Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana
Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana
Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana
Ebook73 pages3 hours

Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345422
Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana

Related ebooks

Reviews for Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ni Jambo Zuri Sana Kumtumikia Bwana - Dag Heward-Mills

    SURA YA 1

    Mtumishi wa Mungu ni Nani?

    Si lazima uwe mchungaji au mmisheni ili uwe mtumishi wa Mungu. Sisi sote tunajua kuwa makuhani, manabii, wainjilisti na wachungaji ni watumishi wa Bwana.Tunajua kuwa watu hao wamependelewa kuitwa watumishi wa Mungu Aliye Juu. Ni baraka kwao kumtumikia muumba wao. Hata hivyo, habari nzuri ni kuwa watu wengine ambao si watumishi wa injili ya Yesu Kristo, pia, wanaweza wakawa watumishi wa Mungu..

    Hakika, Biblia imejaa habari za watu ambao hawakuwa wachungaji lakini walikuwa watumishi wa Mungu. Mungu alisema ni watumishi wake na na ndivyo walivyokuwa.Baadhi ya watu hawa walikuwa wafalme, wanasiasa, wafanya biashara, matajiri wakubwa, wakulima na hata wasio Wayahudi.

    Ukweli kuwa watu wengine tofauti na makuhani na wainjilisti, kuitwa watumishi wa Mungu kuna matokeo chanya kwa kila mtu. Inamaanisha unaweza ukawa mtumishi wa Mungu! Mtumishi wa benki, mwanasheria, daktari, mwanasiasa, mfamasia na mtoza ushuru anaweza akawa mtumishi wa Mungu.

    Si lazima uwe katika huduma wakati wote ili uwe mtumishi wa Mungu. Unaweza ukawa unafanya kazi katika sekta yoyote na bado ukawa mtumishi wa Mungu.Ni muhimu kuwatambua watu wote ambao Mungu aliwatambua kuwa watumishi wake.

    Mtumishi ni mtu anayeyapeleka mapenzi ya Mungu kwa mtu mwingine. Mtumishi ni mtu anayeitumikia shauku ya mtu mwingine. Kuanzia sasa unaweza ukajichukulia kuwa mtumishi mtarajiwa wa Mungu.Mwanafunzi anaweza kuwa mtumishi wa Mungu! Mfanyabiashara anaweza akawa mtumishi wa Mungu! Mwalimu anaweza akawa mtumishi wa Mungu!Unaweza ukayabeba mapenzi ya Mungu pasipo kujali kazi yako. Kazi kuu unayoweza kufanya ni kuwa mtumishi wa Mungu.

    Si ajabu kwamba makuhani, Walawi na manabii wanaitwa watumishi wa Mungu. Ibrahimu, Isaka na Yakobo hawakuwa wachungaji lakini Mungu aliwachukuliwa kuwa watumishi wake. Ninajua kuwa unaweza kumfikiria Ibrahimu kama mchungaji.Lakini A brahimu hakuwa mchungaji. Alikuwa mtumishi wa Mungu tu. Pia ninajua kuwa unaweza kumchukulia Musa kama mchungaji. Hata hivyo, Musa alikuwa mkuu wa taifa la Israeli.Mungu alimwita Mfalme Daudi kuwa mtumishi wake. Hakika, wote wawili Musa na Daudi walikuwa wakuu wa taifa la Israeli na walikuwa watangulizi wa watu kama David Ben Gurion, Shimon Peres, Yitzhak Rabin, Ehud Barak, Ariel Sharon na Benjamin Netanyahu. Mkuu wa taifa si mchungaji. Mkuu wa taifa anaweza akawa mtumishi wa Mungu. Wote wawili, Musa na Daudi wanaweza wakawa watumishi wa Mungu. Hakikisha ya kuwa katika kila nafasi unayoipata, unakuwa mtumishi wa Mungu.

    Ayubu alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa mashariki.Kwa kuwa Ayubu alikuwa mtu wa Mashariki, pengine alikuwa Mchina, Mkorea au Mjapani. Ayubu alikuwa tajiri sana na bado aliitwa mtumishi wa Mungu. Mungu alidiriki hata kujivuna kwa ibilisi kuhusu Ayubu, mtumishi wake.Kwa mtazamo wa mbinguni, Ayubu alikuwa mtumishi wa Mungu. Leo hii, ni vigumu wafanyabiashara matajiri kumtumikia Bwana. Ikiwa wewe ni mfanyabiashara, unaweza ukawa kama Ayubu na ukawa mtumishi wa Mungu. Kitabu hiki kimeandikwa ili uwe mtumishi wa Mungu. Mungu anataka uwe mtumishi wake. Ningekushauri uwe mtumishi wa Mungu.Kuna faida nyingi kwa kuwa mtumishi wa Mungu. Na ndicho ambacho kitabu hiki kinaelezea! Amua kuwa mtumishi wa Mungu. Amua kwamba utaitwa mmoja wa watumishi wa Mungu. Ifanye mbingu ikuone kuwa mtumishi wa Mungu. Hebu tuangalie orodha ya kushangaza ya watu walioitwa watumishi wa Mungu katika Biblia.

    1. Makuhani na Walawi walikuwa watumishi wa Mungu.

    Na tazama, hizo zamu za makuhani na Walawi ziko, kwa utumishi wote wa nyumba ya Mungu; nao watakuwapo pamoja nawe kwa kazi ya kila namna, kila mtu mwenye hiari, aliye stadi kwa utumishi wowote; tena maofisa na watu wote watakuwa chini ya amri yako kabisa.

    1 Mambo ya Nyakati 28:21

    2. Manabii walikuwa watumishi wa Mungu.

    Nawe utawapiga nyumba ya Ahabu, bwana wako, ili nijilipize kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa BWANA, mkononi mwa Yezebeli.2 Wafalme 9:7

    Lakini maneno yangu, na amri zangu nilizowaagiza hao manabii, watumishi wangu, je, Hazikuwapata baba zenu? Nao wakatubu na kusema, BWANA wa majeshi ametutenda kulingana na njia zetu, na matendo yetu, kama alivyokusudia kutenda.

    Zekaria 1:6

    3. Ibrahimu, Isaka na Yakobo, wafanyabiashara wakuu, wote walikuwa watumishi wa Mungu.

    Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.

    Kutoka 32:13

    4. Yakobo, tajiri milionea, alikuwa mtumishi wa Mungu.

    Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Abrahamu, rafiki yangu; wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1