Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hatua za Ukuaji wa Kiroho
Hatua za Ukuaji wa Kiroho
Hatua za Ukuaji wa Kiroho
Ebook181 pages2 hours

Hatua za Ukuaji wa Kiroho

Rating: 4 out of 5 stars

4/5

()

Read preview

About this ebook

Hiki ni kitabu ambacho ni msaada mkubwa sana kwa waamini, kwani kinatoa funguo muhimu na kweli muhimu zitakazomsaidia mwamini kukua katika kumjua Mungu. Kimejawa na miongozo mingi yenye kufaa katika mazingira halisi na ya kimaandiko, inayohusu ukuaji wa kiroho wa mwamini. Masomo yaliyotajwa hapo chini yametazamwa kwa upana:

  • Nini maana ya kuokolewa
  • Umuhimu wa Neno la Mungu
  • Ubatizo wa maji, agizo
  • Maombi, kipaumbele
  • Umuhimu wa ushirika
  • Umuhimu wa neema ya Mungu
  • Ukombozi kutoka katika vifungo
  • Kujawa na Roho Mtakatifu

Inapendekezwa kwamba wachungaji, walimu, na viongozi wa kanisa wakitumie kitabu hiki. Kitabu hiki ni muhtsari wenye kujitosheleza kwa mada zenye kufaa ambazo zitajenga msingi mzuri kwa waamini. Pia, kitakupatia mpangilio mzuri wa muundo wa ufundishaji utakaokusaidia kuwafundisha na kuwafunza wale wote ambao Mungu amekupatia dhamana ya kuwalea.
LanguageKiswahili
Release dateDec 2, 2021
ISBN9781596658738
Hatua za Ukuaji wa Kiroho

Related to Hatua za Ukuaji wa Kiroho

Related ebooks

Reviews for Hatua za Ukuaji wa Kiroho

Rating: 4 out of 5 stars
4/5

3 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hatua za Ukuaji wa Kiroho - Rev. David R. Wallis

    HATUA ZA UKUAJI WA KIROHO:

    Kitabu kwa ajili ya Waamini

    Rev. David R. Wallis

    Hatua za Ukuaji wa Kiroho—Kitabu kwa ajili ya Waamini"

    Toleo 1.0 kwa Kiswahili

    © 2021 na David Wallis

    Kazi hii ni tafsiri ya Kiswahili ya kitabu:

    Steps to Spiritual Growth  © 2006 na David R. Wallis

    Toleo 2.1 kwa Kiingereza

    Kimetafsiriwa kutoka Kiingereza na Joshua Silomba na Richard Yalonde

    Ubunifu wa Jalada la Mbele:

    ©  na Zion Fellowship, Inc.

    Haki Zote Zimehifadhi Hakuna sehemu ya kitabu hiki inayoweza kutolewa tena kwa njia yoyote au kwa njia yoyote ya kielektroniki au njia ya kiufundi bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mchapishaji, isipokuwa kwa nukuu fupi katika nakala au hakiki.wa

    Nukuu zote za Maandiko zilizotumika katika kitabu hiki zinatoka katika toleo la Biblia ya Kiswahili la Union Version isipokuwa itakapotajwa tofauti.

    Iliyochapishwa kama e-kitabu mnamo novemba  2021

    huko Merika

    Kitabu cha E-ISBN 1-59665-873-8

    Kwa habari zaidi juu ya e-vitabu, tafadhali wasiliana na:

    Wachapishaji wa Kikristo wa Sayuni

    Ushirika wa Sayuni Ushirika ®

    P.O. Sanduku 70

    Waverly, New York 14892

    Simu: (607) 565 2801

    Usitoe malipo: 1-877-768-7466

    Faksi: 607-565-3329

    www.zcpublishers.com

    Kwa maswali juu ya vitabu vilivyochapishwa, tafadhali wasiliana na:

    Kimechapishwa Tanzania

    ISBN 1-59665-880-0

    Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali wasiliana na:

    Zion Fellowship Incorporated

    S.L.P 2148

    Mbeya, Tanzania

    Simu: +255 (0) 686-170157

    Barua Pepe: blviola@gmail.com

    SHUKRANI

    Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watu wafuatao ambao wamefanya kazi ya toleo la Kiingereza la kitabu hiki:

    Carla Borges, Betsy Caram, Tonya Coursey, Abigail Erb, Mary Humphreys, Carolyn Kilpatrick, Justin Kropf, Sarah Kropf, Mke wangu Marilyn.

    Na kwa watu waliofanya kazi ya toleo la Kiswahili;

    Stan Da, Justin Kropf, Asubisye Mejala, na Benjamin Viola.

    WAKFU

    Kwa Bwana Yesu Kristo, Kapteni wa wokovu wetu, ambaye alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.

    Kwa Dkt. Brian J. Bailey, mwalimu wangu wa chuo cha Biblia, na baba wa kiroho, ambaye maisha yake ya kiungu yamekuwa mfano mkubwa sana wa kuigwa nami na ambaye huduma yake imenigusa kuichuchumilia taji ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

    Kwa Marilyn, mke wangu mpendwa na rafiki wa karibu, ambaye amenisaidia na kunitia moyo sana katika kukiaandaa kitabu hiki.

    UTANGULIZI

    MWONGOZO KWA AJILI YA UKUAJI

    Katika kitabu hiki, kitabu cha kwanza, kuna funguo nyingi za kumsaidia Mkristo kukomaa. Hatua hizi za ukuaji ni kweli za muhimu ambazo tunazihitaji kwa ajili ya kusimama imara tunapoendelea katika Bwana. Kuanzia mwanzo hadi mwisho, ufunguo wa muhimu sana kwa ajili ya ukuaji binafsi kama Mkristo unathibitishwa kuwa ni ujuzi wetu wa Neno la Mungu. Jambo hili ni la muhimu kwa ajili ya waamini wote, kwa kuwa Zaburi 119:105 inasema, Neno lake kweli ni "taa ya miguu yetu, na mwanga wa njia zetu."

    Kwa namna nyingi, kumtumikia Mungu kunahitaji nidhamu na nguvu ya mwanariadha, na njia daima si rahisi. Kwa hiyo, tutakushirikisha kweli nyingi za muhimu ambazo zinahitajika katika kutuandaa sote kama waamini.

    Hatua za Ukuaji wa Kiroho Kitabu. 1

    Ubatizo wa Maji

    Moja ya kweli za muhimu za kiroho ambazo zimezungumziwa katika kitabu hiki ni kuhusu ubatizo wa maji, kwa sababu tendo hili la utii ni ishara ya nje ya kile kinachotokea ndani mioyoni mwetu. Neno la Mungu linatuagiza kwamba tubatizwe kwa maji. Mathayo 28:19-20 inatuambia: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi."

    Roho Mtakatifu

    Katika somo hili, mengi yatazungumzwa kuhusu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ni wa muhimu sana kwetu, kwa kuwa Yeye has ani Nafsi ya Tatu ya Uuungu. Yuko Mungu Mmoja, lakini nafsi tatu Hai katika Uungu – Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wakati hii ni siri kubwa ya Mungu, si jambo gumu kuielewa kama tunayo imani katika Neno la Mungu.

    Pia kuna mfano wa kawaida ambao utatusaidia kuelewa siri hii. Kama maji yakichemshwa hadi kiwango cha juu cha kuchemka, yatakuwa na mvuke; lakini katika joto la chumbani maji hayohayo yanaweza kuwa kimiminika safi na chenye utulivu. Lakini kama joto likipunguzwa hadi katika kiwango cha kugandisha, maji hayo yatageuka na kuwa barafu. Katika namna hizi zote, bado yanakuwa ni maji au H2O. Kwa maneno mengine, bado ni formula ileile ya kikemikali, bali katika namna tatu tofauti. Kwa namna hiyo hiyo, Utatu Mtakatifu wa Mungu unatuonyesha vipengele vitatu vya nafsi hai ya Mungu: Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu. Yohana 14:26 inatangaza kwamba Roho Mtakatifu hutumwa kutoka kwa Mungu: "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." Roho Mtakatifu ni wa muhimu kwa sababu Anatusaidia kuelewa ni nini moyo wa Mungu unasema nasi katika Neno Lake.

    Ubatizo wa Roho Mtakatifu pia ni uzoefu wa muhimu sana kwa waamini wote kuupokea, na kisha kuendelea kutiririka na kuendelea nao. Ubatizo huu kwa awali huonyeshwa na uthibitisho wa kunena kwa lugha mpya. Ni wa muhimu katika kutuwezesha kupata ujasiri wa kuwashuhudia watu kwa habari ya Kristo, na pia kutuandaa kumtumikia Mungu kwa nguvu na upako wake (Matendo 2:3-4; Marko 16:17-20). Kwenye siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu alipomwagwa, watu walilia, "Tufanyeje? Petro alipotoa jibu alisema, Tubuni! (Matendo 2:37-38). Hiki ndicho hasa hutokea kwenye maisha ya mwamini wakati wa kuokoka. Tulipotambua kwamba tulihitaji kuokolewa kutoka dhambini, na kusema ndiyo" kwa Bwana mioyoni mwetu, majina yetu yaliandikwa kwenye kitabu cha uzima cha Mwanakondoo (Ufu. 20:12; 21:27). Hata hivyo, kuna mengi zaidi kwenye maisha ya Mkristo kuliko tendo rahisi la kumkubali Kristo wakati wa kuokoka. Tunapokua na kukomaa katika imani na ujuzi wa Yesu Kristo, tunajifunza anachohitaji Bwana kutoka kwetu ili kwamba tuweze kutembea karibu naye katika maisha haya. Hatua hizi za awali za ukomavu na ukaribu na Bwana Yesu Kristo pia zitajadiliwa katika kitabu hiki.

    Kufunguliwa

    Pia tutachunguza kuhusu somo la kufunguliwa. Kufunguliwa hutokea pale nguvu za Mungu zinapovunja vifungo katika maisha yetu, na kutuweka huru mbali na roho chafu ambazo pengine zilishuka kutoka kwenye vizazi vilivyopita (Hes. 14:18; Mk. 16:17). Mungu anataka kuwaweka mateka huru. Kimsingi, Yesu alikuja kwa ajili ya kutuweka sisi sote huru kabisa! Neno la Mungu linaweka hilo wazi: "Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli" (Yn. 8:36).

    Hatua za Ukuaji wa Kiroho-Kitabu. II

    Masomo ya ziada hayajajumuishwa kwenye toleo hili, lakini kwa umuhimu uleule kwetu waamini, yatazungumziwa katika mfululizo wa kitabu hiki.

    Kusifu na Kuabudu

    Kwa Hatua Zaidi kwa Waamini tutakazia umuhimu wa kusifu na kuabudu katika maisha ya mwamini. Kumwabudu Mungu kunatuleta kwenye uwepo wake, na ni hapo ndipo tunapobadilishwa na kugeuzwa kuwa kwa mfano na sura yake (Zab. 17; 115:1-8).

    Utoaji wa Zaka

    Katika toleo la pili pia tutazungumzia kwa kina kuhusu somo la kutoa zaka, hili ni eneo la muhimu katika maisha ya Mkristo. Tutajadili tofauti kati ya zaka na sadaka, huku tukitoa mifano mingi ya kimaandiko ambayo inaufunua moyo wa Mungu na hamu ya kutubariki katika jambo hili la muhimu.

    Ndoa na Familia

    Katika macho ya Mungu, familia ni msingi mkubwa wa Kanisa na jamii. Kwa hiyo, katika kitabu hiki cha pili, tumejumuisha funguo za thamani za kuwasaidia waamini kuja katika mpagilio wa Kiungu aliouweka Mungu katika eneo la muhimu la mahusiano ya kifamilia. Tutajadili uhusiano wa mume na mke, huku tukitoa ushahidi mkubwa wa kibiblia wa shauku ya Mungu ya kuziweka ndoa pamoja. Katika siku hizi za mwisho, moyo wa Mungu ni kuleta urejesho kwenye familia. Shauku yake ni "kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao" (Mal. 4:5-6).

    Kuja kwa Yesu Mara ya Pili

    Kitabu cha pili pia kitazungumzia kwa kina kwa habari ya kweli za Kimaandiko kuhusiana na Kuja kwa Yesu Mara ya Pili. Kama waamini, lazima tujiandae kwa ajili ya kuja kwake; somo letu limekusudia kutusaidia kuishi katika nuru ya ukweli huu na kwa ajikli ya umilele.

    Kwa hiyo, tunapendekeza kusoma kitabu hiki cha kwanza, na kuomba kwamba Bwana akitumie, kwa neema Yake "kuwatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu" (1 Pet. 5:10). Unapopata ufahamu kuhusu mambo ya kina ya Mungu na kuongeza katika maarifa na utambuzi, pia ni matumaini yetu kwamba Roho Mtakatifu ataiongoza miguu yako katika njia nzuri, hata unapoanza safari inayofurahisha lakini wakati mwingine yenye changamoto kuelekea kwenye ukamilifu wa Kikristo.

    Sura ya Kwanza

    Kuweka Msingi

    YESU ALIKUJA KWA AJILI YA KUTOA UZIMA

    Uamuzi wa kuokoka ni pale tunapogeuka kutoka dhambini na kuchagua kumuomba Yesu aingie mioyoni mwetu. Maamuzi haya ni ya muhimu kuliko maamuzi yoyote ambayo mtu anaweza kufanya, kwa sababu yana maana ya msingi kwa ajili ya maisha yetu ya hapa duniani na pia kwa ajili ya umilele wetu. Bwana alizungumza na mwanadamu kwenye Yohana 10:10 kwamba Alikuja ili tuwe na uzima, na kisha tuwe nao tele. Hivyo hili ndilo kusudi lake katika

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1