Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Vile Unavyopaswa Kuwa: kujitambua na kuchukua hatua: Kujitambua, #1
Vile Unavyopaswa Kuwa: kujitambua na kuchukua hatua: Kujitambua, #1
Vile Unavyopaswa Kuwa: kujitambua na kuchukua hatua: Kujitambua, #1
Ebook184 pages5 hours

Vile Unavyopaswa Kuwa: kujitambua na kuchukua hatua: Kujitambua, #1

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Vile unavyopaswa kuwa ni kitabu kuhusu mabadiliko chanya katika maisha. Kitabu kinakumbusha kwamba haturithi tabia zote. Kila mmoja ana silika zaidi ya moja na zaidi ya hayo, kila mmoja ana saa 24 tu katika siku. Kwa kutumia tafiti mbalimbali, nukuu za wenye hekima na za Biblia na mifano halisi, kitabu kinaonesha jinsi kila mtu anavyoweza kujitambua na kuchukua hatua. Kwa kuzingatia mashauri katika kitabu hiki, utaweza kutimiza njozi zako ungali na nguvu na kumaliza siku za maisha yako kwa amani. Kitabu hiki  kitaongeza hamasa na matumaini ya jinsi unavyoweza kuanza au kuboresha hatua yoyote ya maisha yako. Unaweza kuishi maisha ya mafanikio katika viwango vya kidunia na vya Mbinguni pia.

LanguageKiswahili
Release dateApr 6, 2023
ISBN9789987452958
Vile Unavyopaswa Kuwa: kujitambua na kuchukua hatua: Kujitambua, #1

Related to Vile Unavyopaswa Kuwa

Titles in the series (1)

View More

Related ebooks

Reviews for Vile Unavyopaswa Kuwa

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Vile Unavyopaswa Kuwa - Pr. Deogratius Samba

    Vile Unavyopaswa Kuwa

    Kujitambua na kuchukua hatua

    Pr. Deogratius Samba

    GDY PUBLICATIONS COMPANY LIMITED

    S.L.P. 32172

    Simu: +255 717326061 au +255 752882235

    www.gdypublications.com

    Dar es Salaam

    TANZANIA

    ––––––––

    © Pr. Deogratius Samba

    Toleo la kwanza 2023

    ISBN 978-9987-452-95-8

    ––––––––

    Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri, kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila idhini ya GDY Publications Company Limited. 

    ––––––––

    Mwandishi: Pr. Deogratius Samba

    Mhariri: GDY Publications Company Ltd.

    Mpanga kurasa: GDY Publications Company Ltd.

    Aliye sanifu jalada: GDY Publications Company Ltd.

    ––––––––

    Yaliyomo

    Shukrani..........................................vi

    Utangulizi..........................................1

    Kujitambua.........................................4

    Wewe ni nani...................................4

    Kwa nini unaishi ................................8

    Unataka nini maishani .........................11

    Tambua na tumia talanta yako.................12

    Namna na kuitambua talanta yako.................15

    Tambua silika ya tabia yako.....................16

    Melankoli ......................................18

    Flegmatiki.......................................24

    Koleriki........................................27

    Sanguini........................................31

    Majumuisho kuhusu silika za tabia ............41

    Mambo ya kuzingatia baada kujua silika ya tabia yako...........44

    Tambua yakupasayo kufanya katika umri wako..46

    Tambua fursa ulizonazo na mahitaji yako........47

    Kujiendeleza, kujiwezesha na kujiongezea thamani......50

    Maendeleo binafsi...............................51

    Umuhimu wa maendeleo binafsi ................52

    Kutambua maeneo ya maendeleo binafsi........54

    Hatua za vitendo kwa maendeleo binafsi........57

    Kusimamia maendeleo yako.....................62

    Weka vipaumbele maishani.....................64

    Yatambue mambo ya msingi kwako na uyape kipaumbele........65

    Uwezeshaji binafsi...............................67

    Kukuza mahusiano kijamii.........................71

    Kujiendeleza kitaaluma .........................83

    Maana ya taaluma ...............................84

    Maendeleo ya kitaaluma na kujiendeleza............86

    Kutunza kumbukumbu za maendeleo yako..........89

    Kujiwezesha kifkra: namna ya kupata mawazo

    mapya.........................................90

    Kama wakili wa muda: kuwekeza katika muda..96

    Kutengeneza chapa (jina).......................98

    Kujiendeleza kikazi: teknolojia na uchaguzi wa

    fani...........................................100

    Hatua 10 muhimu katika ukuaji na maendeleo ya kikazi101

    Kujiandaa kwa ajili ya misimu ya maisha......109

    Misimu ya maradhi; kuugua au kuuguza na

    kufiwa..........................................110

    Msimu wa kuanza maisha ya familia ...............111

    Msimu wa kustaafu na uzee......................112

    Kanuni muhimu za kujiongezea thamani.........121

    Falsafa ya teolojia ya mafanikio.......................124

    Falsafa na mitazamo ya maisha na mafanikio...124

    Teolojia ya mafanikio...........................126

    Mafanikio katika mtazamo wetu wa kibinadamu 134

    Mafanikio na baraka tukimtumainia Mungu....135

    Tujifunze kutoka kwa Ibrahimu....................136

    Usimamizi na tathmini ya mipango.....................141

    Mpango wa maendeleo binafsi..................141

    Kuendeleza njozi binafsi.......................144

    Kuboresha na kupanua maono yako binafsi ....149

    Uchambuzi binafsi wa kupima uwezo na uhitaji 153

    Kupitia, kuboresha na kurekebisha mipango...158

    Tathmini na usimamizi wa malengo............168

    Maswali muhimu kujiuliza kila siku.............172

    Mambo 10 ya kujiuliza kabla ya kusema umeshindwa............172

    Rejea...........................................177

    ––––––––

    Shukrani

    Kwanza kabisa natanguliza shukrani za dhati kwa Mungu. Amekuwa mwema na mwaminifu kwangu. Amenipatia afya, uzima, akili na uwezo wa kuandika kitabu hiki na kunilinda katika wakati wote wa kukitayarisha.

    Shukrani za dhati ni kwa rafiki yangu Anna Paul. Anna amenitia moyo na kunishauri kwa hali zote, hasa wakati wa kukiandaa kitabu hiki. Amekuwa mhamasishaji wangu mkubwa.

    Ninawashukuru wazazi wangu, baba na mama, wamekuwa na mchango mkubwa kwangu kwa malezi wakinijenga vyema na kunihudumia katika mahitaji yote mpaka kufikia hapa nilipo.

    Shukrani pia ni kwa ndugu na rafiki zangu wote ambao kwa namna moja ama nyingine tumeshirikiana na kusaidiana katika mengi na kwa muda mrefu zaidi na kwa upendo mkubwa.

    Zaidi ninawashukuru wengine wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha uandishi wa kitabu hiki. Asanteni kwa mawazo yenu na michango yenu kukiboresha.

    Shukrani kwa wahariri waliohariri rasimu za awali na hatimae ya mwisho ya kitabu hiki na kukiboresha kuwa kilivyo sasa. Bila kujali mpangilio wa majina yao, shukrani za pekee zinamstahili Mch. Misper Sombera, Mch. Jackson Shayo na wahariri wa GDY Publications Company Ltd.

    Utangulizi

    Maneno ya mwanafalsafa nguli wa Kirumi, Seneca katika kitabu chake kidogo On the Shortness of Life yamekuwa na mchango mkubwa wa kuifungua akili na macho yangu kuyatazama maisha upya. Anasema;

    Sio kwamba tuna muda mfupi wa kuishi, lakini ni kwamba tunaupoteza mwingi. Maisha ni ya kutosheleza, na tumekirimiwa kiasi cha kutosha, tulichopewa ili tuwe na mafanikio makubwa ikiwa maisha yote yangewekezwa vizuri. Lakini yanapopotea kwa mambo yasiyo ya maana bila kujali na pale ambapo hayatumiwi kwa shughuli yoyote nzuri, tunalazimishwa mwishowe na kizuizi cha mwisho cha kifo kutambua kwamba yamepita bila kujua yalikuwa yanapita. Ndivyo ilivyo: hatupewi maisha mafupi lakini tunayafanya mafupi, na sio kwamba hatupatiwi yote tunayohitaji kwa ajili ya maisha ila ni kuwa tunayatumia tu vibaya ... Maisha ni marefu ikiwa unajua kuyatumia. (kama ilivyonukuliwa katika Costa, (1997))

    Vile unavopaswa kuwa ni kitabu chenye nyenzo za uwezeshaji kwa maendeleo binafsi kitakachokuwezesha kukuza wasifu na utu wako. Katika kitabu hiki nimetumia uzoefu wa taaluma zangu mbili; taaluma ya utawala na maendeleo na taaluma ya teolojia, ili kuleta uwiano wa kimtazamo katika tasnia hii ya maendeleo binafsi na falsafa ya maendeleo katika mtazamo halisi wa vile tunavyopaswa kuwa.

    Kitabu hiki ni zao la uzoefu niliopitia katika kipindi cha kuishi kwangu. Nimejumuisha uzoefu na changamoto za maisha ya ujana nilioupitia, ambazo kiuhalisia ndizo changamoto za vijana wengi wapambanaji. Pia ni utafiti wa mawazo tofauti toka kwenye machapisho mbalimbali kutoka katika vyanzo mbalimbali na vitabu zaidi ya 50 tofauti nilivyovisoma toka mwaka 2012 – 2020 vinavyohusiana na maendeleo binafsi na suala zima la kuboresha utu. Zaidi ya hayo, ni usomaji wa makala mbalimbali za wanafalsafa wa maisha ikijumuisha pia vyanzo vya mitandao toka katika tovuti kadhaa za kimaendeleo ambazo huwa najifunza kwazo. Baadhi ya vyanzo hivi nimeviorodhesha kwenye sehemu ya rejea ili kuwasaidia watakaopenda kujifunza zaidi angalau wapate pa kuanzia.

    Kuna sehemu kubwa ya uzoefu nilioupata toka kwa watu walionizunguka na mazingira niliyoishi katika vipindi fulani vya maisha, hii ikijumuisha ndugu, marafiki, wanafunzi wenzangu niliosoma nao mahali mahali na baadhi ya wale ambao kwa namna moja ama nyingine tulikutanishwa na matukio fulani. Lakini pia fursa nilizopata kufanya kazi na taasisi kadhaa zilizonikutanisha na watu tofauti wenye uwezo tofauti na mitazamo tofauti ambao kwa namna moja ama nyingine mawazo na maoni yao yalinipelekea si tu kujua haya mambo bali pia kuhamasika kuandaa kitabu hiki ili niweze kushirikisha wengi wengine.

    Kitabu hiki ni nyenzo ya kumuwezesha mtu yeyote kuwa vile anavyopaswa kuwa maishani na kuzikabili ndoto bila hofu. Kinawezesha kuona fursa kwenye kila changamoto, kuona daraja na sio ukuta. Ni kitabu kitakachomfanya msomaji kuona maana ya maisha na kuyaishi maisha ya kutimiza kusudi la uwepo wake; kuyaishi maisha ambayo hayatakuwa na majuto katika miisho yake.

    Katika jalada la kitabu hiki iko picha ya kipepeo katika hatua zake za ukuaji. Wengi wetu tunamfahamu kipepeo kama mdudu wa kuvutia kutokana na rangi zake, wengi tunapenda kumuona hata akiwa katika bustani zetu nyumbani. Lakini huyo kipepeo mpaka aonekane katika uzuri wake, umbo na rangi za kuvutia anapitia hatua kadhaa za mabadiliko kuwa vile anavyopaswa, kutoka kuwa yai hadi kuwa buu na kutoka kuwa buu mpaka kuwa kipepeo. Kwakweli kama kipepeo angebaki kuwa buu hawezi kuwavutia watu na mazingira na atakuwa moja kati ya wadudu wa kutisha na kuogopesha sana kwa maumbo yao, lakini baada ya mabadiliko hayo makubwa ndipo tunamuona katika umbo na rangi za kuvutia.

    Na sisi kama binadamu tuna kitu alichoweka Mungu ndani yetu cha kuivutia dunia na kuipendezesha na ndilo kusudi la kuwepo kwetu katika dunia hii lakini inahitaji badiliko kuwa vile tunavyopaswa kuwa. Jambo lingine tunaloweza kujifunza kwa kipepeo nje ya rangi zao za kuvutia, ni maeneo wanapopatikana, hasa kwenye bustani za maua mazuri, yenye rangi nzuri na harufu nzuri. Hivyo suala la mazingira yanayotuzunguka yanaathiri mvuto kwa wengine. Karibu tujifunze vile unavyopaswa kuwa.

    Mawazo ya mtu yanaunda vazi la ndani la tabia, na vazi la nje la mazingira. Tazama mawazo yako, yatakuwa maneno yako. Tazama maneno yako, yatakuwa matendo yako. Tazama matendo yako, yatakuwa tabia yako. Tazama tabia yako, itakuwa mwenendo wako. Tazama mwenendo wako, utakuwa hatima yako. Allen, James (2017).

    Wewe ni nani

    Unapotaka kujifahamu, ni lazima uanze kwa kujiuliza kuwa wewe ni nani. Suala la kwamba wewe ni nani halibebwi na historia yako, aina ya familia unayotoka, ndugu au marafiki ulionao. Ni zaidi ya kufahamu jina lako na jinsia yako. Sio tu habari ya wapi umetoka ila ni kujiuliza kwanini nimetokea huko, sio wapi ulipo bali kwanini upo hapo na sio wapi unataka kwenda bali unakwenda kufanya nini na kwanini. Ni mchakato unaohusisha maswali kwa kila hatua, na kabla hujaenda hatua nyingine unapaswa kujibu maswali yote ya hatua ya awali.

    Haufanani na mtu yeyote katika ulimwengu huu. Hii inatosha kukuambia kuwa una kusudi kuwapo katika ulimwengu huu; kusudi ambalo hakuna mtu mwingine anayeweza kulibeba zaidi yako. Hivyo ni vizuri kujiuliza hili swali mpaka utakapojua kusudi la uwepo wako katika dunia hii, na kwa kujibu swali hili utajipatia amani ya kweli ndani ya moyo wako kwa kuishi vile ulivyopaswa kuishi.

    Nimetangulia kusema kuwa suala la wewe ni nani halijibiwi tu kwa aina ya familia unayotoka kwakuwa unaweza kuzaliwa katika familia ya kawaida, lakini wewe ukawa si wa kawaida na hii ni kwasababu kwa Mungu kila mmoja wetu ni wa pekee, na ana upekee wake tofauti na ndugu zake na hata wazazi wake. Hata katika vitabu vya dini kuna watu waliozaliwa katika familia za kawaida lakini wao hawakuwa watu wa kawaida.

    Katika vitabu vya dini tunafahamu watu hawa: Yusufu, Sauli na Daudi. Hawa ni baadhi tu ya watu waliozaliwa katika familia za kawaida lakini hawakuwa watu wa kawaida. Sitawaongelea wote kwakuwa visa vyao vinafahamika, ila nitamwongelea Sauli aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Israel, ambaye alizaliwa katika familia ya kawaida lakini yeye hakuwa wa kawaida na hakujua kuwa yeye hakuwa wa kawaida maana alijitazama katika mtazamo wa kibinadamu na si kama Mungu alivyomtazama.

    Katika Biblia 1 Samweli 9, kuna kisa ambacho tunaweza kujifunza kitu ndani yake kwa muktadha wa mada tunayoizungumzia katika sehemu hii; Kisa cha Mfalme wa kwanza wa taifa la Israel - Sauli tokea kuitwa kwake mpaka kuwa mfalme. Hapa tunaipata Historia yake, lakini kuna mambo nataka tuyaangalie kuhusu Sauli.

    a)  Sauli aliishi na baba yake mzee Kishi, aliyekuwa mtu wa kabila la Benyamini,

    b)  kabila la Benyamini lilikuwa dogo na lililokuwa na watu wachache katika Israel lakini pia lilikuwa kabila lisilokuwa na nguvu sana.

    c)  Si tu kwamba Kabila la Benyamini lilikuwa dogo bali pia jamaa ya Sauli ilikuwa ndogo zaidi katika kabla la Benyamini. 1 Samweli 9:21

    Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila ya Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?

    Sura hii inavyoanza, anatajwa Mzee Kishi baba yake Sauli kama mtu shujaa na mwenye nguvu, lakini anatokea katika kabila lililo dogo miongoni mwa makabila ya Israel, Mungu anaona huko shujaa na mwenye nguvu. Huenda hata mzee Kishi mwenyewe hakuwahi kutambua kuwa yeye ni shujaa. Kutokana na asili ya kabila lake, hakujihesabu kuwa miongoni mwa watu mashuhuri katika Israel. Lakini Mungu anapokutambua haijalishi wanadamu wanakuonaje lazima utakuwa juu.

    Kisa hiki hakiishii kwa mzee Kishi bali kisa hiki kinamuongelea mwanae Sauli, huo ulikuwa utangulizi tu. Katika mianzo ya kisa hiki, Sauli anatajwa kama kijana mzuri na katika Israel hapakuwa na mwingine kama yeye kwa wakati wake, hii inamaanisha hata katika makabila yale makubwa ya Israel hapakuwa na kijana kama Sauli machoni pa Mungu kwa wakati wake. Lakini ikumbukwe anatoka katika kabila lisilo na nguvu na dogo katika Israel. Ukisoma sura yote hiyo utaona huyu Sauli kwa namna ya pekee anaitwa na Mungu kuwa mfalme wa kwanza wa Israel.

    Safari ya Sauli ya wito wa kuwa Mfalme inaanza kwa kwenda kutafuta punda wa babaye waliopotea. Akiwa ameagizwa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1