Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mwongozi Wa Roho: Safari Maishani
Mwongozi Wa Roho: Safari Maishani
Mwongozi Wa Roho: Safari Maishani
Ebook171 pages4 hours

Mwongozi Wa Roho: Safari Maishani

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

”Nini Maana ya Maisha”?

Mwongozi wa Roho
LanguageKiswahili
PublisherTektime
Release dateSep 28, 2022
ISBN9788835444084
Mwongozi Wa Roho: Safari Maishani

Related to Mwongozi Wa Roho

Related ebooks

Reviews for Mwongozi Wa Roho

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mwongozi Wa Roho - Ken Luball

    Mwongozi wa Roho: Safari Maishani

    ––––––––

    Riwaya ya Kiroho na Ken Luball

    & Bodhi ( Mwongozi wa  Kiroho )

    ––––––––

    Translator: Samwel Lubisia

    Copyright Claimant: Ken Luball

    Ujumbe wa mwandishi:

    Nini Maana ya  Uzima?

    Maana ya uzima,

    Sababu tupo hai,

    Ni kumusikiliza kimya kimya kwa makini Roho  aliye ndani yetu ,

    Na kuifuata katika njia atakayotuongoza.

    Vipo vitabu vinne  katika Tetralojia ya Kuamka :

    Leo Naenda Kufa: Uchaguzi Maishani

    Mwongozi wa  Roho: Safari Maishani

    Utulivu: Kijiji Cha Matumaini

    Mauzauza ya Raha: Kuchagua Upendo badala ya Hofu

    Maisha ya kiroho ni hali ya ni kuamini  yuko Mungu (Roho au Nafsi) katika kila maisha,  na kwa sababu hii maisha ya kila mmoja ni muhimu , ni sawa na  yameunganishwa.

    Lengo langu la  kukiandika kitabu hiki  ni Kuwaamsha  na kuwasaidia wengine Walioamka, kuelewa kikamilifu maana  ya  Kuona Nuru, na kwa hivyo,  Safari yao katika Maisha inaweza kutambulika kikamilifu.

    Hadithi tatu zimeandikwa katika nafsi ya  kwanza, kufuatilia  safari ya Kiroho Maishani mwa mtoto. Wanapopata  mafunzo ya jinsi ya  kuyajibu maswali  hayo [niliyouliza mwanzo] kwa njia ya  kueleweka, kuvutia, na ya kipekee, ambayo  sio tu ya kufikirisha bali pia  kusisimua.

    Bodhi ni Mwongozi wangu wa Kiroho ; ananizungumzia kwa urahisi huku nikiandika mawazo yake. Japo safari yangu ya   Kuiona Nuru, haijakamilika, Bodhi, akiwa Mwongozi wa Roho, Bila Shaka  Amelimika. Tulikiandika kitabu hiki kwa ajili ya  wote wanaotaka kuianza safari ya Kuamka  au Wameamka na wanatafuta njia ya  Kuiona Nuru

    Ni kwa upendo tu na msaada wa Bodhi

    tuliweza kuviandika vitabu hivi kwa pamoja

    Japo Mwongozi Wa Roho ni hadithi ya kubuni, ningependa ufikirie hili, kwa kuwa Bodhi alikuwa mhusika mkuu kwangu pamoja na Amara katika kitabu hiki, Mwongozi wa Roho. Yamkini hadithi inayosimuliwa huenda isiwe ya kubuni, ila iliyo halisi. Kwa kuwa hadithi hii nilisimuliwa  na Bodhi,  alivyokuwa Mwongozi wa Roho hapo awali kwa Amara, nadhani uwezekano wa kila kitu anachosema, na onyo anazojaribu kuwasilisha, ni halisi na  kweli, hadithi hii inaweza kuwa kweli pia.

    Ili kujua mengi kuhusu vitabu vyote vinne katika Tetralojia hii katika wavuti wangu http://kenluball.com .

    Dibaji:

    Hatua Tatu za Kuona Nuru

    Hatua ya kwanza – Usingizi (Kulala)

    Hatua ya kwanza huanza tunapozaliwa,

    Tunapojumuishwa na Kufunzwa tunayofaa

    Kuamini (Ego) tunavyoendelea kuyaona na Kukubali mengi kutoka kwa  jamii tulivyozaliwa kwayo.

    Tunapozaliwa, picha iliyopo hapo juu  inaonyesha  kwamba

    Utambulisho wetu tayari hua umeamuliwa.

    Rangi ya ngozi yetu, nchi  tunayozaliwa, Dini na ulinganisho mwingine wowote ulioundwa na binadamu

    Huamua mustakabali wetu ulimwenguni.

    Tunaamini ulinganisho huu ni wa kweli  kwa kuwatazama wengine,

    Kusoma kuwahusu kwenye vitabu na  magazeti na  kuwatazama katika Runinga na Filamu.

    Watu wengi hukubali tofauti  hizi na kuzifanya  sehemu yao,

    Au wanaenda zaidi  kudhibitisha

    Kwamba  wao ni bora na wa maana zaidi kuliko wengine.

    Wanaoyakubali na  kuyaamini wanayofunzwa

    Kuwa ya kweli, hubakia  wamelala licha ya mafaniko yao Maishani, hatima yao ni maisha duni ya kiwango cha chini sana.

    Wanaamini  furaha na maana itatoka ulimwenguni,

    Kamwe haiwezi [kutoka ulimwenguni].

    Hatua Ya Pili –Kuamka

    Wanaoamka huanza  kudadisi kila Tulichojifunza na  Kukubali kuwa halisi na kweli maishani Tulipokuwa  tukikua wakubwa.

    Wale ambao Huamka huanza kudadisi ikiwa kila kitu Tulijifunza Na Kukubali kuwa halisi maishani, tulipokuwa tukikua, ilikuwa kweli.

    Hisia inaanza kukua ndani yetu, Haiwezi kupuuzwa tena,

    Kuhoji uhalisia wa Kila kitu tulichoamini hapo awali.

    Ingawa  tunaweza kuwa tunaishi maisha yenye Mafanikio, tuna utajiri, tuna umaarufu, Au ulinganisho mwingine wowote wa Kujifunza kuhusu Mafanikio ni nini, Haiondoi tena hisia za wasiwasi tulonazo

    Zinatoka Ndani yetu.

    Uchungu tunaohisi unatoka kwa Roho wetu, aliye maishani mwa kila kitu.

    Wengine wanaweza kumwita Roho Mungu/Nafsi hai au kumpa jina lingine; haijalishi.

    Inawakilisha Mwongozi wetu maishani na huyapa maisha yetu Maana.

    Tunaamka pindi tu  tunapohisi kuna jambo lisilo sawa,

    Tunaanza kudadisi kama yote tulojifunza na kukubali kuwa kweli huenda  hayakuwa kweli,

    Basi hatuna budi  kuianza safari yetu,

    Safari ya Kuona Nuru.

    Hatua Ya Tatu – Kuona Nuru.

    Tunaelimika pindi Tunapokubali

    Kwamba kila jambo tulojifunza na Kuamini kuwa kweli  hakika  haikuwa kweli.

    Licha ya jinsi  Tunavyoonekana, Mali yetu, Kazi, Vitu tunavyomiliki

    Au mengine yote  tuliyofunzwa yanatofautisha na wengine, tunang'amua sasa kwamba  hatuko bora au wa maana  zaidi  kumliko yeyote.

    Tunaanza Kuiskia Roho  aliye ndani mwetu, Tunaukumbatia ujumbe wake kwa kushiriki Upendo Wetu bila Masharti na wote.

    Japo tuliyojifunza (Ego)  tukiwa wadogo  daima inasalia nasi,

    Ushawishi wake hubaki finyu.

    Badala ya  kushindana, sasa tunashirikiana.

    Badala  ya  kuishi  kwa hofu, tunaazimia kuishi kwa upendo.

    Badala ya  kutamani yaliyo bora kwa ajili yetu tu,

    Sasa tunatamani kuwasaidia  wengine  bila  ubinafsi,

    Kurahisisha safari yao maishani.

    Kwa madiliko na Kukubali ujumbe wa  Roho tunaendelea  kuifuata njia yetu  ya Kuona Nuru.

    Table of Contents

    Sura Ya 1: Kusudi Langu Maishani

    Sura Ya 2: Roho Azaliwa

    Sura Ya 3: Nafsi Yazaliwa

    Sura Ya 4: Nafsi Nzuri

    Sura Ya 5:Uhusiano wa Roho na Nafsi

    Sura Ya 6: Kutawaliwa na Nafsi.

    Sura Ya 7:Miaka Mitano Ya Kwanza Maishani

    Sura Ya 8:Kuishi Maisha Chanya

    Sura Ya 9:Kuishi Katika Ulimwengu wa Mwanga

    Sura Ya 10: Mafanikio Maishani ni Nini?

    Sura Ya 11: Vijimambo vidogovidogo Visikutoe Roho

    Chapter 12: Happiness and Love

    Sura Ya 13:Maisha Ulimwenguni kote

    Sura Ya 14:Mafunzo Maishani

    Hitimisho: Safari ya mwandishi (Ken) maishani

    Kumhusu Ken

    Sura Ya 1:

    Kusudi Langu Maishani

    N

    itakutambia hadithi tofauti na yoyote ambayo umewahi kusikia hapo awali. Hadithi hii itasimuliwa na "Mwongozi wa Roho", ambaye,  katika Safari hii Maishani, yupo ndani ya msichana mdogo anayeitwa Amara, jina ambalo lina maana ya milele katika lugha ya kale ya Sanskrit ya India. Hadithi hii itafuata maisha yake, tangu wakati yeye ni kijuzi tu ndani ya mamake, hadi kifo chake miaka mingi baadaye. Hadithi yenyewe nitakusimulia mimi, ambaye ni Mwongozi wake wa Roho; jina langu ni "Bodhi".

    Nina uhakika una hamu ya kujua zaidi kidogo kunihusu, hivyo kabla nianze hadithi yangu, nitajieleza kidogo. Jina langu ni "Bodhi, ambalo katika lugha  ya Sanskrit humaanisha Kuamka au Kuona Nuru." Nimekuwa Mwongozi wa Roho kwa muda wote wa maisha; Viongozi wa Roho ni wa milele. Kusudi Langu Maishani ni kusaidia kiumbe hai katika Safari yake Maishani, kwa kushiriki maarifa yangu nao. Kwanza najiunga na maisha kabla hawajazaliwa nabaki ndani yao, katika Safari yao Maishani, hadi wanapoiaga dunia.  Ninaponza, niko hapa kumsaidia Amara. Kusudi langu ni kushiriki naye maarifa ya maisha, ili aweze kupata Maana, Kuelewa na Upendo usio wa Masharti  maishani mwake. Mwongozi wa Roho ni nguvu  na msukumo uliopo katikati ya maisha; kwa Amara, kama ilivyo kwa wengine wengi, nitakuwepo ndani ya Moyo wake. Ndani ya nguvu yangu, yapo maarifa  mengi ya historia ya ulimwengu. Hekima yote, ya milele, ipo ndani yangu, kama ilivyo ndani ya kila Mwongozi wa Roho. Sababu yangu kuwepo, katika Safari hii Maishani, ni kumsaidia Amara kuelewa kusudi la maisha yake. Niko hapa ili ajifunze kutoka kwangu na ashiriki haya na wengine; kwa kushiriki Kiini changu na Upendo wangu na wengine bila ubinafsi, maisha yake  yatakuwa yamekamilika. Atazaliwa na maarifa yote atakayohitaji kuishi maisha ya furaha, yenye maana; atazaliwa "Amelimika". Hii ndiyo sababu kila Mwongozi wa Roho yupo, na Safari yetu Maishani itafanikiwa tu ikiwa tunaweza kutimiza hili ili tuweze kuyapa maana maisha ambayo tupo kusaidia.

    Amara atakiandika kitabu hiki muda mfupi kabla ya kuaga dunia, miaka mingi baada ya kuzaliwa. Hadi wakati huo, mara nyingi alishindwa kusikia mawazo yangu vizuri. Kila mmoja ana Mwongozi wake wa Roho, hivyo unaweza kufikiria jinsi  tulivyo wengi. Kwa kuwa Mwongozi wa Roho hajawahi kuandika kitabu kamwe, nadhani ni muhimu kukujulisha kwanini nachukua hatua hii isiyo ya kawaida. Ninaelewa jinsi ilivyo vigumu kuamini ninachokuambia; hata hivyo, singewahi kamwe kujitambulisha na kukiandika kitabu hiki, kwa msaada wa Amara, kama haingebidi kabisa.

    Niko hapa kukuonya. Mabadiliko yasipokuja haraka, maisha yote  katika sayari hii yanaelekea kikomo. Pupa, inayowakilishwa na tamaa iliyokithiri kwa wengi  ili wapate utajiri, imesababisha vita, chuki, hofu, njaa, ukosefu wa makazi, dhana sisizo za  uhakika, mabadiliko ya Tabianchi, vifo visivyo na maana na mengine mengi; haya yote yanatishia maisha. Vitisho vingi vinavyoweza kuleta mwisho wa haraka wa maisha ni sababu moja tu ya kitabu hiki kinaandikwa. Pia kinaandikwa kukujulisha jinsi janga hili linaweza kuepukika. Dunia iko kwenye ukingo wa hali ya hatari sana. Ingawa muda unakimbia na kuisha vilivyo, hatujachelewa sana kubadilisha athari inayotukodolea macho. Ili kufanya hivyo, hata hivyo, ni

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1