Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Wajue Maadui Zako Wasioonekana...
Wajue Maadui Zako Wasioonekana...
Wajue Maadui Zako Wasioonekana...
Ebook229 pages6 hours

Wajue Maadui Zako Wasioonekana...

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345484
Wajue Maadui Zako Wasioonekana...
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Wajue Maadui Zako Wasioonekana...

Related ebooks

Reviews for Wajue Maadui Zako Wasioonekana...

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Wajue Maadui Zako Wasioonekana... - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Orodha ya Maadui Wasioonekana

    Bibilia inatupatia orodha nzuri ya maadui wasioonekana Ni wajibu wetu kuamini Neno la Mungu na kupigana na kila mmoja wao mpaka tuwakanyage chini ya nyayo zetu. Usiukadirie uhalisi wa ulimwengu wa kiroho kuwa pungufu. Ulimwengu wa roho ndio ulimwengu halisi. Ulimwengu huu ni ulimwengu wa muda (usiokuwa halisi). Hapa kuna orodha ya maadui wasioonekana ambao ni lazima utarajie kukutana nao wakati unapokuwa ukiishi hapa duniani. Yesu hakukaa sana kabla kukutana na pepo. Alikutana na pepo katika maisha yake yote na hudumaa hapa duniani.

    1. Falme ni maadui wasioonekana.

    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Waefeso 6:12

    2. Mamlaka ni maadui wasioonekana.

    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Waefeso 6:12

    3. Wakuu wa giza la kiroho ni maadui wasioonekana.

    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Waefeso 6:12

    4. Uovu wa kiroho ni adui asiyeonekana.

    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

    Waefeso 6:12

    5. Pepo wachafu ni maadui wasioonekana.

    Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili! Maana awaamuru PEPO WACHAFU kwa uwezo na nguvu, nao hutoka.

    Luka 4:36

    Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

    Mathayo 10:1

    6. Pepo wachafu ni maadui wasioonekana.

    Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule PEPO MCHAFU, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena.

    Marko 9:25

    7. Malaika waliokosa ni maadui wasioonekana.

    Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, , lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.

    Yuda 1:6

    8. Watawala wa ulimwengu huu ni maadui wasioonekana.

    Ambayo WENYE KUITAWALA dunia hiihawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu.

    1 Wakorintho 2:8

    9. Pepo ni maadui wasioonekana.

    Wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza.

    Marko 6:13 (SWU)

    10. Vitu vya enzi ni maadui wasioonekana.

    Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni VITU VYA ENZI, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

    Wakolosai 1:16

    11. Usultani ni maadui wasioonekana.

    Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au USULTANI, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.

    Wakolosai 1:16

    12. Inzi wa kiroho ni maadui wasioonekana.

    Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.

    Akawaita, akawaambia kwa mifano, Awezaje Shetani kumtoa Shetani? Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama.

    Marko 3:22-24

    13. Ndege wa kuchukiza wa kiroho ni maadui wasioonekana. Pepo wengine wanaitwa ndege wa kuchukiza.

    Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza.

    Ufunuo 18:2

    14. Pepo vyura ni maadui wasioonekana. Pepo wengine wanaitwa vyura.

    Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.

    Ufunuo 16:13-14

    15. Nge wa kiroho ni maadui wasioonekana: Pepo wachafu wengine wanaitwa nge.

    Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na NGE, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.

    Luka 10:19

    16. Majoka wa kiroho ni maadui wasioonekana: Pepo wachafu wengine wanaitwa majoka.

    Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

    Ufunuo 12:9

    17. Nyoka wa kiroho ni maadui wasioonekana: Pepo wachafu wengine wanaitwa njoka. Ni wazi kwamba hawa si nyoka wa kimwili bali ni nyoka wa kiroho.

    Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

    Ufunuo 12:15

    18. Farasi wa kiroho na wanaowapanda ni maadui wasioonekana

    Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi.

    Ufunuo 6:8

    19. Madubwana wa baharini wa kiroho ni maadui wasioonekana. Pepo wachafu wengine wanaitwa Lewiathani. Lewiathani ni dubwana la baharini au mnyama wa baharni mwenye vichwa vingi.

    Wewe uliviseta vichwa vya lewiathani, Awe chakula cha watu wa jangwani.

    Zaburi 74:14

    20. Madubwana wa baharini wenye vichwa vingi, wako kwenye orodha ya maadui wasioonekana. Pepo wengine ni madubwana wenye vichwa vingi wanaoishi baharini. Wengine huwaita pepo wa baharini.

    Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.

    Ufunuo 13:1

    21. Madubwana wa chini ya ardhi, wako kwenye orodha ya maadui wasioonekana. Pepo wengine ni madubwana wenye vichwa vingi wanaoishi katika ardhi. Hawa ni pepo wa duniani.

    Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.

    Ufunuo 13:11

    Sura ya 2

    Kazi Kumi za Pepo Dhidi Yako

    Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako WENGI WANIPINGAO.

    1 Wakorintho 16:9

    Hakuna Mwito Uendao bila kupingwa

    Hakuna kupewa wajibu au mwito ambao huenda bila kupingwa. Mungu akikuita, utapingwa na shetani. Shetani atapigana nawe, kwa sababu yuko hapo kwa sababu hiyo. Kila mwito mkuu huenda na upinzani mkali.

    Kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.

    1 Wakorintho 16:9

    Musa alipoitwa kuwakomboa Waisraeli na kuwaweka huru, alikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa Farao. Farao ni aina ya Shetani ambaye hatawachilia watu wa Mungu waende. Farao anamwakilisha shetani anayechukia dhana ya watu kumtumikia Mungu. Watoto wote wa kiume wa Waisraeli walichinjwa katika majaribio ya kuwaangamiza kutoka ulimwenguni.

    Yesu alipozaliwa hapa ulimwenguni kuwaokoa wanadamu alikutana na Herode aliyeamuru kuchinjwa kwa watoto wote katika majaribio ya kumwangamiza Mwokozi. Mwito mkuu na wajibu wa Yesu kama Mwokozi wa ulimwengu huu ulikutana na aina ya juu sana ya upinzani.

    Mwito wako vile vile utakutana na upinzani mkali. Viumbe vyote vilivyotajwa katika sura ya awali wataungana dhidi yako kuhakikisha kwamba humalizi mwito wako. Ukisisitiza juu ya kumfanyia kazi Mungu, utapingwa, kuvunjwa moyo, kushutumiwa, kusumbuliwa na kupingwa na adui usiyemwona katika maisha yako yote na huduma yako yote. Kama huombi, na kama hukiroho, hutakaa kwa muda mrefu katika vita hivi vikali visivyoonekana. Pepo ni halisi. Viumbe waovu ni halisi. Wakati umefika wa kutafuta ni kitu gani hasa unachokabiliana nacho na ukishinde.

    Hatima Yako inategemea na Kumshinda Adui na Uwezo

    Bila uwezo wa Mungu hutatimiza mwito wako. Andiko liko wazi; unapokea vitu vyote unavyopewa kupitia kwa uwezo wa Mungu. Uwezo wa Mungu ndio njia ambayo kwa hiyo tunapokea vitu vingi tunavyohitaji. Uwezo wa Mungu ni wa lazima ili tupate kumshinda huyo adui. Adui anaelewa lugha ya uwezo.

    Kwa kuwa UWEZA WAKE WA UUNGU UMETUKIRIMIA vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.

    2 Petro 1:3

    Kazi Kumi za Pepo Dhidi Yako

    1. Upinzani na Ushindani

    Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa MSHITAKI wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

    1 Petro 5:8

    Adui zako wanapinga dhana ya wewe kuwa chochote muhimu. Aina zote za upinzani unazohisi unapojaribu kutii mapenzi ya Mungu zinasababishwa na adui wengi. Nimehisi upinzani kutoka kila mahali tangu nianze huduma yangu.

    Wakati mwingine upinzani huo unatoka nje ulimwenguni, lakini wakati mwingine ni kutoka kwa maaskofu wangu, wakati mwingine unatoka kwa wasaidizi wangu; wakati mwingine unatoka katika jamaa yangu. Hata iweje, ni lazima utambue upinzani kama unaotoka kwa pepo.

    Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

    1 Petro 5:8

    Adui ni mtu anayepinga, anayeweka vikwazo, anayezuia na kukusitisha kupata kile ulichoamua kukikamilisha.

    Unapowaza juu ya maneno upinzani, kuvunjwa moyo, ugumu, ukawiaji, waza juu ya pepo. Fikiri juu ya shughuli za kishetani kila wakati unapoona ukawiaji, kuvunjwa moyo na vikwazo vya mwito wako.

    Kuvunjwa moyo kwingi katika huduma kunasababishwa na pepo. Hata mambo yaonekane mazuri namna gani kwa nje, pepo wachafu wako. Pepo wachafu wako kupinga, kuvunja moyo na kupigana na watumishi wa Mungu.

    Ugumu mwingi na changamoto nyingi anazopata mhudumu, zinasababishwa na pepo wachafu. Jinsi unavyokuwa kiroho zaidi, ndivyo utakavyozidi kufahalmu juu ya shughuli za pepo wachafu.

    2. Kuvunjwa moyo

    Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye ATAWADHOOFISHA WATAKATIFU wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.

    Danieli 7:25

    Kama sehemu ya mipango ya kukupinga, shetani huanza kukuvunja moyo. Kila aina ya maudhi, usumbufu na hasira unayopata vyote ni dalili za shughuli za pepo. Wakati mwingine, maudhi na hasira hutoka kwa masuala ya ndani. Kazi rahisi inaweza kwenda polepole na kuwa tukio refu lisilopendeza.. Ni uwepo wa kila mara wa mashetani yaliyotumwa kukupinga na kutatiza kazi ya Mungu ndiko kunakoleta tukio la aina hii.

    3. Kuwazuia watu

    Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, HAYO HAYATAKUPATA.

    Mathayo 16:19-20

    Kusitisha kazi ya Bwana kabisa ni moja wapo ya matukio yanayompatia shetani furaha kuu zaidi. Ameweza kuzidisha jitihada zake kutatiza kazi ya Mungu. Katika matukio mengi ameweza kuikomesha kabisa. Chunga vitu vinavyositisha kazi ya Mungu kabisa.

    4. Kuwajaribu watu

    Mara Roho akamtoa aende nyikani. Akawako huko jangwani siku arobaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu, na malaika walikuwa wakimhudumia.

    Marko 1:12-13

    Kuwajaribu na kuwatahini watu wa Mungu wanapomfanyia kazi Bwana ni kazi ya mashetani. Watu wa Mungu wengi wanapata majaribu kila mara wanapokuwa wakimtumikia Mungu. Watu wengi wanaangushwa kupitia kutosamehe, tamaa, kutovumilia na majaribu mengine.

    5. Kuwatisha watu

    Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa MSHITAKI wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.

    1 Petro 5:8

    Aina zote za hofu hutoka kwa shetani Wanaume na wanawake wengi wanathibitiwa kabisa na hofu zao. Hofu ni pepo anayeshawishi na kuelekeza. Anatafuta kukuelekeza na kukuongoza katika njia inayoishina na wewe kupiga kichwa ukuta.

    6. Kuwadanganya watu

    Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.

    2 Wakorintho 11:3

    Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.

    Ufunuo 12:9

    Shetani anajulikana vizuri sana kwa kutia sumu mioyo ya Wakristo. Wengi wametiwa sumu ya kutoamini, uchungu, udanganyifu, kukosa uaminifu na kuchanganyikiwa. Shutuma ni moja wapo ya sumu kali zaidi ambazo zinaweza kutupwa katika mioyo ya Wakristo. Watu wengi hupoteza kutokuwa na hatia kwao kwa sababu shetani huangusha sehemu ya sumu yake katika mioyo yao. Unapokutana na kundi la watu walioathiriwa na vitu walivyokumbana navyo, yamkini wametiwa sumu na shetani.

    7. Udanganyifu

    Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.

    Yohana 8:44

    Kusema uongo na udanganyifu ni shughuli za mashetani. Unapokutana na mtu mwongo unakutana na kuvunjika moyo. Mwongo kawaida ni mwizi na hukupokonya kitu chako. Watu wanaosema nusu ukweli na watu wanaokuongoza visivyo wote hutumwa na shetani wakuvunje moyo na kukuharibu. Katika maisha yako yote na huduma utakutana na watu kama hao. Wote ni mawakala wa shetani, waliotumwa wakuharibu.

    Kila mhudumu wa injili lazima wawe macho na kitu au mtu anayejaribu kumdanganya. Shetani siku zote anajaribu kukuelekeza visivyo, kukukosesha njia, kukuzuia na kukupa habari za uongo. Siku zote anajaribu kukuficha kitu na akufanye utembee gizani, kwenye kutojua na kwenye udanganyifu. Hii ni kazi ya kila mara na isiyogeuka ya pepo wachafu. Hii ndiyo sababu ni lazima uombe kila mara upate hekima, ufahamu, ujuzi, ushauri, nuru na ufunuo. Danieli alionekana kama mtu aliyekuwa amekombolewa kutoka kwenye giza la udanganyifu. Alielezwa kama mtu mwenye nuru, ufahamu na hekima. Kwa sababu ya nuru, ufahamu na hekima aliyokuwa nayo, alichaguliwa na kuteuliwa na mfalme. Aliitwa kwa sababu alikuwa ameshinda giza na kupokea nuru na ufunuo kutoka kwa Mungu. Wale ambao wana uwezo zaidi ni wale ambao wameshinda giza katika ulimwengu na wamepokea nuru.

    Yuko mtu katika ufalme wako, ambaye roho ya miungu watakatifu inakaa ndani yake; na katika siku za baba yako nuru na ufahamu na hekima, zilionekana ndani yake; na mfalme Nebukadreza, baba yako, naam, mfalme, baba yako, akamfanya kuwa mkuu wa waganga, na wachawi, na Wakaldayo, na wanajimu;

    Kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionyesha tafsiri.

    Danieli 5:11, 12

    Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1