe na Roho Mtakatifu na uwe ndani ya mapenzi ya Mungu.

    Tutahitaji kupigana vita ili tuweze kupambanua tofauti iliyoko kati ya sauti mbalimbali zinazojaribu kutushawishi. Utahitaji kupigana vita ili uweze kutenganisha sauti ya mwili, sauti ya akili yako na sauti ya Roho. Mahali pazuri zaidi pa kuishi ni kuishi ndani ya mapenzi ya Mungu. Sauti nyingi zitataka uzisikilize. Pepo wengi watapigana ili wakupotoshe. Utahitaji kupambana ili uwe katika mapenzi ya Mungu. Wakati mwingine, sauti ya mke au mume wako au sauti ya mwili wako, inaweza kuwa na nguvu sana kiasi kwamba utahitaji kuikaripia. Je, uko tayari kupigana na rafiki yako wa karibu zaidi ili uwe katika mapenzi ya Mungu?

    Yamkini ziko sauti za namna nyingi duniani, wala hakuna moja isiyo na maana.

    1 Wakorintho 14:10

    3. Pigana ili uwe mtu anayefuata roho wala si mwili. Utahitaji kupambana ili uwe mtu wa kiroho.

    Ni kawaida zaidi kutosheleza mahitaji ya kimwili. Ni kawaida zaidi kula, kulala, kupumzika na kushiriki ngono kuliko kutofanya vitendo hivyo. Katika maisha yako yote, utahitaji kupambana ili uwe mtu wa kiroho. Pia utahitaji kupambana sana ili uweze kuomba. Kuamka mapema na kuwa na muda na Mungu si jambo la kawaida. Utahitaji neema na nguvu ya Mungu ili uingie katika himaya ya kiroho.

    Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.

    Warumi 8:6

    4. Pigana ili uzae matunda ya Roho. Pigana ili uenende katika upendo.

    Utahitaji kupambana ili uzae matunda ya upendo, furaha na amani. Ni kawaida zaidi kuwa na hasira, machungu na kunung'unika. Utahitaji kupigana dhidi ya asili yako mwenyewe ili uweze kuzaa matunda ya upendo, furaha na amani.

    Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

    Wagalatia 5:22-23

    5. Pigana ili uingie katika huduma.

    Mojawapo ya vita vikuu zaidi ni vita vya kuingia katika huduma. Hivyo vitakuwa mojawapo ya vita vikuu zaidi maishani mwako. Ni hatua isiyo ya kawaida kabisa kuacha kazi yako nzuri ya kidunia ili uwe mchungaji. Ikiwa uko tayari kumfuata Mungu na unataka kupigana vita vilivyo vizuri, basi jaribu kupigana ili uingie katika huduma ya Bwana Yesu Kristo.

    Akamwambia mwingine, nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu.

    Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu.

    Luka 9:59-60

    6. Pigana ili usalie katika mwito wako.

    Ukishajiunga na huduma, utahitaji kupambana ili usalie katika njia sahihi ukiwa katika huduma. Kuna mamishonari vijana ambao walihitaji kufanya kazi kwa hivyo wakawa wachungaji walei ili waweze kujikimu wakiwa katika kazi zao za misheni. Baada ya muda mfupi, mioyo yao ilitoka katika huduma halisi na wakaingia katika biashara za kidunia. Ukiwa katika huduma, ni rahisi kupotea njia na kuacha mwito wako halisi. Mungu anapobariki huduma yako na uwe na kanisa kubwa, ni rahisi kugeuka na kuwa mhubiri wa mambo ya kiupuuzi. Unapokuwa na kanisa kubwa, huenda ukachukulia kwamba kweli za kimsingi za Neno la Mungu ni za kimsingi sana kiasi kwamba hakuna haja ya kuhubiri kuzihusu. Huenda ukahitaji kupigana vita vilivyo vizuri ili ujiepushe na kuwa mnenaji wa kidunia wa kutia watu motisha.

    Maana DEMA ALINIACHA, AKIUPENDA ULIMWENGU HUU WA SASA, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia.

    2 Timotheo 4:10

    7. Pigana ili ujihusishe na watumishi mashuhuri wa Mungu.

    Si rahisi sana kuwa karibu na watumishi wa Mungu. Nimejaribu kuwa karibu na watumishi kadhaa wa Mungu lakini sikufaulu kila wakati. Itachukua miaka mingi ya kupigana, kuwa na mahusiano na kujinyenyekeza ili upate karibu na watu wenye upako. Watu wengi hawako tayari kupigana vita hivyo. Watu wengi hukata tamaa katika kujaribu kuwa na uhusiano na watumishi wa Mungu wanapogundua kwamba ni sharti wapambane ili wawe karibu na watu hao na pia hawana budi kuendelea kupambana ili wadumishe uhusiano wa karibu na watu hao. Si kuwa na uhusiano na watu wenye upako. Elisha alihitaji kupigana ili awe karibu na Eliya. Na alishinda vita hivyo. Je, uko tayari kupigana ili upokee upako wako?

    Ikawa, hapo Bwana alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha.

    2 Wafalme 2:1

    Eliya akamwambia Elisha, Tafadhali, kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Betheli. Elisha akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, SITAKUACHA. Basi wakashuka mpaka Betheli.

    2 Wafalme 2:2

    Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana Bwana amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, SITAKUACHA. Nao wakafika Yeriko.

    2 Wafalme 2:4

    Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana Bwana amenituma niende mpaka Yordani. Akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, SITAKUACHA. Wakaendelea mbele wote wawili.

    2 Wafalme 2:6

    8. Pigana ili upate upako.

    Utahitaji kupambana ili upate upako. Ndio maana Eliya alimuambia Elisha, Umeomba neno gumu. Kwa kweli ni jambo gumu kupata upako na uwe na upako. Ikiwa hauko tayari kupigana, huwezi kupata upako. Ni wale ambao wako tayari kupigana kwa ajili ya kupata upako ndio wanastahili kupata upako!

    Hata ikawa, walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lo lote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yangu.

    Akasema, Umeomba neno gumu; lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati.

    2 Wafalme 2:9-10

    9. Pigana ili upate mwanandoa mwema katika maisha yako.

    Utahitaji kupambana ili upate mwanandoa. Ruthu alihitaji kupigana ili amvutie Boazi. Pia utahitaji kupambana ili usalie katika ndoa. Wanyama wengi hawawezi kuwa na uhusiano wa kingono na mnyama mmoja peke yake. Silikia zetu za kinyama hutufanya tutake kushiriki ngono na watu wengi mbalimbali. Ni lazima upigane vita ili ujizuie kuwa mtu anayeshiriki ngono na watu wengi mbalimbali.

    Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo.

    Ruthu 3:6-7

    10. Pigana ili ufanikiwe. Mafanikio hayaji kwa urahisi.

    Itakubidi upigane ili ufanikiwe. Utajiri umewekwa mahali pa siri. Hazina zimefichwa sehemu zenye giza. Pasipo kupigana, kamwe hutagundua utajiri ulio katika dunia hii yote. Watu wenye haiba ya flegmatiki, ambao wanafanya mambo polepole na ni wavivu, hawawezi kuwa matajiri kwa urahisi. Hiyo ni kwa sababu vita vya dhati vinahitajika ili dunia iachilie matunda yake. Ni sharti upigane ili upate elimu. Ni sharti upigane ili upite mitihani yako. Ni sharti upigane ili upate kazi nzuri. Baada ya kupata kazi nzuri ni sharti upigane ili upandishwe cheo. Kisha ni sharti upigane ili uweze kutumia pesa zako vizuri.

    Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.

    Marko 4:25

    11. Pigana ili ujenge nyumba yako. Ni sharti upigane ili ujenge nyumba yako binafsi.

    Sehemu kubwa ya watu hawamiliki nyumba na kamwe hawatamiliki nyumba. Ingawa ni sharti upambane ili umiliki nyumba, kuna faida katika kupambana ili umiliki nyumba yako binafsi.

    Nyumba hujengwa kwa hekima, na kwa ufahamu huthibitika:

    Mithali 24:3

    12. Pigana ili uishi maisha marefu na umtumikie Bwana kwa muda mrefu.

    Utahitaji kupambana ili uwe na afya bora, usalie hai na umtumikie Bwana kwa miaka mingi.

    Wakamwambia wakasema, Ukikubali kuwa mtumishi wa watu hawa leo, na kuwatumikia, na kuwajibu, na kuwapa maneno mazuri, basi WATAKUWA WATUMISHI WAKO DAIMA.

    1 Wafalme 12:7

    13. Pigana dhidi ya hulka hasi za haiba yako.

    Haiba yako ya felgmatiki, koleriki, melankoliki na sanguini ina hulka hasi.

    Hulka ya kufanya mambo polepole na kutokuwa mchangamfu kutamzuia mtu mwenye haiba ya flegmatiki kutimiza kitu chochote katika huduma. Kufanya mambo polepole na kutokuwa mchangamfu kutakufanya usiwe na ari ya kusonga mbele au kupigana vita. Hulka hiyo huleta umasikini.

    Uhuru wa sanguini utasababisha kutokuzingatia mipangilio maalum, mkanganyo na dhambi za kimwili.

    Kununa na sonona ya mtu mwenye haiba ya melankoliki itaharibu mahusiano na itasababisha ukosefu wa furaha. Mtu mwenye haiba ya melankoliki atahukumu watu na atawaondoa watu wanapofanya makosa.

    Uovu, ukali na ujeuri wa mtu menye haiba ya koleriki utaharibu mahusiano. Maamuzi ya haraka ya mtu mwenye haiba ya koleriki yanaweza kumfanya aasi. Shughuli nyingi za mtu mwenye haiba ya koleriki zitamzuia kuwa na muda na Mungu.

    Itakubidi upambane ili ujizuie kufanya kile ambacho wewe hufanya kwa kawaida! Naona kwamba hilo ndilo pambano gumu zaidi kwa watu wengi: pambano la kujikana mwenyewe. Pigana vita vilivyo vizuri vya kukana asili yako uliorithi wewe kama mwanadamu.

    Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.

    Marko 8:34

    14. Pigana dhidi ya hulka zako za kiume au za kike.

    Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana MTU MUME WALA MTU MKE. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.

    Wagalatia 3:28

    Ikiwa wewe ni mwanaume, utagundua kwamba ni vigumu kuwa mwaminifu kwa mwanamke mmoja. Lakini huna budi kupigana dhidi ya hulka hiyo ya kiume na ung'amue jinsi utakavyofanya ili usalie muaminifu kwa mwanamke mmoja. Mwanaume hana budi kupambana ili asalie mwaminifu. Lakini vita hivyo ni lazima vishindwe! Hulka ya kiume pia hudhihirishwa na hamu ya kushiriki ngono. Hamu kubwa ya kushiriki ngono inaweza kukufanya ujihusishe na ponografia, kupiga punyeto, usherati na uzinzi. Usipojikana mwenyewe, utajipata katika mashaka makubwa katika huduma.

    Wanawake kwa upande wao watajipata wanakabiliwa na hofu, wivu na tabia ya kushtakiana. Ni sharti udhibiti hulka zako za kike ili zisiangamize huduma yako. Ni muhimu kudhibiti hulka zako za kiume au za kike mpaka ifikie mahali ambapo hakuna tofauti za kihulka ambazo zitadhihirika uwe mwanaume au mwanamke.

    15. Pigana dhidi ya kuwa na hulka za aina fulani zinazohusishwa na kabila lako au taifa lako.

    Mtu wa kwao, nabii wao wenyewe, amesema, WAKRETE NI WAONGO SIKU ZOTE, hayawani wabaya, walafi wavivu.

    Ushuhuda huo ni kweli. Kwa sababu hiyo uwakemee kwa ukali, ili wapate kuwa wazima katika imani;

    Tito 1:12-13

    Kila kabila, jamii au taifa lina hulka zake za aina fulani. Nchini Ghana, watu wa jamii ya Ashanti ni maarufu kwa kuwa na hulka za aina fulani na watu wa jamii ya Ewe pia ni maarufu kwa kuwa na hulka za aina fulani. Unapoingia katika huduma ni sharti uwe muangalifu ili usiwe na hulka za Kiewe au za Kiashanti kupita kiasi. Ukionekana una hulka za mojawapo ya makabila hayo, hiyo itaathiri uwezo wako wa kuzaa matunda miongoni mwa jamii ya watu wa kabila hilo lingine. Baadhi ya wachungaji wanapenda sana mataifa yao kiasi kwamba hawawezi kutekeleza huduma katika mataifa mengine. Wamarekani wengi wanazingatia sana taifa lao la Marekani kiasi kwamba hawawezi kutekeleza huduma katika mataifa mengine ya dunia. Asiliamia tano pekee ya watu wa dunia ndio wanaoishi katika eneo la Amerika ya Kaskazini na wachungaji wengi raia wa Marekani sasa wanahudumia asilimia tano tu ya watu wa dunia hii. La kushangaza ni kwamba asilimia hiyo tano ya watu wa dunia ina asilimia tisini ya wahubiri wa injili duniani.

    Raia wa Nigeria wameanzisha makanisa mengi makuu. Raia wa Nigeria pia ni maarufu kwa kuwa na hulka za aina fulani. Ikiwa wewe ni mchungaji wa Kinigeria, ni sharti utie juhudi katika kujiepusha na hulka hasi zinazohusishwa na raia wa Nigeria. Kuna faida katika kupigana ili uwe Mkristo zaidi kuliko kuwa kitu chochote kingine.

    Nchi za zilizokuwa chini ya ukoloni wa Ufaransa ni maarufu kwa kuwa na hulka za aina fulani. Ni muhimu kujiepusha na hulka hasi zinazohusishwa na raia wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni wa Ufranasa. Ni sharti uwe Mkristo zaidi kuliko kuwa kitu chochote kingine.

    16. Pigana dhidi ya kuwa na hulka zinazohusishwa na jamii ya watu wenye rangi fulani.

    Akasema,Na alaaniwe Kaanani; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.

    Akasema, Na atukuzwe Bwana,Mungu wa Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake.

    Mungu akamnafisishe Yafethi,Na akae katika hema za Shemu; Na Kaanani awe mtumwa wake.

    Mwanzo 9:25-27

    Jamii ya Waafrika inajulikana kwa ukosefu wa maendeleo, umasikini, uchakavu, uchafu, mkanganyo, kutokuwa na mipango maalum na kutoweza kufaulu! Jamii ya Wazungu inajulikana kwa kupenda pesa, ukosefu wa mahusiano dhabiti, ushoga, talaka, ndoa za jinsia moja, kukana kuwepo kwa Mungu, unywaji pombe kupita kiasi na viwango vya juu vya kujitoa uhai!

    La kusikitisha ni kwamba hizo ni tabia halisia ambazo tunahitaji kupambana nazo. Ikiwa wewe ni Mzungu au Mwafrika, pambana ili ujiepushe na hulka zinazohusishwa na jamii yako. Jiepushe kabisa na hulka hizo. Kuwa na hulka za Kikristo badala ya kuwa na hulka za mtu mweusi au mtu mweupe. Hivyo ni vita vilivyo vizuri na kuna faida katika kuvipigana!

    17. Pigana dhidi ya tamaa za kimwili.

    Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

    2 Timotheo 2:22

    Tamaa za kimwili ni moto unaochoma utakatifu wako. Tamaa za kimwili hudunisha hali yako ya kiroho. Ndio maana Paulo alisema ni bora kufunga ndoa badala ya kuwaka tamaa. Ikiwa unawaka tamaa, unapitia hali ambayo si nzuri. Tamaa zako za kimwili zina ufungamano na hali yako ya kiroho. Maswala ya ngono ni ya kiroho kwa sababu yana ushawishi wa hali ya juu sana katika maisha ya wanadamu. Tamaa ya kimwili ni kitu hasi na hudunisha hali yako ya kiroho. Ni sharti upambane na tamaa za kimwili kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote.

    Njia ya kwanza ya kupambana na tamaa za kimwili ni kujizuia kupenda aina fulani za ngono. Punde unaposhikwa na tabia ya kupenda aina fulani za ngono, itakuwa vigumu kwako kudhibti tabia hizo.

    Pili, ikiwa tayari umeshikwa na tabia ya kupenda aina fulani za ngono, kama vile ponografia, kupiga punyeto na ushoga, ni sharti uombe dhidi ya mambo hayo maisha yako yote.

    Kitu cha tatu cha kufanya ili upigane na tamaa za kimwili, ni kupata njia halali ya kutosheleza tamaa hizo. Njia hiyo inaweza kuwa ni ndoa ambayo itakupatia nafasi ya kushiriki ngono mara kwa mara. La kusikitisha ni kwamba hata katika ndoa, hamu yako ya kushiriki ngono huenda haitatoshelezwa ikiwa una mke mbaya. Haijalishi unakabiliwa na hali gani, bado itakubidi upigane dhidi ya tamaa za kimwili kwa maisha yako yote.

    18. Pigana ili uzae matunda.

    Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.

    2 Petro 1:8

    Pambano dhidi ya utasa wa kiroho ni pigano gumu na la kudumu kwa muda mrefu. Pambano hilo linahusu kudhihirisha sifa zako nyingi zilizofichika na kuishi maisha yako kwa njia sahihi kadiri unavyomtumikia Bwana. Utagundua kwamba kuzaa matunda kuna ufungamano na bidii, imani, kuumcha Mungu, moyo wa kiasi, ufahamu, maadili mema na subira. Hizi ni sifa za kiroho ambazo zinaonekana hazina ufungamano wowote na kuzaa matunda. Lakini zina ufungamno na kuzaa matunda! Sifa zote hizi ni viamuzi vya kiwango chako cha kuzaa matunda. Katika maisha yako yote, utapambana ili uwe na bidii, moyo wa kiasi, imani, ufahamu, ukarimu na moyo wa kutoa.

    Kuna faida katika kupigana vita hivyo kwa sababu ni vita vya kuzaa matunda.

    Sura ya 4

    Jizoeshe Mazingira ya Vita

    Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni.

    Isaya 9:5

    Tuko katika vita vya mwisho vya kuleta nafsi za wanadamu kwa Kristo. Tusipozoea mazingira ya vita, kamwe hatutaweza kuishi kama inavyostahili. Sikiliza kile ambacho Biblia inasema: Maana silaha zote za mtu mwenye silaha wakati wa mshindo, na mavazi yaliyofingirishwa katika damu, yatakuwa tayari kuteketezwa, yatakuwa kuni za kutiwa motoni. (Isaya 9:5) Hayo si mazingira ya amani, utulivu na furaha.

    Hayo ni mazingira ya vita ambapo kuna hatari, mkanganyo, kuchanganyikiwa, kiwewe, wasiwasi, ukosefu wa furaha, hofu, kifo, uchungu, masikitiko na mshtuko. Mungu anatutumia kueneza Neno lake na kupigana dhidi ya ulaghai na uwongo unaoongoza watu wengi katika kuingia jehanamu. Tuna adui ambaye hafurahi anapoona ufalme wa Mungu ukisonga mbele. Punde Yesu alipoingia duniani, alishambuliwa na ibilisi mara kwa mara. Yesu Kristo aliishi katika mazingira ya vita. Ibilisi hakukaa mbali naye. Yesu alishambuliwa na roho ya mauaji ambayo iltaka kumuangamiza kabla hajakuwa mtu mzima. Alishambuliwa nyikani alipokuwa katika hali ya kufunga na kuomba. Alishambuliwa kupitia Mafarisayo na hatimaye alishambuliwa kupitia Yuda Iskariote.

    Mazingira ya Huduma Halisi ni Mazingira ya Vita.

    Punde unapoitikia mwito mkuu wa Mungu, utakuwa umejitosa katika vita vya mwisho kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Yesu alikufa msalabani na tukio hilo lilianzisha kampeni ya dhati ya kukomboa ulimwengu huu kutokana na ibilisi muovu mno

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1