Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Maono Niliyoona
Maono Niliyoona
Maono Niliyoona
Ebook75 pages52 minutes

Maono Niliyoona

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Maono-1(TETEMEKO NA VOLKANO)
Mwaka 2017, niliona maono ya kutisha. Maono yalianza kama ndoto wakati nimelala kitandani na nilipoamka bado maono hayo yaliendelea nikiwa macho na akili zangu timamu. Katika maono hayo niliona kama mlipuko wa volkano kubwa iliyochanganyikana na tetemeko ndani yake. Niliona watu na milima wakiinuliwa juu na kurudishwa chini kiasi cha kutengeneza mzunguko kama vile mtu anavyopatwa na kizungunguzu baada ya kujizungusha kwa muda mrefu. Maono hayo yalikuwa juu ya anga nilipokuwa nimelala kifudifudi nikiangalia kama sinema. Baadae katika maono hayo niliona kama watu wanapigana ndani ya huo mzunguko wa volcano. Wakati naangalia sana, maono yalifika mwisho wake.

Maono-2(KUPANDA MILIMA NA KUSHUKA MABONDE)
Katika maono ya kupanda vilima, nilijikuta napanda jabali lenye ukingo mkali sana unaotisha sana na kuogopesha sana. Wakati napanda kilima hicho nilikuwa peke yangu bila msaada wa mtu. Nilitumia nguvu nyingi na maarifa katika kupanda kilima hicho na baadae nilifanikiwa baada ya kuhangaika na kutumia nguvu kubwa sana.Wakati natafakari maono hayo nilipata ujumbe kuwa kuna nyakati ngumu na majaribu zinakuja mbeleni. Nakumbuka ilinitokea mfululizo zaidi ya mara tano, kuona maono ya kupanda vilima na kuvuka mito yenye kingo ndefu sana. Kupanda vilima na vigongo ilimaanisha nyakati ngumu za kujaribiwa binadamu na kubadilika kwa kawaida ya Maisha ya binadamu. Katika maoni hayo Mungu alikuwa ananionya kuwa Mungu anaenda kuchuja wamwabuduo Mungu kwa dhati na watu wanamtafuta Mungu ili kujipatia faida.Katika maono ya pili tulikuwa tunakimbia kama mashinndano ya watu wasiopungua watano. Maono hayo nakumbuka yalijirudia mara nyingi kidogo kwa siku tofautofauti. Tulikuwa kunakimbia nyikani sehemu ambayo haina watu bali kuna nyika, miiba, vichaka na vikwazo vingi sana. Katika kukimbia tulikutana na mito yenye kina kirefu ila haina maji. Mito hiyo ilikuwa na vikwazo sana kama mizizi ya miti mikubwa, matawi ya miti na zaidi ya yote ukingo wa mto ulikuliwa mrefu sana kiasi cha kutatiza namna ya kupanda ili kuendelea na mashindano yetu. Wakati najaribu kuvuka vikwazo hivyo nilijikuta wenzangu wamenicha nyuma. Nilipomuuliza Mungu kuhusu maono hayo alinifunulia kuwa wakati unakuja kila mtu atasimama katika zamu yake na kujaribiwa imani yake mbele za Mungu.

Maono haya na mengine yalinisukuma kuandika kitabu ili watu wajue mambo yaliyokusudiwa na yale yatakayokuja na namna ya kukabiliana nayo.

LanguageKiswahili
Release dateMay 19, 2020
ISBN9780463109731
Maono Niliyoona
Author

Charles Nakembetwa Shamsulla

Charles Nakembetwa Shamsulla a author and preacher of Gospel of Jesus Christ. He is also the author of BWANA OKOA NDOA YANGU, YOU CAN EASILY KILL FEAR [CONQUERING FEAR FACTOR] and KUSHINDWA SASA BASI. He holds Masters Degree in Public Administration specializing in Human Resources Management.

Read more from Charles Nakembetwa Shamsulla

Related to Maono Niliyoona

Related ebooks

Reviews for Maono Niliyoona

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Maono Niliyoona - Charles Nakembetwa Shamsulla

    Maono-5 (Kuangua kwa Gholiati)

    Maono-6 (Ushindi wa majaribu)

    Maono-7 (Ndege na Vifaranga)

    Vitabu zaidi

    UTANGULIZI

    Maono-1(Tetemeko na Volkano)

    Mwaka 2017, niliona maono ya kutisha. Maono yalianza kama ndoto wakati nimelala kitandani na nilipoamka bado maono hayo yaliendelea nikiwa macho na akili zangu timamu. Katika maono hayo niliona kama mlipuko wa volkano kubwa iliyochanganyikana na tetemeko ndani yake.

    Niliona watu na milima wakiinuliwa juu na kurudishwa chini kiasi cha kutengeneza mzunguko kama vile mtu anavyopatwa na kizungunguzu baada ya kujizungusha kwa muda mrefu. Maono hayo yalikuwa juu ya anga nilipokuwa nimelala kifudifudi nikiangalia kama sinema. Baadae katika maono hayo niliona kama watu wanapigana ndani ya huo mzunguko wa volcano. Wakati naangalia sana, maono yalifika mwisho wake.

    Wakati naomba na kutafakari kujua maana ya maono yale, Roho Mtakatifu alinipa neno la Mungu katika kitabu cha Luka 21:26 watu wakivunjika moyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za Mbinguni zitatikisika.

    Maono hayo yalinisumbua kwa kitambo kirefu bila kuelewa maana yake halisi. Kadiri siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo Mungu alivyozidi kunifunulia na kunifundisha kuhusu maono hayo. Baadae Mungu alianza kunifundisha kwa vitendo, mambo yatakayokuja mbeleni. Mungu alikuwa ananifundisha namna ya kukabiliana na roho ya woga na hofu kuu itakayotikisa ulimwengu na kufanya mioyo ya watu wengi kuyeyuka kama inta mbele ya joto kali.

    Mara zote nilipokuwa nasoma andiko hapo juu, akili na fikra zangu ziliniambia hayo ni mambo ya baadae sana na sio mambo ya wakati huu. Hali hii ilichangiwa na aina ya mafundisho niliyoyapata, kuwa mambo hayo yatatokea wakati wa dhiki kuu. Mungu alinifungua kuacha kulitumia neno la Mungu kama matumizi ya baadae bali kila andiko linafaa kwa mafundisho, kuonya, kuandibisha na kufundisha katika haki. (2Timotheo 3:16).

    Kwa faida ya msomaji wangu, katika kunifundisha Mungu aliruhusu nipitie katika misukosuko mikubwa kimaisha ambayo sijawahi kupitia na wala sikujua ni kwa sababu gani. Baadae niligundua Mungu alikuwa ananiaanda kushinda roho ya woga na hofu wakati utakapofika. Unapopitia katika majaribu usimlaumu Mungu kwani unaweza kushindwa mtihani wa Mungu aliokuandalia ili kukupandisha cheo wakati uliokubaliwa. Simama katika nafasi yako na kumshukuru Mungu kwa kila jaribu, kumbuka majaribu ndio mtaji wako wa kuinuliwa na Mungu.

    Wakati naona maono hayo sikujua chochote kuhusiana na hofu na woga mkubwa utakaoipata dunia miaka michache baadae kuhusiana na mlipuko wa tauni ya covid-19. Ninaita tauni kwa makusudi na nitaelezea hapo baadae. Nilipata maono mengi sana kuhusiana na namna ya kushinda hofu na woga na baadae niliandika kitabu kwa lugha ya kiingereza kinachoitwa Casting the Spirit of Fear (unaweza kukipata (https://www.smashwords.com/books/view/681089).

    Hofu na mashaka yatakayoupata ulimwengu ni makubwa kuliko hata janga lenyewe la tauni ya covid-19. Watu wengi hawajui kuwa hofu ni roho iliyomwagwa toka kuzimu kwa ajili ya kuua, kuchinja na kuharibu, maana neno la Mugu linasema katika kitabu cha Yohana Mtakatifu 10:10 mwizi anakuja kuua, kuiba na kuharibu. Mwizi huyo sio mwingine bali ni shetani. Nimeandika kitabu hiki ili kukushirikisha msomaji wangu umuhimu wa maono haya, ili ujue namna ya kushinda hofu na mashaka makubwa yanayoendelea na yatakayokuja kuikumba dunia siku za usoni. Hata kama wewe ni mvivu wa kusoma, nakuomba ujitahidi kupata maono haya kwa sababu mambo ya kuogofya yanakuja kuupata ulimwengu. Nimejitahidi kukifanya kitabu hiki kuwa kifupi ili kuwasaidi wasomaji wangu wote kuyapata maono haya muhimu ya wakati tulionao na yale yaliyokuja mbele yetu.

    sura ya kwanza: HOFU NI ROHO YA KUZIMU

    Jaribu kivuta kumbukubu zako, kila wakati jambo baya linapotaka kukutokea inatangulia hofu na woga moyoni. Hofu hiyo na woga huo sio wa kawaida bali ni mjumbe maalumu aliyetumwa kukuandaa kupokea jambo baya. Angalia maandiko yafuatayo; Maana jambo hilo nilichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia. Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; lakini huja taabu. (Ayubu 3:25-26).

    Kabla ya Ayubu hajapatwa na majanga ya kufiwa na watoto, majanga ya moto, Majambzi wa Kiseba na hata kansa ya ngozi, kwanza alitumwa mjumbe wa kumwogopesha na kumtisha. Wengine watasema nimejuaje? Jibu ni rahisi sana, katika mlango tuliosoma hapo juu, Ayubu anakiri kwa kinywa chake kuwa mambo aliyokuwa akiyaogopa kila siku na kuangaika nayo usiku kucha ndiyo yaliyompata. Kadiri unavyoogopa kifo ndivyo unavyokaribia karibu sana na kaburi.

    Usifikiri ukiogopa kansa itakuacha, hapana, bali kinyume chake. Ayubu anatukumbusha kuwa haya yaliyonipata ni matokeo ya mapambano ya muda mrefu niliyopitia. Kila alipolala kuna kitu kilikuwa kinamwambia kuna hatari kubwa mbele yako. Ndivyo shetani anavyotumia hofu kuwakamata wanadamu. Atamtanguliza mjumbe wa hofu ili kukutisha na

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1