Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Siri ya Dhabihu
Siri ya Dhabihu
Siri ya Dhabihu
Ebook46 pages35 minutes

Siri ya Dhabihu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kila unapotoa sadaka yako iwe kwa yatima, wajane, kanisani au sadaka yoyote Yesu anakuwepo kusimamia mwenyewe binafsi bila kumtuma mtu kuhakikisha njinsi unavyotoa na kutumia sadaka yako kuyasoma na kufafanua maisha yako. Kumbuka kazi zingine alikuwa anawatuma wanafunzi wake kumwakilisha na mifano ipo mingi; alipotaka wakahubiri injili aliwatuma wawili wawili yeye akabaki mjini; alipotaka fedha ya kodi alimtuma Petro akavue samaki yeye alibaki mjini; walipofika mji wa Samaria aliwatuma kwenda mjini kununua chakula cha mchana yeye akabaki kisimani kuongea na mwanamke msamalia; walipomaliza kuhubiri aliwatanguliza wanafunzi wake kwenda ngámbo yeye akaenda mlimani kuomba.

Lakini wakati wa kutoa sadaka mambo yalibadilika; hakutuma mtu bali alikwenda kusimamia mwenyenye na kuangalia mmoja baada ya mwingine alivyokuwa akitoa sadaka. Hali hii inaonyesha siri kubwa ya kiroho ya sadaka yako katika ulimwengu wa roho. Kumbuka sadaka yako mbele za Mungu ni tendo takatifu na la rohoni kuliko watu wenavyofikiria. Sadaka sio tendo la kukamilisha mtiririko wa ibada bali ni tabia ya Mungu wetu na sisi watoto wake lazima tuishi maisha hayo.

LanguageKiswahili
Release dateSep 24, 2020
ISBN9781005666361
Siri ya Dhabihu
Author

Charles Nakembetwa Shamsulla

Charles Nakembetwa Shamsulla a author and preacher of Gospel of Jesus Christ. He is also the author of BWANA OKOA NDOA YANGU, YOU CAN EASILY KILL FEAR [CONQUERING FEAR FACTOR] and KUSHINDWA SASA BASI. He holds Masters Degree in Public Administration specializing in Human Resources Management.

Read more from Charles Nakembetwa Shamsulla

Related to Siri ya Dhabihu

Related ebooks

Reviews for Siri ya Dhabihu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Siri ya Dhabihu - Charles Nakembetwa Shamsulla

    SIRI YA DHABIHU

    Charles Nakembetwa Shamsulla

    Haki zote zimehifadhiwa@Charles Nakembetwa Shamsulla

    SIRI YA DHABIHU

    ISBN: …. Kimetolewa 2020

    na Charles Nakembetwa Shamsulla. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kutolewa, kutunzwa au kunakiliwa kwa muundo au kwa namna yoyote, iwe kwa elektroniki, kimakanika, kufotokopi, ku-rekodi au vinginevyo pasipo ruhusa ya maandishi ya mwandishi isipokuwa kutoa sehemu kama rejea katika kufundisho. Kwa taarifa na kibali unaweza kuwaasiliana na mwandishi kwa simu na email ifuatayo: +255-714008191

    Email:cshamsulla@gmail.com

    UTANGULIZI

    Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina ya hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi. Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili ndogo za fedha.

    Hapo Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, Kweli nawaambieni, mama huyu mjane maskini ametia katika sanduku la hazina kiasi kikubwa kuliko walichotia wengine wote. Maana wengine wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu alichohitaji kwa kuishi. (Marko 12:41-44).

    Kila unapotoa sadaka yako iwe kwa yatima, wajane, kanisani au sadaka yoyote Yesu anakuwepo kusimamia mwenyewe binafsi bila kumtuma mtu kuhakikisha njinsi unavyotoa na kutumia sadaka yako kuyasoma na kufafanua maisha yako. Kumbuka kazi zingine alikuwa anawatuma wanafunzi wake kumwakilisha na mifano ipo mingi; alipotaka wakahubiri injili aliwatuma wawili wawili yeye akabaki mjini; alipotaka fedha ya kodi alimtuma Petro akavue samaki yeye alibaki mjini; walipofika mji wa Samaria aliwatuma kwenda mjini kununua chakula cha mchana yeye akabaki kisimani kuongea na mwanamke msamalia; walipomaliza kuhubiri aliwatanguliza wanafunzi wake kwenda ngámbo yeye akaenda mlimani kuomba.

    Lakini wakati wa kutoa sadaka mambo yalibadilika; hakutuma mtu bali alikwenda kusimamia mwenyenye na kuangalia mmoja baada ya mwingine alivyokuwa akitoa sadaka. Hali hii inaonyesha siri kubwa ya kiroho ya sadaka yako katika ulimwengu wa roho. Kumbuka sadaka yako mbele za Mungu ni tendo takatifu na la rohoni kuliko watu wenavyofikiria. Sadaka sio tendo la kukamilisha mtiririko wa ibada bali ni tabia ya Mungu wetu na sisi watoto wake lazima tuishi maisha hayo.

    Kutoa sadaka kuna tafsiri ya kiroho zaidi kuliko kuwa ni tendo la kawaida. Sadaka yako sio kitu cha kuchezea na kuchukulia kwa wepesi; kumbuka Anania na Safisa walipochezea sadaka ilibidi wauwawe kanisani. Wengine watasema haiwezi kujirudia tena na kwamba lilikuwa ni tukio la mara moja tu; hapana. Kila andiko lafaa kwa mafundisho na kutuonnya makosa yetu. Biblia inasema wengine wanatembea wakiwa wamekufa kiroho: Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorintho 11).

    Sadaka yako ni jicho la rohoni na mwanga angavu wa kiroho kumfanya Yesu kuyasoma maisha yako bila kufika nyumbani kwako; alijua kiwango cha mali na utajiri wanaomiliki na kuwatangazia wanafunzi wake kupitia sadaka waliyotoa madhabahuni; Petro alijua Anania na Safira waliuza nyumba kiasi gani mara tu alipoleta kiasi kilichobaki kanisani bila wao kusema.

    Aliwaona waliotoa mabaki na wale

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1