Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Namna ya Kuomba
Namna ya Kuomba
Namna ya Kuomba
Ebook121 pages3 hours

Namna ya Kuomba

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Je niombe kwa namna gani? Niombe kuhusu nini? Kwa nini maombi ni fumbo kiasi hicho? Ninawezaje kuomba kwa muda mrefu? Je, Mungu hajui ninachohitaji tayari? Nini kitatokea nisipoomba? Maombi yangu yatajibika kwa kweli?" Gundua majibu kwa maswali haya unapopitia kitabu hiki elekezi na cha muda sahihi uhakika kilichoandikwa na Dag Heward-Mills.

LanguageKiswahili
Release dateAug 8, 2018
ISBN9781613958483
Namna ya Kuomba
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Namna ya Kuomba

Related ebooks

Reviews for Namna ya Kuomba

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Namna ya Kuomba - Dag Heward-Mills

    YALIYOMO

    Sura ya 1: Kama Umetingwa Sana Kuomba, Basi Umetingwa Sana

    Sura ya 2: Kwa Nini Maombi ni Siri

    Sura ya 3: Nini Kinatokea Usipoomba

    Sura ya 4: Jinsi ya Kuongea na Mtu Mkuu

    Sura ya 5: Namna Utakavyoweza Kusaidiwa Kwa Kuomba Kwa Lugha

    Sura ya 6: Mada Kuu Tatu za Maombi

    Sura ya 7: Namna ya Kuomba Kwa Aina Zote Za Maombi

    Sura ya 8: Je Mungu Huyajibu Maombi Yetu Yote?

    Sura ya 9: Hatua Kumi na Mbili za Maombi Yanayojibika kwa Asilimia Mia Moja

    Maandiko yote yamechukuliwa kutoka katika Biblia ya Union Version inayotolewa na vyama vya Biblia vya Tanzania na Kenya

    © Hakimiliki 2013 Dag Heward-Mills

    Jina la Awali: How to Pray

    Toleo asilia lilichapwa mwaka 2014 na Parchment House

    Kimetafsiriwa na Bw. Felix Kwame Sosoo

    Kanisa la Kimataifa la Lighthouse

    Tanzania

    Kwa habari zaidi kuhusu Dag Heward-Mills:

    Kampeni ya Yesu Mponyaji

    Andika kwa:  evangelist@daghewardmills.org

    Tovuti:  www.daghewardmills.org

    Facebook: Dag Heward-Mills

    Twitter: @EvangelistDag

    ISBN: 978–1–61395–738-7

    Haki zote zimehifadhiwa na sheria ya kimataifa ya hakinakili. Idhini ya maandishi lazima itolewe na mchapaji ili kutumia au kuzalisha sehemu yoyote ya kitabu hiki, isipokuwa nukuu fupi katika mapitio ya kiuhakiki

    Sura ya 1

    Kama Umetingwa Sana Kuomba, Basi Umetingwa Sana

    Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

    Danieli 6:10

    tu yeyeote ambaye ametingwa sana kuomba ametingwa sana. Haijalishi wewe ni nani, huwezi  kuwa na mambo mengi ya kukuzuia kuomba. Utagundua kutoka kwenye mstari hapo juu kuwa  Danieli aliomba mara tatu kwa siku. Mstari muhimu katika andiko hili ni, Kama alivyokuwa akifanya tokea hapo. Hii inamaanisha kuwa Danieli alikuwa anaomba maombi haya mara kwa mara. Danieli hakuwa anasali tu kwa sababu alikuwa kwenye shida; alikuwa na tabia ya kuomba.

    Mara nyingi watu wanapofanikiwa wanaacha kwenda kwenye ibada za maombi na hatimaye wanarudi nyuma. Sio hivyo kwa Danieli. Alikuwa Waziri Mkuu wa nchi yake, mtu wa pili pekee katika uongozi kwa mfalme. Alikuwa mtu mwenye mafanikio ambaye aliinuka kutoka utumwani kwenda ofisi ya juu ya Waziri Mkuu. Alikuwa mmoja wapo wa watu walioheshimika sana na watu waliogopwa katika taifa. Alikuwa ni mwanasiasa mkuu wa enzi ile. Alikuwa mtumishi wa umma. Lakini aliomba mara tatu kwa siku, kila siku.

    Ni kanuni zipi zilizomwongoza Danieli kuwa na muda wa kuomba usio wa kawaida na usiobadilika? Hizi hapa, zisome na zifanye ziwe kanuni zako. Wewe pia waweza kuwa na mafanikio ambayo Danieli alikuwa nayo. Ningependa usome, jifunze na chambua kanuni zifuatazo ambazo naamini zilimwongoza Danieli katika maisha yake.

    Kanuni namba 1: Maombi ni Muhimu Sana

    Mtu mmoja aliwahi kusema kwamba ni muhimu zaidi kujua namna ya kuomba kuliko kuwa na shahada kutoka chuo kikuu. Kuna mambo mengi ambayo ni muhimu katika maisha haya. Elimu bora ni muhimu. Hela ni muhimu. Ndoa nzuri ni muhimu. Ila, maisha mazuri ya maombi ni muhimu zaidi!

    Acha hii iingie rohoni mwako- kwa mapato yako yote, pata maombi! Katika shughuli zako zote, tengeneza nafasi kwa maombi!

    Kanuni namba 2: Hakuna Yeyote Aliye na Mambo Mengi sana, Amebarikiwa sana au Amefanikiwa sana Ashindwe Kuomba

    Unaweza kuwa na maisha yenya shughuli nyingi na unaweza kuwa mtu muhimu sana. Hata hivyo, sidhani kuwa umetingwa zaidi ya Danieli alivyokuwa. Danieli alikuwa Waziri Mkuu, kiongozi katika taifa. Watu wengi wanafikiria kuwa Wakuu wa Nchi na Mawaziri wa serikali wana maisha ya huru na ya kufurahia, wakisafiri angani ulimwenguni kote. Hiyo sio kweli!  Mimi mwenyewe ni kiongozi wa shirika kubwa, na ninafahamu kuwa watu wenye nafasi za juu hawana maisha rahisi. Kadiri unavyopanda juu, ndivyo unakuwa na majukumu makubwa.

    Kuna kazi nyingi ya ziada zinazohitajika kuendeleza maisha pamoja na huduma. Je ulikuwa unafahamu kuwa watendaji waliofanikiwa kama Danieli wana msongo wa mawazo kiasi kwamba kutakuwa na uwezekano wa kupata magonjwa kama vidonda vya tumbo na shinikizo la damu. Hali hizi ni kawaida sana kwa watu waliotingwa kwa sababu ya kazi ngumu wanazofanya.

    Danieli alikuwa mmoja wa watu kama hawa. Alikuwa Waziri Mkuu, ila alijihisi kwamba hakutingwa sana kuomba mara tatu kwa siku. Kama unafikiria umetingwa sana kuomba, basi unajidanganya mwenyewe. Kama huombi ni kwa sababu hutaki kuomba. Ni kwa sababu hufikiri kwamba maombi ni muhimu sana! Danieli alikuwa amefanikiwa, ila aliomba. Kwa nini aliweza kuomba mara tatu kwa siku?

    Watu wamekua kutoka kwenye ufukara kwenda kwenye mafanikio. Walivyokuwa maskini, walikuwa na muda mwingi kuhudhuria ibada za maombi. Lakini walivyobarikiwa walihisi kila kitu kipo sawa. Hapana! Kila kitu hakipo sawa! Mafanikio yako si ishara ya kuacha kuomba.

    Kanuni namba 3: Maombi ni Chanzo cha Nguvu  Zetu na Ulinzi

    Lazima utambue kwamba ni maombi ambayo huachilia nguvu za Mungu kwa niaba yetu. Yesu alijua nguvu ya maombi. Ndio maana Yesu alitumia masaa katika maombi. Labda wewe ni mfanyabiashara aliyefanikiwa, na unadhani kwamba huhitaji mambo haya ya kiroho. Labda wewe ni mwanasiasa na unadhani ulinzi wako lazima utoke kwa uganga au nguvu za giza.

    Ngoja nikuambie sasa hivi, kuna nguvu kwenye maombi. Hatuhitaji nguvu yoyote tunapokuwa na nguvu ya maombi. Kuna ulinzi wetu tunapoomba. Sehemu ya mwisho ya silaha za Mungu ni maombi (Waefeso 6:18). Kwa maneno mengine maombi ni sehemu ya muhimu katika ulinzi wa kiroho.

    Watu wengi wanaogopa pale wanapofanikiwa. Ayubu alijawa na hofu alipofanikiwa. Hatimaye alisema, Nilichokihofia zaidi ndicho kilichonitokea. Watu kama hawa huhisi kwamba mtu anaweza  kutumia nguvu za ajabu kujaribu kuwauwa. Huna chochote cha kuogopa ukiwa mtu wa maombi kama Danieli. Watu wengi walitaka kumuuwa Danieli. Watu hawa hawakufikiria kumuuwa tu Danieli, kwakweli walijaribu kumuondoa. Kupitia nguvu ya maombi, Danieli alilindwa kutoka kwa simba.

    Naona simba wote maishani mwako wakitawanyika kwa hofu! Ninaona nguvu yako ya maombi ikipanda. Ninakuona ukisonga mbele kwa sababu ya maisha mapya ya maombi yaliyopatikana!

    …Na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;

    Luka 3:21

    Ninaona mbingu zikifunguka juu ya maisha yako. Usisahau hiki! Mbingu zilifunguka Yesu alipoomba. Baraka zote za kimwili na za kiroho zinyeshe juu yako utakapokuwa mtu wa maombi.

    Kanuni namba 4: Maombi ni Muhimu kwa Kupata na Kudumuisha katika Baraka za Mungu.

    Je una jambo lolote ambalo unajivunia?Je umepata jambo lolote katika maisha haya? Ngoja nikuambie kwamba ni kwa neema ya Mungu. Kwa nguvu ya maombi, utapata mambo ya juu hata zaidi. Ni kwa maombi ndo utahimili kile ambacho Mungu amekiweka mikononi mwako.

    Kuna watu ambao wamepokea maelfu ya dola kama zawadi. Leo hizo hela zimepotea hewani. Mungu anaweza kukupa kitu lakini inahitaji neema yake kuzihimili Baraka hizo. Je, wewe ni mchungaji wa huduma kubwa? Nikwambie, inahitaji maombi kukuhimili wewe katika huduma. Unafikiri kwa nini Yesu alikuwa anakimbilia kwenda kuomba?

    Kuna sheria ya kuzorota inayofanya kazi duniani. Kila kitu kinaoza. Biashara yako inaoza. Kanisa lako linaoza. Maisha yako yanaoza. Inachukua nguvu ya Mungu, kupitia maombi, kuhifadhi kila kitu Mungu amekupatia.

    Kanuni namba 5: Ili Maombi yawe na Nguvu Lazima Yawe ya Kitabia

    Mtu aitwaye Dastoyevsky alisema, Nusu ya pili ya maisha ya mtu inahusishwa na tabia alizozijifunza katika nusu ya maisha yake ya kwanza.

    Pascal alisema, Nguvu ya wema wa mtu unatokana na tabia zake za matendo.

    Kama utakuwa mtu mkubwa katika maisha haya, unahitaji tabia nzuri. Matendo yanakuwa tabia yakirudiwa mara nyingi; wakati mwingine bila kujua. Inakuwa desturi lako!

    Mazoea au tabia inaweza kuwa nzuri au mbaya. Kumbuka kwamba tabia nzuri zinarudiwa kama  tabia mbaya. Tabia nzuri itasababisha upenyo ridadi hata bila wewe

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1