Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mbinu za Kupata Mume Mwema
Mbinu za Kupata Mume Mwema
Mbinu za Kupata Mume Mwema
Ebook105 pages1 hour

Mbinu za Kupata Mume Mwema

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Mbinu za Kupata Mume Mwema ni kitabu kilichoandikwa ili kumsaidia binti au mwanamke wa Kikristo ambaye yuko tayari kujihusisha na mahusiano na mwanaume ili kuyakuza mahusiano na upendo wao hadi kufikia kufunga ndoa.

Kitabu hiki kimeandikwa na mwanaume kwa hiyo kinakupa mbinu za kushinda changamoto za mahusiano- uchumba na ndoa, kutoka katika macho ya mwanaume. Ukisoma kitabu hiki utajua ni vitu gani ambavyo wanawake wanakosea katika mahusiano ya awali na uchumba na utajua ni mambo gani ufanye ambayo yatamfanya mwanaume akuone unafaa kuchumbiwa.

Kitabu hiki kinaongelea hatua za awali kuanzia mnakutana mara ya kwanza na anakuomba namba ya simu mpaka inafika anaamua kukuchumbia ni mbinu gani zitakutofautisha na mabinti wengine wenye sifa za kuchumbiwa na mtu huyo huyo unayetamani akuchumbie wewe. Kama unataka mwaka usiishe uwe umeshachumbiwa ingawa sasa hivi huna hata boyfriend basi soma kitabu hiki leo na ukiweke katika matendo.

LanguageKiswahili
Release dateFeb 24, 2023
ISBN9798215080757
Mbinu za Kupata Mume Mwema
Author

Msafiri J. Mwaikusa

MSAFIRI J. MWAIKUSA is an assistant pastor at a local Assemblies of God church in Dar es Salaam, Tanzania, where he lives with his wife, Tracy, and their children. He also hosts a weekly podcast named Biblia Inasema Usiogope which can be listened to through Radio Public, Google Podcast, Apple Podcast and other platforms. He holds a bachelor degree in Bible and Theology from the Global University of Springfield MO, U.S.A; Msafiri has an MBA and business experience in food industry and publication. He also has a teaching experience from the University of Dar es Salaam where he obtained his Bachelor of Science in Molecular Biology and Biotechnology.

Read more from Msafiri J. Mwaikusa

Related to Mbinu za Kupata Mume Mwema

Related ebooks

Reviews for Mbinu za Kupata Mume Mwema

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Mbinu za Kupata Mume Mwema - Msafiri J. Mwaikusa

    Kwa Nini Usome Kitabu Hiki

    Mahusiano na uchumba ni kitu kizuri lakini kuna hatari zake pia kwa hiyo unahitaji umakini na pia ushauri kutoka kwa watu ambao wamepitia huko.

    Mabinti wengi wameumizwa kwa mambo mengi, wengi kwa kudanganywa. Wengine wamejeruhiwa unakuta wanasema wanasubiri kidogo kwa sasa hawataki mahusiano. Lakini muda haukusubiri kwa hiyo wakati anarudi kwenye kuanza mahusiano anakuwa ameshachelewa na soko limevamiwa na mabinti vijana zaidi na pengine kwa muonekano ni warembo zaidi. Kwa changamoto nyingi kama hizi utajua unahitaji aina fulani ya muongozo utakaokusaidia ili usipoteze muda lakini pia ufanye mambo kwa usahihi kama vile umekuwa kwenye gemu kwa miaka mingi sana.

    Kitabu hiki kitakupa ujuzi huo. Mbinu hizi ni maalum kwa ajili ya kukufanya uingie kwenye mahusiano na kupata unachokitaka, yaani mume umpendaye na anayekupenda sana. Kama hutaki jambo hili liwe la bahati nasibu basi unapaswa kusoma kitabu hiki. Hii ni kwa sababu lengo la kitabu hiki ni kukuongezea nafasi wewe kuolewa – ifike mahali siyo wewe unayehaha kutafuta mume lakini vijana wawe wanapishana nyumbani kwenu wakileta barua za posa.

    UTANGULIZI

    Mambo ya kutafuta mke au mume ni mambo ya mapenzi na mapenzi ni mambo ya kimwili zaidi kuliko kiroho. Simaanishi kwamba siyo ya kiroho kabisa, hapana, kwa sababu kuna suala la kiroho katika nani awe mke wako au mume wako, lakini ni suala la kimwili zaidi kwa sababu mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa.

    Kama ni msomaji wa Biblia utakuwa unakumbuka kwamba wakati Yesu anasemezana na Masadukayo na Mafarisayo kama ilivyoandikwa katika Mathayo 22:23-33 alisema kwamba wakati wa ufufuo watu hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa Mungu mbinguni. (Mathayo 22:30). Kwa neno hili ni dhahiri kwamba masuala ya kuoa na kuolewa na hata masuala ya chumbani tunamalizana nayo hapa hapa katika ulimwengu huu. Mambo ya mapenzi ni ya kimwili tu kama chakula cha kimwili. Yana kiroho kidogo ila kimwili zaidi.

    Sasa kwa sababu mambo ya kimwili yanaenda kimwili zaidi sio sawa kumtegemea mchungaji au mama mchungaji awe ndio mtaalamu wa kukufundisha mambo ya kimwili. Mchungaji sio lazima akufundishe mambo ya mapenzi na ya chumbani kwa kutumia cheo chake cha uchungaji kwa sababu uchungaji ni wa mambo ya kiroho zaidi. Kama ambavyo sio lazima mchungaji akufundishe namna ya kupika biriani nzuri ila mpishi mzuri bila kujali imani yake ndiye atakayekufundisha basi ndivyo ambavyo mambo ya mapenzi na chumbani unapaswa kufundishwa na mtu ambaye anayajua hayo mambo bila kujali imani yake. Cha muhimu ni kwamba mafundisho hayo yawe ya kimwili zaidi yasiingie kiroho na pia ni vema unayefundishwa kukaa imara mafundisho yasikutoe katika imani yako. Kwa mfano mtu anayekufundisha mambo ya chumbani akisema umnyime mwenzio kwa miezi sita na wakati maandiko yanasema msinyimane (1 Wakorintho 7:5) basi ukumbuke kukaa katika imani yako. Hii ni tofauti na ibada ambayo ni suala la kiroho zaidi kuliko kimwili. Ingawa ibada hutumia mwili – kutumia mikono, kinywa na miguu kupiga magoti n.k.- lakini ni jambo la kiroho zaidi ndio maana unaweza kukaa pembeni ya mtu mkiwa ndani ya chombo cha usafiri akawa amefunika uso wake kwa mkono kama amelala kumbe anafanya ibada kwa Mungu. Ibada ni suala la kiroho zaidi kuliko kimwili.

    Wengine hufikiria kwamba ukifundishwa haya mambo na mtu wa imani nyingine utapotezwa kiimani. Hayo ni mawazo hasi sana. Watu wanaenda shuleni na kujifunza masomo mengi na mengine yanafundisha kwamba binadamu alikuwa nyani hapo zamani za kale na baadae ndio akawa kama alivyo sasa, wala hakuumbwa na Mungu. Na bado haiwasumbui watu wanalipa hela nyingi kupeleka watoto wao wakasome wala hawasemi inaharibu imani yao. Ni suala la kuelewa, kuelewa na kukubali au kuamini ni vitu tofauti. Mfano kwenye masomo unaweza kufundishwa ujamaa ni nini na ubepari ni nini. Katika mtihahi ukiulizwa maana ya ujamaa unatakiwa ujibu vile ulivyofundishwa na kuelewa, ukikosea wanaweka kosa. Unaweza kuwa unauelewa Ubepari na kuuamini lakini pia unaelewa Ujamaa ni kitu gani ingawa hukubaliani nao wala kuuamini. Hapa hawapimi vile unavyoamini ila vile unapaswa kuelewa. Kama ungekuwa mcheza mpira na unataka kushinda mechi yenu ya fainali mngekaa na kumsikiliza kocha vizuri na kufanya mazoezi halafu pia mngeleta mchungaji awaombee na kuwapa baraka lakini kwa sababu kucheza mechi ni suala la kimwili zaidi siyo lazima kocha awe ametoka chuo cha Biblia.

    Ndio hivyo hivyo ukijifunza mambo ya mapenzi unapaswa kuelewa halafu ukae baadae uone kama haina upinzani na imani yako ili uendelee kutendea kazi uone kama italeta matokeo mazuri katika maisha yako. Lakini ukitaka kukazana na vile mchungaji wako anasema kila siku ingawa umeona haileti matunda utapoteza muda wako bure. Utazeeka na hutapata mume.

    Kwa hiyo katika kitabu hiki naenda kukufundisha mambo kama mwanaume aliyepitia changamoto za mahusiano na akazishinda na anatajiriba ya kutosha katika mambo ya mapenzi na mahusiano. Zaidi ya hapo, nimeokoka kwa hiyo maelekezo ninayokupa yamevuviwa na yapo katika muongozo wa Kibiblia ili nisikutoe katika imani yako. Naamini yapo mambo mazuri sana utakayojifunza kutoka kwa mwanaume kwa kujua ni vitu gani ambavyo sisi wanaume tunaona mabinti wanakosea katika kuanzisha na kukuza mahusiano. Lengo langu kupitia kitabu hiki ni kusaidia mabinti ambao bado hawajaolewa wapate kupata waume lakini pia hata kama umeshaolewa kuna mambo utajifunza yatasaidia kutia chachu katika ndoa yako.

    1.  Mbinu ya Kwanza: KUJIFUNZA

    Katika maisha hakuna kupiga hatua kama hutajifunza. Kama umefika mahali umekwama, ni vema kuwa na mtazamo wa kujifunza. Hapo utajua ni kwa nini umekwama na nini ufanye ili uweze kujikwamua. Kujifunza inajumuisha pia kutendea kazi yale uliyojifunza kama kweli unataka kupiga hatua. Hutaweza kukabili changamoto ulizonazo au zitakazojitokeza kama huko tayari kujifunza. Na hata kabla ya vita, wanajeshi huwa wamepita katika mafunzo ya kutosha kuweza kumkabili adui. Kujifunza kunafanya mtu aweze kujiamini anapokabiliana na changamoto za maisha. Kama unafanya mambo yale yale za zamani tegemea matokeo yale yale. Njia pekee ya kupata matokeo mapya ni kufanya jambo jipya, na ukifanya jambo jipya bila kujifunza unaweza kuharibu kabisa. Kwa hiyo ni lazima tujifunze.

    Biblia inatuasa kujifunza katika mambo mbalimbali hapo ambapo akili zetu hazijafamu

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1