Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
Ebook105 pages1 hour

Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari

Rating: 3 out of 5 stars

3/5

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345460
Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari

Related ebooks

Reviews for Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari

Rating: 3 out of 5 stars
3/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Namna Unavyoweza Kuwa Mkristo Aliyehodari - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Nini Maana ya Kuwa Mkristo Hodari

    Hatimaye, MZIDI KUWA HODARI KATIKA BWANA na katika uweza wa nguvu zake.

    Waefeso 6:10

    Katika biblia nzima, Wakristo wanahamasishwa kuwa hodari. Utaona neno kuwa hodari likijitokeza mara nyingi katika Biblia. Ili uwe hodari lazima ujiimarishe wewe mwenyewe. Wakristo wengi ni hodari katika miili yao, hodari katika siasa, hodari katika elimu, hodari katika biashara, hodari katika mahusiano lakini si hodari katika Bwana. Mungu anasisitiza ya kwamba lazima uwe hodari katika Bwana.

    Kuwa hodari katika Bwana ni kuwa Mkristo hodari. Watu wengi huja kumjua Bwana lakini hawakuwa hodari katika Bwana. Wao hubaki kuwa Wakristo wachanga maisha yao yote. Hiki kitabu kitakufundisha namna ya kuwa Mkristo mzuri na hodari. Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinamuelezea Mkristo hodari mzuri. Lazima ulenge kukuza viashiria hivi vyote kama utakuwa muumini hodari mzuri. Kuwa Mkristo hodari lazima ukue kiroho, uwe na shauku, uwe mkomavu, uwe na utakatifu na uimarike katika Bwana.

    Kuna sehemu mbalimbali tofauti katika maisha yako ambazo lazima uzikuze kama utaitwa tena Mkristo hodari. Kitabu hiki chote kinahusu kukuza sehemu hizi ambazo zinakugeuza kuwa Mkristo hodari. Sehemu tisa ambazo unapaswa kuzikuza kama unataka kuwa hodari katika Bwana zimetajwa chini.

    1. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa na maisha ya Kikristo ya undani

    Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.

    Zaburi 42:7

    2. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa imara.

    Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

    1 Wakorintho 15:58

    3. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa mtu asiyetikisika.

    Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.

    1 Wakorintho 15:58

    4. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa wa kiroho.

    Lakini, ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo.

    1 Wakorintho 3:1

    5. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa mtakatifu.

    Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;

    Waebrania 1:14

    6. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa mkomavu.

    ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

    Waefeso 4:14

    7. Kuwa Mkristo hodari ni kuonewa shauku katika neno jema siku zote. Kuwa Mkristo hodari ni kujawa na shauku.

    Navyo ni vizuri kuonewa shauku katika neno jema sikuzote, wala si wakati nikiwapo mimi pamoja nanyi tu.

    Wagalatia 4:18

    8. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa mwenye kuzaa matunda.

    Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende MKAZAE MATUNDA; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni.

    Yohana 15:16

    9. Kuwa Mkristo hodari ni kuwa katika hali ya utayari wa kukutana na Mungu wakati wowote

    Basi nitakutenda hivi, Ee Israeli, na kwa sababu nitakutenda hivi, ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli.

    Amosi 4:12

    Sababu Sita kwa Nini Unapaswa Kujiimarisha Mwenyewe.

    1. Jiimarishe mwenyewe ili uweze kumshinda yule mwovu.

    Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, KWA SABABU MNA NGUVU, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, NANYI MMEMSHINDA YULE MWOVU.

    1 Yohana 2:14

    Yule mwovu si mdhaifu. Ni pale tu unapokuwa hodari ndipo unaweza kumshinda yule mwovu. Ukifanya mzaha na adui, utajilaumu mwenyewe. Kupigana na shetani ni kupigana na shujaa aliyebobea ambaye ameona vita vingi. Ibilisi amepigana na Wakristo wengi miaka mingi iliyopita. Amebobea katika kuharibu na kushawishi Wakristo. Ibilisi alikuwa hai Yesu alipokuwa hai. Yeye si mgeni, lakini wewe ni mgeni! Amka na uwe hodari ili uweze kumshinda yule mwovu.

    Nilipokuwa shule ya sekondari, nilinyanyaswa na wale wanafunzi ambao walikuwa mbele yangu ambao walikuwa waovu. Nilipitia kila aina ya mateso na adhabu niliyosababishiwa na watu ambao walikuwa mwaka mmoja mbele yangu. Wakati huu, nilitambua undani wa uovu ambao ulidumu katika moyo wa mwanadamu. Hawa wavulana wenye miaka kumi na tatu na kumi na nne walijaribia nguvu zao kamili juu yangu kwa sababu ilitokea walikuwa mwaka mmoja mbele yangu.

    Wakati mwingine, niliulizwa kufanya kile wanachokiita ‘mchezo wa tumbili.’ Wakati mwingine niliambiwa kufanya adhabu ya ‘Mnara wa Uhuru.’ Wakati mwingine ilinibidi kusugua vyoo na mabafu hadi saa tisa usiku. Wakati mwingine ilinibidi kubeba ndoo kadhaa za mbolea umbali wa zaidi ya kilometa tano. Wakati mwingine niliambiwa kulinda na kuua mbu wowote ambao walizungukia kitandani. Adhabu zingine ambazo zilikuwepo zilikuwa kula gari (vipande vidogo vya mihogo) na vidonge vya quinine vilivyosagwa. Kwa miezi kadhaa, nilitaabika chini ya mikono ya hawa wanafunzi wakubwa waovu. Siku moja niligundua kwamba mmoja wa wanafunzi wenzangu hakuwahi kuitwa, hakuwahi kutumwa popote, hakuwahi kusumbuliwa na hakuwahi kuadhibiwa! Lakini nilijua ni kwa nini. Alikuwa mkubwa sana kuliko wale waandamizi. Huyo mwana darasa mwenzangu alikuwa mkubwa zaidi mwenye nguvu zaidi kuliko wengine darasani na wale waandamizi walikuwa wanamwogopa. Angeweza kumpiga yeyote kati yao wakati wowote.

    Kuna wakati mwingine wale waandamizi wangepiga kelele. "Kijana mmoja mdogo! hii ilimaanisha kwamba wale wadogo walitakiwa kumkimbilia mkubwa aliyekuwa amewaita kijana mmoja mdogo!" sote tungekimbia lakini yule kijana mkubwa mwenye nguvu angewapuuzia wale waandamizi na angeendelea kufanya kile alichokuwa akifanya. Hakuna aliyethubutu kumuuliza chochote. Walimwogopa kwa sababu alikuwa na nguvu sana. Lakini mimi nilikuwa sina nguvu. Nilikuwa dhaifu, wakupigika, na kuadhibika. Nilikuwa ni mawindo mzuri kwa wale waandamizi waovu wasio na ubinadamu. Laiti kama ningekuwa na nguvu na mkubwa na mwenyewe misuli kama mwanadarasa mwenzangu.

    Hapo ndipo nilipojifunza umuhimu wa nguvu! Unapokuwa na nguvu wale waovu hulazimika kukuacha mwenyewe. Wale waovu hujua kwamba watashindwa. Shetani hatathubutu kuanzisha tatizo kwa sababu anafahamu halitaishia vyema kwake. Lazima uwe na nguvu kwa sababu pale kitu fulani chenye nguvu zaidi kitakapokujia kitakushinda na kukuharibu.

    Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.

    Luka 11:21-22.

    Hii inatakiwa kuwa motisha kubwa ya kukuimarisha! Unavyokuwa na nguvu, yule mwovu analazimika kukuacha mwenyewe kwa sababu anafahamu kwamba kuna vishawishi vingi ambavyo haviwezi kukudhuru. Kuwa hodari katika Bwana!

    2. Lazima ujiimarishe mwenyewe katika bwana kwa sababu adui yako anapanga kukushambulia tena

    Wakapiga kila mmoja mtu wake; Washami wakakimbia, na Israeli wakawafuatia; Ben-hadadi mfalme wa Shamu akaokoka amepanda farasi, pamoja na wapandao farasi. Mfalme wa Israeli akatoka, akawapiga farasi na magari, akawapiga Washami pigo kubwa. Naye yule nabii akamjia mfalme wa Israeli, akamwambia, ENENDA, KUSANYA

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1