Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku
Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku
Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku
Ebook67 pages1 hour

Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dkt. Dag Heward-Mills, kiongozi Mkristo wa kipekee, anafichua moja wapo ya siri zake. "kama mtu angeniuliza siri kubwa ya mahusiano yangu na Mungu ni nini, ningesema, bila kusita kwamba ni nguvu ya muda wa faragha ninaokuwa naye kila siku". Ameamua kuandika kitabu hiki ili nawe uweze kunufaika kutokana na nguvu ya muda wa faragha.

LanguageKiswahili
Release dateMay 16, 2018
ISBN9781641353762
Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku

Related ebooks

Reviews for Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Namna Unavyoweza Kuwa na Muda wa Faragha Mzuri na Mungu Kila Siku - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Muda wa Faragha - Tabia Muhimu Zaidi Kwa Maisha Yako

    Sehemu ya pili ya maisha ya mtu hutokana na tabia alizopata katika sehemu ya kwanza ya maisha yake.

    Maneno ya Dostoyevsky

    Nguvu ya sifa ya mtu hutokana na matendo anayofanya kama tabia yake.

    Maneno ya Pascal

    Tabia ni kitu unachofanya bila kufikiria, au bila kukusudia. Kila Mkristo mzuri ana tabia nyingi nzuri. Hizo ndizo zimemfanya awe kama alivyo.

    Watu wote maarufu wana tabia ambazo zimewafanya kuwa wakuu. Bwana wetu Yesu alikuwa na tabia ambazo zilimfanya kuwa mkuu.

    Yesu Kristo

    1. Kwenda kanisani kila mara

    Je, ulijua kwamba Yesu alikuwa na tabia nzuri? Biblia inatufundisha kwamba alikuwa na tabia ya kwenda kanisani siku ya Sabato.

    Naye akafika Nazareti, mji aliolelewa, na KAMA ILIVYOKUWA TABIA YAKE, alikwenda katika sinagogi siku ya Sabato, akasimama asome.

    Luka 4:16, TLR

    2. Kwenda kuomba peke yake

    Yesu pia alikuwa na tabia ya kwenda kwenye bustani moja ili kukaa peke Yake. Hapo alikwenda mara kwa mara. Na kila mtu alijua tabia yake hiyo ya kwenda bustanini kuomba.

    Baada ya Yesu kusema hayo, alitoka na wanafunzi Wake kuvuka kijito cha Kidron, palipokuwa na bustani. Akaingia huko pamoja na wanafunzi wake. Na Yuda, msaliti wake, alipajua: kwa sababu MARA NYINGI YESU ALIKWENDA HAPO NA WANAFUNZI WAKE.

    Yohana 18:1, 2, TLR

    Danieli

    Danieli aliomba nyakati maalum kila siku. Ni kitu alichokuwa amezoea kufanya. Ndiyo ilikyokuwa siri kubwa ya maisha yake.

    Basi, Danieli alipojua kwamba lile andiko limetiwa sahihi, alikwenda nyumbani kwake; na huku madirisha yake ya chumbani yakiwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu, alipiga magoti mara tatu kwa siku na kuomba, na kumshukuru Mungu wake, KAMA ALIVYOKUWA ANAFANYA KABLA YA HAPO.

    Danieli 6:10, TLR

    Mambo Kumi Ambayo Kila Mkristo Anatakiwa Ajue Kuhusu Tabia

    1. Tabia ni TENDO LINALORUDIWA KIRAHISI bila kufikiri au hata kupanga.

    2. Tabia ni TENDO LINALOKUJA KUWA DESTURI YAKO, ujue au usijue.

    3. Tabia mara nyingi huwa TENDO LISILOKUWA NA MAANA, LENYE KUONEKANA KAMA HALINA NGUVU za kuathiri wakati ujao. Ndiyo sababu watu wengi hawatambui dhana ya kuwa na tabia nzuri kama chombo chenye nguvu sana kwa ajili ya mafanikio ya baadaye.

    4. Tabia inaweza KUWA NZURI AU MBAYA, YA KAWAIDA AU YA KIROHO. Tabia za kiroho ni mambo kama maombi ya asubuhi,na kuwa na faragha kila siku. Tabia za kawaida ni kama kusugua meno asubuhi na kuoga kila siku.

    5. TABIA NZURI HUTENDWA KWA KURUDIWA KIRAHISI TU KAMA TABIA MBAYA.

    6. TABIA MBAYA HUPELEKEA KUSHINDWA MARA KWA MARA bila mtu kutambua nini kinachofanyika.

    7. TABIA NZURI HUPELEKEA MAFANIKIO MARA KWA MARA NA USHINDI, bila hata mtu kutambua anafanya nini.

    8. Tabia mbaya ni rahisi kukuzwa, lakini ni ngumu kuishi nazo. TABIA NZURI NI NGUMU KUZIKUZA, LAKINI NI RAHISI KUISHI NAZO.

    9. KILA MKRISTO ANA KIASI CHA TABIA NZURI AMBAZO zimemfikisha kwenye mafanikio. Miaka mingi iliyopita, rafiki yangu mmoja alinifundisha jinsi ya kuwa na faragha na Mungu kila asubuhi. Nikaendeleza hizo kama tabia binafsi, nayo imekuwa siri yangu kuu katika Ukristo na baadaye katika huduma. Karibu kila kitu ninachohubiri kinatokana na tabia hii njema.

    10.TABIA NI UTARATIBU SALAMA KWA AJILI YA WAKRISTO. Hii ni kwa sababu, hata wakati ambapo kiongozi amesongwa sana, atafanya mambo fulani mazuri kwa kufuata tabia, kwa asili na kirahisi kabisa. Akiwa amebanwa, kiongozi anaweza asipate muda wa kufikiri cha kufanya au jinsi ya kufanya. Ni ile tabia nzuri ya kuomba au kuwa na faragha itakayomwongoza kutoka kwenye hali hiyo ngumu. Sawa na Yesu, mimi nina mahali pangu ninapokwenda ili kuomba. Na mimi pia ninakwenda huko na wachungaji wangu. Tabia hii inanitunza kiroho, hata wakati sijui hatari iliyoko au inayokuja.

    Sura ya 2

    Muda wa Faragha - Siri Ya Watu Wengi Walio Wakuu

    Musa Alikuwa Na Faragha Na Mungu

    Kisha BWANA akamwambia Musa, ‘Chonga mbao mbili za mawe mfano wa zile za kwanza; nami nitaandika juu ya mbao hizo maneno hayo yaliyokuwa juu ya mbao za kwanza, hizo ulizozivunja. NAWE UWE TAYARI ASUBUHI, NA ASUBUHI UKWEE JUU KATIKA MLIMA WA SINAI, NAWE HUDHURISHA NAFSI YAKO KWANGU HUKO KATIKA KILELE

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1