Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
Ebook105 pages1 hour

Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Neno la Kigriki LAIKOS linamaanisha "kutokuwa na ujuzi". Historia imetufundisha tena na tena kwamba mambo makubwa yamefanyika na watu "wasio na ujuzi". Jifunza, kupitia kitabu hiki cha kipekee cha Dag Heward-Mills, Nini kinatokea kama hakuna watu wa kawaida wakifanya kazi kanisani; namna ya kushirikisha mzigo na watu wa kujitolea na kwa nini tunapaswa kupambana kulinda huduma ya kiuchungaji ya kawaida.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781613958490
Laikos: Watenda Kazi wa Kawaida na Huduma
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Laikos

Related ebooks

Reviews for Laikos

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Laikos - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    LAIKOS: Mtu wa Kawaida

    Neno mtu wa kawaida limetokana na neno la Kigirki LAIKOS linalomaanisha kutokuwa na ujuzi.

    Historia inatufundisha kuwa vitu vikubwa vinaweza kukamilishwa na watu wasio na ujuzi. Ukitazama kwa haraka kwenye mafanikio ya watu wa kawaida utatiwa moyo kuwatumia katika huduma. Kupitia watu wa kawaida, roho zitaokolewa, mikutano mbalimbali ya nyumbani itaimarishwa, makanisa yatakua na kazi ya Mungu itastawi.

    Zifuatazo ni maana chache za neno mtu wa kawaida

    1. Mtu wa kawaida ni mtu wa hali ya kawaida

    2. Mtu wa kawaida ni mtu yeyote wa kawaida

    3. Mtu wa kawaida ni mtu wa mahali panapojulikana.

    4. Mtu wa kawaida ni mtu wa kawaida tu.

    5. Mtu wa kawaida ni mtu yeyote.

    7. Mtu wa kawaida mtu wa kila siku.

    9. Mtu wa kawaida ni mtu ambaye si mtaalamu.

    10. Mtu wa kawaida ni mtu asiye mjuzi.

    11. Mtu wa kawaida ni mtu asiye mbobezi

    12. Mtu wa kawaida ni mtu ambaye hana ujuzi

    13. Mtu wa kawaida ni mtu ambaye hana mafunzo.

    14. Mtu wa kawaida ni mtu ambaye hana cheti.

    15. Mtu wa kawaida ni mtu ambaye hana leseni.

    Mafanikio Makubwa katika Ulimwengu wa Kanisa

    1. Watu wa kawaida walikuwa nguzo za mabadiliko makubwa ya kanisa.

    Tafsiri ya Biblia ya Martin Luther katika lugha ya watu wa kawaida ilibadilisha dunia. Badala ya kuwa katika lugha ya Kilatini tu, Biblia ilifanywa iweze kupatikana kwa watu wa kawaida.

    Pindi ambapo watu wa kawaida walipokuwa na maarifa ya ufunuo mikononi mwao walibadilisha dunia. Kutambua kwamba wokovu unapatikana kwa watu wote kupitia neema ya Mungu waliinuka na kupigania kile tunachojua kama mabadiliko.

    2. Watu wa kawaida ni nguzo za kanisa kubwa la Kimethodisti.

    Katikati ya karne ya 20, Umethodisti ulikuwa ni dhehebu kubwa la kiprotestanti Marekani. Kanisa kubwa la Kimethodisti liliendeshwa migongoni mwa watu wa kawaida.

    Utamaduni wa mwanzo wa kuhubiri katika kanisa la Kimethodisti ilikuwa ni kwa Mhubiri wa kawaida kuteuliwa kuongoza huduma ya kuabudu na kuhubiri katika makundi ya makanisa iliyoitwa mzunguko au kundi dogo.

    Mhubiri wa kawaida alitembea au aliendesha farasi katika maeneo husika ya kundi dogo ya kuhubiri kulingana na mfumo uliokubaliwa na muda uliokubaliwa.

    Baada ya uteuzi wa wahudumu na wachungaji, huu utamaduni wa kuhubiri uliendelea na Wahubiri wa Kienyeji wa Methodisti wakiteuliwa na makanisa mbalimbali, na kisha wakikubaliwa na kualikwa na makanisa yaliyokaribu kama mhubiri wa ziada kwa anayehubiri kwenye lile kanisa au kama hayupo.

    3. Watu wa kawaida ni nguzo ya kanisa kubwa moja duniani.

    Moja ya kanuni za msingi ambazo kanisa la Yoido Full Gospel Church limejengwa, ni kanuni ya kufanya kazi na watu wa kawaida.

    Kanisa la Yoido Full Gospel Church, ilianzishwa na David Yonggi Cho na mama mkwe wake, Choi Ja-shil, wote wachungaji wa Assemblies of God, wakiwa na ibada ya kwanza tarehe Mei 15, 1958 pamoja na wasichana wengine wanne nyumbani kwa Choi Ja-shil.

    Washirika wa kanisa walifikia elfu hamsini katika mwaka 1977, idadi ambayo ilikuwa mara mbili kwa miaka miwili tu. Tarehe 30 Novemba 1981, washirika walifikia laki mbili. Kwa muda huu, lilikuwa dhehebu kubwa zaidi duniani na ilitambuliwa hivyo na jarida la Los Angeles Times.

    Mwaka 2007 washirika wake walikuwa 830,000, lenye huduma saba za Jumapili zinazotafsiriwa katika lugha kumi na sita.

    4. Watu wa kawaida ni nguzo za mtandao mkubwa wa kanisa linalochimbuka kutoka Nigeria na Ghana.

    Kanisa la Redeemed Christian Church of God lenye makazi yake Nigeria pamoja na Kanisa la Pentekoste lenye makao yake makuu huko Ghana yanajulikana sana kwa kuwatumia watu wa kawaida. Huduma hizi zote zina mtandao mkubwa wa makanisa na huwatumia watu wa kawaida kwenye mahubiri na kazi za kiuchungaji.

    Kanisa la Pentekoste lilianzishwa na James McKeon, Mmishonari kutoka Urusi aliyetumwa na Kanisa la Mitume (Apostolic Church), Bradford, UK kwenda hiyo nchi iliyoitwa Gold Coast.

    Limekua na likaweza kuwa na zaidi ya washirika milioni 1.7. Kanisa la Pentekoste lina zaidi ya makanisa 13,000 katika nchi 70 kila bara duniani.

    Mwaka 1952, Pa Josiah Akindayomi alianzisha Kanisa la Mungu la Wokovu wa Kikristo (Redeemed Christiian Church) huko Nigeria chini ya uongozi wa Msimamizi mkuu, Kaasisi E.A. Adeboye, limekua na likawa na makanisa katika nchi zaidi ya 140, na mamiliono ya washirika.

    Hakika, haya ni mafanikio makubwa na yamewezekana kupitia jitihada za watu wa kawaida.

    Mafanikio Makubwa katika Dunia ya Kawaida

    1. Mfumo Mkubwa wa Kidemokrasia wa serikali ulizaliwa kupitia watu wa kawaida.

    Demokrasia ni kuwapa watu wa kawaida nafasi ya kutenda na kubadilisha serikali kama wanapenda.

    Demokrasia ni uwezo wa mtu wa kawaida kukataa kuishi chini ya hali zisizokubalika.

    Demokrasia ni ushiriki wa mtu wa kawaida na ushawishi wake nchini.

    Demokrasia hujengwa juu ya kanuni ya nafasi sawa kwa watu wote wa kawaida.

    2. Taifa kubwa lenye nguvu lilizaliwa kupitia watu wa kawaida.

    Mapinduzi ya Marekani ni mfano mzuri wa nguvu za watu wa kawaida katika kutengeneza historia. Mtu wa kawaida alizaa taifa kubwa lenye nguvu. Mwishoni mwa karne iliyopita, Mapinduzi ya Marekani yalifanikisha jaribio ambalo liliweka mpito wa dunia iliyoongozwa na watu wachache kwenda kwenye dunia iliyoongozwa na watu wengi. Mapinduzi kwa kiasi kikubwa yalitengenezwa na shirika au vyama vidogo vya kimapinduzi kama vile Wana wa Uhuru (Sons of Liberty). Vyama hivi havikuongozwa na watu matajiri na watu wenye nguvu wanaomiliki ardhi bali watu wa kawaida wenye hadhi au uwezo wa kati waliokuja pamoja kupanda mibegu ya Mapinduzi.

    3. Ushindi wa kihistoria wa uchaguzi wa Barack Obama ulikuja kupitia watu wa kawaida.

    Mei 2008, Barack Obama, Rais mweusi wa kwanza wa Marekani, alishinda utenzi wa kidemokrasia ya urais wa Marekani. Ingawa matajiri wa nchi na wenye uwezo kidemokrasia walikuwa ni wafuasi wa Clinton na walitoa mamilioni ya dola, Obama alikusanya zaidi ya wagombea wengine wote wa urais katika historia kwa kutumia nguvu ya watu wa kawaida.

    Obama alikusanya zaidi ya dola milioni 80 katika kampeni yake, nyingi ambazo zilitoka kwa watu wa kawaida waliofanya michango midogo midogo.

    Sura ya 2

    Nini Kinatokea Kama Hakuna Watu wa Kawaida na Watu wa Kujitolea

    1. Kama huruhusu watu wa kujitolea wafanye kazi katika huduma utaua kanuni ya Ukristo ya kujitoa dhabihu kanisani.

    Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

    Mathayo 16:24

    Alama ya Ukristo ni msalaba. Msalaba huzungumzia mateso na kifo. Mungu alizungumza na Ibrahim na alimwambia atoe hazina yake kubwa - mtoto wake wa kiume. Usimsikilize yeyote anayekwambia

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1