Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Siri za Ushindi
Siri za Ushindi
Siri za Ushindi
Ebook214 pages2 hours

Siri za Ushindi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Dag Heward-Mills ni mwandishi wa vitabu vingi, ikiwemo kitabu kinachouzwa sana "Uaminifu na Ukosefu wa Uaminifu". Yeye ni mwanzilishi wa dhehebu lenye makanisa zaidi ya elfu moja linaloitwa "The Lighthouse Chapel International". (Kanisa la Kimataifa la Lighthouse). Dag Heward-Mills, mwinjilisti wa kimataifa huhudumu katika Mkutano wa Injili wa Kimataifa na Yesu Mponyaji na mikutano duniani kote. kwa taarifa zaidi, tembelea www.daghewardmills.org.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345552
Siri za Ushindi
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Siri za Ushindi

Related ebooks

Reviews for Siri za Ushindi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Siri za Ushindi - Dag Heward-Mills

    Siri ya Ushindi ya 1

    Siri ya Ushindi ni Nini?

    Je! Umesikiza ushauri wa SIRI YA MUNGU? Nawe je! Wazuia hekima iwe yako tu?

    Ayubu 15:8

    S iri ya ushindi ni siri ambayo hukufanya wewe uwe shani iliyo hai! Siri ya ushindi ni siri ya Mungu!

    Je, umewahi kusikia kuhusu siri ya Mungu? Je, umewahi kusoma kuhusu siri ya Mungu? Je, umewahi kufunuliwa siri ya Mungu? Hekima ya Mungu iliyofichika ndiyo siri ya Mungu! Umewahi kupokea hekima ya Mungu? Umewahi kupokea ufunuo kutoka juu? Iwapo hujasikia siri ya Mungu, basi kwa kweli umekosa kile unachohitaji hasa. Siri ya Mungu ni hekima ya Mungu katika fumbo ambalo liliazimiwa kwa utukufu wako na kurembeshwa kwako tangu milele.

    Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu:

    1 Wakorintho 2:7

    Unachohitaji si hekima ya kidunia. Hekima ya kidunia ni mafunzo kuhusu uchumi, sheria, hisabati, sayansi, uhasibu n.k. Mafunzo haya yote ya kidunia ni mazuri lakini ni hekima ya kibinadamu ya kidunia. Kuna mahali pa mambo haya yote. Lakini hayana nafasi kanisani. Kanisani, tuko na mambo ya kiwango cha juu zaidi "Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu (1 Wakorintho 2:4) Kunayo aina ya juu zaidi ya hekima itokayo kwa Mungu. Hekima ya Mungu ina siri ya Mungu. Hiyo ndiyo unayohitaji kwa ajili ya maisha yako. Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu" (1 Wakorintho 2:7). Aina hii ya hekima imeazimiwa kwa utukufu wako na kukugeuza wewe uwe shani inayoishi.

    Hebu tutazame manufaa ya ajabu ya kugundua siri ya Mungu.

    Sababu Sita Za Kukufanya Sharti Ugundue Siri ya Mungu

    1. Uzima na mauti vinategemea ugunduzi wako wa siri ya Mungu:

    Mfalme akajibu, akasema, Najua hakika ya kuwa mnataka kupata nafasi, kwa sababu mmeona ya kuwa lile neno lenyewe limeniondoka. Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionesha tafsiri yake.

    Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala mtawala, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo. Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili. Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. Basi ile amri ikatangazwa, na hao WENYE HEKIMA WALIKUWA KARIBU NA KUUAWA; na WATU WAKAMTAFUTA DANIELI NA WENZAKE ILI WAUAWE.

    Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonesha mfalme tafsiri ile. Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; ILI WAOMBE REHEMA KWA MUNGU WA MBINGUNI KUHUSU SIRI HIYO, ILI KWAMBA DANIELI NA WENZAKE WASIANGAMIZWE PAMOJA NA WENYE HEKIMA WA BABELI. NDIPO DANIELI ALIPOFUNULIWA SIRI HIYO katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni. Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. Yeye hubadili majira na nyakati; hutengua na kuteua wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; YEYE HUFUNUA MAMBO YA FUMBO NA SIRI; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake.

    Danieli 2:8-13, 16-22

    Danieli na wenzake walikuwa katika hatari kubwa ya kuuawa. Kifo kilikuwa kikiwakodolea macho. Mfalme alijua kwamba wengi wa wale wenye hekima, wanajimu na wachawi walikuwa wanafiki, waliojaa udanganyifu. Mfalme Nebukadineza alitaka sana kuondoa walaghai wote katika ikulu yake. Mtihani ambao mfalme alitoa ungehakikisha kwamba ni wenye hekima wa kweli ndio wangesalia katika ikulu yake kama washauri. Kuwa mshauri mzuri, unahitaji kujua siri fulani. Kuna siri fulani katika mafanikio yote makubwa na katika umaarufu wote mkubwa wa kila mtu.

    Mara nyingi, tunakisia kimakosa kuhusu kile kilichomfanya mtu fulani kuwa maarufu. Mara nyingi tunakuwa kwa kweli hatufahamu siri ya ufanisi wa mtu fulani. Kugundua siri fulani kunakuzuia wewe usiangamie. Roho wa ufahamu pia ni Roho wa Mungu. …maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA (Isaya 59:19). Adui atakapokuja kukuua, Roho wa ufahamu utainua kinga dhidi yake. Neno ‘kinga’ ni neno la Kiebrania nus linalomaanisha kusababisha kutoweka. Kupitia kwa ufahamu, mambo fulani yanasababishwa kupotea. Miaka iliyopita, kila mtu aliyeugua maleria, pumu, shinikizo la juu la damu au kisukari alifariki tu kutokana na magonjwa haya. Kupitia kwa ufahamu, magonjwa haya yamesababishwa kupotea na kutanguliwa.

    Uzima na mauti vinaweza kutegemea ufahamu wako wa siri fulani. Kuna siri ambazo ni muhimu sana kwa maisha yako. Yeyote aliyejaliwa kufurahia siri za Mungu anajua kwamba uzima na mauti kwa hakika vinategemea ufahamu wao wa siri fulani. Hii ndiyo maana unahitaji kutafuta ufunuo kutoka kwa Mungu. Ufahamu wako wa siri fulani unakupa wewe udhibiti mzuri zaidi. Maendeleo yote ya kisayansi, tiba, elimu ya sayari, ukulima, uhandisi wa mitambo na fizikia yanategemea siri ambazo zimegunduliwa. Siri hizo ni ukweli uliodumu kwa maelfu ya miaka. Kimsingi, wavumbuzi ni wagunduzi wa siri. E wakati wote imekuwa sawa na mc². Einstein alikuwa tu mgunduzi wa siri iliyodumu kwa maelfu ya miaka.

    Siri ya Ushindi ni ufunuo ambao unakuletea wewe ushindi! Siri za ushindi ni mafunuo ya kutoka kwa Roho Mtakatifu ambayo yanaweza kuleta utofauti katika kazi yako na huduma. Mara nyingi, tofauti baina ya uzima na mauti ni ufahamu mdogo tu. Mungu aweza kukupa ufahamu leo hii! Mungu anaweza kukusababishia wewe ujue siri kidogo ambayo inaweza kubadilisha kila kitu kuhusu maisha yako na huduma. Watu wengine huita vipande hivi vya ufahamu ufunuo. Vyovyote utakavyo kuyaita haya, siri hizi za ushindi zitakuelekeza kwa ushindi mkubwa na mafanikio.

    Mifano mingi mizuri kuhusiana na athari za siri za ushindi yaweza kupatikana katika vitabu vya historia. Katika karne ya kumi na nne, ugonjwa ulioitwa Tauni uliingia ulimwenguni na ukamaliza mamilioni ya watu. Watu wengi walifariki na idadi kubwa ya watu iliangamizwa. Hofu ya ugonjwa huu ilidumu kwa miaka kadhaa huku Tauni hiyo ilipoendelea kuchipuka maeneo tofauti ya dunia, ikitishia watu na kuangamiza makundi makubwa ya watu.

    Kwa kweli, Uropa ya zama hizi miaka ya mapema ilikumbwa na janga baya kabisa la kibinadamu katika historia ya Uropa, wakati Tauni hiyo ilipolipuka Uropa mwaka wa 1347. Tauni hii kwa kweli iliangamiza theluthi moja ya idadi ya watu wa Uropa. Waweza kufikiria huo ni ugonjwa wa aina gani unaoenea katika bara zima na kuangamiza theluthi moja ya idadi ya watu wa bara hilo? Hata nyakati hizi za sasa, wakati virusi vya Ebola viliposambaa Sierra Leone, Liberia na Guinea, ni watu elfu kumi tu waliofariki. Hebu fikiria kuhusu ugonjwa ambao uliweza kuangamiza mamilioni ya watu na kusafisha idadi kubwa ya watu wa bara zima.

    Waathiriwa wa tauni walikuwa na uwezekano mdogo sana wa kuepuka kifo kwa sababu ya dalili za ugonjwa kama vile joto kali mwilini, na kuvuja damu kwa ndani, ambako kulisababisha alama nyeusi na uvimbe. Yeyote aliyeambukizwa ugonjwa huu alifariki kwa muda wa siku tatu hadi tano.

    Madaktari wakati huo walidhani tauni ilisababishwa na unyevunyevu uliochafua hewa, miili iliyokuwa ikioza ambayo haikuzikwa na mazingira machafu. Watu wengine walidhani ugonjwa huo ulikuwa ukienezwa na Wayahudi. Madaktari wa kimatibabu wa karne ya kumi na nne hawakujua kwamba ugonjwa huo ulienea kupitia kwa bakteria anayebebwa na viroboto na panya. Taaluma ya kimatibabu haikujua kuhusu dawa ya antibiotiki! Hawakuwa na njia yoyote ya kupambana na ugonjwa huu. Ufahamu wa siri ya dawa ya antibiotiki ingeokoa mamilioni ya watu kutokana na kifo.

    Hilo halikuwezekana hadi mwaka wa 1877 ambapo Louis Pasteur na Robert Koch walichunguza kwamba bacillus anaesambazwa na hewa anaweza kuzuia ukuaji wa bakteria mwingine, bacillus anthracis. Kioja hiki kilichodhihirishwa na dawa za anti-bakteria kiliitwa antibiosis. Ilikuwa hadi mwaka wa 1942 ambapo dawa zilizofanya kazi kwa njia hiyo ziliitwa antibiotics na mwana mikrobiolojia wa Kimarekani, aliyeitwa Seiman Waksman.

    Ilikuwa siri hii ya antibiotiki ambayo haikuweko katika karne ya kumi na nne! Hii ndiyo siri ambayo ingezuia mamilioni ya watu wasiangamie kutokana na tauni katika karne ya kumi na nne. Dawa rahisi kama vile streptomycin, gentamicin na ciprofloxacin zingezuia ugonjwa katika uharibifu wake. Leo hii, uwezekano wa mtu kufa kutokana na tauni ni mdogo sana.

    Hakungekuwa na hata mtu mmoja wa kufa kutokana na tauni iwapo tungekuwa na siri ya antibiotiki. Siri ya ushindi hubadilisha maisha kwa kiwango kikubwa. Siri ya ushindi huokoa maisha ya watu wengi. Siri ya ushindi hubadilisha kila kitu.

    Mojawapo ya ombi muhimu sana maishani mwako sharti liwe ombi la kupata roho ya ufunuo. Ombea siri za ushindi! Hili ni ombi la kupata ufunuo na ufahamu kwa wakati mwafaka ambao utaleta mabadiliko maishani mwako.

    2. Ufanisi wako unategemea ugunduzi wako wa siri ya Mungu:

    Haya ndiyo BWANA amwambiayo Koreshi, masihi wake, ambaye nimemshika mkono wake wa kulia, ili kutiisha mataifa mbele yake, nami nitalegeza nguvu za wafalme; ili kufungua milango mbele yake, hata malango hayatafungwa.

    Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; Nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukatakata mapingo ya chuma;

    Nami nitakupa HAZINA ZA GIZANI, na MALI ZILIZOFICHWA ZA MAHALI PA SIRI, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.

    Isaya 45:1-3

    Siri za ushindi zitakuelekeza kwenye ufanisi. Utajiri mwingi umefichwa usionekane. Utajiri mwingi halisi umefichwa usionekane. Ndiyo maana umeitwa hazina za gizani. Utajiri mwingi katika dunia yetu umefichwa mahali pa siri. Ili uweze kugundua utajiri wa dunia hii, utahitaji kupata ufunuo wa kung'amua jinsi ya kutambua pale utajiri ulipo. Unahitaji kugundua mahali pa siri ambapo utajiri umefichwa.

    Kwa nini watu wengine ni matajiri bado limebaki kuwa fumbo kwa watu wengi. Watu hufanya mambo mengi ili waweze kufanikiwa, lakini ni wachache tu wanaopewa siri ya ufanisi. Fedha zimefungiwa mahali pa siri. Bila kuwa na ufahamu wa siri fulani, utaishi katika hali ya ufukara maisha yako yote. Unahitaji roho ya ufunuo ikupatie siri za ustawi na ufanisi. Ukuaji wa kanisa unaachiliwa kupitia kwa ufahamu wako wa siri fulani. Shida zetu zote zinaweza kufikishwa mwisho wake ghafla iwapo tutagundua siri ya ufanisi halisi.

    Unahitaji kugundua siri kwa sababu umaarufu na ufanisi vinategemea ugunduzi wa siri muhimu. Watu waliovumbua magari, ndege, padi za kielektroniki (kama vile iPad), simu na televisheni ndio mamilionea wa dunia yetu. Mataifa mengi hayajui siri za jinsi ya kufanya mambo haya yafanye kazi. Yale mataifa yaliyogundua siri hizi yamekuwa ndio matajiri wakubwa duniani. Hebu fikiria utofauti uliopo baina ya wale ambao wamegundua siri ya kutengeza simu za rununu na wale ambao huvuna tu nyanya na machungwa. Huhitaji siri yoyote maalum ya kuweza kuvuna nazi au pilipili. Lakini unahitaji kujua siri fulani kuweza kufanya televisheni ifanye kazi. Kujua siri fulani kunafanya watu wawe wenye thamani kubwa sana. Sio tu kwamba Danieli alihifadhiwa hai, bali pia alifanyika mtu wa tatu maarufu sana mjini na akapokea ufanisi uliodhihirishwa na mkufu wa dhahabu ambo alivikwa shingoni mwake. Wakati unapogundua siri ya Mungu kupitia roho ya ufunuo, wewe pia utakuwa mtu maarufu. Utafunikwa kwa dhahabu, na roho ya ufunuo.

    Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.

    Danieli 5:29

    3. Siri ya Mungu imepewa wanyofu na manabii Wake.

    Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, bali siri yake ni pamoja na wanyofu.

    Mithali 3:32

    Huwezi kuambia kila mtu siri zako. Kwa nini unamtarajia Mungu amuambie kila mtu siri zake? Watu ambao Mungu amewapa siri yake ni wale ambao amewaona kuwa wanyofu. Mungu huzuia ufunuo wake kwa watu ambao ni waovu na huwapa ufunuo wake wanyoofu.

    Watumishi wanakuwa karibu na mabwana zao na hufanya kazi katika zamu zao. Kwa hiyo si jambo la kushangaza kwamba watumishi wanajua siri nyingi ambazo watu wa nje hawawezi kuzijua kamwe. Jitahidi uwe mtumishi wa Mungu na ujitahidi kuwa nabii wake nawe utakuwa na uhakika wa kupokea kwa wingi bubujiko la siri za ajabu.

    Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

    Amosi 3:7

    4. Siri ya Mungu hutolewa kwa majira maalum ya maisha yako:

    Laiti ningekuwa kama nilivyokuwa katika miezi ya zamani, kama katika siku hizo Mungu aliponilinda;

    Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;

    Kama nilivyokuwa KATIKA SIKU ZANGU ZA KUKOMAA, HAPO SIRI YA MUNGU ilipokuwa hemani mwangu;

    Ayubu 29:2-4

    Ayubu alifurahia kujua baadhi ya siri hizi katika majira fulani ya maisha yake. Alizungumzia kwa hisia nyingi kuhusu majira yale ambayo Mungu alimpa siri na ufunuo. Utakuwa ukiangalia nyuma kila wakati kwa majira ambayo Mungu alikupa mafunuo fulani.

    Ayubu alitamani sana kupitia tena nyakati zile za ufunuo. Manabii wa kweli watakuambia wakati wanapopata ufunuo na wakati wanapokuwa hawana ufunuo. Ukweli ni kwamba ufunuo hauji kila wakati. Ayubu alikuwa anasema anatamani angekuwa kijana tena, wakati ambapo siri za Mungu zilikuwa zikifunuliwa kwake (Ayubu 29:4).

    Kenneth Hagin alielezea jinsi Mungu alivyombariki na njozi nane za Yesu Kristo baina ya mwaka wa 1950 na 1958. Alielezea jinsi ambavyo Bwana hakumtokea kwa njia hiyo tena kuanzia mwaka wa 1958 na kuendelea. Kenneth Hagin alikuwa na umri wa miaka thelathini na tatu tu wakati Bwana alipomtokea. Alihudumu hadi pale alipofikia

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1