Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya
Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya
Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya
Ebook75 pages1 hour

Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Bibilia inatuamabia kwamba sisi sote tunafanya makosa mengi- wakiwamo pia wachungaji. Makosa yana uwezo wa kukurudisha nyuma badala ya kwenda mbele. Kosa linaweza kukuzuia kuendelea. Ni makosa yapi mchungaji anaweza kuyafanya? Ni makosa yapi ambayo yanaweza kuwa makosa kumi makuu ya mchungaji? Unakaribishwa kupitia kurasa za kitabu hiki maalum na ugundue mwenyewe makosa ambayo uko katika hatari ya

LanguageKiswahili
Release dateJul 28, 2016
ISBN9781613958568
Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya

Related ebooks

Reviews for Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Makosa Kumi Makuu Ambayo Wachungaji Wanafanya - Dag Heward-Mills

    Sura Ya 1

    Kuwa Polepole Kuhusu Huduma

    Wachungaji wengi wanachelewa kuendeleza huduma yao. Wakati mwingine wanachelewa kutii wito wa Mungu. Labda, hili ni kwa sababu wachungaji wengi wana silika ya uflegimatiki au upolepole. Upolepole ni jambo hatari kwenye huduma. Moja ya viashiria vya uhai wetu ni kasi tunayoenda nayo.

    Ni wakati gani kulingana na saa ya Mungu? Kuna nyakati tatu zinazoendana moja kwa moja. Hizi ni  wakati wangu, wakati wako na wakati.

    Basi Yesu akawaambia, Haujafika bado wakati wangu; ila wakati wenu sikuzote

    Yohana 7:6

    Hebu itazame saa yako sasa hivi. Kiaasili huo ndiyo wakati wako. Itazame saaya mtu mwingine. Huo ndiyo wakati wake. Lakini wakati ni upi?

    Katika  maisha halisi, kila saa  hutofautiana kidogo kimuda. Huwa naweka saa yangu iwe na dakika chache mbele ili kushinda roho ya kuchelewa. Watu wengine wanakuwa na saa sahihi. Tendo hili linasababisha kuwapo kwa saa (muda) mbalimbali kwa kila mtu

    Katika ulimwengu wa kiroho, sisi sote tuna muda tofauti. Muda wangu ni tofauti na muda wako. Ndiyo maana Yesu àlisema, wakati wangu bado haujafika lakini wakati wako upo tayari.

    Miaka michache iliyopita, Binti wa mfalme Diana aliushtua ulimwengu kwa kutoweka ghafla. Hakuna aliyemtegemea kuwa angefariki kwa muda ambao alifariki. Hakuna mtu yeyote aliyetegemea angalifariki Jumapili asubuhi  kama ilivyokuwa.

    Wiki moja kabla ya kufa kwake, kama ungeniuliza, ni muda gani? Ningalisema, Ni jumapili asubuhi, na muda wa kanisani. Kama ungelimuuliza yeye swali hilohilo yamkini angelijibu, Ni asubuhi nyingine ya jumapili; na siku chache kabla ya kukutana na mpenzi wangu huko Ufaransa. Lakini muda ulikuwa takribani siku saba kabla ya kifo chake. Kwa bahati mbaya hakulijua hilo.

    Jumamosi kabla ya kufariki, alikuwa anakula chakula cha jioni akiwa na mpenzi wake wa Misri kule Paris. Kama mtu angekuuliza, Ni saa ngapi? Labda ungesema, ni saa mbili kamili. Kama mtu angelimuuliza angeliweza kusema, Ni usiku wa Jumamosi muda wa kuonyesha mapenzi na kuwa na ndoto nzuri ya maisha mazuri ya baadae. Lakini alikosea; muda wake halisi ulikuwa masaa machache kabla ya kufa. Pia alikuwa na juma moja karibu na msiba wake.

    Muda wangu huzungumzia pale nilipo kutokana na ratiba ya maisha yangu. Muda wako huzungumzia pale ulipo kutokana na ratiba ya maisha yako, na Muda huzungumzia pale tulipo kutokana na ratiba ya jumla ya Mungu.

    Bila kujulikana na watu wengi, maisha ya dunia hii yanahusiana sana na muda. Kila maelekezo au fursa ina husiana na muda. Lisikie hili na ulisikie kwa makini. Kila elekezo au fursa ambayo Mungu anakupa ina mtu asiyeonekana ambaye anahesabu muda. Hesabu yake inaanza mara tu Mungu anaposema na wewe. Muda uliopewa wa kulifanyia hilI jukumu hupungua kila baada ya saa kupita. Wengi hudhani wanakwepa muda na watakuwa makini na Mungu baadaye. Usidanganywe!  Kipindi cha neema kinakaribia kuisha haraka.

    Kama nilivyosema, Malkia Diana yamkini angekuwa anapanga harusi yake. Kile ambacho hakukijua ni kwamba hakuwa mbali na usiku wa kutoweka kwake. Hakujua ukweli kwamba alitakiwa awe mlengwa wa mazishi makubwa ambayo hayajawahi kutokea.  Hakuujua wakati.

    Je, unaujua wakati? Je, tunaujua wakati?

    Kama Mungu akikuambia ufanye kazi fulani, saa nayo  imeanza kupiga alama. Muda utafika pale ambapo utashindwa kulitekeleza hili agizo.

    Wakati mwingine Mungu huzungumza na wewe: "Toa fedha kwenye ufalme wangu. Labda hili linaweza kukuchukua kipindi cha miaka mitano ya kumtii. Labda anakuambia: Enenda kama mishonari." Labda agizo hili lina muda wa miaka kumi. Baadhi ya watu hutumia miaka minane ya kipindi hicho kufanyia mambo mengine na miaka miwili ya mwisho, hujaribu kumtii Mungu. Lakini muda wao huwa mdogo. Hakuna chochote chenye maana kinachoweza kufanyika kwa miaka miwili iliyobaki.

    Siku moja, Mungu atakiondoa kipengele cha muda kwenye maisha yetu. Hili limetabiriwa kwenye Kitabu cha Ufunuo pale alipoapa kuwa hapatakuwa na muda tena. Lakini kabla muda huo,  kila kitu tunachotakiwa kufanya kina uhusiano wa karibu sana na saa inayopiga alama

    Mpendwa mkristo, kama unadhani una umilele wa kumpendeza basi unaishi kwenye udanganyifu wa hali ya juu.

    Akaapa kwa yeye aliye hai hata milele na milele, yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya:

    Ufunuo 10:6

    Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.:

    Mhubiri

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1