Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka
Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka
Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka
Ebook158 pages3 hours

Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Yesu alisema: basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua. Je, nyoka ni wenye busara kweli? Kwa nini Yesu alitoa ushauri kama huo? Anza safari katika kitabu hiki cha kuvutia cha Dag Heward-Mills, na ugundue busara iliyofichika ya nyoka.

LanguageKiswahili
Release dateApr 7, 2018
ISBN9781641345569
Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka

Related ebooks

Reviews for Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Inamaanisha Nini kuwa na Busara kama Nyoka - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Busara ya Nyoka

    . . . basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.

    Mathayo 10:16

    Nyoka Wana Busara

    Si jambo la ajabu kwamba binadamu huogopa nyoka. Pia si jambo la ajabu ikiwa watu wana heshima inayostahili kwa nyoka. Ni ukweli kwamba nyoka ni viumbe vya ajabu, wanaoendelea kuishi vizuri sana na kuzaana licha ya chuki ya jumla ambayo iko kwao.

    Iwapo Yesu hangezungumza kuhusu busara ya nyoka tungekuwa tumepuuza busara kuu ambayo wanaishi kwayo. Kwa sababu Yesu aligusia busara ya nyoka, sote lazima tuzingatie vilivyo viumbe hawa na kujifunza kile tunachoweza kutoka kwao. Kwa hiyo, busara ya nyoka ni nini? Ni kitu gani kinachomfanya nyoka kuwa mwenye busara?

    Je, wewe hungetaka kupata busara ambayo ingekufanya ustawi kuliko wenzako?

    Je, wewe hungetaka kupata busara ambayo ingekufanya wewe uwe na ufanisi katikati ya upinzani mkali na chuki?

    Je, wewe hungetaka kupata busara ambayo ingekufanya wewe ustawi kupitia kwa mandhari zote za maisha zinazobadilika? Hata hivyo, ni watu wangapi wanaoweza kusalia kuwa matajiri na wenye ufanisi katika misimu yote ya maisha?

    Je, wewe hungetaka busara ambayo ingefanya watu kukuogopa na kukuchukulia wewe kwa heshima inayostahili? Je, wewe hutaki busara ambayo itakufanya uyafikie kimya kimya malengo yako yote katika maisha haya?

    Nina uhakika unataka busara kama hiyo. Hakika, hiyo ndiyo busara ya nyoka! Hiyo ndiyo sababu Yesu alisema lazima tuwe na busara kama nyoka.

    Sababu Saba Za Kwa Nini Nyoka Wanachukuliwa Kuwa Na Busara

    1. Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu wamezaana na kustawi zaidi kuliko mnyama mwingine yeyote wa mwituni.

    2. Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu wameendelea kuishi katika dunia ambayo wakati wote imeendelea kufanyika ya kisasa. Utagundua kwamba wanyama wengi wa mwituni wanatoweka katika dunia yetu ya kisasa.

    3.Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu wameweza kustawi hata ingawa wamechukiwa na kila mtu.

    4. Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu huzua hofu na heshima katika binadamu. Binadamu hawaogopi na kuheshimu wanyama wengi lakini wanaogopa na kuheshimu nyoka.

    5. Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu ya uwezo wao wa kuishi katika kila bara na kila sehemu ya dunia.

    6. Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu ya uwezo wao wa kufanya kazi katika mazingira yote; ardhini, baharini, kwa maji baridi na hata kwenye anga.

    7. Nyoka wanachukuliwa kuwa na busara kwa sababu ya uwezo wao wa kuyafikia malengo katika dunia hii. Licha ya vipingamizi vilivyoko dhidi ya nyoka, wanaweza kuishi, kula na kuzaana.

    Kuwa mwenye busara, lazima ufikirie, utafakari na kuwaza kuhusu kanuni, ukweli na kauli. Huwezi tu kufunika kwa juu misemo yenye maana ya ndani sana. Yesu aliposema, 'basi iweni na busara kama nyoka,' alikuwa anatoa msemo wa gizani; msemo ambao umejaa busara, maana na maelekezo. Kila sura ya kitabu hiki ina kipengele kimoja cha busara kuu ya nyoka ambayo imeifanya kuwa na ustawi zaidi kuliko mnyama yeyote wa mwituni anayepatikana mahali wanyama pori wanapofugwa.

    Je, umewahi kufikiria kuhusu ukweli wa kwamba hakuna simba wanaozunguka karibu na nyumba yako? Lakini pengine kuna nyoka katika eneo lako. Angalau, nimeona nyoka katika kila nyumba ambayo nimewahi kuishi. Simba hawapatikani tu katika eneo lako. Wamemalizwa kabisa kwa sababu hawafanyi kazi kwa busara ya nyoka. Wao hufanya kazi kwa aina nyingine ya busara - busara ya simba.

    Busara ya simba hutufanya sisi kuwa na heshima inayostahili na hofu ya simba. Lakini busara ya simba haijamuwezesha simba kustawi na kuzaana kwa ufanisi katika miji duniani kote. Idadi ya simba inafifia! Simba wanatoweka! Nyoka, kwa upande mwingine, hupatikana kiajabu katika kila jiji na kitongoji. Kwa mtazamo huo, nyoka ni mwenye busara kuliko simba kwa sababu ameweza kushinda, kustawi na kufanikiwa ilhali simba wamekuwa wachache zaidi na wanakaribia kutoweka kabisa.

    Sura ya 2

    Stadi wa Maisha ya Kutotegemea Wengine

    Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, WALA MSIWE NA HAJA YA KITU CHOCHOTE.

    1 Wathesalonike 4:11

    Nyoka Wana Busara Kwa Sababu Hawategemei Wengine

    K iongozi lazima asitegemee yeyote ili kuweza kupata heshima ya wengine. Mhuduma lazima ajitahidi ili kuepuka mambo ya ombaomba kwa mifumo yake yote. Ombaomba ni ombaomba hata kama inafanywa na marais, wanasiasa au wachungaji! Ombaomba ni ombaomba hata kama itapewa majina ya kuheshimika kama kutafuta wawekezaji, kutafuta msaada au kuhudhuria makongamano ya ufadhili. Njia mbadala na kutegemea wengine ni kufanya shughuli zako na kufanya kazi kwa mikono yako mwenyewe.

    Kwa nini uzunguke ukiombaomba na kuulizia vitu? Haujaweza kusoma wakati Daudi aliposema, … sijamwona mwenye haki ameachwa wala mzawa wake akiomba chakula (Zaburi 37:25). Je, huoni haya kuishi maisha yako ukitarajia mtu mwingine kukupatia kitu? Unadhani watu wengine watakuheshimu wewe kwa njia yoyote unapowategemea wao wakati wote? Hapana, hawatakuheshimu! Soma andiko hili kwa umakini na ulitafakari. Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu chochote (1 Wathesalonike 4:11).

    Nyoka wanadhihirisha kwamba wao ni stadi wa maisha ya kutotegemea wengine. Wanaweza kuendelea kuishi peke yao kuanzia siku waliyozaliwa. Kuwa na busara kama nyoka lazima uweze kuwa wa kujitegemea au usiyetegemea wengine. Ni jambo la kusikitisha kuona marais wa mataifa maskini wakizunguka kutafuta misaada na mikopo kutoka kwa nchi tajiri zaidi.

    Kwa bahati mbaya, mataifa mengi ambayo yalikuwa chini ya ukoloni hayajaweza kuendelea mbele bila hao mabwana zao wa kikoloni. Hawajaweza tu kumudu huo uhuru. Nchi nyingi maskini ni dola zilizoanguka, zisizoweza kujitawala zenyewe! Zilipigania uhuru lakini haziko huru kamwe. Husherehekea uhuru kila mwaka ilhali wanastahili kuwa wakiomboleza hali yao ya kutoweza kujitegemea!

    Viongozi wasiokuwa na uwezo wala matumaini wametawala mataifa na kuyaongoza kwa kuyadidimiza katika hali ya ufukara. Ukweli wa kwamba viongozi hawawezi kujenga barabara kati ya miji, kutoa huduma za umeme, maji, shule na hospitali ni ushahidi wa uongozi mbaya na usioweza. Kwa viongozi wa baadhi ya nchi maskini, uongozi wa taifa unamaanisha kuzunguka na kuomba fedha.

    Nyoka kwa upande mwingine, wanajitegemea kuanzia siku wanayozaliwa na wanaweza kuishi kwa ufanisi kando na wazazi wao. Nyoka wengi wanaweza kuua kuanzia siku wanayozaliwa na mara nyingi huishi peke yao kuanzia siku ya kwanza ya maisha yao. Tofauti na mataifa fulani ambayo yanahitaji matoleo na tunu kutoka kwa mataifa mengine ili kuweza kuishi, nyoka hawahitaji usaidizi na wanaweza kuanzisha maisha yao ya ufanisi wa kujitegemea.

    Jinsi Unavyoweza Kudhihirisha Kwamba Unao Uwezo wa Kujitegemea

    1. Ikiwa wewe una busara kama ya nyoka utaishi maisha yako pasipo kutarajia fedha, tunu, ridhaa, misaada au hata mikopo.

    Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,

    ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala chochote kilicho chako, USIJE UKASEMA, NIMEMTAJIRISHA ABRAMU;

    Mwanzo 14:22-23

    Ibrahimu hakuhitaji yeyote wa kumfanya yeye tajiri. Kwa kweli, hakutaka yeyote wa kufikiria kwamba walimfanya yeye kuwa tajiri.

    Watoto ndio hutarajia wakati wote kwamba Mama na Baba watawapatia kitu cha kusuluhisha shida zao. Mtu anapokuwa hawezi kuishi kwa kujitegemea, mara nyingi hutarajia watu wampe kitu. Watu wengi hutazamia Marekani na Uingereza, wakitarajia kupata kitu. Ukweli wa kwamba hata unatarajia kwamba Wamarekani na Wazungu watakuja kukusaidia inaonyesha kwamba huwezi kuishi maisha ya kujitegemea.

    Lazima usitarajie kwamba mtu yeyote mwingine atakufanya wewe uwe tajiri. Kwa nini wataka mtu fulani akupatie wewe kitu? Kwa nini unaangalia, unatumaini na kutarajia tunu, mkopo au matoleo? Hakika, viongozi wasiokuwa na uwezo hufunga watu macho wanapotangaza kwamba wanatafuta mikopo ya kuanzisha miradi. Mara nyingi, hakuna uhitaji huo wa mkopo. Kuna hitaji tu la kupunguza uharibifu, ufisadi na usimamizi mbaya wa rasilimali. Viongozi hawa wabaya hupumbaza umma kwa usemi wao kuhusu kupata mikopo. Lakini wale wenye macho wanaweza kuona kwamba kwa kweli hakuhitajiki mkopo.

    Lazima uongoze maisha yako kwa njia ambayo itakufanya wewe uwe huru kutokana na mfadhili wa kutoka nje. Viongozi wasiokuwa na uwezo wowote wakati wote wanafurahia kwenda kwa makongamano ya ufadhili kusikiliza kama kuna ufadhili na usaidizi gani ambao utatolewa kwao. Jambo la kushangaza ni kwamba, baadhi ya viongozi hawa huanza kulala katika mikutano hiyo ya ufadhili kwa sababu tu hawako mahali wanapostahili haswa kuhusiana na uongozi.

    2. Ikiwa wewe una busara kama nyoka utakuwa stadi wa maisha yako mwenyewe na hutahitaji yeyote kukujengea wewe vitu.

    Busara yako itakuongoza uinuke na kujijengea mwenyewe. Hii ndiyo sababu mtu anasemekana kuwa mwenye busara anapojenga vitu. Kutokuwa na uwezo wa kujenga inadhihirisha ukosefu wa busara. Ikiwa wewe una busara kama ya nyoka utainuka na kujenga vitu ambavyo unahitaji. Sulemani alijenga vitu vingi mwenyewe. Alijenga majumba, akapanda mashamba ya mizabibu, akatayarisha bustani na mashamba ya matunda na kupanda miti ya kila aina ya matunda na kufanya mabwawa.

    Nikajifanyia mambo makuu; nikajijengea nyumba; nikajipandia mashamba ya mizabibu;

    nikajifanyia bustani na viunga, na kuipanda humo miti yenye matunda ya kila namna;

    nikajifanyia mabwawa ya maji, ya kuunyweshea msitu mlimopandwa miti michanga.

    Mhubiri 2:4-6

    Mchungaji anayeendesha kanisa akitarajia mtu wa kuja amjengee jengo huyo hana uongozi uliokomaa na wa kujitegemea. Hadi pale utakapojifunza kuangalia raslimali chache ulizo nazo na kupanga maisha yako kulingana na kile ulicho nacho, wewe huwezi kuishi maisha ya ukomavu wa kujitegemea.

    3. Ikiwa wewe una busara kama ya nyoka hutaomba tunu, mikopo na kuomba usaidizi wakati wote.

    Lazima usiombe tunu au kuombaomba fedha. Wewe unapokuwa na busara kama ya nyoka unajua kwamba unajitegemea kuanzia siku ya

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1