Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ukuaji Wa Kanisa
Ukuaji Wa Kanisa
Ukuaji Wa Kanisa
Ebook297 pages8 hours

Ukuaji Wa Kanisa

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Ni nini jukumu kuu la mchungaji? Je, ni kufanya mazishi na kusimamia harusi? Kamwe sio! Haya ni majukumu ya mtumishi lakini sio majukumu kuu. Ikiwa utumishi wako umezorota hadi majukumu yako kuu ni kuendesha harusi na kuzika watu, basi unafaa kusoma Biblia yako tena! Jukumu kuu la mtumishi ni kutimiza Utume Mkuu.

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613954010
Ukuaji Wa Kanisa
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Ukuaji Wa Kanisa

Related ebooks

Reviews for Ukuaji Wa Kanisa

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

2 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ukuaji Wa Kanisa - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Ukuaji wa Kanisa na Shauku Inayochoma

    Pasipo maono…

    Mithali 29:18

    Je, Maono Kwa Hakika Yanafanya Kanisa likue?

    Miaka mingi iliyopita, nilisoma gazeti la Yonggi Cho kuhusu jinsi ilivyokuwa muhimu kuwa na maono na ndoto kwa ajili ya Ukuaji wa Kanisa. Sikujua kwa nini na kwa jinsi gani jambo hili lilikuwa ni la lazima kwa ajili ya Ukuaji wa Kanisa.

    Dr. Yonggi Cho, mchungaji mwenye kanisa kubwa kuliko yote duniani na mwenezaji wa dhana ya Ukuaji wa Kanisa, alisema kitu kingine ambacho sikukielewa. Alisema hivi, Maono yako hukutengeneza. Huwezi kuyatengeneza maono yako. Pia sikulielewa jambo hili.

    Kwa uaminifu kabisa, Nilichukulia kwamba jambo la kuwa na maono kila wakati lilitajwa kama kiwango cha kuanzia kwa mafundisho yote juu ya uongozi.

    Kadri nilivyowasikiliza watu wakifundisha kuhusu umuhimu wa kuwa na maono, kuorodhesha malengo, n.k., bado sikuelewa jinsi maono hayo yanavyoleta Ukuaji wa Kanisa.

    Kila mchungaji ambaye alihudhuria makongamano ya Ukuaji wa Kanisa alionekana akiwa amejaa maono na shauku kwa ajili ya Ukuaji wa Kanisa.

    Niliwaza mwenyewe, Wachungaji wote wana shauku ya kukua kwa makanisa yao, lakini makanisa yao yako vile vile, hayakui. Kama shauku na maono vingekuwepo vitu ambavyo ndivyo vingefanya kanisa likue, basi kila kanisa lingekuwa kubwa!

    Maono Yako Lazima Yawe Maono Yanayochoma

    Kadri miaka ilivyoenda, ndivyo nimegundua kwamba maono uliyo nayo lazima yawe maono yanayochoma. Huwezi kuwa na maono ya juu juu kwa ajili ya kuwa na kanisa kubwa. Maono ya juu juu hayawezi kulifanya kanisa lako likue hata kidogo. Maono lazima yakutafune kwanza na kukuchoma ndani ya nafsi yako. Kisha, kila kitu alichosema Dr. Cho ndipo kitakapotokea. Maono yale yanayochoma yatakufanya uwe mchungaji wa kanisa kubwa hasa.

    Kukosekana kwa maono hayo yanayochoma kwa ajili ya kuwa na kanisa kubwa, kwa hakika hakutakuwepo na Ukuaji wa Kanisa lililo halisi.

    Jinsi gani maono yanayochoma yanavyosababisha Ukuaji wa Kanisa? Ni kwa njia ya uvuvio na kuongozwa katika njia ngumu ya kuelekea kwenye Ukuaji wa Kanisa halisi, njia ambayo hakuna mwanadamu yeyote anayeiweza.

    Maono Yanayochoma Huwa ni Zana Isiyoonekana kwa Ukuaji wa Kanisa Lote

    Ni safari ndefu na yenye kona kona ya mtu kuwa mchungaji mwenye kanisa kubwa.

    Maono yanayochoma na ndoto ni zana isiyoonekana ambayo inamwongoza mtumishi katika safari hiyo ya kutoka kuwa mchungaji wa kanisa dogo hadi kuwa mchungaji wa kanisa kubwa.

    Baadhi ya wachungaji hawana zana hiyo ya ndani ambayo inahitajika, kwa kuwafanya watu wafanye mambo mengi mazito na magumu yaliyo ya lazima, kwa ajili ya Ukuaji wa Kanisa.

    Ushawishi wa Nje Hautakufanya Uwe Mchungaji Mwenye Kanisa Kubwa

    Hakuna ushauri wa nje au wa ndani unaoweza kumtosheleza mtu mmoja kumpeleka katika njia hiyo ngumu ya kuwa mchungaji mwenye kanisa kubwa. Ushawishi wote wa kutoka nje utafifilia mbali hata kabla hujawa mchungaji mwenye kanisa kubwa. Ushauri wa nje, kutiwa moyo na mawaidha mbalimbali, vinadumu kwa muda mfupi sana, wala haviwezi kusababisha mtumishi yeyote wa Injili aendelee katika njia ile ngumu ya Ukuaji wa Kanisa.

    Jinsi Maono Yanavyoweza Kukufanya Ufanye Mambo Mbalimbali

    Kuna jambo amabalo maono yanayochoma na ndoto hufanya kwako na jambo hilo hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kulifanya kwa ajili yako.

    Ili kuwe na hali ya Ukuaji wa Kanisa, maono ya ndani yanayochoma na ndoto hukufanya uwe mnyenyekevu hata uweze kufanya mambo yote unayolazimika kuyatenda.

    Maono yanayochoma na ndoto ya kanisa kubwa hukufanya uombe sana kwa ajili ya Ukuaji wa Kanisa. Bila kuwa na maono yanayochoma na ndoto, huwezi kuomba vya kutosha kuvuta usikivu wa Mungu.

    Maono yanayochoma na ndoto ya kuwa na kanisa kubwa hukufanya utafute hekima na mikakati inayohitajika kwa Ukuaji wa Kanisa. Bila kuwa na maono yanayochoma na ndoto, hutatumia muda unaohitajika kwa ajili ya kutafuta hekima inayoleta Ukuaji wa Kanisa. Ghafla tu utawashwa na mikakati ya Ukuaji wa Kanisa inayofundishwa na mchungaji wa kanisa. Bila maono yanayochoma utasema kwamba mafundisho haya hayafanyi kazi yoyote.

    Maono ya ndani yanayochoma pamoja na ndoto vitakufanya uendelee kusoma na kusoma juu ya jambo lile lile mpaka litakapoanza kufanya kazi kwa namna asha.

    Bila kuwa na maono yanayochoma na ndoto ya kanisa kubwa, hutakuwa na muda wa kusoma vitabu ambavyo vitakuongoza kwenye kuwa na kanisa kubwa.

    Maono yanayochoma na ndoto ya kanisa kubwa vitakuongoza kukutana na watu ambao watakusaidia jinsi ya Ukuaji wa Kanisa. Jambo hili litakufanya uwe mnyenyekevu kadiri ya kuweza kuhusiana na wengine na kushirikiana na watu sahihi mpaka mvuto na upako wao utakapokuwa juu yako.

    Bila ya kuwa na maono yanayochoma na ndoto ya kanisa kubwa hutasikiliza ujumbe wowote unaoleta Ukuaji wa Kanisa. Utapinga zaidi kila kitu ambacho ujumbe huo unahitaji na hata kufanya ujumbe huo uwe kama kitu cha kujifurahisha tu.

    Maono yanayochoma na ndoto ni chanzo cha kweli cha kuwa na nguvu, uthabiti na msimamo unaohitajika, katika safari ndefu ya kukua kwa kansia.

    Sehemu ya 2

    Ukuaji wa kanisa na walei

    Sura ya 2

    Jinsi Unavyoweza Kufikia Mambo Makuu Kwa Kupitia Walei

    Laikos Mlei

    Historia inatufundisha kuwa mambo makuu huweza kukamilishwa kwa kupitia watu wasio na ujuzi. Ukitazama kwa haraka haraka, mafanikio ya walei au watu wa kawaida, yatakutia msukumo uwatumie kwa ajili ya Ukuaji wa Kanisa lako.

    Neno mlei linatokana na neno la Kiyunani laikos lenye maana ya kuwa bila ujuzi. Yafuatayo ni maelezo kuhusu neno mlei.

    1. Mlei ni mtu wa kawaida.

    2. Mlei ni mtu wa desturi.

    3. Mlei ni mtu anayefahamika kuwa ni mtu mwenye mazingira ya kawaida.

    4. Mlei ni mtu wa mila.

    5. Mlei ni mtu wa mazoea.

    6. Mlei ni mtu anayepatikana karibu kila mahali.

    7. Mlei ni mtu wa kila siku.

    8. Mlei ni mtu wa wastani.

    9. Mlei ni mtu ambaye hana weledi.

    10. Mlei ni mtu ambaye si bingwa.

    11. Mlei ni mtu ambaye si mtaalamu.

    12. Mlei ni mtu ambaye hakuendelezwa ili awe na ujuzi.

    13. Mlei ni mtu ambaye hakupewa mafunzo yoyote.

    14. Mlei ni mtu ambaye hakuthibitishwa.

    15. Mlei ni mtu ambaye hana kibali chochote.

    Mafanikio Makubwa Katika Ulimwengu wa Kanisa

    1. Walei walikuwa nguzo ya matengenezo makuu ya kanisa.

    Tafsiri ya Biblia ya Martin Luther iliyotafsiriwa katika lugha ya watu wa kawaida ilibadilisha ulimwengu. Badala ya Biblia hiyo kubaki katika lugha ya Kilatini, ilipotafsiriwa ilifanywa iwe rahisi kuwafikia hata na watu wa kawaida.

    Mara tu watu wa kawaida/Walei walipokuwa na maono mikononi mwao walibadilisha ulimwengu. Wakitambua kuwa wokovu ulipatikana kwa watu wote kupitia neema ya Mungu, waliyoiinua na kuishindania ambayo kwa sasa tunaifahamu kuwa kama Mageuzi.

    2. Walei ni nguzo za Kanisa Kuu la Kimethodisti

    Katikati ya karne ya 20, Umethodisti ulikuwa ndio dini ya Uprotestanti huko Amerika. Kanisa kuu la Kimethodisti lilibebwa juu ya migongo ya walei.

    Utamaduni wa mwanzo kabisa wa mahubiri katika makanisa ya Kimethodisti, ulifanywa na watu wa kawaida, waliopendekezwa kuongoza ibada za kuabudu na kuhubiri katika vikundi vya makanisa vilivyoitwa makanisa ya mzunguko.

    Wahubiri wa kawaida walitembea kwa miguu au walipanda farasi katika mizunguko ya sehemu za mahubiri kulingana na mpango na muda halisi uliokubaliwa.

    Baada ya uteuzi wa watumishi na wachungaji, mahubiri haya ya kitamaduni yaliendelea na Wahubiri wa Mtaa wa Kimethodisti walioteuliwa na makanisa ya mahali, na kwa zamu walithibitishwa na kualikwa na makanisa jirani kama nyongeza kwa watumishi au wakati wale waliopangwa watakapokosekana.

    3. Walei walikuwa nguzo za kanisa moja kubwa kuliko yote ulimwenguni

    Moja kati ya kanuni za msingi ambayo kanisa la Yoido Full Gospel liliijenga ni kanuni ya kufanya kazi kwa kupitia walei.

    Kanisa la Yoido full Gospel, lilianzishwa na David Yonggi asha Mama Mkwe wake, Choi Ja-shil, wote wawili wakiwa wachungaji wa Assemblies of God, walifanya ibada ya uzinduzi wa kanisa tarehe 15 Mei, 1958 pamoja na wanawake wengine katika nyumba ya Choi Ja-Shil.

    Mwaka 1977, Washirika wa kanisa hilo walifikia elfu hamsini, idadi yao iliyoongezeka maradufu zaidi kwa miaka miwili tu. Tarehe 30 Novemba 1981, Washirika walifika jumla ya watu laki mbili. Kwa wakati huu, likawa kusanyiko kubwa kuliko yote duniani na likatambuliwa hivyo na Los Angeles Times.

    Mwaka 2007 Washirika wake walifikia 830,000, wakawa wanafanya ibada saba kila siku ya Jumapili ambazo zilitafsiriwa katika lugha kumi na sita.

    4. Walei ni nguzo za mtandao mkubwa wa makanisa ulioanzishwa kutoka Nigeria na Ghana.

    Makanisa ya Redeemed Christian of God pamoja na kanisa la nyumbani la Nigeria, The Church of Pentecost lenye makao makuu Ghana yanafahamika kwa matumizi mazuri ya walei. Huduma hizi zote zina mtandao mkubwa wa makanisa na kila siku walitumia huduma za walei kwa kuhubiri na kwa kazi ya kichungaji.

    Kanisa la The Church of Pentecost lilianzishwa na Mmisionari wa Kiireland aliyetumwa na kanisa la Apostolic Church, Bradford, la Uingereza, zamani zile ikiitwa Gold Coast.

    Kanisa hilo kwa sasa limekua na kuwa na Washirika zaidi ya milioni 1.7; kanisa la Church of Pentecost lilikuwa na zaidi ya makanisa 13,000 katika nchi 70 katika mabara yote ya ulimwengu.

    Mwaka 1952, Kanisa la Redeemed Christian Church of God lilianzishwa Nigeria na Pa Josiah Akindayomi.

    Chini ya uongozi wa Askofu wake Mkuu, Rev. E. A. Adeboye, limekua na kuwa na makanisa mengi katika nchi zaidi ya 140, zenye mamilioni ya watu wanaohudhuria ibada mbalimbali.

    Kwa hakika, haya ni mafanikio makubwa ambayo yamefanywa na hata kuwezekana kwa msaada wa walei.

    Mafanikio Makubwa Katika Mambo Mbalimbali ya Kiulimwengu

    1. Mfumo wa serikali kuu ya kidemokrasia ilizaliwa kupitia walei.

    Demokrasia inatoa fursa kwa watu wa kawaida kutenda na kubadilisha serikali kama watu wanavyotaka.

    Demokrasia ni nguvu ya kawaida ya watu ya kukataa kuishi chini ya sheria zisizokubalika.

    Demokrasia ni ushiriki wa kawaida wa mtu na ushawishi katika nchi.

    Demokrasia inajengwa juu ya kanuni ya fursa sawa inayotolewa kwa watu wote wa kawaida.

    2. Taifa kubwa lilizaliwa kupitia walei.

    Mapinduzi ya Amerika ni mfano bora sana wa nguvu ya watu wa kawaida au walei katika kutengeneza historia.

    Mtu wa kawaida tu alizaa taifa kubwa. Katika karne ya mwisho, majaribio ya mapinduzi ya Amerika yalifanikiwa ambayo yalionesha kipindi cha mpito cha ulimwengu kuongozwa na watu wachache hadi kwenye ulimwengu wa kuongozwa na watu wengi.

    Mapinduzi hayo kwa sehemu kubwa yalitengenezwa na taasisi ndogo ndogo za kimapinduzi kama vile Sons of Liberty. Taasisi hizi hazikuongozwa na matajiri na wamiliki wakubwa wa ardhi bali ziliongozwa na watu wa kawaida wenye hali ya maisha ya wastani katika kijamii ambayo iliwaleta pamoja na kupanda mbegu ya mapinduzi.

    3. Ushindi wa uchaguzi mkuu ulikuja kupitia walei.

    Mei mwaka 2008, Barack Obama Rais mweusi wa kwanza wa Amerika, alikazia demokrasia ya mapendekezo kwa ajili ya urais wa Amerika.

    Ingawa utajiri wa nchi na demokrasia yenye ushawishi ulikuwa wa wategemezaji wa Clinton nao walitoa mamilioni ya dola, Obama akapata kura nyingi zaidi za Urais kuliko mwingine yeyote aliyewahi kugombea katika historia kwa kutumia nguvu ya watu wa kawaida.

    Katika kampeni yake Obama alipata zaidi ya dola milioni 80, ambazo karibu zote zilitoka kwa watu wa kawaida waliochangia kidogo kidogo kwa kila mtu binafsi.

    Sura ya 3

    Jinsi Walei Walivyosaidia Kukua Kwa Makanisa

    Nina uzoefu na aina mbili za ulimwengu wa huduma – huduma ya kudumu na huduma ya walei. Wachungaji wengi wanajihadhari na kuwepo kwa huduma ya kudumu kuwa ndiyo kubwa. Shauku yangu ni kukusaidia ili uweze kugundua uhalisia wa jinsi walei wanavyoweza kusababisha Ukuaji wa Kanisa.

    Mlei ni mtu yule mwenye kazi yake ya kawaida ya kidunia na wakati huo ni mtendaji wa huduma ya Bwana Yesu. Mtumishi wa kudumu katika huduma ni yule aliyeacha kazi ya kidunia na kujiunga muda wote na huduma.

    Watumishi wengi ambao wako katika huduma ya kudumu hawafurahishwi na wazo la walei kujihusisha na huduma. Hii ni kwa sababu watumishi hao wanataka kudumisha huduma hiyo kuwa kama vile imetengwa kwa ajili ya watu maalumu walio wachache wanaoitwa watu wa Mungu.

    Baadhi ya watumishi wa huduma ya kudumu hawapendi kuupokea ukweli kwamba walei nao wanaweza kuchangia mchango (si wa kifedha) mkubwa katika huduma. Watumishi wengi wa huduma ya kudumu wanafurahi walei wanapodumu kuwa wategemezaji wanaofanana na ziwa dogo la fedha.

    Wachungaji wanataka kujisikia kuwa ni watu muhimu, wasiotakiwa kuchanganyika na wengine kadiri wanavyofanya wajibu wao. Wao wanasema kuwa, Kwa nini mlei afanye mambo yale ninayoyafanya? Wanadhani kuwa, Baada ya hayo yote, kama unaweza kufanya kazi ninayoifanya, ni kitu gani kitakachonifanya niwe mtu muhimu? Kinachonifanya (mchungaji) niwe tofauti na mlei ikiwa naye atafanya mambo ninayoyafanya ni nini?

    Watumishi wengi hawashawishiki kuwa walei wanaweza kufanya kazi ya huduma. Mchungaji mmoja aliniuliza, Je, watakuwa na muda wa kushughulikia mahitaji ya kundi?, na Wanaweza kusimamia mambo ya dharura? Na je, wanaweza kuhudumu kwa nguvu kama vile tunavyofanya sisi?

    Jibu la maswali haya yote ni rahisi – nalo linasikika hivi, NDIYO! Nimekuwamo katika huduma hii ya walei kwa miaka mingi na nimeona kuwa inawezekana kabisa kiutendaji.

    Ninaandika kitabu hiki ili kukufahamisha wazo mbadala kwa ile dhana ya mafundisho ya zamani juu ya makuhani kwamba wao walidumu hekaluni kumsubiri Mungu tu. Huduma ya walei ni ufunguo wa Ukuaji wa Kanisa. Makanisa yaliyopitia ukuaji wa wajabu wa kanisa yote yametumia kanuni ya kuwatumia walei katika huduma. Ninaamini kuwa huu ni ufnguo wa kutimiza agizo kuu. Hakuna njia ya kutufanya tuushinde ulimwengu huu kwa kuwa na makuhani na wachungaji wachache. Kila mmoja wetu lazima ahusishwe katika huduma. Watu wengi lazima wajihusishe katika huduma kwa kiwango cha juu kabisa. Hapo kutakuwa na uamsho wa huduma ya walei ndani ya kanisa.

    Kuna jambo linalohusu mchungaji mlei, mf. Mchungaji ambaye anajumuisha mambo mawili, kazi ya kawaida ya kidunia na huku anafanya kazi ya huduma kama kawaida. Katika kanisa langu asilimia tisini na tisa ya wachungaji ni wachungaji walei.

    Wachungaji wa huduma ya kudumu lazima wajione kuwa wako salama, wawatie moyo walei ili nao waweze kujihusisha na huduma. Katika huduma hakuna mambo ya siri! Wapo wachungaji wanaotaka huduma iwe imegubikwa sirini ili kwamba washirika wao siku zote wajisikie kuwa ni tegemezi kwao.

    Huu ni wakati wa kuweka wazi sanaa hii ya kuchunga na kulisha watu. Hili ni jambo ambalo watu wengi wanaweza kujihusisha nalo. Jambo la baraka kwa walei ni kugundua kuwa kumbe wanaweza kutumiwa katika huduma. Pia jambo la baraka kwa mchungaji nao ni wakati ule anapogundua kuwa mchango wa walei unaweza kufanya kanisa lake likue.

    Sisemi kwamba hakuna hitaji la watumishi wa huduma ya kudumu. Mimi mwenyewe ni mtumishi wa huduma ya kudumu. Kuna hitaji kubwa la watumishi wa huduma ya kudumu wanaotakiwa hata ikiwezekana wafikie asilimia mia moja kabisa. Hata hivyo, kuna mambo ambayo watumishi hao wa kudumu ndio wanaoweza kuyafanya tu.

    Nilikuwa Mchungaji Mlei

    Nilikutana na Bwana nilipokuwa na umri usiopungua miaka kumi na tano, nilipokuwa shule ya sekondari. Tangu siku hiyo niliyompa Kristo maisha yangu, nikawa mtendaji wa huduma zaidi. Nilijihusisha na huduma ya kuleta watu kwa Kristo na kufuatilia waongofu wapya. Nilijihusisha zaidi katika kuimba na kupiga vyombo vya muziki kwa ajili ya Bwana.

    Katika hatua ya mwanzo ya maisha yangu ya Kikristo, sikuwa mtu wa mapokeo ya kuhudhuria Jumapili asubuhi tu. Kwa hakika, nilikwenda kanisani kwa bidii yangu yote kila Jumapili. Maisha yangu ya Kikristo yalikuwa ya kiutendaji tangu Jumatatu hadi Jumamosi ambayo yaliishia na mapumziko siku za Jumapili tu! Siku ya Jumatatu na Jumatano zilikuwa siku za kukutana kwa ajili ya maombi na kujifunza Biblia. Jumanne na Alhamisi nilikuwa na mazoezi ya muziki. Katika siku ya Ijumaa tulikuwa tunafunga na kuomba. Kisha siku ya Jumamosi tulikuwa na faragha kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni.

    Kwa muda wote niliojihusisha na shughuli hizi zote sikuacha masomo yangu shuleni. Nilimaliza masomo yangu ya sekondari na nikafaulu kwa kupata alama za juu – nilikuwa na saba moja (moja ni kiwango cha alama za juu za ufaulu). Hiyo ilikuwa ni ukamilisho mkuu kwa kiwango chochote kile. Nilikamilisha madara yangu katika masomo yangu ya darasa la kumi na tano na kumi na sita, nikawa mtu pekee

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1