Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Wale Wana ambao ni Hatari
Wale Wana ambao ni Hatari
Wale Wana ambao ni Hatari
Ebook144 pages7 hours

Wale Wana ambao ni Hatari

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

"Pengine mmoja wa maadui wakubwa ambaye utawahi kukutana naye ni "mshtaki kati ya ndugu". Pokea maelekezo juu ya namna silaha hii ya mashtaka inavyotumiwa na ujifunze namna ya kuishinda, unavyosoma kitabu hiki cha kiwango cha juu, cha Dag Heward- Mills.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345538
Wale Wana ambao ni Hatari
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Wale Wana ambao ni Hatari

Related ebooks

Reviews for Wale Wana ambao ni Hatari

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Wale Wana ambao ni Hatari - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Namna ya Kumpata Baba

    Kwakuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia yaInjili.

    1Wakorintho 4:15.

    Zawadi ya kupata baba ni nadra. Si kila mtumishi wa Mungu ni baba. Si kila mtu anayefundisha Neno la Mungu ni baba. Si wahubiri na walimu wageni wote wana sifa ya kuwa baba.

    Si kila nabii ni baba, na Paulo alilieleza jambo hili kwa Wakorintho.

    Baba ni Zawadi Nadra

    Kutakuwa na watu wengi watakaokuwa na mchango mzuri katika maisha yako. Wakufunzi na walimu ni wengi lakini hawa ni tofauti na baba. Mchango wa baba ni mkamilifu. Baba hukupatia fungu kamili ambalo ni zaidi ya mafundisho mazuri. Mwalimu anajali sana kutoa somo zuri. Nabii anajali kutoa huduma ya nguvu za Mungu kwa njia ya maono, ndoto na neno la maarifa. Lakini baba anajali zaidi hali ya maisha yako yote.

    Kwa sababu kazi ya baba ina mambo mengi, ndiyo maana baba si wengi! Ni rahisi kupitia maelezo yaliyoandaliwa kuliko kutoa uangalizi kamili. Watu wanaweza kuwa wagumu na wasio na shukurani kiasi kwamba ni baba tu anaye weza kuwastahimili kwa kipindi kirefu.

    Kuna wachungaji wengi, wainjilist lakini nani awezaye kumpata nabii mwenye sifa ya baba? Ndiyo maana Paulo alisema: Kwakuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi.

    Sifa kuu ya baba siyo umri wake bali uwezo wake wa kuzaa watoto wanaofanana naye. Kinyume na maoni kadhaa, kuna vijana wengi wenye moyo wa baba.

    Kwa kawaida, watu mara nyingi huwa baba katika umri mdogo. Uthibitisho wa ubaba uko ndani ya watoto ambao wamezaliwa na baba. Hubeba upendo, kujitoa na uvumilivu kulea watoto. Mwisho wake watoto huthibitisha ubaba wako.

    Kama utalinganisha huduma ya Eliya na ile ya Elisha, kwa mfano, utaona tofauti kati ya nabii mwenye sifa ya baba na nabii asiye na sifa ya baba. Tofauti hizi zinakuwa wazi zaidi unaposoma kwa makini huduma zao. Kwa kulinganisha huduma ya Eliya na ile ya Elisha, mara moja utaona tofauti kati ya mtu mwenye moyo wa baba na yule asiyekuwa nao.

    Eliya na Elisha wote walikuwa manabii mahiri. Lakini Eliya alikuwa na karama ya nyongeza ya kuwa baba. Ndiyo maana alikuwa na mrithi wa huduma yake. Elisha hakuwa na mrithi. Alimlaani Gehazi ambaye angekuwa mrithi wake. Alimlaani Gehazi kwa kufanya makosa katika mambo ya fedha. Moyo wa baba haumlaani mtoto wa pekee.

    Roho ya baba ni kile kitu kinachosababisha mtu wa Mungu kuzaa watu kama yeye mwenyewe katika huduma. Kwa maneno rahisi ni kwamba, karama ya baba ni udhihirisho wa upendo wa Mungu. Inahitajika upendo ili kuwalea watu wasioelewa ni kitu gani wanachofanyiwa.

    Inahitajika upendo kuwalea watu ambao hawatakuelewa kwa miaka mingi. Hakika, Mungu hutuma walimu wengi sana ambao huhudumia maisha yetu. Watafundisha masomo na mambo muhimu ya mafundisho makuu. Lakini baba atakwenda hatua nyingi zaidi. Pamoja na kukufundisha atakuonyesha upendo na uvumilivu unaohitajika kukufikisha katika kusudi kamili la Mungu.

    Mchakuro kwa ukamilifu humfanya mtumishi atafute ukamilifu wakati wote. Watu wanaotafuta ukamilifu wakati wote sio baba wazuri. Mara nyingi hawaoni kwamba neema ya Mungu inafanya kazi pole pole katika maisha ya mtu fulani. Wao hukazia ukamilifu wakati wote, kitu ambacho hakiwezekani kwa binadamu.

    Unaweza kumpokea mtu wa Mungu kama mwalimu. Pia unaweza kumpokea kama mchungaji. Unaweza kumpokea mtu wa Mungu kama nabii au mwinjilisti. Inawezekana pia kumpokea kama baba.

    Nakutakia upate baba katika maisha haya! Na upate uwezo wa kupenda na kuwa baba wewe mwenyewe.

    Sura ya 2

    Namna ya Kutambua na Kuwapokea Baba Tofauti katika Majira Tofauti Maishani

    Mungu atakutumia baba tofauti katika nyakati tofauti.

    Kwakuwa ijapokuwa mna waalimu kumi elfu katika Kristo, walakini hamna baba wengi. Maana mimi ndiye niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya injili.

    1Wakorintho 4:15.

    Mungu atatuma watu kadhaa kukulea. Wa kwanza kabisa ni baba yako wa kimwili ambaye ni lazima umpokee vyema. Usimuone baba yako wa kimwili kama mzee wa zamani ambaye haendani na uhalisia wa maisha ya kisasa. Kumwona baba yako wa kimwili kama mtu aliyepitwa na wakati kutakuzuia kupokea hekima yake kuu.

    Huyu baba yako wa kimwili atakuwa na mipaka yake katika kukulea. Mara mwendo utaanza na mtu mwingine atakayetumwa na Bwana kuwa baba yako atajitokeza. Kwa huduma yake, utapokea malezi ya baba unayohitaji kuyapata ili kwenda hatua nyingine ya maisha yako. Kisha mtu mwingine anaweza kuinuka na kuwa baba yako katika maisha yako. Mbio za kupeana kijiti huendelea! Kijiti cha ubaba kinatoka mtu mmoja kwenda mwingine.

    Kuna mambo mengi ambayo baba yako wa kimwili hawezi kukuambia. Labda angezungumzia kila kitu, lakini hafanyi hivyo. Kwa wengi wetu, wazazi wetu hawakutupatia hatua kwa hatua ushauri wa namna ya kuchagua mke au mume. Wazazi wengi wa kimwili walitoa maoni tu kuhusu mambo mbali mbali katika ndoa.

    Mara nyingi hapo ndipo wanaweza kufika kuhusu ushauri wa ndoa. Ashukuriwe Mungu kwa ajili ya wachungaji ambao hupokea jukumu hilo na kuwaongoza watoto katika ndoa. Mara kwa mara wachungaji huwa ndio wazazi wanaofuatia katika mbio hizi za kupeana kijiti.

    Siku moja binti yangu aliniuliza swali, Baba, hivi watu hupataje mimba?

    Nilishtushwa na swali hilo lakini nikajibu, Mungu huwawezesha kupata mimba.

    Lakini akasisitiza, Ninajua kwamba Mungu huwawezesha kupata mimba, lakini inatokeaje?

    Nilisita katika kujibu na nikamudu kubadili mazungumzo. Baadaye mke wangu akaniambia, Nilazima uongee na watoto wako kuhusu kujamiiana.

    Nikamjibu, Kwanini nifanye hivyo? Nitamke mambo hayo kwao.

    Tulianza kubishana na akasema, Wewe ni kichwa cha nyumba kwahiyo unapaswa kuwaeleza.

    Lakini nikamjibu, Wewe ni mama yao na wewe husema nao mara nyingi, hivyo kwa nini usiseme nao jambo hili?

    Akaendelea kusema, Ni wajibu wako na ni lazima utimize jukumu lako!

    Lakini sikukubali. Nilitumia mamlaka yangu kama kichwa cha nyumba nikampa jukumu la kuongea na watoto kuhusu mambo haya yote.

    Unaona, tulikuwa tumefika mahali uwezo wetu wa baba na mama ulikuwa unyumba. Tulitamani kwamba Mungu angetuma watu wengine kuwahudumia watoto wetu kama nasi tulivyokuwa tukiwahudumia watoto wa wengine. Tulikuwa tunaomba kwamba baba atakayefuatia katika mbio hizi angejitokeza mara moja na kuwapa watoto mwongozo salama.

    Kati ya mamia ya wakufunzi na walimu, ni muhimu wakati wote kutambua nani ni baba. Baba wana upeo mkubwa katika kujali maisha yako. Mchango wao unakwenda zaidi ya yale wayasemayo. Utagundua kwamba huduma yao hujihusisha na maisha yako yote. Huduma yao ina matokeo makubwa na ya ajabu katika maisha yako.

    Moja ya vigezo vya kumtambua baba ni kutambua upendo, kujali mwongozo wa Baba yetu wa Mbinguni kwa mwelekeo wake katika maisha yetu.

    Watu wengi hufikiri kimakosa kwamba kifungu hiki cha maandiko husema mnao walimu elfu kumi lakini mna baba mmoja. Andiko hili husema kwamba hamna baba wengi. Kwa maneno mengine kinasema kwamba mna baba wachache.

    Yesu alisema, Msimuite mtu yeyote baba.

    Wala msimuite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

    Mathayo. 23: 9.

    Hii ni kwa sababu hakuna binadamu anyeweza kutosheleza kuwa impasavyo baba. Watu wote hupungukiwa katika jukumu hili na ni Baba wa Mbinguni pekee ambaye hutoa kielelezo halisi cha baba.

    Je hujatambua jinsi ambavyo baba wa duniani hushindana na kupigana na watoto wao? Hata baba wa kimwili wanaweza kusababisha maumivu na mateso makali kwa watoto wao.

    Watu wengi huwachukia baba zao. Na kuna watu wengi ambao maisha yao yameharibika kwa sababu ya wazazi wao. Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba kuwa baba kwa njia ya binadamu wa kawaida kuna mapugufu mengi. Hii ndio sababu kunahitajika kile ninachokiita, Mbio za kupeana.

    Mbio hizi za kupeana huhusisha Mungu kutuma mtu mmoja baada ya mwingine katika awamu tofauti za maisha yako na huduma. Ni muhimu kutambua hawa watu mbalimbali wanapokuja maishani mwako.

    Hiki ndicho Yesu alichokifafanua kwa mfano katika Mathayo 21. Hakika tutahukumiwa kwa jisi tunavyowapokea baba tofauti watumwao na Mungu kwetu.

    Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri. Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale waklima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe. Akawatuma tena watumwa wengine wengi kuliko wa kwanza, wakawatenda vile vile. Mwishowe akamtuma mwanawe kwao, akisema, Watamstahi mwanangu. Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi, haya na tumwue, tuutwae urithi wake. Wakamkamata, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu wakamwua.

    Mathayo 21:33 – 39.

    Mungu hutuma baba kadhaa katika maisha yetu na mara nyingi hatuwafahamu. Wakati mwingine watu hupigana na baba zao! Tunapaswa kujifunza baba wanaotumwa na Mungu katika maisha yetu.

    Je, kuna tofauti gani katika kumpokea baba na kumpokea mkufunzi?

    Kumpokea mkufunzi kunahusisha kupokea masomo anayotoa kutoka neno la Mungu. Kumpokea baba kunahusisha kumpokea mtu Fulani kwa namna kwamba huduma muhimu iletayo uhai itakujia.

    Kwa kawaida, baba yako wa kimwili ana mvuto mkubwa kwako kwa amna nyingi. Yeye hukufundisha namna ya kula, kuvaa na kuishi. Hukupatia hekima, ushauri na masomo machache kuhusu maisha. Yeye huwa kielelezo cha maisha na huwa ni chanzo cha hamasa na mwelekeo katika maisha.

    Linganisha haya na walimu wako wa shule. Walimu hawa hawatoi mwongozo kamili kama wanavyofanya

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1