Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Sayansi ya Kupata utajiri
Sayansi ya Kupata utajiri
Sayansi ya Kupata utajiri
Ebook95 pages2 hours

Sayansi ya Kupata utajiri

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Hiki kitabu kitakufundisha sayansi ya jinsi ya kupata utajiri

 

Sayansi ya kupata utajiri ni kitabu ambacho kimeleta matokeo ya kifedha ya kustaajabisha kwa baadhi ya watu mashuhuri katika dunia ya magharibi. Kinaweza kulinganishwa na vitabu kama The Master Key System cha Charles F. Haanel (1912), Think and Grow Rich cha Napoleon Hill (1937) na vingine vichache. Lakini kipo katika kikundi cha kipekee. Kiukweli , kinajulikana kuhamasisha filamu maarufu ya 2006/2007 ya Rhonda Byrne inayoitwa "The Secret" "Siri". Lakini licha ya hivi vyote, matokeo yake utayagundua katika kufikiri kwako na katika utekelezaji wako kuanzia siku utakayoanza kwenda kwenye undani zaidi wa kurasa zake. Nguvu ya kitabu hiki ipo kwenye matokeo kinayoweza kuyafanya kwenye maisha yako!

LanguageKiswahili
PublisherBARTAHSIA
Release dateJan 23, 2023
ISBN9798215472958
Sayansi ya Kupata utajiri

Related to Sayansi ya Kupata utajiri

Related ebooks

Reviews for Sayansi ya Kupata utajiri

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

1 rating1 review

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

  • Rating: 5 out of 5 stars
    5/5
    Kichwa cha habari kimenivutia sana hvyo kama wadau twaweza kushere pamoja

Book preview

Sayansi ya Kupata utajiri - Wallace D Wattles

Iliyochapishwa kwa mara ya kwanza Merekani mnamo 1910 na

Elizabeth Towne Holyoke, Mas. Marekani

Hakimiliki (C) 1910 W.D WATTLE

Hakimiliki (C) Uchapishaji wa AfricanCnturyBooks / Bartahsia 2020

*

Hakimiliki (C) Uchapishaji wa AfricanCnturyBooks / Bartahsia 2020

*

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu ya toleo hili inayoweza kutolewa nakala kwa njia yoyote au kwa namna yoyote ya elektroniki au mitambo, pamoja na uhifadhi wa habari na mifumo ya kurudisha, bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mchapishaji, isipokuwa na mhakiki ambaye anaweza kunukuu vifungu vifupi kwenye ukaguzi.

Kutoka Kwa Mhariri

Watu wengi wakijua kuhusu maelezo haya ndivyo hivyo maisha ya binadamu yataimarishwa.

*  *  *  *  *  *  *

Mara ya kwanza kusikia juu ya kitabu hiki kidogo nilikuwa naangalia tovuti ya biashara ya mwanamke mmoja anaitwa Tasha. Kusudi langu kwenda kwenye tovuti hii ilikuwa ni kutafuta baadhi ya habari kuhusu mwanamke aliyeibuka kutoka kwenye umaskini na kuwa tajiri.

Sitasahau siku ya kwanza nilipoanza kufyonza maneno ya kitabu hiki. Ilikuwa jioni. Nilikuwa nikisikiliza kwa sauti.

Nakumbuka sikuweza kunyanyuka mahali nilipoketi. Ilikuwa kana kwamba nilikuwa nimeingia katika ukweli mtupu - mahali ambapo uwezekano unajionyesha. Nilipokuwa nikisikiliza, na baadaye nikasoma kitabu hicho, mimi pia nilianza kuuliza swali la Rhonda Byrne - au angalau na mengine tofauti : Inawezaje kuwa sehemu kubwa ya ulimwengu, inaonekana, haina taarifa na kitabu hiki? Inawezaje kwamba hii siri ya wazi sio uasili wa pili kwa kila mwanadamu kwenye sayari - bila kujali lugha, historia ya nyuma au uwezo?

Ni Mungu tu (au ulimwengu ukipenda) ndiye angeweza kuniletea elimu ya kitabu hiki. Na uerevu huo huo,, nina hakika kwamba sasa uerevu huo umeupata.

Kwa maisha yako – kuanzia siku ya leo na kuendelea!

B.A.M TAH

YALIYOMO

1  HAKI YA KUWA TAJIRI

2  KUNA SAYANSI YA KUPATA UTAJIRI

3  FURSA INAWEZA KUTAIFISHWA?

4  KANUNI YA KWANZA KATIKA SAYANSI YA KUPATA UTAJIRI

5  KUONGEZEKA KWA MAISHA

6  NAMNA UTAJIRI UNAVYOKUJIA

7  MOYO WA SHUKRANI 

8  KUFIKIRIA KWA NAINA FULANI

9  NAMNA YA KUTUMIA  MATAMANIO

10  NAMNA ZAIDI YA KUTUMIA MATAMANIO

11  KUFANYA MAMBO KWA NAMNA FULANI

12  KUFANYA MAMBO KWA UFANISI

13  KUINGIA KWENYE BIASHARA SAHIHI

14  ISHARA YA KUONGEZEKA

15  MTU ANAYESONGA MBELE

16  TAHADHARI NA HITIMISHO LA MAONI

17  MUHTASARI WA SAYANSI YA KUPATA UTAJIRI 

UTANGULIZI

Kitabu hiki ni cha uhalisia na sio kifalsafa; Mwongozo wa kitaalam na sio ushauri juu ya nadharia. Imekusudiwa kwa wanaume na wanawake ambao uhitaji wao mkubwa ni pesa; ambao wanataka utajiri kwanza, na falsafa baadaye. Ni kwa wale ambao hadi sasa hawajapata wakati, njia, au fursa ya kwenda kwa undani katika kusoma kwa nadharia, lakini wanataka mafanikio na wako tayari kuchukua matokeo ya sayansi kama msingi wa kazi zao bila kupitia mchakato wowote wa kisayansi.

Inatarajiwa kwamba msomaji atachukua taarifa za kimsingi kwa imani, ni sawa na kuchukua taarifa kuhusu sheria za kanuni za umeme kama zilivyobainishwa na Marconi au Edison; na kwa kuchuchukua taarifa hizo kwa imani, itathibitisha ukweli wao kwa kufanya kazi bila uoga wala kusita.  Kila mwanaume au mwanamke anayefanya hivi hakika atakuwa tajiri; kwa maana sayansi inayotumika hapa ni sayansi halisi, na kutofaulu haiwezekani. Hata hivyo kwa faida ya wale ambao wanataka kuchunguza nadharia za falsafa hupata msingi mzuri wa imani, hapa nitataja baadhi ya mamlaka.

Nadharia ya ukweli wa ulimwengu - nadharia ya kwamba moja ni jumla yote na jumla yote ni mmoja, nadharia hii   inajidhihirisha vitu vya kilimwengu vinavyo vinavyoonekana ni ya asili ya Kihindu, na  kwa taratibu imekuwa ikishinda kwa aina yake mawazo ya nchi zinazoendelea zaidi ya miaka elfu mbili. Ni msingi wa falsafa zote za Mashariki, na zile za Descartes, Spinoza, Leibnitz, Schopenhauer, Hegel, na Emerson.

Msomaji ambaye anaangalia kwa undani misingi ya kifalsafa anashauriwa kusoma Hegel na Emerson; na atafanya vizuri kusoma Habari za Milele, kijitabu kizuri kabisa kilichochapishwa na JJ Brown, Barabara 300 ya Cathcart, Govanhill, Glasgow, Scotland. Anaweza pia kupata msaada katika safu ya nakala yaliyoandikwa na mwandishi, ambayo yalichapishwa katika Nautilus (Holyoke, Mass.) Wakati wa kiangazi na majira ya joto ya 1909, yakiwa na kichwa cha habari Ukweli ni Nini?

Kwa kuandika kitabu hiki nimecha mambo mengine yote ili niweze kuandika kwa uwazi na lugha rahisi, ili kila mtu aweze kuelewa. Mpango uliowekwa hapa ulitokana na hitimisho la falsafa; imechunguzwa kwa undani, na inaleta matunda mazuri ya majaribio ya vitendo; inafanya kazi. Ikiwa unataka kujua jinsi hitimisho zilifikiwa, soma maandishi ya waandishi yaliyotajwa hapo juu; na ikiwa unataka kuvuna matunda ya falsafa zao kwa mazoea halisi, soma kitabu hiki na ufanye kama vile inavyokuambia ufanye.

Mwandishi.

SURA YA 1

HAKI YA KUWA TAJIRI

Chochote kinachoweza kusemwa kusifu umasikini, ukweli unabaki kuwa haiwezekani kuishi maisha kamilifu au yenye mafanikio kama huna utajiri. Hakuna mwanadamu anayeweza kuinuka kwa kiwango cha juu zaidi katika kipaji au ukuaji wa roho isipokuwa kuwa na pesa nyingi; ili kufunua roho na kukuza talanta lazima awe na vitu vingi vya kutumia, na hawezi kuwa na vitu hivyo isipokuwa tu ana pesa za kununua.

Mwanadamu hukua kiali, kiroho, na kimwili kwa kuwa na matumizi ya vitu, na jamii ina amini   kwamba mwanadamu lazima awe na pesa ili aweze kumiliki vitu; kwa hivyo, msingi wa maendeleo yote kwa mwanadamu lazima iwe sayansi ya kupata utajiri.

Lengo kuu la maisha ni maendeleo; na kila kitu kinachoishi kina haki ya kupata   maendeleo yote yanayoweza kupatikana.

Haki ya bidamu katika maisha inamaanisha haki yake ya kuwa huru na kutokuzuiliwa matumizi ya kitu chochote ambacho ni muhimu kwakwe kutumia kwama mwanadamu aliekamili kiakili, kiroho na kimwili. Kwa maana nyingine, haki yake ya kuwa Tajiri.

Kwenye kitabu hiki, sitazungumzia juu ya utajiri kwa njia ya mfano; kuwa tajiri sana haimaanishi kuridhika au kutosheka na kidogo. Hakuna mtu atapaswa kuridhika na kidogo ikiwa ana uwezo wa kutumia na kufurahiya zaidi. Kusudi la uasilia ni

Enjoying the preview?
Page 1 of 1