Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hatari za Kiroho
Hatari za Kiroho
Hatari za Kiroho
Ebook108 pages1 hour

Hatari za Kiroho

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Mkristo hutembea katikati ya hatari nyingi, mitego na mitambo. Kitabu hiki kitafumbua macho yako kwa hatari nyingi za kutatiza zinazoongoja kutuumiza, kutujeruhi na kutuharibu. Jisaidie, Jiokoe na jiondoe kupitia kitabu hiki cha nguvu kuhusu hatari za kiroho!

LanguageKiswahili
Release dateAug 8, 2018
ISBN9781613958513
Hatari za Kiroho
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Hatari za Kiroho

Related ebooks

Reviews for Hatari za Kiroho

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hatari za Kiroho - Dag Heward-Mills

    Kwa nini Mambo Kadhaa Yanapaswa Kufanyika Kwanza

    Vipaumbele visivyo sahihi ni hatari sana kwa Wakristo.  Ukiwa mwenye dhambi, huwa unachagua kati ya maamuzi mawili: mazuri na mabaya. Kadiri unavyokua katika Bwana, chaguo lako linaongezeka na unaanza kuwa na vitu vingi zaidi vya kuchagua.

    Wakati huo chaguo lako si kati ya mema na mabaya tena, bali kati ya mema na mema. Kwa yale unayofanya, huwa kunakuwa na mambo mengi mema ya kuchagua. Ukifika katika hatua hiyo ni muhimu kuelewa mtazamo wa vipaumbele:  Napaswa kufanya kipi kwanza? Yesu alitupa ufunuo mkubwa kuhusu mambo kadhaa ambayo yanapaswa kafanywa kabla ya mengine.

    Inapendeza kujifunza kuhusu mambo mangapi ambayo Yesu alisema yanapaswa kufanyika kwanza. Kila Yesu alipoongea kuhusu jambo la kwanza au la kwanza kabisa, Alitumia neno la kiyunani proton. Katika kitabu hiki, tunaangalia mambo ya proton; mambo  ambayo Yesu alisema yanapaswa kufanyika kwanza.

    Kama Mkristo, unapaswa kufanya mambo yale ya kwanza, kwanza. Mambo ya kwanza inamaanisha kwanza kimuda, kimpangilio, kiidadi, kicheo na kithamani.

    Mkristo anapaswa kufanya mambo yale ya muhimu kwanza.

    Kwa nini Mambo Kadhaa Yanapaswa Kufanyika Kwanza?

    1. Jambo lolote ambalo halifanyiki kwanza linauwezekano wa kupoteza umuhimu wake.

    Mungu anatuvumilia sana. Wengi wamemuasi na wanaonekana kunusurika. Umuhimu wa neno la Mungu unaonekana kufifia kadiri tunapoendelea  kutomtii. Punde kile ambacho ni muhimu kuliko kitu chochote kinadharaulika na kuwa sio muhimu tena.

    Leo nahubiri chini ya upako na watu wengi wananiheshimu kwa sababu ya huduma. Lakini laiti ningelikuwa sijamtii Mungu kwa wakati nilipomtii, ningaliishi maisha yangu kama Daktari wa kawaida. Mjadiliano kuhusu wito wa Mungu yangeonekana kutofaa na kutokuwa muhimu.

    Kukaa pamoja na madaktari wenzangu katika hospitali mbalimbali, wazo la kuwa mchungaji lingesikika kutokuwa muhimu kabisa. Ningewaambia rafiki zangu, Niwaambie kuhusu wazo la kipuuzi nililokuwa nalo wakati fulani. Je mnajua kwamba wakati fulani nilitaka kuwa mchungaji? Tulipokua wadogo tulikuwa wakiroho sana na bila vitendo.

    Je hujawahi kukutana na watu wazima ambao wanasema waliwahi kuwa kwenye njia ya kuwa padri? Katika uzee wao wanajaribu kufidia uasi wao kupitia watoto wao.

    Namjua mtu mmoja aliyemlazimisha mmoja wa watoto wake kuwa padre. Alimuambia kijana wake, Mungu aliniita kuwa padrii lakini sikufanya. Sasa wewe uwe yule padri nami nitakupa mali na pesa ili usikose chochote. Mwishoni mwa wa maisha yao wanahangaika sana kufidia maisha ya kutotii na  kukosa ushirikiano na Mungu.

    Rafiki mpendwa, naweza kukuhakikishia kwamba, kadiri unavyotembea katika njia zako, ndivyo utakavyokuwa mbali na kutoona umuhimu wa amri za Mungu. Kuna sababu ya proton.

    Proton, kuyafanya mambo ya kwanza, kwanza, inakuokoa kutoka katika udanganyifu.

    Mungu atashugulikia mambo yako na kuwa pamoja na wewe kadiri unavyoendelea katika mapenzi yake.

    2. Kitu chochote ambacho hakifanyiki kwanza kinaweza kisifanyike kabisa.

    Mara nyingi ucheleweshaji unamaanisha Kusitishwa Kitu chochote ambacho hakifanyiki kwanza kinaweza kisifanyike kabisa. Sikujua kwamba kuchelewesha jambo kunaweza kusababisha jambo hilo lisitishwe.

    Kulikua na siku nilipaswa kusafiri kutoka London kwenda New York kuhubiri. Nilikuwa nimepangwa kuhubiri katika mji wa Maryland usiku huo.  Kwa bahati mbaya, nilipata usafiri wa ndege ya asubuhi sana kutokea uwanja wa ndege wa Healthrow huko London, kwenda Amsterdam na ilikua niunganishe safari toka Amsterdam kwenda New York. Kwa namna moja sikuamini muda niliouona kwenye tiketi yangu. Nilidhani huo muda ni mapema sana kwa kweli.

    Nilipofika uwanja wa ndege, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu, nilikuwa nimechelewa sana kufika, au kupanda ndege. Nilichelewa muda niliopaswa kufika kama dakika 20. Niliangushwa sana. Ilinibidi nisubirie ndege inaofuata ya kuelekea Amsterdam!

    Huwezi Kuunganisha ndege yako ya kwanza kwenda New York lakini unaweza kupata ndege ya baadaye walivyoniambia. Niligundua wakati huo kwamba naweza kufika mji wa New York  na kujiandaa kuendesha gari kwenda Maryland. Kwa hiyo nilipiga simu New York na kumwambia mchungaji wakati gani nitaweza kuwasili na nilimuambia kwamba tutahitaji kuendesha haraka kuelekea Maryland. Nilimhakikishia kwamba bado tupo katika muda mzuri uliopangwa na kwamba kipindi kitaendelea sawasawa japokuwa tumechelewa kidogo.

    Kule Amsterdam, nilipanda ndege kwa ujasiri ndege ya kuungansiha kuelekea New York nikijua ya kwamba itaanza safari muda si mrefu na nitakua njiani. Baada ya muda kidogo, niliangalia dirishani na niliona watu wanapulizia mabawa ya ndege. Hapo kukawa na tangazo: "Kuna barafu kali kwenye injini hivyo haitakuwa salama kwa ndege kuanza safari. Itatuchukulia lisaa limoja kuondoa barafu. Tafadhali tunaomba mtuvumilie.

    Nikafanya mahesabu mengine ya muda na nikaona bado nitaweza kufika Maryland kwa wakati na  kipindi kuendelea. Kanisa zima watakuwa wananisubiri. Walikuwa wananitarajia kwa wiki kadhaa. Bahati mbaya, haikuwa hivyo.

    Baada ya kutatua tatizo la barafu, tatizo lingine likaanza, likisababisha kuchelewa zaidi. Mara hii walisema vyoo ndani ya ndege havifanyi kazi na vinahitaji kutengenezwa. Nilikua sijawahi kusikia eti vyoo kwenye ndege havifanyi kazi lakini hiyo ilikuwa inatokea waziwazi! Ilichukua masaa mawili mengine kabla ya kuwa tayari kuanza safari yetu.

    Nilikaa kwa maumivu makali ya mawazo kadiri dakika zilivyozidi kupita, nikifikiria ni watu wangapi watakuwa wamekusanyika kwa ajili ya mkutano. Hatimaye ilinibidi  nikubali kuwa mkutano unabidi uhairishwe kwa sababu nisingeweza kufika kwa wakati. Nilipokaa kwenye kiti changu, nilifikiria juu ya namna zile dakika 20 tulizochelewa pale Londoni zimebadilisha ratiba yangu yote.

    Hapo ndipo Mungu aliongea nami: Je unaona jinsi ucheleweshaji unavyoweza kumaanisha kusitisha?

    Bwana alinionyesha kwamba kuchelewa katika kutii neno lake kunaweza kunifanya nisitimize mapenzi yake kabisa. Bwana akanionyesha kwamba ameniruhusu nipitie uzoefu huu ili nijifunze ni namna gani ucheleweshaji katika kufanya mapenzi yake wakati mwingine unaweza kunifanya nisifanye kabisa.

    Wengi ambao wana kusudi la kumtii Mungu hawataishia kwa kumtii kwa sababu wanatanguliza vitu ambavyo sio sahihi. Ndoa zao, Uzamivu wao, umahiri wao na safari yao ya nje ya miaka mitano yote hayo yanatangulia kufanyika kabla ya kumtii Bwana. Utiifu kwa Mungu, ambao unapewa nafasi ya  pili hautimii kamwe.

    Nimetazama kwa huzuni sana ninapoangalia watu ambao walipaswa kuwa watumishi wa muda wote katika huduma wakihairisha hadi pale watakapomaliza mambo fulani. Kwa bahati mbaya ucheleweshaji huo ulifunga kabisa fursa yao ya kuwa katika huduma ya kudumu milele. Kitu ambacho watu hawatambui ni kwamba kuhusu muda, hali au mambo yanabadilika sana kiasi kwamba

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1