Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mrembo, Mnyama na Mchungaji
Mrembo, Mnyama na Mchungaji
Mrembo, Mnyama na Mchungaji
Ebook282 pages4 hours

Mrembo, Mnyama na Mchungaji

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345521
Mrembo, Mnyama na Mchungaji
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Mrembo, Mnyama na Mchungaji

Related ebooks

Reviews for Mrembo, Mnyama na Mchungaji

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mrembo, Mnyama na Mchungaji - Dag Heward-Mills

    SEHEMU YA 1:

    MAONYO

    SURA YA 1

    Onyo: Ndoa za Watumishi Ziko Tofauti na Ndoa za Kawaida

    Je! Mmeusahau uovu wa baba zenu, na uovu wa wafalme wa Yuda, na UOVU WA WAKE ZAO, na uovu wenu wenyewe, na UOVU WA WAKE ZENU, walioutenda katika nchi ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu?

    Yeremia 44:9

    Kitabu hiki si kwa ajili yako ikiwa wewe si mchungaji.Usiendelee kusoma kitabu hiki ikiwa wewe si mchungaji.

    Ikiwa wewe si mchungaji, tafadhali komea hapa!

    Ikiwa wewe si mchungaji na unaendelea kusoma utakosoa mambo usiyoyaelewa.

    Ikiwa wewe si mchungaji, tafadhali tafuta kitagu kingine kuhusu ndoa. Vipo vitabu vingi vizuri kuhusu ndoa ambavyo vitakusaidia sana katika maisha yako. Ikiwa unahitaji maelezo ya namna ya kupata kitabu kizuri cha ndoa, tafadhali tembelea duka la vitabu lililo karibu nawe.

    Ni Baraka kuwa na ndoa nzuri na ninazifahamu ndoa nyingi nzuri zenye baraka za ajabu. Je, baadhi ya baraka za ndoa nzuri ni zipi?

    1. Ndoa nzuri ni Baraka kwa sababu wawili ni bora kuliko mmoja. Yapo Maandiko mengi yanayothibitisha ukweli huu.

    Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

    Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.

    Mhubiri 4:9-12

    2. Ndoa nzuri ni Baraka kwa sababu wanandoa wanaweza kufanya vitu mara kumi zaidi ya u mmoja.

    Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, kama mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwanaasingaliwatoa?

    Kumbukumbu la Torati 32:30

    3. Ndoa nzuri ni Baraka kwa sababu mwaume aliyeoa ana upendeleo mkubwa kwa Mungu.

    Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

    Mithali 18:22

    Ijapokuwa ndoa nzuri ni baraka kuu, kuna aina nyingi tofauti za ndoa. Si ndoa zote hufikia lengo la kuwa baraka kwa wanandoa.

    Ndoa bandia zipo kwa sababu kuna ndoa halisi na nzuri.

    Kitabu hiki ni kwa ajili ya aina fulani tu ya ndoa. Kitabu hiki ni kwa ajili ya wachungaji na ndoa zao na kwa ajili ya Wakristo wa Kawaida au wasio waamini. Sehemu kubwa ya kitabu hiki haitakufaa wewe ikiwa wewe si mchungaji au mke wa mchungaji.

    Vitabu vingi kuhusu ndoa huwafanya wachungaji wajisikie kuwa wameoa watu wasio sahihi kwa sababu ndoa zao huonekana si nzuri kama za waandishi.

    Kisha hushtuka na kushangaa wanaposikia kuwa wachungaji wenye ndoa zinazoonekana kuwa nzuri wanatalikiwa.

    Hiki si kitabu kuhusu ndoa za kawaida. Kitabu hiki siyo cha majadiliano ya pande mbili kuhusu masuala ya ndoa.. Kwa hakika ningeweza kuandika kitabu kuhusu wote wawili, mume na mke. Pia, ningeweza kuandika kitabu kuhusu namna ya kuwa na ndoa yenye mafanikio. Ningeweza hata kuandika kitabu kuhusu namna ya kutatua matatizo mbalimbali ambayo wanandoa hukabiliana nayo katika ndoa. Lakini sifanyi hivyo katika kitabu hiki. Nimeamua kuandika kitabu juu ya mada ambayo kwa kawaida huwa haijadiliwi.

    Kitabu hiki kinahusu uovu wa wake. Ninaandika kitabu hiki kuhusu uovu uliojificha chini ya uzuri wa wake wengi. Ikiwa unatafuta kitabu kizuri kuhusu ndoa, tafadhali tafuta kitabu kingine, kwa kuwa hiki si kitabu hicho.. Kitabu hiki kinahusu urembo, unyama ulio ndani ya baadhi ya wake wa wachungaji na jitihada walizonazo wachungaji juu ya wake zao. Wachungaji wengi huoa warembo! Lakini warembo wengi ni wanyama pia!

    Ninatambua kuwa watu wengi wataogopa kusema kuwa wake wazuri na wanaoonekana kuwa wema wanaweza kuwa na uovu ndani yao. Kama nilivyosema, sina nia ya kuwa na majadiliano ya usawa wa pande mbili kuhusu ndoa. Ikiwa unataka majadiliano yaliyo sawa kuhusu pande mbili za uzuri na ubaya wa wanaume na uzuri na ubaya wa wanawake, tafadhali acha kusoma sasa. Kitabu hiki kinahusu uovu wa wake, hasa uovu wa wake Wakristo na baadhi ya wake wa watumishi.

    Nabii Yeremia alilia kuhusu uovu ambao wake walikuwa wameutenda katika Yuda na katika Yerusalemu. Wake hawa hawakuwa wake wasioamini bali wake wa nyumba ya Israeli. Uovu ambao Yeremia aliusema ulikuwa uovu wa ibada ya sanamu na uasi dhidi ya Mungu. Pia, uovu ninaouandika unahusu uasi dhidi ya Mungu wa baadhi ya wake wa watumishi.

    Kwa hakika hiki ni kitabu kwa ajili ya watumishi na wake zao. Ni kitabu kinachoeleza kuhusu uzoefu ambao Wakristo walioyatoa maisha yao kwa Mungu na watu wa Mungu wanapitia katika ndoa zao. Kitabu hiki kwa hakika kinahusu hali ya mahusiano ambayo watumishi wanajikuta wanapitia, lakini hawawezi kuzungumza.

    Lakini, kama ukioa, huna hatia; wala mwanamwali akiolewa, hana hatia; lakini watu LAKINI KAMA HAO WATAKUWA NA DHIKI katika mwili nami nataka kuwazuilia hayo.

    1 Wakoritho 7:28

    Paulo alitabiri kuwa wale wanaooa watakuwa na matatizo katika mwili. Pengine ndiyo sababu hakuoa. Na si kwamba ninaandika kitabu hiki kwa sababu sijui mambo mabaya kuhusu wanaume. Ninayajua! Pia, si kwamba nimeandika kitabu hiki kwa sababu ninataka kuandika mambo mabaya kuhusu wanawake. Ninaamini sana katika huduma, upako, hekima na jukumu la wanawake wengi niliowateua na kuwachagua katika huduma. Sijui ye yote aliyewaona na kuteua wanawake wengi kama wachungaji kuliko nilivyofanya, ijapokuwa nina uhakika wapo wengine.

    Kadri unavyosoma, unaweza kujiuliza kwa nini silinganishi kati ya ubaya wa wanawake na ubaya wa wanaume. Sababu yake ni rahisi; siyo lengo la kitabu hiki! Ikiwa ningeandika kuhusu dhambi za kutisha za wanaume katika ndoa, ningeupoteza kabisa ujumbe niliopewa na Mungu. Ikiwa ningetakiwa kufanya hivyo, kitabu hiki kingekuwa kikubwa sana na watu kama wewe, ambao hamsomi vitabu sana, msingethubutu hata kujaribu kukisoma.

    Lengo la kitabu hiki ni kuelezea baadhi ya majukumu ya ajabu ambayo wanawake wamehusika katika maisha ya watumishi. Tunawasifu wanawake wetu na tunawashukuru kwa wajibu wao katika ndoa na huduma. Bila msaada wa wanawake, tusingefanya mengi katika kazi ya Mungu. Ninaamini kwamba moja ya siri ya kukua kwa kanisa ni kufanya kazi pamoja na wanawake na kuwapa nafasi.

    Wanawake husifiwa lakini njia zao mbaya husemwa kidogo, kwa sababu kila mmoja huogopa kuonekana mbaya au anapitia mambo magumu katika ndoa yake. Lakini sitapenda kuficha kitu chochote kitakacho kuwa na faida kwako

    … ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba,

    Matendo ya Mitume 20:20

    Uzuri ni halisi na unyama ni halisi pia! Machache yamesemwa kuhusu jukumu la wanawake kwa uharibifu katika huduma. Kitabu chetu, Biblia, hakiko kimya juu ya wajibu wa wanawake katika kuuharibu ulimwengu huu. Kupitia Hawa, maisha na huduma ya Adamu viliharibiwa. Kupitia Hawa, jamii yote ya wanadamu imeingizwa katika giza na shida.

    Kuna wachungaji wengi walio katika shida, giza na magumu kupitia wake zao warembo wa kuigiza.

    Sababu ya kitabu hiki ni kusaidia kutoa picha halisi kuhusu kile ambacho baadhi ya watu wanapitia.

    Sababu nyingine ya kitabu hiki ni kuwasaidia wale wanaokaribia kuchagua urembo. Ni muhimu kwao kutambua kuwa warembo wao wanaweza kugeuka wakawa wanyama! Ninatumai kuwa kitabu hiki kitawasaidia wanawake warembo wote wasigeuke kuwa wanyama.

    Akiwa bado hajaoa, John Wesley aliugua na akakaa na mwanamke ambaye baadaye akawa mke wake. Alielezea namna alivyokuwa mrembo, alivyokuwa anapendeza na alivyokuwa mzuri. Maneno yake yalikuwa ya ukumbusho. Sauti yake ilikuwa laini! John Wesley alivutiwa bila kupinga kwa upendo wake wa faraja! Kwa maneno yake, Molly, mkewe mtarajiwa, alimpa uhakika wa yote aliyohitaji.. Alielezea aina ya upendo aliokuwa nao kama upendo mzito! Alizungumza kuhusu upendo wenye wakfu Neno hili (wakfu) linazidi uwezo wangu wa kutafsiri. Eiii! Upendo wenye wakfu! Ninapenda kumnukuu John Wesley, alipomwona kwa mara ya kwanza mrembowake", Molly (kabla hajamuoa).

    John Wesley alisema, NILIKUWA NA UHAKIKA WOTE AMBAO MANENO YANAWEZA KUSEMA KUHUSU UPENDO MZITO NA UPENDO WA WAKFU

    Lakini siku moja, baada ya miaka kadhaa ya ndoa yao, alitumia maneno tofauti kabisa kumwelezea. Uzuri wake uligeuka na kuwa unyama. Siku moja mke wake alikuwa anaondoka nyumbani na kwenda safari. Huyu ni mwanamke aliyesema kuwa na upendo mzito wenye wakfu kwake. Alipokuwa anatoka mlangoni alimwambia: NINATUMAINI SITAUONA USO WAKO MBAYA TENA.

    Ninatumaini sitauona uso wako mbaya tena lilikuwa hitaji la John Wesley baada ya kumwona mnyama katika urembo wake. Huu ni mfano halisi wa mchungaji anayemwoa mrembo anayegeuka kuwa mnyama!

    Hakika, kitabu hiki kinadhamiria pia kuwaimarisha wale walio katika ndoa zilizo katika hali mbaya ya kufa. Ni matumaini yangu kuwa kitabu hiki kitasaidia kuzuia watumishi wasiwataliki wake zao kwa kuwapa uelewa wa kile wanachopitia.

    Nina uhakika watu wengi watatambua mambo yaliyo katika kitabu hiki yanayowahusu wao. Tumia ujuzi, ufahamu na hekima utakayopokea kutoka katika maneno haya kupigana vita vizuri vya imani. Ndoa ni moja ya majaribio tunayokumbana nayo na ni lazima tushinde! Kwa baadhi ya watu, ndoa ni faraja kubwa zaidi waliyowahi kupata! Kwa wengine, ndoa ni msalaba mkubwa waliowahi kuubeba! Wengine wana ndoa bora. Lakini si watumishi wote wana uzoefu mzuri au simulizi njema kuhusu ndoa zao. Hakika, kuna watumishi wengi ambao wanaweza kuzielezea ndoa zao kuwa ni vita.

    Watu wa Mungu wengi wakuu huzungumza kuhusu ndoa zao bora katika namna ambayo inawatisha na kuwachanganya Wakristo na wachungaji wengine. Watumishi wengine wanaposikia maelezo yao kuhusu ndoa zao, wananyong’onyea. Wow, wanajisemea mioyoni, Sithubutu kuzungumza kuhusu hali yangu ya ndoa na wabarikiwa hawa. (Hii hutokea pia wachungaji wanapohudhuria makongamano ya wachungaji na kusikia hadithi za ajabu kuhusu makanisa makubwa yenye maelfu ya washirika) Wachungaji wengi wa kawaida hujisikia kutishika kwa sababu hawana maelfu ya washirika wanaohudhuria katika makanisa yao.

    Wachungaji husikia maelezo ya kushangaza kutoka ndoa hizi za kuchora:

    Mke wangu ni mrembo zaidi ulimwenguni.

    Nina deni la maisha na huduma yangu kwa mke wangu!

    Sijui ningekuwa wapi bila kuwa na mke wangu!

    Kusingekuwa ‘mimi’ pasipo ‘wewe’!

    Hakuna aliye kama wewe! Hakuna mwingine anayeweza kuugusa moyo wangu kama unavyofanya!

    Siwezi kwenda mahali popote pasipo kuwa na mke wangu!

    mke wangu ni msaidizi wangu mkuu, mdau na msaada wangu!

    "Sijawahi kuzozana na mke wangu!’

    Kila siku ninamwambia mke wangu’ ninakupenda mara kumi!

    Siwezi kuiwazia kuishi bila mke wangu hata kwa siku moja!

    Mimi na mke wangu hulala usiku tukiwa tumekumbatiana!

    Mke wangu ndiye rafiki yangu wa karibu ulimwenguni!

    Ninapomkumbuka mke wangu, huwa ninabusu picha yake. Lakini nikimwona ninabusu kitu halisi!

    Mke wangu ni mwanamke mrembo zaidi katika ulimwengu wote, mwenzi wangu wa maisha, mwenzi wangu wa maisha, rafiki yangu, furaha yangu, mpenzi wangu na moyo wangu!

    "Ikiwa maksi zingetolewa kwa ajili ya ndoa nzuri, ningepata asilimia 99!’

    Wow! Hizi ni kauli za kupendeza! Laiti kila mmoja angeweza kusema mambo hayo yote yaliyo juu. Hizi ndiyo aina ya ndoa tunazohitaji ikiwa tunataka kufanikiwa katika huduma.

    Lakini huu si uzoefu ambao watumishi wote wanaupitia! Ninajuaje? Ninajua kwa sababu nimekuwa katika huduma kwa miaka mingi na ninawafahamu maelfu ya wachungaji. Pia ninalijua hili kwa undani kwa sababu ya kiwango cha talaka miongoni mwa wachungaji. Watumishi wengi wamesema kauli hizo juu, kuonyesha upendo mkubwa zaidi ya wote, na baadaye wanatangaza kuwa wanatalikiana.

    Kwa watu wengine, kinyume cha sentensi hizi kinaweza kuwa kweli. Wapo baadhi ya wachungaji ambao wangependa kusema mambo kama:

    "Mke wangu ni mwanamke mrembo zaidi ulimwenguni, lakini si rahisi kuishi naye!’

    Laiti ningeokolewa kutoka kwa mke wangu!

    Mke wangu ndiye mpinzani mkuu wa maisha na huduma yangu.

    Mke wangu ndiye mshtaki na mtesaji mkuu wa maisha yangu!

    Hatujafanya mapenzi kwa miezi kadhaa!

    Mimi na mke wangu hatuzungumzi tangu mwezi uliopita!

    Huwa simwambii mke wangu, ‘Ninakupenda’ kwa sababu sitaki kusema uongo!

    Naisubiri siku ambapo sitakuwa na mke wangu!

    Mimi na mke wangu kila mmoja analala pembezoni mwa kitanda!

    Siko karibu na mke wangu tena!

    Simkumbuki mke wangu tena. Kila ninapoiona picha yake, ninalia kwa huzuni moyoni mwangu!

    Ndoa yangu ni kosa kubwa la maisha yangu!

    Ningekuwa na mke tofauti, ningefanikiwa mengi katika huduma.

    Wengi wetu hutenda kama waganga wa kienyeji wa Afrika linapokuja suala la ndoa. Kwa nini ninasema hivyo? Daima mganga wa kienyeji wa Afrika huwa na kipande kimoja cha dawa kinachotakiwa kutibu magonjwa yote. Kipande hiki cha dawa kinaweza kutibu ugonjwa wa macho, jino, bawasiri, shinikizo la damu, kisukari, kansa, uvimbe, pumu, maumivu ya kiuno, nguvu za kiume, kuvimbiwa, kuhara, udhaifu wote, ugumba nk. Utamsikia mganga wa kienyeji akitangaza dawa yake na kuwashawishi hadhira yake kwa bidii kubwa. Ni wajinga tu ndiyo huyaamini madai kwamba dawa moja inaweza kutibu magonjwa hayo yote. Tunajua kuwa dawa moja haiwezi kutibu uwezo wako wa kuona, maumivu ya paja, kuhara, vipele pamoja na shinikizo na damu.

    Na linapokuja suala la ndoa, watu wengi wana mfumo mmoja wanaoutumia kwa ndoa zote. Hudhani ndoa zinafanana na hivyo hutumia mfumo sawa kwa kila aina ya ndoa. Hili ni kosa kubwa kwa sababu kuna aina tofauti za ndoa.

    Katika baadhi ya matukio, unakuwa na mume mwaminifu sana anayefanya kila kitu ambacho mume anapaswa kufanya. Na wakati mwingine mume mwaminifu ana mke mzuri anayefanya mambo ambayo mke mwaminifu anapaswa kufanya. Kwa upande mwingine, mume mwaminifu anaweza kuwa na mwanamke mbaya kama mke wake. Mke mwaminifu anaweza kuwa na mume mwovu asiyepaswa kuwa na mke.

    Hali nyingi zinapaswa kueleweka kutokana na tukio husika. Ni makosa kusulubisha vyote vizuri na vibaya kwa siku moja. (Yesu Kristo alisulibiwa pamoja na wezi na ilitoa taswira kuwa Yesu Kristo alikuwa mwizi aliyezoeleka, kwa sababu alitendewa kama ambavyo mwovu wa kawaida angetendewa).

    Kila ndoa hutoa uzoefu tofauti. Baadhi ya watu wanapaswa kufuata Hatua saba kwa ndoa nzuri na hupata furaha kubwa. Kuna wengine wanaweza kufuata Hatua saba kwa ndoa nzuri, lakini hawatakuwa na furaha.

    Hakika, nimekutana na watu wasiooleka.. Hawawezi na pengine wasiolewe kwa sababu hawastahili kuwa katika ndoa. Hawawezi kamwe kuwa na furaha katika hali yoyote ya ndoa. Kwa bahati mbaya mwanamke asiyeoleka anapokuwa mrembo, huingizwa katika ndoa haraka haraka na anaishia kumsababishia mchungaji mazingira yasiyovumilika. Ushauri anaopewa mtu asiyeoleka lazima uwe tofauti na ushauri anaopewa mtu wa kawaida.

    Kitabu hiki kimeandikwa ili kuwashauri watu walio katika aina Fulani ya ndoa. Uwe makini ikiwa uko katika mojawapo ya ndoa nzuri kwa sababu unaweza ukajaribiwa ukaanza kukosoa ndoa usizozielewa.

    Katika kitabu hiki chote, kwa makusudi sitataja baraka binafsi nilizofurahia katika ndoa yangu mimi mwenyewe. Pia, sitasema changamoto katika ndoa yangu. Kwa nini? Kwa sababu ikiwa nitataja baraka za ndoa yangu mwenyewe, unaweza ukahisi kutishika na ukadhani kuwa ndoa yako si nzuri. Kwa hakika, ikiwa ninazungumza kuhusu changamoto zangu mwenyewe, pengine hutazielewa! Hivyo ubarikiwe tu na upokee uponyaji kwa ajili ya maisha na ndoa yako kupitia maneno katika kurasa hizi.

    SURA YA 2

    Onyo: Mabadiliko ya Mizani ya Mamlaka Katika Ndoa za Watumishi

    Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, LAKINI MIMI SITATIWA CHINI YA UWEZO WA KITU CHOCHOTE.

    1 Wakoritho 6:12

    Inavutia kuangalia mabadiliko ya mizani nguvu miongoni mwa wanyama. Kuangalia kundi na kiburi cha simba wanaoingia katika kundi la tembo kinaweza kukupa ufunuo mkubwa kuhusu namna mizani ya nguvu inavyoweza kuhama kutoka kundi moja kwenda lingine. Mchana, tembo wanaweza kuona vizuri na kuua simba yeyote anayewakaribia. Tembo hawafanyi mzaha nyakati za mchana wanapowaona simba.

    Lakini usiku unapoingia, simba wanaona vizuri na tembo hawaoni vizuri. Mizani ya mamlaka huhamia kwa simba, na wanaweza kuwashambulia na kuwaua tembo. Simba wamejulikana kuwaua tembo nyakati za usiku mizani ya mamlaka inapobadilika. Ni jambo la kushangaza kuona simba wakimla tembo!

    Ndoa pia hupata mabadiliko ya mizani ya mamlaka. Kuna njia mbili ambazo mizani ya mamlaka inaweza kuhama.

    Ndoa kwa asiye mwamini (au mume X5 na A1 kuwa bora zaidi), mizani ya mamlaka huhamia kwa mwanaume. Mtu asiyeamini, au mume X5, hafungwi na Neno la Mungu. Hana utii kwa Biblia. Atafanya cho chote kinachomfurahisha. Mke Mkristo aliye mtiifu atajinyenyekeza kujaribu kumfurahisha ili abadili tabia yake. Biblia imejaa simulizi za waume waliowatendea vibaya wake zao. Sheria nyingi za talaka zinawapendelea wanawake kwa sababu wamekuwa wakitendewa vibaya na wanaume wasio waamini kwa karne nyingi.

    Kitabu hiki hakizungumzii ndoa za aina hiyo. Kitabu hiki ni kwa ajili ya watumishi. Ikiwa wewe si mtumishi hupaswi kuwa unasoma kitabu hiki kwa sababu hakikuandikwa kwa ajili yako. Usikosoe jambo usilolielewa. Sisemi pia kuwa watu walio katika huduma watakuwa na ndoa mbaya. Ninasema kuwa mizani ya uwiano wa nguvu hubadilika. Mwanamke ana uwezo mkubwa wa kuharibu huduma ya mumewe.

    Katika ndoa kwa mume na mchungaji mtiifu (mume A1), mizani ya mamlaka huhamia kwa mwanamke. Mtu wa Mungu anatakiwa kutii Neno la Mungu, na hivyo mke wake anaweza kufanya karibia kitu chochote pasipo kutalikiwa. Matokeo yake mizani ya mamlaka au mamlaka imehamia kwa mwanamke, na anaweza kusababisha maovu mengi kwa mumewe A1. Hii humfanya mke kuwa na nguvu sana.

    Mchungaji A1 ameapa kutotalikiana au kutengana na mkewe, bila kujali chochote kitakachotokea! Cha kushangaza, kwa kuithamini ndoa kunampa mkewe nguvu kubwa ya kuenenda vibaya. Ndivyo ambavyo waajiriwa ambao hawawezi kufukuzwa kazi huenenda. Vyo vyote anavyofanya, hawezi kufukuzwa na hivyo nguvu na uasi wake hukua.

    Je! Umefungwa kwa mke? Usitake kufunguliwa. Umefunguliwa? USITAFUTE MKE.

    1 Wakoritho 7:27

    Kwa nini Paulo anawashauri Wakristo wasitafute mke? Kwa nini

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1