Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu
Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu
Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu
Ebook80 pages1 hour

Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Watu wa Mungu wanatakiwa kujua majira na wakati sahihi wa unyakuo na saa ya kurudi kwa Bwana Yesu kulichukua kanisa na kukusanyika mbele zake na kukaa katika makao yetu ya milele. Nimeandika kitabu hikio kuwasaidia watu wa Mungu kujua tupo katika majira gani ya kanisa ili waweze kujiandaa kwa ajili ya tukio hili kubwa litakalotokea muda wowote kuanzia sasa. Maandiko matakatifu yanasema kama mtu angelijua siku na saa atayokuja mwizi angelikesha. “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake”. (Mathayo 24:36).

LanguageKiswahili
Release dateFeb 4, 2021
ISBN9781005522223
Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu
Author

Charles Nakembetwa

Charles Nakembetwa Shamsulla a author and preacher of Gospel of Jesus Christ. He is also the author of BWANA OKOA NDOA YANGU, YOU CAN EASILY KILL FEAR [CONQUERING FEAR FACTOR] and KUSHINDWA SASA BASI. He holds Masters Degree in Public Administration specializing in Human Resources Management.

Related to Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu

Related ebooks

Reviews for Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Ijue, Dhiki Kuu na Unyakuo wa Watakatifu - Charles Nakembetwa

    IJUE

    DHIKI KUU NA

    UNYAKUO WA WATAKATIFU

    Charles Nakembetwa Shamsulla

    Haki zote zimehifadhiwa@Charles Nakembetwa Shamsulla

    Ijue, Saa ya Kunyakuliwa Watu wa Mungu ISBN: 9781005522223 Kimetolewa 2021

    Na Charles Nakembetwa Shamsulla. Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kutolewa, kutunzwa au kunakiliwa kwa muundo au kwa namna yoyote, iwe kwa elektroniki, kimakanika, kufotokopi, ku- rekodi au vinginevyo pasipo ruhusa ya maandishi isipokuwa kutoa sehemu kama rejea katika kufundisha. Kwa taarifa na kibali unaweza kuwaasiliana na mwandishi kwa simu na email ifuatayo: +255-714008191

    Email: cshamsulla@gmail.com

    DIBAJI

    Napenda nianze kwa kufafanua kuwa biblia ni neno la Mungu na Mungu tunayemzingumzia ni Roho wala sio kiumbe unachoweza kukiona katika umbile la mwili. Kama Mungu ni Roho ni wazi kuwa na neno lake ni Roho pia. Kama neno la Mungu ni Roho maana yake ni kuwa, bila Roho wa Mungu binadamu wa kawaida hawezi kulifahamu neno la Mungu, badala yake atafahamu historia za biblia.

    Mtu wa Mungu kila unaposoma neno la Mungu omba Mungu akufunulie katika Roho wake ndipo utakapoelewa neno la Mungu; Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.

    Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. 2Wakoritho 2:14-16). Bila mafunuo ya Mungu hatuwezi kulielewa neno la Mungu badala yake tutaelewa historia nzuri za Musa, za Yusufu, za Daudi na wengine waliotangulia. Watu wengi wanashindwa kutafsiri mafunuo katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana kwa sababu wanataka kutafsiri kama kitabu cha hadithi badala ya kumwomba Roho Mtakatifu awafafanulie na kuwapa maana aliyokusudia Mungu. Mafunuo kuhusu dhiki kuu na unyakuo ni mafumbo ya Roho Mtakatifu, ndio, lakini maandiko yanasema kuwa; Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. (1Wakoritho 2:26).

    Wakati naomba Mungu nipate maana nzuri ya kuelezea maana ya UNYAKUO, Roho Mtakatifu akanipa maana yake kuwa ni kutengwa kwa watu wa Mungu. Kila wakati Mungu anapotaka kuwaangamiza waovu lazima kwanza huwatenga watu wake.

    Kamwe Mungu hataangamiza wenye dhambi pamoja na watoto wake, akifanya hivyo atakuwa anavunja agano lake mwenyewe; na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, Kama kundi la watu wake; Kwa maana watakuwa kama vito vya taji, Vikimeta-meta juu ya nchi yake; (Zek 9:16 SUV).

    Wote tunasoma kuwa wana wa Israeli walitengwa kabla ya mapigo kwa taifa la Misri. Sote tunajua yale mapigo kumi kwa mkono wa Musa, lakini katika ulimwengu wa roho hawakutoka Misri baada ya mapigo hayo, bali Mungu aliwatenga kwa kuwanyakua kwa mbawa za tai. Sikiliza nabii Miriamu alichotabiri; ‘Nyinyi wenyewe mmeona nilivyowatenda Wamisri na jinsi nilivyowachukua kama tai anavyochukua watoto wake kwa mabawa, nikawaleta kwangu (Kutoka 19:4 BHN).

    Watu wote waliona wakitoka Misri kwa misururu mikubwa pamoja na mali zao na watoto wao lakini nabii Miriamu anasema nimeonyeshwa katika ulimwengu wa Roho wana wa Israeli wakichukuliwa na kubebwa kwa mbawa za tai. Kwa maneno mengine walinyakuliwa na Mungu au kutengwa na Mungu na kupelekwa katika nchi ya ahadi.

    Katika ulimwengu wa nyama tunaona Nuhu akiokolewa kwa njia ya Safina lakini katika ulimwengu wa roho Nuhu na familia yake walishaokolewa zamani sana; Na Mungu aliwaadhibu watu waovu walioishi zamani. Alileta gharika katika ulimwengu uliojaa watu waliokuwa kinyume na Mungu. Lakini alimwokoa Nuhu na watu wengine saba waliokuwa pamoja naye. Nuhu ndiye aliyewaambia watu kuhusu kuishi kwa haki (2 Petro 2:5).

    Ndivyo Mungu alivyofanya kwa Lutu, ndivyo alivyofanya kwa wale waasi katika mkutano wa Abiramu na Kora jangwani. Ndivyo alivyomtenga Miriamu kabla ya kuadhibiwa baada ya kumsengenya Musa mtumishi wa Mungu. Unyakuo ni kutengwa, Yesu naye alikuja kutunyakua tutoke dhambini na kuingia katika nuru ya uzima wa milele.

    Kunyakuliwa ni kutolewa kwa nguvu baada ya kushilikiwa mateka na nguvu ya jeshi la maadui. Mungu ametupa ufunuo wa jinsi unyakuo au kutengwa kwa watu wa Mungu utakavyotokea, katika kitabu cha Ufunuo kwa kutumia maneno yafuatayo; Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hadi mahali pake, hapo alishwapo kwa nyakati tatu na nusu, mbali na nyoka huyo. (Ufunuo 12:14 SRUV).

    Katika maandiko tuliyosoma hapo juu, tunaona mwanamke anapewa mabawa mawili makubwa ya Tai ili aruke na kwenda kustarehe jangwani katika mahali alipotengenezewa na Mungu ambapo angekaa kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Kumbuka haya ni maono. Tutaweza kumjua mwanamke huyu kwa kuangalia watu gani wanaopewa mabawa ya tai. Kwanza tunaona Isareli walichukuliwa kwa mabawa ya tai wakati wa kutoka katika utumwa nchini Misri.

    Pia tuangalie Isaya anatuonyesha ni kina nani wanaopewa mabawa ya tai; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia. (Isa 40:31 SUV). Tunapata jibu kwa kulinganisha maandiko ya Mungu kuwa, wanaopewa mabawa ya kuruka kama tai au kuokolewa kwa mabawa ya tai ni watu wake au watakatifu wake.

    Kwa kufuata mafunuo hayo tunaona kuwa, mwanamke anayeongelewa hapa anawakilisha watu wa Mungu watakao nyakuliwa kwa mbawa za tai kabla ya dhiki kuu. Kwa kudhibitisha zaidi hili, maandiko yanafafanua kuwa, watapelekwa katika makao ya starehe kwa muda wa miaka mitatu na nusu ambacho ndicho kupindi cha dhiki kuu.

    Kuonyesha kuwa wanao ongelewa hapa ni watu wa Mungu, maandiko yanasema kuwa Ibilisi ataenda kufanya vita na uzao wa mwanamke waliosalia, maana yake watu watakaoendelea kumwamini Mungu wao wakati wa dhiki kuu na kukataa kupigwa chapa katika viganja vya mikono yao na vipaji vya vyuso zao.

    Mwanamke tunayemwona hapa anawakilisha watu au uzao wa Mungu kama unavyotofautishwa na uzao wa Shetani kama inavyoelezwa katika kitabu cha mwazo; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino (Mwa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1