Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Bwana Okoa Ndoa Yangu
Bwana Okoa Ndoa Yangu
Bwana Okoa Ndoa Yangu
Ebook153 pages2 hours

Bwana Okoa Ndoa Yangu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kuna matatizo mengi yanayokabili ndoa za watu wa Mungu katika siku za mwisho. matatizo na vikwazo unavyopitia katika ndoa yako ni mashambulio ya adui na shetani. mwenza wako sio sababu ya matatizo ya ndoa yako. Watu wengu wanawashambulia wanandoa wao kama sababu ya matatizo yanayokablia maisha yako ya ndoa. kitabu hiki kitakuonyesha kuwa umekosea kuwaza hivyo. Bwana Okoa Ndoa Yangu kitakufahamisha adui halisi wa ndoa yako na namna ya kukabiliana naye.

kitabu hiki kitakuonyesha namna ya kuwatambua walinzi wa ndoa yako na namna ya kuwatumia kurejesha matumaini ya ndoa yako yaliyopotea kwa muda mrefu. Nakukaribisha unaposoma.

LanguageKiswahili
Release dateNov 12, 2016
ISBN9781370265756
Bwana Okoa Ndoa Yangu
Author

Charles Nakembetwa Shamsulla

Charles Nakembetwa Shamsulla a author and preacher of Gospel of Jesus Christ. He is also the author of BWANA OKOA NDOA YANGU, YOU CAN EASILY KILL FEAR [CONQUERING FEAR FACTOR] and KUSHINDWA SASA BASI. He holds Masters Degree in Public Administration specializing in Human Resources Management.

Read more from Charles Nakembetwa Shamsulla

Related to Bwana Okoa Ndoa Yangu

Related ebooks

Reviews for Bwana Okoa Ndoa Yangu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Bwana Okoa Ndoa Yangu - Charles Nakembetwa Shamsulla

    Vita sio kwa ajili ya wenye nguvu bali wenye maarifa ya ki-Mingu wala mbio sio kwa ajili ya wanaojua kukimbia bali ni kwa wanaojua mbinu za Mungu watakaoshinda. Anza na ufahamu kabla ya kuingia vitani na kujua siri za vita ni kupata zaidi ya nusu ya ushindi. Waliopotea njia ni wale walijiaminisha kujua njia. Kujua siri kutakuondolea kuvuja jasho. Utapokea ushindi wako kwa urahisi na kwa ufanisi zaidi

    Siri ya ndoa ni ya Mungu mwenyewe. Katika kitabu cha mwanzo tunaona kusudi na mpango wa Mungu kuhusu ndoa. Ndoa ni familia ya Mungu na imeanzishwa kwa mpango na kusudi la Mungu. Utaona kuwa Mungu alifanya maandalizi makubwa sana kabla ya kuanzisha familia yake. Alifanya maandalizi ya kuumba bahari, mito, mabonde, wanyama, matunda na majani mazuri ya kondeni na hata kuweka bustani nzuri kwa ajili ya maandalizi ya kuanzisha familia yake. Hakuna bustani nzuri wala haitatokea bustani nzuri kama ile aliyoitengeneza Mungu pale Edeni. Mungu aliweka aina mbalimbali za matunda, ndege wazuri na hata mawe mazuri na madini kwa ajili ya familia ya mfalme Adamu na malkia Hawa. Hii ndio bustani maarufu ya vizazi vyote vya binadamu.Mungu akasema nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zako zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vema Mwanzo 1:12

    Baada ya kukamilisha maandalizi ndio mwishoni tunaona anawaweka wanandoa wa kwanza mashuhuri katika bustani ya Edeni, Adamu na Hawa, ili kuitunza bustani ya kifame. Tunaona jambo la kwanza lililomkera Shetani katika uumbaji wa Mungu sio wanyama wazuri, sio mito mizuri na madini ya utajiri aliyoweka Mungu katika bustani ya Edeni wala matunda na ndege wa kupendeza. Kilichomkera Shetani katika uumbaji wote wa Mungu ni ndoa ya mfalme Adamu na malkia Hawa. Mara baada ya ndoa ya kwanza kuanzishwa, Shetani akaanza kutafuta njia ya kuiangusha na kuudhalilisha mpango wa Mungu. Jambo hili linaonyesha tangu mwanzo kuwa adui wa ndoa yako sio mume wako wala mke wako, hata kama ana onekana anatabia za kushindikana. Na kama ilivyo kwa wanandoa wengi leo, tunaona wana ndoa wa kwanza waliposhambuliwa waliacha kumkabili adui yao namba moja ambaye ni Shetani na mawakala wake, wakaanza kushambuliana wao kwa wao. Adamu anasema ni huyu mwanamke uliyenipa ndiye kasababisha haya yote. Adamu akasema, Ni huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Mwanzo 3:12

    Sehemu kubwa ya matatizo ya ndoa yanazaliwa na kukuzwa na lawama na shutumu ya wanandoa wenyewe. Wanandoa wanashindwa kuona zaidi ya upeo wa kibanadamu unaowatenganisha wao na adui yao wa ukweli, yaani Shetani na mawakala wake. Katika sura hii tutakuwa tunazifunua na kuziangalia siri za Mungu kuhusu ndoa na namna Mungu alivyokusudia na kupangilia kuhusu taasisi ya ndoa. Daima mpango wa Mungu ni kukuona kukifurahia na kufaidi mafanikio na matunda ya ndoa yako. Ndoa za watu wa Mungu zinamtukuza na kumpa Mungu utukufu na sifa. Katika tafsiri rahisi kabisa ndoa ni sifa na utukufu kwa Mungu wetu. Katika kitabu cha ufunuo tunaona biblia inasema kuwa ndoa ni mfano wa bibi-harusi wa Mwana-Kondoo wa Mungu. Akaja mmoja wa malaika saba waliokuwa na vile vitasa vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule BIBI- HARUSI, MKE WA MWANA-KONDOO (nimeweka msisitizo) Ufuo 21:9

    NDOA NI ALAMA YA IBADA NA UTUKUFU WA MUNGU

    Siri kubwa ya kwanza ya ndoa ni kuurudisha na kuuonyesha utukufu, heshima na ibada kwa Mungu wetu. Ndoa sio suala la kutimiza mahitaji ya kimwili ya kuoa/kuolewa na kuwa na watoto tu, kama wengi wetu wanavyodhani. Ndoa ni moja ya ibada za kumtukuza na kumwabudu Mungu wetu. Kila unapoamka asubuhi na kuona ndoa yako inadumu katika amani na mafanikio, tambua kuwa Mungu anatukuzwa na kuabudiwa siku hiyo. Ndio maana biblia inasema kuwa ukikwazana na mwenza wako maombi yako yatazuiliwa mbele za Mungu, kwa sababu ndoa yenu inapopata ufa ibada ya ndoa inaharibika mbele za Mungu. Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema, KUSUDI KUOMBA KWENU KUSIZUILIWE (nimeweka msisitizo). 1 Petro 3:7

    Siri hii ni kubwa sana mbele za Mungu wetu. Ndoa ni alama ya utukufu na ibada ya Mungu na inatimizwa na wanandoa. Ndoa za watakatifu zinampa Mungu utukufu na kumwabudu kila siku na kila wakati katika muda wote wa uhai wa ndoa yao hadi watakapokufa na kurudi kwa Muumba wao. Kama ndoa inamtukuza na kumpa Mungu utukufu, maana yake ni kwamba ndoa ni utumishi mbele za Mungu wetu na wanandoa ni watumishi muda wote wanapokuwa katika ndoa yao.

    Suala la kufahamu ni kuwa utumishi huu wa ndoa ni nguzo imara inayoshikilia utumishi na huduma zingine katika nyumba ya Mungu. Tunasema ni nguzo kwa sababu, uimara wa ndoa ni mafanikio ya huduma zingine katika nyumba ya Mungu wetu. Hakuna mhubiri atafanikiwa hata angekuwa na upako kiasi gani kama maisha yake ya ndoa yatatikisika na kushambuliwa na adui. Hata ungefunga na kuomba na kuwa na imani ya kung’oa milima, kama maisha yako ya ndoa yameharibika huwezi kufanikiwa katika huduma. Upako wa kweli na mafanikio ya kwanza katika safari yako ya utumishi ni mafanikio katika taasisi ya ndoa. Mtu mwingine atasema mbona kuna watu wamefanikiwa na kuwa na utumishi bila kuwa na ndoa. Unachotakiwa kufahamu ni kuwa unaweza kukaa bila ndoa na ukafanikiwa au ukaachana na mwenza wako katika misingi ya biblia, yaani kuachana na kukaa bila kuoa au kuolewa hakuna tatizo na wala hutakuwa na hatia mbele za Mungu.

    Vilevile unaweza kuishi kama towashi au mwanamwali na kukaa bila kuolewa wala kuoa kama biblia inavyosema katika kitabu cha Mathayo mlango wa 19 mstari wa 12 na 1Wakorintho 7 mtari wa 25 na 26. Ukifanya hivyo hutakuwa na hatia mbele za Mungu. Ukiamua kukaa bila kuolewa wala kuoa huna hatia mbele za Mungu. Vilevile unaweza kuamua kuachana na mwanandoa wako kwa misingi ya biblia na usiwe na hatia mbele za Mungu, yaani baada ya kuachana huruhusiwi kuoa au kuolewa bali unaishi maisha ya utowashi au mwanamwali na kumtumikia Mungu, hapo hakuna hatia mbele za Mungu. Lakini mimi naongelea watu walio katika ndoa na ambao wanaishi maisha ya ndoa. Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini, naye amwoaye yule aliyeachwa, azini. Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo tangu tumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wapo matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Awezaye kulipokea neno hili na alipokee. Mathayo 19:12 Lakini, kama ukioa huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia…mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai, lakini ikiwa mumewe amefariki, yu huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye; katika Bwana tu. 1Wakorintho 7:28,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1