Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu
Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu
Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu
Ebook93 pages2 hours

Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kitabu hiki ni mwongozo mkuu kwa kuelewa wokovu kupitia Yesu Kristo. Katika kitabu hiki cha kipekee, utaelewa ni kwa jinsi gani Yesu anavyokupenda, namna unavyoweza kuokoka, namna unavyoweza kuepuka kwenda kuzimu na nini maana ya kuwa kiumbe kipya katika Yesu Kristo. Mpe mtu yeyote kitabu hiki na wataelewa nini maana ya kuokolewa kupitia damu ya Yesu Kristo.

LanguageKiswahili
Release dateApr 8, 2018
ISBN9781641345439
Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu
Author

Dag Heward-Mills

Bishop Dag Heward-Mills is a medical doctor by profession and the founder of the United Denominations Originating from the Lighthouse Group of Churches (UD-OLGC). The UD-OLGC comprises over three thousand churches pastored by seasoned ministers, groomed and trained in-house. Bishop Dag Heward-Mills oversees this charismatic group of denominations, which operates in over 90 different countries in Africa, Asia, Europe, the Caribbean, Australia, and North and South America. With a ministry spanning over thirty years, Dag Heward-Mills has authored several books with bestsellers including ‘The Art of Leadership’, ‘Loyalty and Disloyalty’, and ‘The Mega Church’. He is considered to be the largest publishing author in Africa, having had his books translated into over 52 languages with more than 40 million copies in print.

Related to Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu

Related ebooks

Reviews for Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Jinsi Ya Kuzaliwa Mara Ya Pili na Kukwepa Kuzimu - Dag Heward-Mills

    Sura ya 1

    Mungu Anakupenda kwa Upendo Mwingi (Mkuu)

    Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na UPENDO MWINGI KULIKO HUU, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo

    Yohana 15:12-14

    Upendo mkuu wa Mungu utabadilisha maisha yako milele. Upendo huu ni mkuu kuliko chochote kinachopatikana duniani. Mwanaume akimwambia mwanamke, nakupenda, haiwezi kulinganishwa na upendo mwingi ninaouzungumzia katika kitabu hiki. Mama yako anaweza kukupenda, Baba yako anaweza kukupenda lakini hakuna yeyote atakayekufa kwa ajili yako. Mpenzi wako wa kiume anaweza kukupenda na mpenzi wako wa kike anaweza kukupenda, lakini hakuna atakayekufa kwa ajili yako.

    Kitabu hiki kinahusu upendo mwingi wa Mungu. Ukifungua moyo wako kupokea upendo huu mkuu, utazaliwa mara ya pili. Ukifungua moyo wako kwa upendo huu mkuu kutoka kwa Mungu, utakuwa kiumbe kipya na kuishi maisha tofauti kabisa. Ukifungua moyo wako kwa upendo huu mkuu kutoka kwa Mungu, utaepuka adhabu yako ya Kuzimu. Unastahili kwenda Kuzimu naMimi pia. Lakini kupitia upendo wa Mungu aliyemtuma mwanawe pekee ili tusipotee, tunaweza kuzaliwa mara ya pili! Haleluya! Tunaweza kuwa viumbe vipya! Tunaweza kuepuka giza la nje na mateso ya Kuzimu. Huu ni upendo wa namna gani kwamba tunaweza kuitwa wana wa Mungu? Tumeonyeshwa wokovu wa namna gani kana kwamba Yesu alitoa damu yake kutuokoa kutoka katika dhambi zetu!

    Nataka ufungue moyo wako na kufurahia wokovu mkuu ambao Kristo anakupa. Nahuzunika kusema kuwa Wakristo wengi hawaelewi wokovu. Hii ndio sababu ya ninaandika kitabu hiki. Ni nadra sana kwa wokovu kuhubiriwa siku hizi. Huu ndio muda kwetu sisi kurudisha misingi imara ambayo Ukriso utasimama milele.

    Vitu Saba Unavyopasua Kuvijua Kuhusia na Upendo Mwingi

    1. Kuna aina mbalimbali za upendo, lakini upendo wa Yesu ndio mkuu zaidi

    Mungu ana upendo wa kipekee ambao ni upendo mkuu zaidi unaopatikana. Hebu angalia maandiko haya yanayouelezea upendo wa Mungu. Huu ni upendo wa namna gani? Upendo wa Mungu ndio upendo mkuu, upendo wa milele na upendo mwingi.

    Tazameni, ni PENDO LA NAMNA GANI alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye

    1Yohana 3:1

    Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, KWA MAPENZI YAKE MAKUU aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

    Waefeso 2:4-5

    Nasi tumelifahamu PENDO ALILO NALO MUNGU KWETU SISI, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.

    1Yohana 4:16-17

    BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam nimekupenda kwa UPENDO WA MILELE, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.

    Yeremia 31:3

    Mchumba na Upendo Mkuu

    Niliwahi kumfahamu dada mmoja aliyekuwa na mchumba (mpenzi). Huyu kijana (mpenzi wake) alitaka kumuoa lakini hakumtendea vizuri. Inaonekana pamoja na mchumba wake, pia alikuwa na wasichana wengine. Uhusiano wao ulikuwa na ghasia, kwa kusema tu machache. Siku moja, huyu binti hatimaye alikuja nyumbani na kusema imekwisha. Dada alilia sana kwa sababu moyo wake umevunjika kwa kuvunjika kwa uhusiano. Lakini nilimfarijii na nilimwambia kwamba Mungu atampa mtu mwingine na hata mchumba mzuri zaidi.

    Baada ya miezi michache, mungu alijibu maombi yetu na ghafla kulikuwa na kijana mmoja aliyetokea na kumpenda sana. Walionekana wanafurahia uhusiano wao na siku moja nikamuliza binti, Vipi kuhusiana na uhusiano wako mpya

    Alitabasamu na kusema, ni bora zaidi kuliko uhusiano wa kwanza. Mungu amekuwa mwema kwangu.

    Kwa maneno mengine, alikuwa anapata upendo mwingi na uhusiano ulio bora zaidi. Kwa hiyo nilimwuliza, kwa nini uhusiano huu ni bora?

    Alisema hata sikujua kama ningekuwa na furaha namna hiyo. Sikujua kwamba kulikuwa na upendo mkuu zaidi ambao ningeweza kuupitia

    Kwa kweli, binti huyu alipitia aina ya upendo mwingi. Huu ndio namna upendo wa Mungu ulivyo. Ni aina ya upendo mkuu zaidi. Huu ni upendo wa namna gani?

    2. Upendo wa Yesu ni mkuu kuliko upendo wa ndugu

    Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia UPENDANO WA NDUGU USIO NA UNAFIKI, basi jitahidini kupendana kwa moyo.

    1 Petro 1:22

    Familia nyingi zimechanguka ingawa zinahusiana. Zinavunjika na watu wanagombana mara kwa mara. Lazima upendo wa Yesu uwe mkuu kuliko upendo baina ya ndugu.

    Utoaji Msaada wa Figo

    Siku moja, kulikuwa na mkutano wa maombi ambapo kaka mmoja aliyekuwa anahitaji figo aliombewa. Walitangaza upendo wao kwa kaka huyu na walitaka aweze kuendelea kuishi kupitia utoaji msaada wa figo.

    Lakini kadiri mkutano wa maombi ulivyoendelea, waligundua kwamba hakuna aliyekuwa tayari kutoa figo yake ingawa haya ndio maombi yao. Hatimaye, kiongozi wa maombi aliamua kumruhusu Mungu kuamua itolewe figo ya nani. Kwa hiyo alichukua unyoya na akasema atarusha unyoya hewani na yeyote ambaye utaangukia anatakiwa atoe msaada figo yake. Kila mtu alikubaliana na utaratibu huo wa uchaguo wa kiunabii.

    Kisha alirusha unyoya hewani. Unyoya ukaenda juu na taratibu ukaanza kushuka, kwa mshangao, ulielekea kwa kiongozi mwenyewe. Gafla, kiongozi alianza kupiga kelele na kuupuliza unyoya ili usije kwake. Ilikuwa wazi hakuna aliyekuwa tayari kutoa figo yake msaada; hata kiongozi. Ni kitu kimoja kusema unampenda mtu na ni kitu kingine kuwa na upendo mwingi unaokufanya kujitoa dhabihu kwake.

    3. Upendo wa Yesu ni mkuu kuliko upendo wa wanawake

    Kuna nyimbo nyingi zimeandikwa kuhusu upendo wa wanawake. Hata hivyo, nyimbo nyingi zimeandikwa kuhusu upendo baina ya wanaume na wanawake lakini maumivu mengi duniani yanatokana na kuvunjika kwa mahusiano mengi baina ya wanaume na wanawake. Oh, jinsi ilivyo rahisi kwa upendo wa wanawake kuwa mchungu! Upendo ninaouandika ni upendo mwingi.

    Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; UPENDO WAKO KWANGU ULIKUWA WA AJABU, KUPITA UPENDO WA WANAWAKE.

    2 Samweli 1:26

    YAKOBO AKAMPENDA RAHELI AKASEMA, Nitakutumikia miaka saba kwa kumpata Raheli, binti yako mdogo. Labani akasema, Afadhali nikupe wewe kuliko mtu mwingine; kaa kwangu. Yakobo akatumika miaka saba kwa kumpata Raheli.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1