Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Binti Unaweza Kufanikiwa
Binti Unaweza Kufanikiwa
Binti Unaweza Kufanikiwa
Ebook167 pages3 hours

Binti Unaweza Kufanikiwa

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kitabu hiki kitayaponya maumivu ya mabinti! Katika kitabu hiki kilichotarajiwa kwa muda mrefu, wanawake wamehamasishwa kutumia hekima ya Mungu kuwasaidia kushinda hali ngumu nyingi ambazo wanakumbana nazo. Mungu atagusa maisha yako na kukutia nguvu wakati unafurahia hiki kitabu kizuri kipya hasa kilichoandikwa kwa mabinti.

LanguageKiswahili
Release dateJul 26, 2016
ISBN9781613954225
Binti Unaweza Kufanikiwa
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Binti Unaweza Kufanikiwa

Related ebooks

Reviews for Binti Unaweza Kufanikiwa

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Binti Unaweza Kufanikiwa - Dag Heward-Mills

    Ninaandika kitabu hiki kwa ajili ya Wanawake. Ni ujumbe kwa wanawake wa mahali pote. Wanawake wameumbwa tofauti na wanaume na ninaamini kuwa wanahitaji ujumbe maalumu.

    Yesu aliwataja wanawake kwa njia mbili tofauti. Aliwaita wanawake au mabinti.

    Kuna tofauti kati ya binti na manwamke. Kama ningekuwa mwanamke, ningependa kama Yesu angeniita binti. Nafikiri hivyo kwa sababu binti kwa kawaida hukubaliwa zaidi, hili liko wazi na unyenyekevu zaidi. Kwa asili, mwanamke mtu mzima si rahisi kwake kuchochea mambo kama binti alivyo.

    Uchungu wa Maisha

    Wanawake wengi wametiwa uchungu sana na maisha yao wanayoyapitia. Wana shida nyingi, ni watu wasiosamehe na wasio na rehema. Uzoefu wa maumivu ya maisha wanayopitia umetowesha uzuri wa imani na kuaminiwa. Usimwamini mwanaume kamwe, wanasema. Wanaambiana wao kwa wao, Usimwamini mwanamke mwingine. Ninatambua ni wanawake wangapi wanaoishi katika upweke. Ni wapweke nusura wakose marafiki kabisa.

    Angalia jinsi Yesu alivyosema kwa mwanamke Msamaria. Alikuwa anajaribu kumfanya mwanamke huyu aamini mambo aliyokuwa anasema.

    … MAMA, UNISADIKI, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.

    Yohana 4:21

    Angalia jinsi Yesu alivyosema kwa mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi. Huyu alikuwa ni mwanamke ambaye angepoteza maisha yake katika mikono ya Wanaume wasio na msamaha. Alitaka aamini katika upendo tena.

    … MWANAMKE, WAKO WAPI WALE WASHTAKI WAKO? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? Akamwambia hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.

    Yohana 8:10, 11

    Pia angalia jinsi Yesu alivyoongea na mwanamke ambaye aliteseka kwa miaka kumi na minane. Mwanamke huyu aligharimiwa vitu vingi. Alikuwa katika uchungu na maumivu kwa muda mrefu. Mwanamke huyu alihitaji muujiza. Angalia jinsi Yesu alivyomhubiria katika kanisa:

    … MAMA, UMEFUNGULIWA katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.

    Luka 13:12, 13

    Sura ya 2

    Mabinti

    Kuna msemo wa asili usemao, mabinti hawajajaa uchungu na kutokusamehe. Kuna baadhi ya mambo yanayovutia na yasiyo na hatia ambayo yanamwonesha binti. Pamoja na hayo yote, kuna kuaminiwa maalumu na kujiamini ambako binti huwa navyo kwa baba. Kwa bahati mabaya, imani, tumaini na pendo la mabinti linafifia kadiri wanavyokua kuelekea kuwa wanawake watu wazima.

    Yesu aliwaita baadhi ya wanawake mabinti. Ninaamini kuwa ilikuwa ni kwa sababu ya imani ambayo walikuwa nayo katika yeye. Alitambua upendo halisi waliokuwa nao juu yake.

    Hebu tuangalie kundi hili la wanawake ambao Yesu aliwatumikia. Wakati huu, tunatambua jinsi alivyowahutubu kwa njia tofauti.

    Katika moja ya miujiza mikubwa ambayo Yesu aliifanya, ni uponyaji wa mwanamke aliyetokwa na damu. Tunamwona Yesu akimwita binti! Mwanamke huyu alikuwa tayari kuingilia kati upako ingawaje watu wengine waliowazunguka hawakujisikia kitu chochote.

    … naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona ...

    Marko 5:29

    Yesu akasema, MTU ALINIGUSA, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.

    Luka 8:46

    Kuna jambo ninalotaka ulitambue kuhusu binti huyu. Kwanza kabla ya mambo yote, alikuwa na imani kuu katika uwezo wa Yesu. Katika ugonjwa na udhaifu wake, alipenya katika mkutano mpaka alipogusa pindo la vazi lake.

    Ilikuwa lazima ichukuliwe imani kubwa kwa mwanamke huyu katika msongamano wa mkutano wa watu waliojazana. Jambo hilo ndilo jambo sahihi lililomfanya awe binti mkuu: imani na kuamini. Miaka yake kumi na mbili ya kupitia uchungu na watu mbalimbali haikutosha kuzuia moyo wa iamni.

    Wanawake Waangalifu

    Wakati mwingine, usuli wa uzoefu wa dhambi kwa wanaume mbalimbali hufanya kuwa ni vigumu kwa mwanamke kumwamini mwanaume yoyote. Anakuwa na ujasiri kidogo kwa baba yake, mchungaji wake au kwa mtu wa Mungu. Hawezi kuamini kuwepo kwa wema na usafi. Wakati mwingine, kukua katika desturi ya mashaka na umbeya, mbegu ya kutokuamini hupandwa daima. Wanawake kama hao huelekea kudumu kuwa wenye wasiwasi, wasioamini, wenye kushuku na mashaka. Kwa jinsi iyo hiyo, mwanamke ambaye hawezi kuamini hawezi pia kupenda. Amejawa na mashaka. Pendo kamili huitupa nje hofu. Biblia inasema pendo …

    … huamini yote …

    1 Wakorintho 13:7

    Mabinti Hupokea Upako wa Baba Zao

    Ishara nyingine iliyosimama ya binti huyu, (mwanamke mwenye suala la damu), ni ukweli kwamba alipokea upako wa Yesu. Hii ndiyo taarifa pekee iliyoandikwa katika Biblia, upako unaotiririka kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mwingine ambao wote wawili wanahisi upako huo. Yesu alihisi upako ukimtoka na binti yule naye akahisi upako ukija mwilini mwake.

    Unaona, watoto ndio ambao hupokea zawadi nono kutoka kwa wazazi wao. Ni watoto pekee wanaopokea urithi kutoka kwa baba zao bila kifani au mwenzi yeyote.

    Hapo unakuja wakati katika maisha ya mwanamke ambao unaelekea mwanamke atashindana na mamlaka ya mwanaume. Simlaumu mwanamke kwa sababu wanaume wengi hawawajibiki na si waaminifu.

    Hata hivyo, kushindana na wanaume na kufanya kampeni kinyume cha mamlaka inaweza kukuzuia kupokea upako. Utakuwa na fikra za upinzani zitakazodumu kwa muda mrefu kuelekea kwenye karama ya Mungu. Unaona, vyombo hivi vingi ambavyo Mungu anavitumia ni wanaume.

    Unapompata mtu kama baba, unajiachilia katika kupokea kipawa cha mwisho kutoka kwake. Pengine, hii ndiyo maana Yesu anamtaja mwanamke huyo kama binti.

    … BINTI, IMANI YAKO IMEKUPONYA; enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.

    Marko 5:34

    Mabinti Ni wa Milele

    Katika tukio lingine, wakati Yesu alipokuwa anaelekea msalabani, mkutano mkubwa wa watu ulimfuata. Katika umati huu, kulikuwa na wanawake ambao hawakufurahia kuhusu alivyotendewa isivyo haki. Walimsaidia waziwazi na wakatambuliwa naye mbele ya watu wote.

    Katika muda ambao wanaume wote na mitume walimwacha Bwana, wanawake walisimama kidete. Yesu akawageukia na kuwahudumia kwa neno la kinabii kutoka moyoni mwake. Hakunena juu ya hawa waliomsaidia kama wanawake, lakini kama mabinti.

    … ENYI BINTI ZA YERUSALEMU, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu.

    Luka 23:28

    Amua kuwa mwanamke ambaye Yesu atakuona kuwa kama binti. Mtu aliyefunguka kwa ajili ya upako! Mtu ambaye ni msaada kwa mtu wa Mungu! Mtu aliyeandaliwa kutambulisha maono waziwazi na kwa shauku kubwa!

    Sura ya 3

    Kifuniko

    Wanawake wanahitaji kifuniko

    Wanawake wanahitaji kifuniko kwa ajili ya maisha yao. Kifuniko hiki kinatumika kama ngao ya ulinzi. Kwa bahati mbaya, kuna wanawake wengi ambao hawatambui ukweli huu. Wanajiona wako sawa na wanaume na ni wema kama mtu mwingine yeyote.

    Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake …

    1 Wakorintho 11:5

    Ni kwa kuwa na roho ya unyenyekevu tu ndipo unaweza kuukubali ukweli huu. Ufalme huu wa Mungu unaweza kuendelea kuwa bora kwa kuwa na mtazamo wa mtoto mdogo.

    … Msipoongoka na KUWA KAMA VITOTO, hamtaingia kamwe katika ufalme …

    Mathayo 18:3

    Ni jambo la maana kwa mwanamke kufunikwa kiroho na kufunikwa huku kunatokana na kichwa. Ama mwanamke ameolewa au siyo, anaweza kuwa na kifuniko anachopenda.

    … na kichwa cha mwanamke ni mwanaume …

    1 Wakorintho 11:3

    Wakati mwingine kifuniko hiki hutolewa na waume, wachungaji au baba wa kiroho. Mwanamke anayefanya huduma bila kifuniko hiki ametoka nje ya mstari. Ni dhahiri, kama umeolewa na mtu asiyeamini, hawezi kuwa kifuniko cha kiroho kwako.

    Kama umeolewa na mume goigoi kiroho, huyo si kifuniko chako. Mtu aliye juu yako kiroho lazima awe na kifuniko. Hii ndiyo sababu kinaitwa kifuniko.

    Dada mpendwa, je, una kifuniko cha kiroho? Uko wazi kwa ushauri wa wanaume ambao Mungu amewatoa kwa ajili ya kifuniko chako? Ni nani aliye kifuniko chako cha kiroho? Je, wewe ni mwasi? Usisahau kwamba hakuna hata mmoja kati yetu aliye juu ya Neno la Mungu.

    Sura ya 4

    Binti, Hii Ni Heshima Yako

    Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi. Basi akasema, hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea HAITAKUPATIA HESHIMA WEWE, MAANA BWANA  ATAMWUZA SISERA KATIKA MKONO WA MWANAMKE. Debora akainuka,

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1