Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji
Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji
Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji
Ebook258 pages3 hours

Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Hakika hiki ni kitabu cha ukaribisho. Askofu Dag Heward- Mills, yeye mwenyewe akiwa mchungaji pia, anaelezea ni kwa nini na jinsi gani unaweza kuifanya huduma ya uchungaji iwe bora zaidi.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613953877
Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji

Related ebooks

Reviews for Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Badilisha Huduma yako ya kiuchungaji - Dag Heward-Mills

    Sura 1

    Kwa Nini Uepuke Huduma ya Bandia

    Katika Agano la Kale, huduma halisi iliwakilishwa kwa dhahabu hekaluni.  Kila kitu muhimu hekaluni kilipakwa dhahabu halisi. Mungu alitoa mchoro wa jengo la hekalu kwa Musa.

    Bwana akanena na Musa, akamwambia, Waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka… Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Nawe fanya kiti cha rehema cha dhahabu safi… Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema…

    Kutoka 25:1, 2, 8, 17, 21, 22

    Hivi ndivyo Mungu alivyotaka Hekalu lake lifanane. Hakuna mtu aliye na haki ya kuanzisha aina zake mwenyewe kwenye mpango mkuu wa Mungu. Wakati Mfalme Sulemani alipojenga hekalu, alifuata mpango wa Mungu halisi.

    Na ndani yake chumba hicho cha ndani mlikuwa na nafasi, mikono ishirini urefu, na mikono ishirini upana, na mikono ishirini kwenda juu kwake; akaifunika na DHAHABU safi. Akaifunika madhabahu nayo kwa mwerezi. Hivyo Sulemani akaifunika nyumba ndani kwa DHAHABU SAFI. Akaitenga kwa mikufu ya DHAHABU mbele ya chumba cha ndani; akapafunika na DHAHABU. Akaifunika nyumba yote kwa DHAHABU, hata ilipokwisha nyumba yote; tena madhabahu yote iliyokuwa ya chumba cha ndani akaifunika kwa DHAHABU. Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono kumi. Akayafunika makerubi kwa DHAHABU... Na sakafu ya nyumba akaifunika na DHAHABU ndani na nje.

    1 Wafalme 6:20-23, 28, 30

    Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Bwana; madhabahu ya DHAHABU, na ile meza iliyokuwa na mikate ya wonyesho juu yake ilikuwa ya DHAHABU; na vinara vya taa, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vya DHAHABU safi; na maua, na taa, na koleo ya DHAHABU; na vikombe, na makasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya DHAHABU safi; na bawaba za DHAHABU, za milango ya nyumba ya ndani, yaani, patakatifu pa patakatifu, na za milango ya nyumba, ndiyo hekalu.

    1 Wafalme 7:48-50

    Miaka mingi baadaye, mfalme mwingine aliweka shaba nyeupe mahali pa dhahabu. Shaba nyeupe huonekana kufanana sana na dhahabu. Iko karibu sana na sambamba, lakini sio dhahabu. Mfalme Rehoboamu alileta shaba nyeupe kwenye nyumba ya Bwana. Iliweza kuonekana kama kitu halisi lakini Mungu hakupendezwa nayo. Shaba nyeupe ni mchanganyiko wa shaba na zinki. Katika hali halisi, shaba nyeupe in tofauti kabisa na dhahabu halisi! Watu wengi hudanganywa wakati kitu bandia kichukuapo mahali pa kitu kilicho halisi! Hii ndio sababu naandika kitabu hiki.

    Basi Shishaki mfalme wa Misri akapanda juu ya Yerusalem akazichukua HAZINA za nyumba ya BWANA, na hazaina za nyumba ya mfalem, akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozifanya Sulemani. Mfalme Rehoboamu akafanya ngao za SHABA mahali pake, akawabidhi wakuu wa walinzi waliongoja malngoni pa nyumba ya mfalme

    2 Mambo ya Nyakati 12:9-10

    Kupitia kitabu hiki, ninataka kukusaidia kuweka dhahabu kanisani. Usiweke kitu chochote mahali pa huduma halisi ya Kibiblia. Kama ilivyo kwa taaluma nyingi, kiuhalisia walei hawajui kile mtaaluma afanyacho. Kwa mfano, kiuhalisia walei hawajui kile rubani au daktari afanyacho. Ni muhimu kwa mtu yeyote anayeingia kwenye huduma kutambua kuwa inahusu nini hasa!

    Natambua kuwa watu wengi wanapenda kuunda matumaini hewa kwa kile wakifanyacho. Wanafanya hivi kusheheneza taswira yao ndani ya taaluma. Hata hivyo, Bwana amenisihi kukufundisha zile zilizo kazi hasa za mchungaji. Katika  kitabu hiki, sitajaribu kupitia kila kitu kinachohusu kazi ya mchungaji. Naenda kukushirikisha mambo makuu tu.

    Ni maombi yangu kuwa utaamini katika urahisi wa huduma. Natambua kuwa mara nyingi watu hupendelea mafundisho magumu badala ya kweli rahisi. Wanajisikia kuwa kadiri ujumbe unavyokuwa mgumu ndivyo unavyoonekana kuwa umetoka kwa Mungu. Lakini kweli zilizo kuu mara nyingi ni rahisi kwa mtu wa kawaida kuzielewa.

    Katika Kitabu cha Matendo ya Mitume, Petro na mitume wengine walifika katika njia panda ya huduma. Katika njia panda hiyo, walipaswa kuamua ni mwelekeo upi wauchukue. Walipaswa kuamua kama wanaenda kuwa watumishi halisi au watawala wa kidunia. Lakini walichagua huduma halisi!

    Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi KULIACHA NENO LA MUNGU NA KUHUDUMU MEZANI. Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; Na SISI TUTADUMU KATIKA KUOMBA NA KULIHUDUMIA LILE NENO.

    Matendo ya Mitume 6:2-4

    Ni lazima uweze kutofautisha kati ya huduma halisi na huduma bandia. Huduma bandia si kitu halisi! Kama ilivyo shaba nyeupe, ambayo ni mbadala hafifu wa dhahabu, unakaribiana na uko sambamba na kitu halisi. Kuna mambo mengi yanayoonekana kama huduma halisi, lakini sio.

    Kwa mfano, kuwa mtawala wa kanisa hukufanya ujishughulishe sana na huduma. Wachungaji wengi kwa kweli ni watawala. Wanaonekana kuwa na shughuli nyingi ndani na katika mazingira ya ofisi za kanisa. Kisaikolojia, wanajisikia kuwa wanamfanyia kazi Mungu. Hata hivyo, dunia nzima imo ofisini na hutumia kompyuta. Watu  huonekana kuwa na jambo muhimu la kufanya tangu saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni kila siku. Wanaenda huko kama makatibu, walinzi, wataalamu wa komputa na kadhalika. Kama mchungaji haonekani kufanya kitu kinachofanana na hicho, hujisikia hajaajiriwa. Nimekuwa na watu wakinipigia simu nyumbani kwangu saa kumi na moja alifajiri. Watauliza kama bado nimelala. Wanadhani kuwa mchungaji hulala wiki nzima.

    Wapendwa watumishi wa Injili, msivutike na maoni ya watu. Msifuate mashinikizo ya kidunia. Ni mfalme wa nguvu za anga ambaye hutawala na kuiongoza dunia. Kila kitu duniani hutawaliwa na nguvu za ulimwengu wa Roho. Shetani ni kiumbe mwerevu na ameudanganya ulimwengu wote. Lakini udanganyifu huu haupaswi kuja kanisani.

    Ambazo mliziendea zamani, kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi…

    Waefeso 2:2

    Ulimwengu umedanganywa kwa kufikiri kuwa hakuna maisha baada ya kifo. Kula, kunywa na ufurahi kwa kuwa kesho utakufa! Utakapo kufa unakufa kama mbwa! Mbingu iko duniani na jehanamu kio duniani! Maisha ni vile utakavyo wewe yawe! Misemo hii tata imewaathiri watu wengi sana kuishi maisha yao wakifukuzia kupata fedha na starehe.

    Wakati aina hii ya kufikiri iingiapo kanisani, watu huhisi kwamba vitu vya kidunia (visivyo vya kiroho) ndivyo vilivyo muhimu. Hata wachungaji wako chini ya mbinyo kununua kompyuta na kukaa ofisini kama mtu mwingine yeyote. Lakini sisi si mtu mwingine yeyote! Sisi ni wachungaji wa kundi la Mungu!

    Wachungaji ni watu wachafu wanaoishi miongoni mwa kondoo. Wachungaji ni watu watoao maisha yao kwa ajili ya kondoo. Mchungaji siyo mtendaji [ofisa] mwenye kiti cha kuweka mikono.

    Unapotamka kuwa kazi yako ni maombi, ghafla unaonekana wa ajabu! Maofisa wa serikali wana ujasiri wa kupendekeza kuwa kanisa litumie muda wake kufanya mambo mengi yenye kuzaa matunda.  Kweli! Kipi chenye kuzaa matunda zaidi kuliko maombi! Kwa nini tuwasikilize wasioamini kutueleza sisi jinsi ya kufanya kazi zetu? Kwa nini watu wasio wacha Mungu walifundishe kanisa kazi zake?

    Kanisa limekuwa katika mbinyo mkubwa kiasi kwamba watumishi wengi wamekaa kando ya Agizo Kuu. Agizo Kuu ni maelekezo makuu kutoka kwa mkuu wa kanisa.

    Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari!

    Mathayo 28:19, 20

    Jisomee mwenyewe!  Ni suala lililo wazi! Hakuna utajaji wa kazi za kijamii, kiafya au kielimu. Afya na elimu vyaweza kuwa ni matokeo ya ziada ya Agizo Kuu lakini matokeo ya ziada hayapaswi kuwa matokeo makuu.

    Leo, sehemu kubwa za kanisa ni hospitali, shule, taasisi za misaada na vilabu vya kijamii. Hiki si kitu kilichotegemewa! Utagundua kuwa taasisi za afya za kidunia na taasisi za elimu za kidunia haziweki kando kazi zao na kuhubiri Neno la Mungu! Shetani huchekelea akiridhika  wakati watumishi wa Injili wajibadilishapo kuwa wanasiasa, wafanyakazi wa mambo ya kijamii na wafanyakazi wa afya.  Mahali pa dhahabu ya huduma pamechukuliwa na shaba nyeupe!

    Mwelekeo huu hujipenyeza hadi kwa Mkristo wa kawaida. Siku moja, mwanafunzi kijana aliniletea taarifa kutoka chuo kikuu.

    Alisema, Mchungaji, Mungu anatembea chuoni!

    Nilisema, Kweli, kipi kinachotokea?

    Alisema, Mungu anafanya kazi!

    Hivyo nikauliza, Kwa namna gani Mungu anatembea? Anafanya nini?

    Aliniambia, Watu wanafaulu mitihani yao!

    Alinifanya nifikiri. Mitihani?

    Ingawa sikusema hilo kwa sauti, nilifikiri mwenyewe, Wakati Mungu atembeapo, watu hupata kuokolewa na kujazwa na Roho. Kufaulu mtihani ni baraka kutoka kwa Mungu lakini si utembeaji wa Mungu. Hebu tusichanganyikiwe juu ya kazi ya Mungu. Hebu tuelewe kile Biblia ifundishacho juu ya huduma. Hebu tusifanye kosa la kuweka shaba mahali pa dhahabu. Hebu tuepuke hukumu ya Rehoboamu kwa kuleta dhahabu tu ndani ya hekalu.

    Ni maombi yangu kuwa kadri usomavyo kitabu hiki utaelewa kile wachungaji, wazee na viongozi wa kanisa hupaswa kufanya. Ni wakati wa kuondokana na huduma bandia. Hatuwezi kukuharakisha kurudi kwa Bwana Yesu Kristo kwa vitu vionekanavyo kama vitu halisi kumbe sio.

    Sababu Tatu

    Kwa ufupi, hizi ni sababu tatu kwa nini tunapaswa kuepuka huduma bandia:

    1. Kanisa ndiyo taasisi pekee ambayo imepewa kazi ya kuhubiri Injili na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi. Hakuna mwingine yeyote atakayefanya kazi yetu kwa ajili yetu!

    2. Hatupaswi kujaribu kuifurahisha dunia kwa kufanya mambo ambayo wanatutaka sisi tuyafanye. Mungu ndiye aliyetuita na yeye ndiye tunayepaswa kumfurahisha.

    3. Twaweza tu kumshinda Shetani na watendakazi wenziwe kwa huduma halisi! Huduma bandia haina nafasi katika vita hii kuu ya wakati wa mwisho.

    Nina kanuni ndogo ambayo itakusaidia wewe na mimi kukumbuka wajibu mnyenyekevu wa mchungaji aliyewekwa wakfu na Mungu. Na inakwenda namna hii: M kwa Maombi, T kwa u-Tembeleaji, F kwa u-Fundishaji (ushauri na uhubiri), na H kwa ma-Husiano (MTFH).

    Sura 2

    Jinsi Uwezavyo Kufikia Ubora katika Huduma

    Unaweza kufikia ubora katika huduma! Huduma yako siyo lazima iwe ya kawaida. Hata hivyo, unapaswa kutambua kuwa ubora ni lazima ufikiwe kwa vipimo vya Mungu, na siyo vipimo vya kibinadamu. Katika sura hii fupi, nataka kukuonesha funguo nne ambazo zilileta ubora katika huduma ya Yesu.

    Yesu Kristo ni kielelezo kikuu kwetu sisi sote. Ametolewa kwetu ili tuweze kuona namna

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1