Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo
Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo
Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo
Ebook145 pages2 hours

Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Shughuli za mapepe zinawekwa wazi katika kitabu hiki kipya cha kipekee na Dag Heward-Mills. Tukitumia ushuhuda wa mwanamme mwenda wazimu wa Gadara, anaonyesha njia ya ushinda thidi ya mapepo na roho mbaya.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613958476
Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo

Related ebooks

Reviews for Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mapepo Na Jinsi Ya Kukabiliana Nayo - Dag Heward-Mills

    Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi. Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo;kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini Na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.

    Na alipomwona Yesu Kwa mbali, alipiga mbio, akamsujudia; akapiga kelele Kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani? Akamjibu, Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tu wengi akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile. Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakilisha.Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini. Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea. Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa. Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na habari za nguruwe. Wakaanza kumsihi aondoke mipakani mwao. Naye alipokuwa akipanda chomboni, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye; lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu. Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.

    Marko 5:1-20

    Somo la kichaa wa nchi ya Wagerasi ni somo linalohusu utendaji wa mapepo. Utajifunza mambo mengi kuhusu shetani na mapepo kwa kuchunguza habari hii ya kichaa wa Wagerasi. Watu wengi hujiuliza uchunguzi huu wa namna gani, na mara nyingi tunajiuliza kwa nini mtu atumie muda wake kuchunguza maiti. Mimi nikiwa mwanafunzi wa udaktari sikuelewa umuhimu wa daktari kutumia muda wake akipasua maiti. Nilifikiri, Watu wakifa wamekufa, we achana nao! 

    Hata hivyo, nilikuja kuelewa kwamba, patholojia (Sayansi au elimu ya magonjwa) ni kujifunza athari za maradhi mbalimbali katika mwili wa binadamu. Ni kujifunza madhara kamili yatokanayo na maradhi mbalimbali katika mwili wa binadamu. Kwa maneno mengine, ili kuelewa madhara ya maradhi yakiachiwa yafanye kazi yake, lazima ujifunze patholojia. Mara nyingi ni katika maiti ndipo unaona madhara kamili ya maradhi. 

    Kwa mfano, ukipasua mwili wa mwanaume aliyekufa kutokana na shinikizo la damu la muda mrefu, utaona mabadiliko katika moyo, mishipa ya damu, na figo. Mabadiliko haya yatakusaidia kuelewa kile shinikizo la damu linafanya kwa wale wanaoishi na maradhi hayo. 

    Kwa kuichunguza maiti ambayo imeathiriwa na maradhi fulani, madaktari huelewa zaidi kuhusu maradhi. Vivyo hivyo, kwa kujifunza kuhusu kichaa wa Wagerasi utaelewa madhara kamili ya mapepo ndani ya binadamu. 

    Habari ya kichaa wa nchi ya Wagerasi, ni kujifunza kwa undani zaidi mapepo yanavyofanya kazi. Ni ufunuo wa kile ambacho shetani angependa akufanyie kama angelipata nafasi. Kila muonekano wa yule kichaa kwa Wagerasi unaonyesha tabia halisi za mapepo. Hali yake huonyesha maeneo tofauti ya maono ya shetani kwa ajili yako wewe na mimi. Kama shetani angeruhusiwa kufanya atakavyo, wewe na mimi tungelikuwa na hali hiyo hiyo. 

    Licha ya kwamba wengi hawatafikia kabisa ukichaa wa yule wa Wagerasi, wengi tutakuwa na sehemu tu ya yale yaliyompata kichaa wa Wagerasi. 

    Ushuhuda wa kichaa wa nchi ya Wagerasi unatuonyesha mambo matatu:-

    1. Kile ambacho mapepo yangependa yakufanyie kama yangepata nafasi. 

    2. Kile mapepo yanawafanyia watu, kwa namna ya taratibu.

    3. Hatua ya mwisho ya mtu ambaye mapepo yamepata nafasi ya kujidhihirisha kikamilifu.

    Usomapo kitabu hiki, Mungu atakufunulia mambo mengi kuhusu utendaji wa mapepo, na athari zake kwako. Utafunguliwa na kazi za mapepo umalizapo kusoma kitabu hiki. 

    Wengi hufikiri kwamba, habari ya kichaa wa nchi ya Wagerasi ni habari ya kichaa anayestahili kuwepo kwenye hospitali ya vichaa. Wanawaza kwamba, Kwa kuwa mimi siyo kichaa, habari hii hainihusu. Kinyume chake, ushuhuda huu unatuhusu sote"

    Kuelewa utendaji na makusudi ya adui yako, ni kwa muhimu sana ili kushinda vita. Ukitaka kuwashinda mapepo wachafu, lazima uelewe ni kwa jinsi gani na wapi adui yako anafanya kazi. Lazima uelewe adui yako amepanga nini juu yako. 

    Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana HATUKOSI KUZIJUA FIKIRA ZAKE.

    2 Korintho 2:11*

    Tena zaidi  ya hayo, kwa kurasa hizi chache, mwanangu, kubali maonyo; hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi.

    Sura ya Mbili

    Giza - Makao ya Mapepo

    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa GIZA hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Waefeso 6:12

    Giza la ulimwengu huu ni makao ya roho chafu, giza ni mazingira ambayo uovu hufanyika kwa wingi. Shetani anatawala giza la ulimwengu huu. Udanganyifu ni aina ya giza la kiroho. Hii ni kwa sababu mazingira ya udanganyifu ni mazalio ya roho chafu. 

    Kwa urahisi, giza ni eneo la udanganyifu ambalo shetani hufanya kazi. Adui yetu aliyeshindwa hufanikiwa sana mahali penye giza nene. Hawezi kutushinda tukisimama katika nuru. Ndio maana shetani analichukia sana Neno la Mungu. 

    Yesu ni nuru inayovunja uwezo wa shetani juu ya mwanadamu. Neno la Mungu ni nuru ing’aayo gizani. Utendaji wa mapepo hupunguzwa sana mahali ambapo Neno la Mungu hufundishwa. 

    NAYO NURU YANG'AA GIZANI, wala giza halikuiweza.

    Yohana 1:5

    Uwezo wa shetani juu ya kanisa unaweza kufananishwa na vita au ugomvi uliopo duniani leo.  Wakati taifa kubwa linapopambana na jeshi dogo, upande dhaifu unajua hauwezi kupigana vita ya wazi. Kwa hiyo, hujificha na kupambana kutoka maeneo ya siri, udanganyifu na giza. Hivyo, hii huwa vita ya kuviziana na mashambulizi ya kigaidi. 

    Kwa mfano, majeshi ya Israeli yana uwezo mkubwa kuliko majeshi ya Wapalestina; Wapalestina hawawezi kushindana na uwezo mkubwa wa majeshi ya Israeli. Inasemekana kuwa, Israeli ina uwezo wa kinyuklia. Kwa kuwa Palestina haiwezi kushindana na Israeli, huishia kutumia mashambulizi ya kushtukiza na ugaidi. Kuteka nyara ndege, kutumia mashambulizi ya kushtukiza na ugaidi. Kuteka nyara ndege na kuua wale Waisraeli walioshiriki mashindano ya olimpiki ni mifano michache ya aina ya vita ambavyo upande dhaifu hupambana. 

    Mashambulizi ya kigaidi kama ya Septemba 11 ni mfano mwingine wa aina ya vita ambayo majeshi madogo na dhaifu hutumia kupambana na majeshi makubwa. Hivyo hivyo, majeshi ya pepo yanayojipanga juu ya kanisa, hayawezi kushindana na uwezo wa Mungu. Silaha za vita vyetu zina uwezo.

    (Maana silaha za vita vyetu si za mwili, BALI ZINA UWEZO KATIKA MUNGU hata kuangusha ngome;)

    2 Wakorintho 10:4

    Shetani hutetemeka jina la Yesu linapotamkwa, mapepo hutetemeka tuimbapo kuhusu Damu ya Yesu. Wanapoona Damu ya Yesu, huikwepa. Neno la Mungu ni upanga wenye nguvu, unaokatakata

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1