Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Sanaa ya Kufuata
Sanaa ya Kufuata
Sanaa ya Kufuata
Ebook248 pages9 hours

Sanaa ya Kufuata

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

"Kumfuata Mungu ni safari ya kusisimua ya ugunduzi. Kufuata na kuiga watu wengine ni sanaa za toka jadi za kujifunza ambazo Yesu Kristo alichagua kama kanuni yake kuu ya kufundisha watu. Badala ya kujitenga na mbinu hii ya kujifundisha ambayo imetumiwa kwa muda mrefu, ni wakati wa kuelewa uzuri na unyenyekevu uliyo katika sanaa ya kufuata.
Katika kitabu hiki utagundua ni nani, ni nini na jinsi unavyopaswa kufuata kwa njia inayostahili. Kitabu hiki kipya na kizuri mno kilichoandikwa na Dag Heward-Mills kinaipatia sanaa ya kufuata nafasi yake inayofaa katika maisha yetu ya Kikristo."

LanguageKiswahili
Release dateMay 15, 2018
ISBN9781641353694
Sanaa ya Kufuata
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Sanaa ya Kufuata

Related ebooks

Reviews for Sanaa ya Kufuata

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Sanaa ya Kufuata - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Sanaa ya Kufuata Ni Nini?

    Kufafanua Sanaa ya Kufuata

    1. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuiga.

    2. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kujifananisha na mtu mwingine.

    3. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuiga kitu fulani.

    4. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kujaribu kuwa kama mtu mwingine.

    5. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuzaa.

    6. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kutoa kloni.

    7. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuwa kama kitu kingine.

    8. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuwa pacha.

    9. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kufika kiwango cha mtu mwingine.

    10. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kusonga mbele.

    Wale Ambao Wametekeleza Sanaa ya Kufuata Kwa Njia ya Kufana

    1. Watoto hutumia sanaa ya kufuata.

    Watoto hutumia sanaa ya kufuata kupiga hatua kubwa mbele; wanafika kiwango fulani na wanajifunza kuzungumza lugha ngumu kwa muda mfupi sana. Sehemu kubwa ya kile ambacho watoto hujifunza, wanajifunza kupitia sanaa ya kufuata, kuiga au kujifananisha na watu wengine.

    2. Kwa karne nyingi, mataifa ambayo yamepata utajiri mkubwa yametumia sanaa ya kufuata.

    Nchi za Uropa na Marekani zimetumia sanaa ya kufuata ili kuwa mataifa makongwe zaidi duniani ambayo yana utajiri mkubwa zaidi duniani. Kupitia kuigizana, kila nchi ya bara Uropa imekuwa kama nchi jirani na nchi hizo zimestawi na kuwa nchi tajiri zinazofanana. Barabara, majengo na miundo msingi mingine ya nchi hizo inafanana. Mifumo yao ya benki na uchumi inafanana kwa karibu mno. Uwezo wao wa kijeshi unafanana. Mfumo wa maisha wa raia wa nchi hizo na hali zao za maisha zinafanana kwa karibu. Kwa kweli, kupitia kujifananisha, kila nchi imefikia kiwango cha jirani wake, kila nchi ilikataa kuachwa nyuma katika mbio ya kuafikia ustawi.

    3. Nchi ambazo zimepata utajiri hivi karibuni zinatumia sanaa ya kufuata.

    Taiwan, China na Korea ni maarufu katika ujuzi wao wa kufuata na kuiga. Kwa kweli, mataifa mengi ambayo yamekuwa tajiri hivi karibuni yametumia sanaa ya kufuata.

    Mataifa ambayo yamepata utajiri katika kipindi cha miaka hamsini iliopita ni maarufu katika ujuzi wao wa kuiga. Sehemu kubwa ya bidhaa zao zinaitwa bidhaa za muigo. Walitengeneza magari ambayo yanafanana na magari maarufu ya bara Uropa. Korea haikuona aibu kutengeneza gari lao aina ya Daewoo lifanane na Opel na Ssangyong iliiga Mercedes Benz na Hyundai iliiga Toyota. Kupitia kuiga kwao kusiokuwa na haya, walifikia kiwango cha Uropa na wakapiga hatua mbele na sasa wako msitari wa mbele katika utengenezaji wa magari.

    Wamefika kiwango cha juu katika karibu kila nyanja ya teknolojia na juhudi na wanaendelea kusonga mbele huku wakizalisha utajiri ambao ni ndoto kwa watu wengine. Wale ambao waliona aibu kuiga walisimama tu na kushuhudia magwiji wa kuiga wakisonga mbele na kuwa mamilionea, mabilionea na matrilionea.

    4. Yesu Kristo Mwana wa Mungu Alitumia Sanaa ya Kufuata.

    Yesu alitumia sanaa ya kufuata kubadilisha wavuvi ambao hawakuwa wamesoma kuwa viongozi na waendeshaji wa vuguvugu lililosambaa dunia nzima. Ikiwa Mwana wa Mungu alitumia sanaa ya kufuata kama njia yake ya pekee ya kufundisha watu, basi lazima hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujifunza na kufunza watu wengine.

    Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuiga mtu mwingine. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuwa kama mtu mwingine anayekuvutia. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kuwa kama kitu kingine kilicho mbele yako. Kupitia sanaa ya kufuata, utaweza kufikia kiwango bora zaidi na upige hatua mbele katika huduma yako.

    Sura ya 2

    Jinsi ya kufaulu Katika Sanaa ya Kufuata

    Ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi...

    Waebrania 6:12

    Biblia hutuagiza mara nyingi tuwe wafuasi wa watu wengine. Biblia ina mifano mingi kuhusu jinsi tunavyopaswa kufuata watu wengine. Katika sura hii, utajifunza kanuni unazohitaji ili ufaulu katika kufuata, kuiga, kujifananisha na kufikia wale walio mbele yako.

    Kanuni Tisa za Kufuata

    1. Unaweza kufaulu katika sanaa ya kufuata kwa kumfuata Mungu mwenyewe.

    Hivyo MFUATENI MUNGU, kama watoto wanaopendwa; MKAENENDE KATIKA UPENDO, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.

    Waefeso 5:1-2.

    Kumfuata Mungu kwa njia ya kufana kunatekelezwa kwa kuenenda katika upendo na kujitolea. Je, unajua kwamba inawezekana mtu kumfuata Mungu? Ni mtu gani bora zaidi kufuata isipokuwa Mungu?

    Neno la Mungu linatuonesha wazi kile tunachopaswa kufanya ikiwa tunataka kumfuata Mungu. Kile tunachopaswa kufanya ni kujifunza jinsi ya kupenda na tujifunze jinsi ya kujitolea. Kufanya vitu hivi viwili kutahakikisha kwamba unamfuata Mungu Mwenyewe.

    Ikiwa unadai kwamba unamfuata Mungu, ni sharti uwe mtu anayeenenda katika upendo wa kiungu kwa sababu Mungu ni upendo.

    2. Unaweza kufaulu katika sanaa ya kufuata kwa kumfuata mtu wa Mungu anayemfuata Kristo.

    Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo.

    1 Wakorintho 11:1

    Paulo aliagiza kanisa la Korintho limfuate yeye lakini aliwaonya kwamba wanapaswa kumfuata alimradi yeye pia anamfuata Kristo.

    Kwa kweli, kuna wahudumu wengi ambao kwa sehemu kubwa wanafuata mamilionea, wafanya biashara na wanasiasa kuliko jinsi wanavyomfuata Mungu. Ukichunguza vitabu wanavyosoma utagundua kwamba wanafuata watu wa kidunia na wana ari ya kuwa kama watu hao zaidi kuliko kuwa kama Yesu. Leo, wachungaji wanasoma wasifu za marais wa Marekani, mamilionea na wafanya biashara mashuhuri.

    3. Unaweza kufaulu katika kumfuata mtu wa Mungu kwa kumfuata mtu ambaye amemfuata mtu ambaye unataka sana kumfuata.

    Ndugu zangu, mnifuate mimi, MKAWATAZAME WAO WAENDAO KWA KUUFUATA MFANO TULIOWAPA NINYI.

    Wafilipi 3:17

    Miaka mingi iliyopita, nilitaka kuingia katika huduma ya miujiza. Nilifahamu kwamba ningehitaji kumfuata mtu ambaye tayari yuko katika huduma ya miujiza. Niliamua kumfuata Kathryn Khulman kwa sababu alikuwa na huduma kuu zaidi ya miujiza ambayo nimewahi kusikia. Mimi kama daktari wa utabibu, nilivutiwa sana na miujiza aliyokuwa anafanya. Lakini nilikuwa na tatizo moja. Sikuweza kumpata duniani kwa sababu alikuwa amefariki. Nilishindwa nifanye nini na sikujua jinsi ambavyo ningemfuata mtu aliyekufa. Ningemkabidhi vipi sadaka mtu ambaye alikuwa ameshafariki. Ningezungumza vipi na mtu ambaye alikuwa ameshafariki. Je, ningeita roho yake kutoka kwa wafu?

    Ghafla Roho Mtakatifu akaniambia, Mfuate Benny Hinn ikiwa kweli unataka kumfuata Kathryn Khulman. Nuru iliangaza katika njia yangu na mara moja nikajua kile nilichopaswa kufanya. Nilianza safari ndefu ya kumfuata Benny Hinn, nilijifunza mambo yote niliyoweza kuhusu kuhudumia watu, uponyaji na miujiza. Hii ndiyo kanuni ambayo Paulo alikuwa anaelezea kanisa la Filipi. Mnaweza kunifuata kwa kufuata wale ambao wamefuata mfano wangu.

    4. Unaweza kuwa mfuasi wa kundi la watu linaloenenda katika neema ya Bwana.

    Nanyi mkawa WAFUASI WETU na wa Bwana, mkiisha kulipokea neno katika dhiki nyingi, pamoja na furaha ya Roho Mtakatifu.

    1 Wathesalonike 1:6

    Badala ya kumfuata mtu mmoja peke yake, unaweza kufuata kundi la watu wanaoenenda katika njia fulani maalum. Kwa mfano, unaweza kufuata viongozi wa kanisa au huduma fulani. Pia unaweza kufuata kundi la marafiki ambao wanamtumikia Mungu pamoja.

    Miaka mingi iliyopita, nilijulishwa kwa Kenneth Hagin na nikaona watu ambao alijihusisha nao. Watu kama Kenneth Copeland, Jerry Savelle, Fred Price, Charles Capps na John Osteen walipatikana katika makongamano yake na majarida yake. Watu hawa wenye imani walinivutia na nikajipata nimeanza kuwafuata. Nilijipata nasoma vitabu vyao na kujifunza kutoka kwao kwa sababu walikuwa ni kundi la watu ambao nilitaka kufuata.

    5. Unaweza kufaulu katika sanaa ya kufuata kwa kuwa mfuasi wa kanisa fulani.

    Maana ninyi, ndugu, mlikuwa WAFUASI WA MAKANISA ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi.

    1 Wathesalonike 2:14

    Unaweza kufuata kanisa fulani kwa kuchunguza viongozi wake, historia yake, kanuni zake, ushindi wake, matatizo yake, makosa yake na kadhalika. Ili ufuate kanisa kwa njia sahihi, ni sharti uchunguze historia yake. Makanisa mengi hupitia mabadiliko makubwa kadiri miaka inavyozidi kupita. Huwezi kulinganisha jinsi kanisa lilivyo leo na jinsi lilivyokuwa miaka mia moja iliyopita.

    Miaka mia moja iliyopita, kanisa la Uswisi lilikuwa na nguvu kiasi kwamba lilikuwa linatuma vijana kufa wakitekeleza misheni katika maeneo ya mbali duniani. Kupitia juhudi za kanisa la Uswisi, ukombozi na Ukristo uliingia katika mataifa kama Ghana na Nigeria. Leo, kanisa la Uswisi limekufa kabisa kiasi kwamba makanisa mengi yamefungwa na Ukristo unachukuliwa kuwa ni kitu kinachofuatwa na wageni na watu kutoka nchi zingine.

    Leo, jengo la shirika la Kiswisi lililowatuma mamishonari kuhudumu duniani limegeuzwa kuwa hoteli na stakabadhi muhimu za kazi za kimoshanari zilizotekelezwa na shirika hilo zimehifadhiwa katika chumba kilicho chini ya hoteli hiyo!

    Nimejifunza mengi sana kutokana na Kanisa la Kimethodisti. Nimefuata mifano yao mingi mizuri na nimechambua maisha ya mwanzilishi wa kanisa hilo. Kwa ajili ya kufuata kanisa hilo, Mungu amenipatia ufahamu na mwelekeo mzuri katika huduma yangu.

    6. Ni sharti ufuate mambo mema ambayo Roho Mtakatifu anakuonesha.

    Naye ni nani atakayewadhuru, MKIWA WENYE JUHUDI KATIKA MEMA?

    1 Petro 3:13

    Ni sharti ufuate mambo mema. Roho Mtakatifu akigusa moyo wako kuhusu jambo fulani katika huduma ya mtu fulani, ni sharti utambue kwamba Mungu anakuelekeza kwa jambo unalopaswa kufanya. Roho Mtakatifu daima hutuonesha mambo mema ambayo ni sharti tufuate. Ni jukumu lako kufungua moyo wako ili uweze kuona mambo mema katika makanisa na huduma zingine.

    Pengine unaweza kuona jinsi mziki wa kanisa la mtu mwingine ni mzuri mno. Pengine unaweza kuona jinsi kwaya ilivyo nzuri katika kanisa hilo; pengine umeona jinsi vyoo vilivyo visafi katika kanisa la mtu mwingine. Pengine umeona jinsi jengo la kanisa la mtu mwingine lilivyo maridadi. Pengine umeona jinsi mtu fulani anavyo jua kuimba. Mambo haya yote mazuri unayoona ni ujumbe kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu mambo unayopaswa kufuata.

    7. Unaweza kufaulu katika kumfuata mtu wa Mungu kwa kufuata watu ambao ameteua kumfanyia kazi.

    ...basi nawasihi mnifuate mimi: Basi, nawasihi mnifuate mimi. Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakayewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.

    1 Wakorintho 4:16-17

    Paulo alitaka Wakorintho wamfuate kwa karibu. Kwa sababu ya hiyo, alimteua Timotheo and akamtuma kwa Wakorintho. Yeyote aliyetaka kuhusiana na Paulo alilazimika kuhusiana na Timotheo.

    Watu ambao hawawezi kuwa na uhusiano mzuri na watu ambao wameteuliwa kufanya kazi fulani hawafahamu kwamba wanapoteza nafasi ya kujifunza na kufuata. Watu wakuu mara nyingi hulazimika kumteua mtu mwingine atakayekutana nawe na kuwa na mahusiano nawe. Usipoweza kuwa na mahusiano na mtu huyo aliyeteuliwa kwa sababu yeye si mtu mwenyewe uliyetaka kuwa na mahusiano naye, utapoteza baraka nyingi. Sanaa ya kufuata ni sanaa ya kufuata watu walioteuliwa.

    Nimewahi kuenda Korea mara nyingi kushirikiana na David Yonggi Cho. Imenibidi nishirikiane na watu wengine aliyewateua kunishughulikia mimi pamoja na wanachama wengine wa bodi yetu. Kuwakubali kwa furaha watu hao aliyewateua kumekuwa ndiyo njia kuu ya kufaidika na uhusiano wangu naye. Mtu yeyote anayeoona kwamba yeye ni muhimu mno kiasi kwamba hawezi kushirikiana na watu wengine walioteuliwa ni mtu ambaye ni muhimu sana kiasi kwamba hawezi kufuata!

    8. Unaweza kufaulu katika kumfuata mtu wa Mungu kwa kufuata imani yake na subira yake.

    Ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

    Waebrania 6:12

    Vitu viwili vikuu unavyopaswa kuangalia katika maisha ya mtu unayefuata ni imani yake na subira yake. Kwa nini nasema hivyo? Maandiko yanatufundisha kwamba ni imani na subira ya mtu ndiyo inamwezesha kurithi ahadi za Mungu.

    Ni imani na subira ya Kenneth Hagin ndiyo iliyomwezesha kuwa na huduma aliyo nayo wakakti huu ambayo imeenea kote duniani. Ni imani na subira ya yonggi Cho ndiyo iliyomwezesha kuwa na kanisa kubwa zaidi duniani. Ni imani na subira ya Benny Hinn ndiyo iliyomwezesha kuwa na mikutano yake ya miujiza. Ni imani na subira ya Fred Price ndiyo iliyomwezesha kuwa na huduma aliyo kuwa nayo. Ni imani na subira ya Reinhard Bonnke ndiyo iliyomwezesha kuwa na mikutano mikubwa zaidi katika bara la Afrika.

    Kilichowapatia watu hawa kile walichokuwa nacho si pesa, watu au matangazo. Ni imani na subira yao ndiyo iliyowapatia kile walichopokea.

    Rafiki mpendwa, je, unataka kufaulu katika sanaa ya kufuata mtu wa Mungu? Basi fuata imani yake na subira yake! Inamaanisha nini kufuata imani ya mtu? Kufuata imani ya mtu ni kuuliza, Aliamini nini na ni kwa nini aliamini kile alichoamini? Nilipokuwa nasoma kuhusu imani ya Billy Graham niligundua kwamba alifanya uamuzi mzuri wa kuamini kwamba kila sehemu ya Biblia ni Neno la Mungu. Kwa ajili ya imani yake, yeye hunukuu Maandiko anapohubiria wenye dhambi. Anaamini kwamba ikiwa Maandiko hayo ni Neno la Mungu, basi yanaposomewa watu, maneno hayo yatakuwa na nguvu kubwa ya kukomboa, kuponya na kuweka watu huru.

    Ukisoma kwa makini utagundua mambo mengi kuhusu imani ya watu mashuhuri. Ni njia gani nyingine unaweza kutumia ili ujue mengi zaidi kuhusu imani ya mtu mashuhuri? Kwa kutazama na kusikiliza vitu ambavyo mtu huyo alisema mapema katika huduma yake! Katika kipindi cha baadaye cha huduma ya mtu, utaona matunda mema ya kile ambacho ameamini. Lakini katika kipindi cha mapema cha huduma ya mtu, utaona na utahisi mtu huyo akitumia imani yake kutekeleza mambo makuu kwa ajili ya Mungu. Katika kipindi cha mapema cha huduma yake hutaona mengi bali kutakuwa na matamko mengi ya imani. Daima ni jambo la kusisimua kuona jinsi watu walisimama imara katika kipindi kigumu na wakaanza kuamini kwamba mambo makuu yatatendeka katika huduma zao.

    Fuata imani na subira ya watu mashuhuri na utakuwa unafuata kile kilicho sahihi. Leo, watu wengine wanataka kuvaa nguo na viatu vinavyofanana na vya watu mashuhuri wa Mungu na waendeshe magari kama yao. Biblia haikusema kwamba walirithi ahadi za Mungu kupitia magari, nyumba na nguo zao! Walirithi ahadi za Mungu kupitia imani na subira yao!

    Basi, unaweza kufuata subira ya mtu kwa njia gani? Unaweza kuchunguza subira ya mtu kwa kujua wakati alipoanza kuamini kwamba atapokea vitu fulani na muda uliyopita kabla hajapokea vitu hivyo. Ukianza kufanya hesabu ya idadi ya miaka ambayo watu fulani wamekuwa wakiamini na kufanya kazi ya aina fulani, utashangazwa na jinsi baadhi ya watu hao wamekuwa na subira maishani mwao.

    Watu wengi wa Mungu wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu pasipo na matokeo mazuri kisha wanapokaribia mwisho wa maisha yao na huduma zao, wanashuhudia Mungu akifanya mambo makuu. Kwa kweli, imani na subira ya watu hao ndiyo siri ya huduma zao.

    9. Ni sharti ushinde uvivu na utepetevu ili uweze kumfuata mtu kwa njia ya kufana.

    Ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

    Waebrania 6:12

    Je, unaweza kuamini kwamba uvivu ndiyo sababu inayofanya watu wengi wasiweze kufuata? Nimewahi kusikia maneno ya watu wavivu ambao hawataki kufuata na kujifunza. Kile wanachosema ni:

    Ah, kweli neema ya Mungu iko juu ya maisha yako.

    Wanasema, Ni neema ambayo Mungu amekupatia ili uwe na makanisa haya yote.

    Wanasema, Ah jamani, napenda jinsi unavyofanya mambo yako. Ni neema uliyo nayo.

    Wanasema, Sina neema uliyo nayo wewe. Si mwito wangu.

    Ndiyo, huenda ni kweli kwamba neema ya Mungu inafanya kazi. Lakini mara nyingi, watu huwa ni wavivu mno kiasi kwamba hawawezi kujifunza kitu kipya! Hawana ari ya kutekeleza mawazo mapya na kanuni mpya wanazoona zikifanya kazi.

    Kwa kweli, itakugharimu juhudi kubwa ili uwe kama mtu aliye mbele yako. Itakugharimu muda mwingi na juhudi za dhati ili uweze kugundua siri ya kiongozi unayetaka kufanana naye. Watu wavivu hawawezi kufaulu katika sanaa ya kufuata.

    Sura ya 3

    Mbinu Saba za Sanaa ya Kufuata

    1. Fuata watu wa Mungu kupitia mafundisho yao au matendo yao.

    Kitabu kile cha kwanza nalikiandika, Theofilo, katika habari ya MAMBO YOTE ALIYOANZA YESU KUFANYA NA KUFUNDISHA.

    Matendo ya Mitume 1:1

    Mafundisho ya mtu pamoja na yale anayofanya yana umuhimu sawa. Ili umfuate Kristo, ni sharti ufuate mafundisho yake na mambo aliyofanya. Kila injili ina mafundisho ya Kristo na pia hadithi ya mambo aliyotenda. Mafundisho ya Yesu yameandikwa kwa wino nyekundu na mambo aliyofanya yameandikwa kwa wino nyeusi.

    Ni muhimu kuelewa kwamba mambo haya mawili ni tofauti sana lakini ni ya muhimu mno. Kuna maswala mengi ambayo Yesu Kristo hakufundisha kuyahusu. Kwa kweli, kuna mambo mengi alifanya bila kueleza kwa nini aliyafanya. Ndiyo maana Theofilo alishauriwa ajifunze kutokana na kile Yesu alichofanya na kile alichofundisha.

    2. Fuata watu wa Mungu kupitia kufuata mafundisho yao.

    Ni muhimu uelewe kwamba kuna watu wenye kipawa cha kufundisha kile wanachofahamu. Hiyo inapelekea watu kuwa na mafundisho, kanuni, sheria na mawazo mengi wanayofundisha. Kwa mfano, Kenneth Hagin, ambaye alikuwa nabii na mponyaji mashuhuri, alifundisha sana kuhusu

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1