Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua
Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua
Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua
Ebook78 pages2 hours

Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345491
Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua

Related ebooks

Reviews for Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Soma Biblia Yako, Omba Kila Siku ...Ukitaka kukua - Dag Heward-Mills

    SURA YA 1

    Soma Biblia yako: Biblia ni nini?

    Biblia ni Neno la Mungu lililoandikwa. Ni sharti ukuze Uhakika na kitabu Kikuu Zaidi katika historia – Biblia.

    Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

    2 Petro 1:20, 21

    1. Biblia ni ufunuo wa kinabii.

    Biblia inafunua asili ya Mungu kwa mwanadamu. Inaeleza asili ya mwanadamu. Inatoa kusudi la kuwepo kwa mwanadamu duniani.

    Inaonyesha hatima ya viumbe vyote. Zaidi ya yote, inaonyesha mpango wa Mungu wenye huruma wa kutukomboa.

    Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba HAKUNA UNABII KATIKA MAANDIKO upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

    2 Petro 1:20, 21

    Mungu, ambaye ALISEMA ZAMANI NA BABA ZETU KATIKA MANABII kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

    Waebrania 1:1, 2

    2. Biblia ni habari njema ya wokovu.

    Injili ni habari njema kwetu sisi ya nguvu ya Kristo ya kutukomboa. Biblia ndio kitabu cha pekee kinachoonyesha jinsi mwanadamu anavyoweza kukombolewa. Biblia ina ujumbe wa Kristo wa uzima wa milele kwa wote wamuaminio Kristo, na adhabu ya milele kwa wote wanaoasi injili.

    Kwa maana siionei haya INJILI; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.

    Warumi 1:16

    3. Biblia ni Onyo la Mungu Kwetu sisi.

    Biblia sio majadiliano ya mawazo na nadharia. Biblia ni tangazo lenye mamlaka ya mambo ya kweli. Kweli ambazo zimefafanuliwa katika Biblia ni za ajabu na haziwezi kubadilishwa. Haiba inayoizingira Biblia kwa kiasi fulani inatokana na jinsi ilivyo na kweli zenye mamlaka na zisizoweza kubadilishwa.

    Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, sisi je! TUTAPATAJE KUPONA, TUSIPOJALI WOKOVU MKUU NAMNA HII? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.

    Waebrania 2:1-4

    4. Biblia imejaa maneno yalionadikwa kwa nguvu ya Kiungu.

    Hii ndiyo inayotofautisha Biblia na vitabu vingine vyote. Biblia ina msukumo na mwongozo kutoka kwa Mungu. Hiyo ni kusema, iliandikwa na Mungu kupitia kwa mikono ya mwanadamu wa kawaida.

    KILA ANDIKO, LENYE PUMZI ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

    2 Timotheo 3:16

    5. Biblia ni ujumbe unaokata ambao umetoka moja kwa moja kutoka kwa Mungu.

    Maelfu ya watu hubadilishwa wanapoelezwa kweli rahisi za Biblia. Nilibadilishwa na Neno la Mungu nilipokutana nalo.

    Maana NENO LA MUNGU LI HAI, TENA LINA NGUVU, TENA LINA UKALI kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

    Waebrania 4:12

    6. Biblia ni hekima ya Mungu kwa ajili ya kufanikiwa kwetu.

    Njia ya Mungu ya kuleta mafanikio sio njia ya kutumia uwerevu na ujanja wa kibinadamu. Ni kupitia Neno lake.

    Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; MAANA NDIPO UTAKAPOIFANIKISHA NJIA YAKO, kisha ndipo utakapositawi sana.

    Yoshua 1:8

    Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu. Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako. Maana ni uhai kwa wale wazipatao, na afya ya mwili wao wote.

    Methali 4:20-22

    7. Biblia ni maelezo ya asili ya uumbaji, dunia, jua, mwezi, nyota na sayari.

    Hapo mwanzo MUNGU ALIZIUMBA MBINGU na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

    Mwanzo 1:1-2

    8. Biblia Inatoa ukweli kuhusu siku za usoni, mbinguni, kuzimu na maisha ya milelel.

    NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA HICHO KITI CHA ENZI; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

    Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1