Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Stadi ya Usikivu [toleo la 2]
Stadi ya Usikivu [toleo la 2]
Stadi ya Usikivu [toleo la 2]
Ebook187 pages7 hours

Stadi ya Usikivu [toleo la 2]

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Hakuna somo lenye umuhimu zaidi ya kuwa ndani ya mapenzi makamilifu ya Mungu. Kitu kimoja ambacho kitawatofautisha wahudumu wa injili ni uwezo wao wa kusikia sauti ya Mungu kwa usahihi. Ni jinsi gani ilivyo muhimu kufuata Roho Mtakatifu katika mapenzi makamilifu ya Mungu. Pale unapokuwa ndani ya mapenzi makamilifu ya Mungu, utastawi na kufikia yote unayotamani kwa ajili ya Mungu. Kazi hii bora ya Dag Heward- Mills itakuwa na mguso mkubwa sana katika maisha yako na huduma yako.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781613958537
Stadi ya Usikivu [toleo la 2]
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Stadi ya Usikivu [toleo la 2]

Related ebooks

Reviews for Stadi ya Usikivu [toleo la 2]

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Stadi ya Usikivu [toleo la 2] - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Mapenzi Kamili ya Mungu na Mapenzi Yasiyo Kamili

    … mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendezaa, na ukamilifu.

    Warumi 12:2

    apenzi ya Mungu yanaweza kuelezwa kuwa ni, hali ya mtu kuwa mkamilifu au kutokuwa mkamilifu. Mapenzi ya Mungu yasiyo makamilifu yanaitwa hivyo kwa sababu yanafanana na mapenzi kamili ya Mungu lakini siyo mapenzi halisi katika yale anayotaka Mungu.

    Mapenzi kamili ya Mungu ni ukamilifu, ukomavu na mapenzi makamilifu ya Mungu. Mapenzi yasiyo kamili ya Mungu ni yale ambayo Mungu anawakubalia watu wafanye hata kama si chaguo lake la kwanza kwao.

    Mapenzi Makamilifu ya Mungu

    1. Mapenzi kamilifu ya Mungu ni mahali ambapo Mungu hasa anataka wewe uwepo. Mungu anapendezwa na       wewe wakati unapokuwa katika mapenzi yake kamili na       anafurahishwa wakati jina lako limeonyeshwa.

    2. Katika mapenzi makamilifu ya Mungu, unawekwa mahali bora, panapofaa katikachimbuko la mpango kamili wa       Mungu.

    3. Katika mapenzi makamilifu ya Mungu, ni hali ya kupata mahitaji kamili ambayo Mungu amekuyakusudia kwa ajili yako.

    Mapenzi ya Mungu Yasiyo Makamilifu

    1. Mungu huwakubalia watoto wake wafanye mapenzi yasiyokuwa makamilifu kama matokeo ya uasi wao na kukataliwa kwao katika chimbuko la mpango kamili wa Mungu.

    2. Unapokuwa katika mapenzi yasiyokuwa makamilifu, Mungu hapendezwi kabisa na wewe. Mungu anakutunza,       anakuvumilia  na anakupa muda wa kutubu.

    3. Katika mapenzi ya Mungu yasiyokuwa makamilifu unaweza kuonekana kuwa una upendeleo wa Mungu usio kamili katika huduma kwa Bwana na hutimizi chimbuko la kusudi la kusudi la Mungu kwa maisha yako.

    4. Mapenzi ya Mungu yasiyo kamili ni mahali ambapo umejitwalia na pia iliyokosa sifa kwa kazi yako.

    Kuacha Mapenzi Makamilifu ya Mungu na Kufanya Mapenzi Yasiyokuwa Makamilifu

    Katika Biblia nzima, utaona mifano ya Mungu akiwakubalia watu wafanye mambo waliyoyataka ingawa hayakuwa katika mapenzi yake kamili. Wakati mwingi, watu wa Mungu walijawa na uasi na chuki juu ya mapenzi kamili ya Mungu. Badala ya kuwapatia hukumu hapo hapo, Mungu aliwakubalia watu wake wapotee katika mapenzi yake (ya kujitakia, yasiyofaa, yasiyokubalika, yasiyo bora) yasiyokuwa makamilifu na halafu kupokea mapigo ya kweli wanayostahili kwa uasi wao!

    Katika kitabu hiki, utagundua jinsi Mungu anavyowakubalia watu kuwa na mfalme lakini baadaye humtumia mfalme huyo kwa kuwaadhibu. Mungu huwakubalia watu wawe na mafanikio lakini baadaye hutuma udanganyifu na ukengeufu katika nafsi zao. Huwakubalia watu wajenge sanamu na kisha huziharibu tena sanamu hizo.

    Mungu huwakubalia manabii waende katika kutimiza ujumbe wao maalumu, lakini baadaye hutuma punda kwenda kuwapinga.

    Mungu hajipingi mwenyewe kwa kuwakubalia watu wapotee katika mapenzi yake yasiyokuwa makamilifu. Hali hii ni mwitikio wake kwa uasi, ukaidi na kukataliwa kwa mapenzi yake makamilifu. Mwishoni, watu wote hupokea hukumu ya Mungu ya kujitakia, inayostahili na iliyoandaliwa hasa!

    Watu wengine huita mapenzi haya yasiyokuwa makamilifu kuwa ni  mapenzi yenye uhuru wa kutenda unachoona au kutaka. Mapenzi haya ya Mungu yasiyo makamilifu ni sehemu ambayo watumishi wengi wa Injili hushughulika nayo. Baadhi ya watu hutoa maisha yao yote katika mapenzi haya ya Mungu yasiyokuwa makamilifu.

    Kila jambo huonekana kuwa sawa kwa watu walio katika mapenzi ya Mungu yasiyo makamilifu. Huduma zao zinastawi na fadhila ya Mungu inaonekana kuwa juu ya kila kitu wanachofanya. Lakini mafanikio tele na dhahiri hayana maana kwamba Mungu anapendezwa nawe.

    Wengi wetu tunadanganywa na fadhila hizo dhahiri na ambazo ndizo watu huziita kuwa ni baraka.

    Fedha na mafanikio tele haviwezi kuwa ishara kwamba Mungu anapendezwa nawe. Shetani pia hutoa fedha kwa wale wanaomtumikia. Shetani alimwambia Yesu amsujudie naye angempatia ulimwengu wote.

    Uwepo wa Mungu na sauti ya Roho Mtakatifu ndiyo mambo unayotakiwa kuyatafuta na siyo uwepo wa fedha au kitu chochote kile cha kimwili!

    Unapoanzisha uhusiano na waziri ni lazima uangalie ikiwa uwepo wa Mungu uko ndani yake. Ni lazima utazame kama sauti ya Mungu na Neno la Bwana vimo ndani yake.

    Biblia imejaa mifano ya watu wa Mungu walioachilia mbali mapenzi makamilifu ya Mungu na kujiingiza katika mapenzi yasiyokuwa makamilifu. Mungu huonekana anawabariki watu walio nje ya mapenzi makamilifu lakini kweli hapendezwi nao.

    Sasa tuone baadhi ya mifano ya watu waliojiingiza katika mapenzi ya Mungu yasiyokuwa makamilifu.

    1. ISRAELI WALIFANYA MAPENZI YA MUNGU YASIOKUWA MAKAMILIFU KWA KUDAI KUWA NA MFALME.

    Kuwa na mfalme lilikuwa ni jambo lisilostahili, wala halikuwa kusudi la Mungu lililopevuka kwa Israeli. Lakini Mungu aliwakubalia juu ya jambo hili na kumwambia Samweli faraghani kuwa watu walikuwa wamemkataa Yeye.

    Kuwa na mfalme hayakuwa mapenzi makamilifu ya Mungu lakini bado Mungu aliwakubalia. Kama utakavyoona, mpango huu haukugeuzwa kabisa na wana wa Israeli nao waliteseka mno wakiwa chini ya uongozi wa wafalme wao.

    Ni jambo la maana kutodanganywa wakati Mungu anakukubalia mambo kadhaa muhimu kwa dhahiri. Moyo wa kweli wa Mungu unajidhihirisha kwa mtu ambaye yuko karibu naye kwa moyo wa dhati kabisa.

    Muda wote tunafanya hayo hayo na tunasema mambo ambayo kisiasa ni haki tunapokuwa kwenye umma wa watu, lakini wakati huo tukidhihirisha mioyo yetu jinsi ilivyo kila mahali. Lazima ujifunze kumtafuta Mungu kwa akili yako timamu na moyo wako halisi.

    Mungu alihuzunika wakati alipomruhusu Samweli ateue Mfalme. Alijua angekataliwa na watu. Alijua watu walikuwa wanawatumia watoto wa Samweli kama kisingizio cha kumkataa Yeye. Mungu aliridhia ombi lao lakini mambo yote yasingekuwa mema kwa Israeli. Angalia vizuri wakati Mungu anapokukubalia mambo katika maisha yako ambayo kwa hakika hayapendi.

    Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama,

    Wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako, basi tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.

    Lakini neno hilo likawa baya machoni pa Samweli, waliposema, Tupe mfalme atuamue. Naye Samweli akamwoimba BWANA. BWANA akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.

    1 Samweli 8:4-7

    2. BALAAMU ALIACHA MAPENZI KAMILI YA MUNGU WAKATI ALIPOENDELEA KUOMBA NAFASI YA KUTOA UNABII KWA MFALME WA MOABU.

    Mungu aliweka jambo hili wazi kwa Baalamu kwamba hakupenda awe na jambo lolote la kufanya na Balaki mfalme wa Moabu. Hata hivyo, Baalamu alitaka hasa achukue fedha ambazo Balaki alizitoa. Alimlazimisha Bwana ili amkubalie azungumze na mfalme. Mwishoni, Bwana akasema aende. Mungu akampa ushauri jinsi ya kuongea nao. Wakristo wa siku hizi wangechukulia jambo hili kuwa ni mapenzi. Aya hii imewekwa kutuonya kwamba mapenzi ya Mungu yanaonekana yanaturuhusu tufanye mambo yetu wenyewe wakati Mungu anafahamu kwamba tumejawa na uasi.

    Mungu akamjia Balaamu, akasema, Ni watu gani hawa ulio nao pamoja nawe?

    Balaamu akamwambia Mungu, Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, amewatuma kwangu, akisema,

    ‘Tazama, kuna watu waliotoka Misri, wanaufunika uso wa nchi; basi njoo unilaanie watu hawa; labda nitaweza kupigana nao, na kuwafukuza.’’’

    MUNGU AKAMWAMBIA BALAMU, USIENDE PAMOJA NAO; WALA USIWALAANI WATU HAWA, MAANA WAMEBARIKIWA.

    Balaamu akaondoka asubuhi akawaambia wakuu wa Balaki, Enendeni zenu hata nchi yenu; kwa maana BWANA amekataa kunipa ruhusa niende pamoja nanyi.

    Wakuu wakaondoka wakenda kwa Balaki, wakasema, Balaamu, anakataa kuja pamoja nasi

    Basi Balaki akatuma wakuu mara ya pili, wengi zaidi wenye cheo wakubwa kuliko wale wa kwanza.

    Wakamfikilia Balaamu, wakamwambia, Balaki mwana wa Sipori asema hivi, Nakusihi, neno lolote lisikuzuie usinijie; maana nitakufanyizia heshima nyingi sana, na neno lolote utakaloniomba mitalitenda; basi  njoo, nakusihi, unilaanie watu hawa."

    Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.

    Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua BWANA atakaloniambia zaidi.

    MUNGU AKAMJIA BALAAMU USIKU, AKAMWAMBIA, KWA KUWA WATU HAWA WAMEKUJA KUKUITA, ENENDA PAMOJA NAO; LAKINI NENO LILE NITAKALOKUAMBIA NDILO UTAKALOLITENDA, BASI.

    Balaamu akaondoka asubuhi, akatandika punda wake , akaenda pamoja na wakuu wa Mobu.

    HASIRA YA MUNGU IKAWAKA KWA SABABU ALIKWENDA, malaika wa BWANA akajiweka njiani, ili kumpinga. Basi alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.

    Hesabu 22:9-22

    3. WANA WA ISRAELI WALIACHA MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU WAKATI WALIPOTAMANI MAFANIKIO.

    Wakayasahau matendo yake kwa haraka; hawakulingojea shauri lake. Bali walitamani sana jangwani, wakamjaribu Mungu jangwani. Akawapa walichomtaka, akawakondesha mioyo zao.

    Zaburi 106:13-15

    Wana wa Israeli, kama vile kanisa la leo, walitamani fedha. Kama ilivyotokea katika siku hizo, Bwana aliwapa wahubiri wa mafanikio ambao walitumia Neno kuhalalisha uchu wao kwa mambo ya kidunia.

    Msisitizo wa kupita kiasi juu ya mahubiri ya mafanikio uliofanywa na watumishi wake  ulivutia na kuonekana kuwa ni mapenzi ya Mungu. Mkusanyiko wa umati wa watu na mafanikio dhahiri ya huduma nyingi unatoa msukumo kwamba Mungu anafurahia vitu vyote.

    Ilionekana kwamba Mungu aliwajibu Waisraeli’ waliotamani mafanikio lakini walikuwa katika mapenzi ya Mungu yasiyo makamilifu kwa sababu Mungu aliwaadhibu kwa kutamani mafanikio hayo. Na hukumu ilikuwa ni kukondeshwa kwa nafsi zao.

    Mungu asingwaadhibu kama wangekuwa wanafanya mambo yaliyo ya haki.

    Mungu anataka watoto wake wastawi lakini si kwa kutumia njia mbaya na makusudi mabaya. Aliwapatia mafanikio kwa sababu hayuko kinyume nayo. Leo, Mungu analipatia Kanisa lake mafanikio lakini inaoenekana yanafuatana na kudhoofika kwa nafsi, kupungua kiroho, magonjwa, talaka, tabia mbaya na ubasha. Tuwe macho na mambo tunayomlazimisha Mungu atupatie kwa sababu tunaweza kukosa furaha na na kuzipata adhabu zinazofuata wale wanaokwenda wakisisitiza katika njia zetu wenmyewe.

    4. WANA WA ISRAELI WALIFANYA MAPENZI YA MUNGU YASIYO MAKAMILIFU WAKATI WALIPOMLAZIMISHA HARUNI ATENGENEZE NDAMA.

    Wana wa Israeli walionekana kufuata njia yao wenyewe walipohitaji kwamba Haruni atengeneze miungu ya kuwaongoza.

    Haruni alipowatengenezea ndama, lazima walidhani kuwa Mungu alikuwa ameanzisha dini ambayo ilihusisha kuabudu sanamu.

    Katika dini yao mpya Waisraeli walishangilia wakidhani kwamba Mungu aliithibitisha kwao kwa sababu Haruni alihusishwa.

    Lakini hawakufanya mapenzi ya Mungu ingawa inaonekana kwamba waliongozwa na mtu wa Mungu. Haingechukua muda mrefu bila kuvuna hukumu ya kufnya mapenzi ya Mungu yasiyo makamilifu.

    Watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.

    Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.

    Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.

    Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sananmu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

    Kutoka 32:1-4

    Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kuyeyuka.Wakaubadili utukufu wao kuwa mfano wa ng’ombe mla majani.

    Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri; Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha bahari ya Shamu.Akasema ya kuwa kama Musa, mteule wake, asingalisimama, mbele zake kama mahali palipobomoka, Ili aigeuze hasira yake asije akawaharibu.

    Zaburi 106:19-23

    5. NADABU NA ABIHU WALIFANYA MAPENZI YA MUNGU YASIYO MAKAMILIFU WAKATI WALIPOTOA SADAKA AMBAYO MUNGU HAKUWAAMBIA.

    Kutoa sadaka kwa Bwana ni jambo jema. Hilo ndilo hasa Nadabu na Abihu walifanya. Walitoa sadaka mbalimbali kwa Bwana lakini Mungu hakupendezwa nao. Kwa ajili ya jambo bila walikufa. Tena, tunaona watu wakifanya mambo mema lakini wanapokea adhabu kwa ajili yahayo kwa sababu mambo hayo hayakuwa mapenzi makamilifu ya Mungu.

    Na Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakatwaa kila mtu chetezo chake, wakatia moto ndani yake wakatia na

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1