Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo
Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo
Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo
Ebook162 pages6 hours

Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Usiku mmoja, wakati akiwa ni mwanafunzi wa utabibu katika mji mmoja huko Ghana, katika hali ya mwujiza Mungu alimpaka mafuta Dag Heward-Mills wakati alipokuwa akimsubiri Bwana. Alipakwa mafuta kwa namna isiyo ya kawaida na kusikia maneno, “Tangu sasa na kuendelea unaweza kufundisha...” Wito huu usio wa kawaida ndio uliomwongoza kwenye huduma iliyosambaa duniani kote.

LanguageKiswahili
Release dateMay 15, 2018
ISBN9781641353687
Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo

Related ebooks

Reviews for Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Nini Maana ya Kuwa Mchunga Kondoo - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Mchungaji ni Nani?

    Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na KUTAWANYIKA kama kondoo WASIO NA MCHUNGAJI.

    Mathayo 9:36

    Hakuna haja ya sisi kupambana na tafsiri ya Mchungaji ni nani. Mchungaji ni muongozaji wa kondoo mwenye upendo na kujali kondoo. Mchungaji ni mtu ambaye ameitwa na Mungu kwa ajili ya kuwaangalia kondoo.

    Katika Biblia, watu wa Mungu huitwa kondoo na anawainua wanadamu anaowaita wachungaji ili wawachunge hawa kondoo. Mungu hatuoni kama kundi la nyoka, mijusi, paka na mbwa. Hapana! Unatuona kama kundi la kondoo wanaohitaji upendo, kujaliwa na uongozo.

    Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, NA SISI TU WATU WA MALISHO YAKE, NA KONDOO ZA MKONO WAKE. INGEKUWA HERI LEO MSIKIE SAUTI YAKE!

    Zaburi 95:6-7

    Ninaandika kitabu hiki kwa sababu ni imani yangu kubwa kwamba watu wengi wanaweza kujiunga katika kuwashugulikia kondoo wa Mungu. Ni wakati wetu sisi kuinuka na kujiunga katika kazi kuu ya kuwachunga watu wa Mungu. Kuwa mchungaji ni mojawapo ya vitu vikuu vya wakati wote kwa sababu Bwana wetu huwapenda watu na huwaona kama kondoo wanaohitaji upendo na mwongozo. Kuwa mchungaji ni kazi iliyo kuu sana. Hiyo ndo maana ni kazi aliyopewa Mtume Petro, ambaye ni kiongozi wa kanisa. Kumbuka! Yesu alimuambia Petro athibitishe upendo wake kwake Yesu kwa kuwalisha na kuwachunga kondoo. Petro, wanipenda? Kama unanipenda, lisha wana kondoo wangu!

    Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.

    Yohana 21:15-17

    Kuna aina mbili za watu katika kila kanisa: wachungaji na kondoo. Ama wewe ni mchungaji au ni kondoo. Mchunga ni kama mchungaji. Hakika, katika lugha nyingi hakuna neno la kutofautisha ‘Mchunga kondoo’ na ‘Mchungaji’. Neno hilohilo linalotumika kwa mchunga ndilo linalotumika kwa ajili ya mchungaji. Napendelea kutimia neno ‘mchunga’ kwa sababu linasaidia kila mtu kuelewa ile kazi husika. Napendelea kutumia neno ‘mchunga’ kwa sababu ni kielelezo kilichowazi zaidi kuhusu mchungaji halisi ni nani. Kuwa mchunga inamaanisha kwamba ni lazima uwaone watu kama kondoo na ushirikiane nao kama kondoo.

    Kuna tafsiri nyingi za neno ‘mchungaji’ zisizo za kawaida na kila mtu ana mtazamo wake kuhusu nini mchungaji anachopaswa kuwa na kufanya. Hata hivyo, ukisema wewe ni mchunga kondoo unajua haraka kuwa kazi yako ni kuchunga kondoo. Kwa hakika, ukiwa mchunga huwezi kuchunga watu ambao hawana sifa za kondoo na hawawezi kuongozwa, kuelekezwa, kufundiswa na kujaliwa. Katika lugha ya kingereza, neno mchungaji kawaida hutumika kumanisha ‘mtu wa Mungu’ au muakilishi wa Mungu. Kwa sababu hiyo, manabii, mitume, wazee na karibia kila muakilishi wa Mungu anaitwa ‘mchungaji’. Mchungaji ni aina ya mfanyakazi ambaye ana muda wa kujali, muda wa kupenda, muda wa kulisha na muda wa kuwakusanya kondoo.

    Ona katika msitari hapo juu kwamba kondoo walitawanyika kwa sababu hapakuwa na mchungaji. Kondoo hawatawanyiki kwa sababu hakuna nabii. Kondoo hawatawanyiki kwa sababu hakuna mwinjilisti au mzee wa kanisa. Kondoo wanatawanyika kwa sababu hakuna mchungaji. Ni imani yangu kubwa kwamba watu wengi wameitwa kuwa wachungaji. Watu wengi wana uwezo wa kutoa upendo, muda wao, nguvu zao ili kumtafuta mtu mwingine. Nalijua hili kwa sababu watu wengi wanakuwa akina mama na akina baba na wana uwezo wa kiasili wa kuwajali watoto zao. Kuwa mchungaji inahusisha sana kuonyesha upendo, kujali na kuwaongoza kondoo kiasi kwamba wanawaita wachungaji wao akina baba zao. Mtu akiinuka na upako wa mchungaji, watu husanyika karibu naye kwa sababu kila mtu anahitaji upendo, kujaliwa na uongozo.

    Jifunze kutumia neno ‘mchunga’ ukiwa unaelezea wale ambao wanawajali watu wa Mungu na kuwalisha, kwa sababu hivyo ndivyo walivyo. Ukijitambulisha kama mchunga, unakusaidia kuweka mtazamo wako juu ya kazi yako kama mchunga. Leo, watu wengi ambao wanapaswa kuwajali, kuwapenda na kuwaongoza kondoo wamekuwa watu wa kidunia ambao wameendana sana na chuo kikuu kuliko kanisa.

    Laiti ungemkuta mchunga ameketi nyuma ya meza ya benki, ungemuuliza haraka, ‘mbuzi na kondoo wako umewaacha wapi? wanaendeleaje? Nani anawaangalia? Leo wachungaji wengi wameacha mbuzi wao na kondoo na wanakutwa katika sehemu za sokoni wakifanya kitu cha tofauti kabisa na uchungaji. Wamedharau heshima ambao tumepewa ya kuwachunga watu wa Mungu na kuwalisha. Usitupe kitabu hiki. Uchungaji ni jukumu muhimu sana. Ni kazi ya Mungu. Ichukulie kwa kumaanisha. Unaweza kuwa mchungaji na kuwajali watoto wa Mungu. Nawe pia unaweza kufanya kitu kwa ajili ya Mungu!

    Kulikuwa na wakati tulipokea lakini ni wakati na sisi tutoe! Kulikuwa na wakati tulifundishwa lakini ni wakati na sisi tufundishe! Kulikuwa na wakati tuliongozwa na mtu lakini ni wakati tuwaongoze wengine! Jitoe kwa ajili ya hii kazi muhimu ya uchungaji – kupenda, kujali na kufundisha watu. Ni heshima. Hata kama wewe ni mtu wa kawaida asiyelipwa na kanisa, unaweza ukawa mchunga. Watu wengi wa kawaida wako katika huduma. Unaweza kuwa mmoja wa hao watu wa kawaida wenye heshima wanaomtumkia Mungu kama wachunga kondoo.

    Kama uko katika huduma ya muda wote, jifikirie kama mchungaji kuliko mtumishi wa Mungu. Hili litakusaidia kuelewa vyema mwito wako. Endelea katika kupenda, kujali, kuongoza na katika vipawa vya Mungu vya kufundisha na utakuwa mchungaji wa watu wa Mungu. Kumbuka kwamba Yesu anawapenda sana kondoo wake. Alikufa kwa ajili yetu. Kwa hakika anatupenda sana! Kila anayewashugulikia kondoo wa Mungu ameingia moja kwa moja katika upendo wa Mungu kwa sababu Yesu aliwapenda na kufa kwa ajili ya hawa kondoo.

    Sura ya 2

    Kwa nini Unaweza kuwa Mchungaji

    Katika sura hii, nataka nikuonyeshe kwamba kuna sababu nyingi za kimaandiko za kwa nini unapaswa kuwa mchungaji. Naamini kwamba katika hatua fulani ya ukuaji wako wa Kikristo, unaweza kuwa mchungaji walau katika hatua fulani. Biblia inatufundisha katika sehemu mbalimbali kuhusu wewe kuzaa matunda katika huduma. Neno pia hutufundisha kwamba wengi na sio wachache waitwao katika huduma.

    Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji [poimen] na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

    Waefeso 4:11, 12

    Tafsiri ya kawaida ya mstari huu ni kwamba Mungu alitoa ofisi maalumu za kihuduma kwa Kanisa kwa sababu kuu tatu:

    1. Kuwakamilisha watakatifu

    2. Kufanya kazi ya huduma

    3. Kujenga mwili wa Kristo

    Hili ni kweli. Halikadhalika, ni lazima tufahamu kwamba watafsiri wa Biblia waliongeza vituo vya uandishi ambavyo wakati mwingine huleta tafsiri mbaya ya matini. Ukiondoa mkato kwenye Waefeso 4:12, inakupa maana tofauti kabisa, ambayo ninaamini inakuwa imekamilika zaidi. Ondoa mkato katika Waefeso 4:12 na uangalie mstari nini unavyosema sasa.

    Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji [poimen] na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

    Waefeso 4:11, 12

    Sasa andiko linasema kwamba Mungu alitoa mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu kwa kuwakamilisha watakatifu ili kazi ya huduma itendeke.

    Kwa maneno mengine, hizi ofisi maalumu za kihuduma zimetolewa ili kuwakamilisha watakatifu wa kawaida ili kuwawezesha (watakatifu) wafanye kazi ya huduma. Hii ina maana gani? Kwa njia rahisi hii inamaanisha kwamba watakatifu wa kawaida wanaweza kufanya kazi ya huduma. Pia inamaanisha kwamba kazi ya huduma sio jukumu tu la baadhi ya mitume na waalimu.

    Wachunga wanaweza kukamilisha sehemu kubwa ya huduma kwa namna ya kuridhisha.

    Ukitafsiri Waefeso 4:11, 12 kwa namana hii inaweka jukumu la huduma juu yetu sote na sio juu ya watu maalumu wachache. Hii lazima ni sababu, kwa sababu Biblia inasema waitwao ni wengi!

    Mungu hajawaita watu wachache ili wafanye kazi yake. Mara zote Mungu amewaita watu wengi zaidi kuliko wanaoitikia.

    Kama wewe ni Mungu na una jukumu kubwa ambalo unataka kukamilisha – jukumu la kuokoa ulimwengu wote je ungewaita watu wachache na kuwatuma? La hasha! Ungewaita watu wengi kadiri iwezekanavyo na kuwatuma nje, Kwa bahati mbaya, watu wachache ndio wanaoitikia wito, hivyo wachache ndio wanaochaguliwa kutumika katika shamba.

    Je Mwito ni Jambo Kubwa kiasi hicho?

    Tumefanya mwito wa Mungu uwe jambo la kutisha au fumbo sana linalohitaji kusikia sauti nyingi, kuona maono, na kupitia uzoefu wa kiroho wa kutisha. Hicho ni mitazamo ya isiyo kawaida. Waitwao ni wengi, lakini wengi hawajaona maono ya Yesu. Biblia inatufundisha kwamba tumeitwa kuwa watakatifu.

    Kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, WALIOITWA KUWA WATAKATIFU…

    Warumi 1:7

    kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, WALIOITWA WAWE WATAKATIFU…

    1 Wakorinto 1:2

    Watakatifu ndio wanaopaswa kufanya kazi kwa mujibu wa Waefeso 4:12. Sasa tuwe wakweli. Katika wito wetu wa kuwa watakatifu, ni wangapi tuliskia sauti za ajabu? Ni wangapi kati yetu tuliosikia radi na kimulimuli cha radi vikitutisha ili tuokoke? Ni wangapi kati yetu tulianguka chini tukiwa tunaelekea Dameski? Ni Wakristo wachache sana ambao wamepata wito wa Mungu kwa namna hiyo.

    Hiyo, haimanishi kwamba hatujaitwa kuwa Wakristo.

    Wakristo wote waliozaliwa mara ya pili wana wito wa ajabu wa kuwa watakatifu katika maisha yao. Inaweza isiwe kwa namna ya kutisha, lakini ni ya ajabu. Kama wewe unajiita Mkristo, hapo umepokea wito ambao umeuitikia. Nakujulisha kwamba bila kujua, kiukweli umeskia wito na umeitikia wito wa kimungu.

    Huo ulikuwa wito gani? Wito huo ulikuwa kwa njia rahisi usadiki ambao ulikujia kuhusu uhalisia wa Yesu Kristo. Usadiki huo huo ulikuongoza umpe Yesu maisha yako, na kukufanya uwe Mkristo aliyezaliwa -mara ya pili.

    Wakati mwingine watu kutafuta mambo ya ajabu wanakosa mgusu waajabu halisi wa Mungu. Katika njia ile ile tulioitwa kuwa Wakristo, ndio Mungu atatuita wengi wetu katika huduma yake katika hatua moja au nyingine. Unaweza usiitwe kwa hatua ya kushitukizwa katika huduma kama Eliya, lakini bado ni wito!

    Tazama huduma ya nabii Samweli. Samweli alikua hekaluni alipopata mwito wa Mungu.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1