Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Stadi ya Huduma
Stadi ya Huduma
Stadi ya Huduma
Ebook205 pages8 hours

Stadi ya Huduma

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kujenga ustadi ni kujenga uwezo au ujuzi. Biblia inasema kwamba kibali huja kwa watu wenye ujuzi. Kazi ya huduma huhitaji uwezo mkubwa. Kitabu hiki kipya, "Stadi ya Huduma" ni rasiliamali inayohitajika sana kwa wale wote wanaotamani kufanya kazi ya huduma. Inawasilisha vizuri mawazo yapi ni sahihi na yapi ni mabaya kuhusu huduma, nini kazi ya huduma, ni kipi kinachotakiwa kwako kama mfanyakazi katika huduma na jinsi gani ya kufanya majukumu ya mtumishi. Je umewahi kuwaza jinsi ya kufanya kazi yako katika huduma? Kitabu hiki cha kipekee cha Dag Heward- Mills kitakupa changamoto kutembea kwa kulingana na wito wa Mungu na kukuongoza katika kujitoa kikamilifu katika kazi ya huduma.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345514
Stadi ya Huduma
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Stadi ya Huduma

Related ebooks

Reviews for Stadi ya Huduma

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Stadi ya Huduma - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Karama na Wito wa Mungu Havina Majuto

    Wito wa kwanza

    Basi neno la BWANA lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu

    Yona 1: 1-2

    Wito wa pili

    Neno la BWANA likamjia Yona MARA YA PILI, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru.

    Yona 3: 1-2

    Mungu ni Mungu wa rehema! Atakupa nafasi ya pili ya kumtii. Yona ni mfano wa mtu ambaye alipata nafasi ya pili ya kusikia na kutii. Wakati mwingine tuna nafasi moja tu!

    Mungu wa nafasi ya pili

    Labda mara kwa mara Mungu amekutaka ufanye kazi kanisani na hiyo ndiyo sababu ya kukuumba. Yamkini umekuwa unaukimbia wito wa Mungu. Lakini Mungu anasema na wewe kwa mara nyingine tena. Mungu aliongea na Yona mara mbili. Katikati ya wito wa kwanza na wa pili, Yona alipitia mambo mengi. Alikumbana na dhoruba za maisha pamoja na gereza la tumbo la nyangumi. Yamkini baada ya mapito magumu mengi, upo tayari kumsikiliza Mungu.

    Labda unavyoshika hiki kitabu, Mungu anakupa nafasi ya pili ya kufanya kazi katika nyumba yake. Ni wakati wa kujiunga na jeshi kwa vita vya mwisho.

    Hakuna badiliko la wito

    Utagundua kuwa wito wa kwanza na wito wa pili unafanana. Wito wa kwanza na wa pili kwa pamoja, Yona alitumwa kwenye mji uleule (Ninawi) kwa ujumbe uleule. Karama na wito wa Mungu havina majuto (Warumi 11:29).

    Mungu habadilishi wazo lake kutokana na mapito ya muda. Hata baada ya kupitia maumivu ya dhoruba na Nyangumi; tumboni, bado Anaweza kukutumia. Miaka kumi yaweza kuwa imepita tangu Mungu alipoanza kukuita. Bado haujachelewa kumtii Yeye. Ninafuraha kumtumikia Mungu ambaye kamwe habadilishi wazo lake.

    Kukubali wito wa Mungu ni kukubali kufanywa kuwa kitu kingine ambacho haukuwa. Yesu alijitoa kumfanya Petro kuwa vile ambavyo hakuwa- mvuvi wa watu!

    Kuingia kwenye huduma haihusiani na kufanya baadhi ya michango mikubwa kwenye ufalme wa Mungu. Hakuna chochote kinachokutegemea wewe na hakuna chochote kitakachoharibika kwa kuipuuza huduma.

    Sisi sote si watu wa muhimu.

    Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli.

    2 Wakorintho 13:8

    Andiko hili linatufundisha kuwa hakuna chochote tutakachoweza kufanya ambacho kitapingana na ukweli wa neno la Mungu. Makosa yetu makubwa hayatazuia ukweli wa injili. Ukubwa wa upuuzaji wa wito wetu hauwezi kubadili lengo la jeshi la ushindi la Mungu. Ni adhama yetu kuitwa kwenye kazi hii. Ni heshima yetu kuhusishwa. Ni wakati wa kuacha kufikiri kuwa utafanya kitu cha kipekee kwa Mungu.

    Kuwa kwenye huduma ni uzoefu wa kujinyenyekeza ambapo unajifunza kuhusu Mungu na kupokea rehema. Yesu aliwaambia wanafunzi wake wamfuate naye atawafanya kuwa watu wa thamani. Kwenye huduma ya muda wote, utafinyangwa kuwa chombo ambacho Mungu anaweza kutumia.

    Yesu akawaambia, Njoni mnifuate, nami NITAWAFANYA kuwa wavuvi wa watu.

    Marko 1:17

    Kwenye huduma ya muda wote, utabadilishwa kwa kufanywa upya fikra zako na kwa uzoefu wa unyenyekevu mwingi unaokungojea. Hata hivyo huduma ya muda wote ni mwanzo wa safari ambayo itakuleta karibu na Mungu. Inakubadilisha na kukufanya mnyenyekevu. Hali ya kazi hii inayopuuzwa na ushirikiano na Wakristo wengine kwenye huduma kwa uhakika itakushusha na kukufanya mtu mzuri! Pia ushirikiano na watu wa nje ambao hawaelewi kuhusu huduma ya muda wote utakuingiza kwa kina katika Mungu.

    Ni nini kisicho huduma ya muda wote.

    Kuwa kwenye huduma ya muda wote ni pale ambapo Yesu amekufanya kuwa wavuvi wa watu. Kulipwa na huduma haikufanyi kuwa mtumishi wa muda wote.

    Kubadilisha chanzo chako cha mshahara kutoka benki kwenda kanisani haina maana upo kwenye huduma ya muda wote. Huduma ya muda wote ni mkusanyiko (mjumuisho) wa hatua zote ambazo kupitia hizo unamfuata Bwana kikamilifu. Wewe kumfuata Yeye itamaanisha mambo mengi ikiwemo baadhi ya dondoo zilizoorodheshwa hapa chini.

    Huduma ya muda wote siyo rahisi kama kubadili kazi. Ni kujitoa kwa maisha. Itameza utu wako wote na utabadilishwa na nguvu za Mungu.

    Huduma ya muda wote siyo kati ya haya:

    Huduma ya muda wote si chaguo la kazi nyepesi

    Huduma ya muda wote si uchaguzi wa kazi rahisi.

    Huduma ya muda wote si mpango wa kustaafu kwa wazee.

    Huduma ya muda wote si mpango kwa wafanyakazi walioondolewa.

    Huduma ya muda wote si kimbilio cha akina mama wenye watoto wadogo.

    Huduma ya muda wote si tumaini kwa watu wenye dakika za mwisho kufa ambao waliitumia miaka yao mizuri kufanya mambo mengine.

    Huduma ya muda wote si mpango wa biashara za siri. Baadhi ya watu wanataka kutumia huduma ya muda wote kujihakikishia mshahara huku wakifanya biashara upande mwingine.

    Biashara ni biashara na huduma ni huduma!

    Huduma ya muda wote si shughuli ya watu wanaofanya kazi mbalimbali.

    Huduma ya muda wote si chaguo kwa watu wenye tamaa za kidunia.

    Huduma ya muda wote si mkakati wa kutokomeza umaskini. Wakati mwingine ni bora kiuchumi kufanya kazi kwenye huduma.

    Huduma ya muda wote si sawa na kuhamisha utaalamu wako kutoka kazi yako ya kawaida kwenda kanisani. Kwa vile wewe ulikuwa mhasibu duniani haina maana kwamba ni lazima uwe mhasibu kanisani.

    Huduma ya muda wote haihusu tu kuhamisha chanzo chako cha mshahara.

    Huduma ya muda wote si kazi ya kufanya kwenye likizo. Huduma ya muda wote si jambo la wanafunzi kufanya wakiwa kwenye likizo

    Udanganyifu kuhusu Huduma ya Muda Wote

    Kuna hali ya udanganyifu wa hali ya kisasa ambao unapiga watu katika hali mbalimbali. Watu walio kwenye huduma ya muda wote wana sehemu zao za udanganyifu. Baadhi ya udanganyifu ambao unamtesa mtumishi wa huduma ya muda wote ni:

    1. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote mimi ni mtu maalum.

    2. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitakuwa na mshahara mzuri.

    3. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nimechukua hatua ya juu ya kiroho na hakuna hatua za kiroho za kuchukua zaidi.

    4. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote mimi ni bora kuliko watumishi wasiolipwa.

    5. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitasafiri kwenda nchi za nje.

    6. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitakuwa na nyumba kubwa.

    7. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitakuwa na gari

    8. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitakuwa tajiri.

    9. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nimekuwa wa kiroho.

    10. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitakuwa na ndoa nzuri na maisha bora ya kifamilia.

    11. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitakuwa na muda zaidi wa kuomba, kuabudu na kusoma neno.

    12. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote Mungu anapendezwa sana na mimi.

    13. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote natembea katika upendo.

    14. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote hukumu yangu itakuwa rahisi.

    15. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nimepakwa mafuta na kulindwa.

    16. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote watoto wangu watakuwa vizuri.

    17. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote nitaenda Mbinguni kwa uhakika.

    18. Kwa sababu nipo kwenye huduma ya muda wote mimi ni mwaminifu.

    Hakuna chochote kilichoorodheshwa hapo juu ambacho ni ukweli hasa. Vinaweza vikawa kweli lakini vingi vya hivyo vinaweza visiwe vya kweli kwa upande wako. Bila shaka siyo vitu ambavyo vitatokea tu. Hauna budi kumtafuta Mungu katika huduma ya muda wote ili mipango yake yote ipate kutimia.

    Sura ya 2

    Tofauti kati ya Kazi ya Kawaida na Kazi ya Huduma.

    Kuna Utofauti

    Walakini watamtumikia; ILI WAPATE KUJUA utumwa wangu, na huo utumwa wa falme za nchi.

    2 Mambo ya Nyakati 12:8

    Rehoboamu alipomuasi Mungu, nabii alimtumia ujumbe wa kutisha. Alimwambia atamuonesha tofauti kati ya kufanya kazi kwa ajili ya Mungu na kufanya kazi kwa ajili ya mataifa ya ulimwengu.

    Kuna tofauti kati ya kufanya kazi kwa ajili ya Mungu na kufanya kazi kwa ajili Ulimwengu. Ukusanyaji wa utajiri katika dunia hii inayopotea hauwezi kufananishwa na wito mkuu wa Mungu.

    Kujenga mji wa milele kwa msingi halisi ni heshima ya hali ya juu kwa binadamu. Watu wengi hutumia maisha yao kujenga vitu vya muda mfupi visivyo na tumaini. Wastani wa binadamu kwa kawaida ni mjenzi wa mambo ya muda mfupi.

    Farao ni nani?

    Farao ni aina ya Shetani. Misri ni aina ya ulimwengu na Israeli ni aina ya watu wa Mungu. Farao aliwatesa watu wa Mungu kwa kazi ngumu na kuwafanya waijenge miji ya anasa. Hili linaonesha wazi kazi ya kidunia leo.

    Muda mwingi unaotumika duniani hutumika kujenga miji ya dunia hii. Siku tutakayokufa na kuondoka, tutakuwa tumeongeza zaidi majengo mazuri ya miji ya dunia hii.

    Kazi za hii dunia zimejaa na msongo na kutoka kwa jasho. Tumefanywa kufanya kazi kwa bidii sana bila kutambua kuwa tunaijenga miji ya starehe ya hii dunia. Mji wa New York, Paris, London, Accra, Lagos na Nairobi ilijengwa kwa jasho la wanadamu wafanyakazi wa bidii.

    Hawa binadamu wamefariki na kuondoka lakini miji ya starehe imebaki. Maisha yao ya kazi yanaweza kujumuishwa kama mchango wa maendeleo kwenye miji ya starehe ya dunia. Angalia, Shetani alimwambia Yesu alipomwonyesha mataifa ya ulimwengu huu

    Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.

    Luka 4:6

    Hili linatuonesha kuwa ni Shetani ambaye ana mamlaka dhidi ya miji ya hii dunia. Shetani ni mungu wa hii dunia (2 Wakorintho 4:4). Ni Shetani ndiye aliyewapa wana wa binadamu kazi ngumu na kuwaongoza kuijenga miji ya hii dunia.

    Wakristo hujiunga kirahisi na jeshi la wajenzi na kuchangia sehemu zao kujenga hii miji ya anasa.

    Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu. Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi. Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii. Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi. Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli. Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali:

    Kutoka 1:8-13

    Kama Farao alivyoitawala Misri, Shetani hutawala dunia na miji yake. Ndiyo maana kuhangaika na kuchanganyikiwa kwa dunia hii kunazidi kuongezeka kwa haraka kufikia kileleni kwake.

    Unapofanya kazi katika taasisi za kifedha, benki na taasisi nyingine za hii dunia, unaweza kufananishwa na Waisraeli walipofanya kazi kwa Farao; palikuwa na hali ngumu, mashaka na kutoka kwa jasho jingi kwa kuyajenga majengo ya muda mfupi.

    Musa aliomba kwamba watu wa Israeli wawe huru ili waweze kumtumikia Bwana. Yeyote mwenye shauku ya kuingia kwenye huduma ya muda wote anaomba kuondoka kutoka mfumo wa dunia. Huduma ya muda wote ni huduma kwa ajili ya Bwana! Ni kama kuondoka kabisa Misri kwenda jangwani kumtolea Bwana dhabihu na kumjengea maskani.

    Mungu anataka watu wake watumie muda wao kumjengea Maskani na kumuabudu.

    Bila shaka kukimbia mfumo wa dunia haitakuwa rahisi. Haikuwa rahisi kwa Musa na wana wa Israeli kuondoka Misri. Ilikuwa tu kupitia jitihada ndo hatimaye watu wa Mungu wakaondoka kwa Farao.

    Rafiki mpendwa, haitakuwa rahisi kuepuka kazi za kidunia. Kama ikitokea itakuwa ni kupitia jitihada pevu.

    Hatua Nne za Kumtoroka Farao

    Basi ilikuwa hapo FARAO ALIPOJIFANYA KUWA MGUMU ILI ASITUPE RUHUSA KUONDOKA…

    Kutoka 13:15

    Farao hakupendezwa kuwaacha wana wa Israeli waondoke kwa uhuru. Kuna hatua nne ambazo kila Mkisto anaweza kupitia ili kuingia katika huduma ya muda wote. Inakupasa kutambua kila hali pindi unapokumbana nazo

    Hatua 1: Farao hataki uache ajira yake.

    Farao akasema, BWANA ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui BWANA, WALA SITAWAPA ISRAELI RUHUSA WAENDE ZAO.

    Kutoka 5:2

    Farao anataka umfanyie kazi mpaka ufe. Anataka utoke jasho na kutaabika hadi ufe. Shetani anajua kwamba watu wengi hawatafikia umri wa kustaafu. Huwadanganya kufanya kazi wakitazamia kustaafu ambako kamwe hakutadhihirika.

    Hatua 2: Farao atakuruhusu umtumikie Mungu lakini anataka ubaki kwake.

    Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu NDANI YA NCHI HII.

    Kutoka 8:25

    Katika hatua hii inayofuata, Farao anakubaliana na baadhi ya shinikizo. Anakubali kwamba ni lazima umtumike Mungu lakini inakulazimu ubaki Misri. Ni lazima uendelee kujenga mapiramidi ya Farao. Aina hii ya huduma kwa kawaida huitwa huduma ya kawaida. Kumtumikia Mungu, lakini kuning’inia kwenye mfumo wa dunia wa kupata fedha!

    Farao atakupangia lini utaweza kwenda kanisani au lini hutaweza. Kwa vile upo katika himaya yake, unakuwa miliki yake na ataamua chochote unachofanya. Atakuamulia wakati gani

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1