Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Hawara
Hawara
Hawara
Ebook119 pages1 hour

Hawara

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Katika maisha tunayoishi, kumekuwa na swali ambalo jibu lake si jepesi kupatikana au halipatikani kabisa. Kwamba, Hivi mwanamke ni nani hasa?! Je, ni mtoto, ni dada, ni shangazi ni Mama au ni Bibi? Wakati ukitafuta jibu la swali hili, huenda unaweza kuchanganyikiwa pale utakapotafakari  kwa kina na kujiuliza tena, Je, nini wajibu na nafasi ya mwanamke katika jamii?! Ni uzazi? Ulezi wa familia, au kiburudisho kwa wanaume walafi wasio na staha?!

Kupitia riwaya hii ya Hawara, Hafidh Kido kwa mara nyingine tena anaitumia kalamu yake vyema kutafuta majibu ya maswali hayo, akiangalia mila, desturi na taratibu za maisha katika jamii za watanzania. Jamii zinazomtazama mwanamke kama aina fulani ya kitu badala ya mtu. Kido anaichambua si tu nafasi ya na wajibu wa mwanamke katika jamii, bali pia anaitazama kwa kina nafasi na wajibu wa jamii kwa mwanamke.

Hiki ni kitabu ambacho kitakufunulia mengi na vingi kuhusu mwanamke na jamii inayomzunguka. 

LanguageKiswahili
PublisherHafidh Kido
Release dateNov 9, 2021
ISBN9789987934553
Hawara
Author

Hafidh Kido

Hafidh Kido ni mwanahabari, mwandishi wa vitabu na mwanaharakati wa haki za binadamu.

Related to Hawara

Related ebooks

Reviews for Hawara

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Hawara - Hafidh Kido

    Hafidh Kido

    Tabaruku

    ––––––––

    NAKITOA kitabu hiki zawadi kwa wanawake wote wanaoteseka katika ujane, mitihani ya kukosa uzazi na zaidi ya yote wale wanaojistiri kwa ahadi waliyowapa wazazi wao kuwa watakapoolewa ndipo watakaposhiriki tendo la kujamiiana.

    Zipo sababu nyingi katika maandishi haya, sikuamka tu asubuhi nikaandika haya utakayosoma kwenye kurasa zilizopimwa kwa adabu, heshima na nidhamu ya Kiafrika.

    Naweza kuwa nimeteleza sehemu moja au mbili nikaandika kisichofaa kwa maadili yetu, lakini ni katika kuweka msisitizo wa kuelewa lengo. Sikukusudia tabia mbaya kwa kuwa kiu yangu ni kuona kitabu hiki kidogo kinasomwa na watu wa rika zote.

    Huenda kitabu kikasomwa zaidi na wanaume kuliko wanawake ambao ndio niliowakusudia hasa, sababu zipo nyingi lakini kwa kuzitaja chache – wanadamu hupenda zaidi kujua habari za mwengine kuliko zake.

    Wakati nikisoma mwalimu wangu alinipa mtihani, akataka kujua kwenye gazeti kukiwekwa picha ya mwanamke ni kina nani watalinunua zaidi hilo gazeti wanaume au wanawake, na ikiwekwa picha ya mwanamme ni kina nani watalinunua zaidi wanaume au wanawake. 

    Jibu katika swali la kwanza ni kuwa gazeti likiwa na mwanamke mzuri mbele, litanunuliwa zaidi na jinsia zote mbili wanaume na wanawake.

    Sababu – wanawake wameumbwa ni washindani, wanapenda kujua zaidi wapi wanakosea na wapi wameshindwa ili waongeze juhudi. Wanaume hupenda vitu vizuri; hivyo watataka kujua zaidi undani wa uzuri wa mwanamke aliye kwenye picha.

    Jibu la swali la pili, wanawake ndio watakaonunua zaidi gazeti lenye picha ya mwanamme mtanashati kuliko wanaume, kwa sababu ile ile kuwa wanawake watataka kujua mwanamme huyu anamilikiwa na nani, siri ya utanashati wake ni ipi. Lakini wanaume watashindwa kulinunua kwa kuwa si washindani.

    Hivyo, kitabu hiki nimekusudia kuandika habari nyingi kuhusu wanawake wanaohangaika mitaani bila kuolewa. Lakini pia inahusu wale wenye bahati ya kuolewa lakini ndoa haziwataki kwa sababu hii au nyingine.

    Najua yapo mafunzo yatakayookotwa na wengi, lakini pia kama kuna nilipokosea nayapokea yote yaliyohifadhiwa kwenye vifua vyenu kwa kuwa pengine haya niliyoyaandika sina elimu nayo kubwa zaidi ya kile kidogo nilichomegewa na Mungu.

    Kuhusu lugha, nimejitahidi kadiri nilivyoweza kuzungumza Kiswahili cha wote, ingawa sehemu moja au mbili kalamu yangu iliteleza nikaandika kama wazungumzavyo wenyeji wa Tanga.

    Hiki ni kilema changu, najitahidi kujipurukusha nisikiweke hadharani hasa mahali ambako nitalazimika kuwasiliana na jamii pana, lakini nashindwa. Mnivumilie.

    Hafidh Kido

    Juni, 2021

    Tanga, Tanzania

    Sura ya kwanza

    MARA zote tunaitazama dunia kwa jicho gumu la hisia hasi au chanya; kulingana na hali zetu za maisha. Kuna wanaotamani kufarakana na dunia hata sasa, kwa sababu hawana raha nayo. Lakini kuna wanaojiona kila siku wanarudi nyuma kiumri, hawakui hawazeeki kwa raha.

    Yote haya yamehifadhiwa kwenye akili. Mwanadamu alivyoumbwa alitofautishwa na viumbe wengine kwa kupewa akili. Wanyama wamepewa matamanio wakanyimwa akili, malaika wamenyimwa vyote - matamanio na akili wamepewa amri. Mungu anawaamrisha tu nao hawahoji, hawamchoki wala kumsinzilia.

    Majini wamepewa matamanio na fahamu ya mema na mabaya, lakini wamenyimwa akili na uwezo wa kutengeneza mambo. Mwanadamu kapewa vyote, akili, fahamu, matamanio na hofu. Ili ajaribiwe.

    ––––––––

    Nafsi dhaifu hubeba, na kuhimili mazito

    Nafsi imara hushiba, ikadharau mapito

    Hutukomaza adhaba, tukapinda kama fito

    Hafungi macho ngariba, akitahiri mtoto

    Usoni hujisiriba, masizi zao la moto 

    Twacheza nao sindimba, werevu vipara ngoto

    ––––––––

    Ajabu kubwa ya maumbie ya mwanadamu ni namna ambavyo Muumba kayaleta machozi kuwa sehemu ya maisha yetu, kazi kubwa ikiwa ni kutoa uchafu wa macho, kuonyesha hisia hasi au chanya na kuondoa ama kupunguza uchungu kwenye mwili.

    Huenda wengi tunaijua kazi moja tu ya machozi, nayo ni kulia baada ya kuumizwa. Hili ndilo tulilowakaririsha watoto wetu tangu wakiwa wachanga. Awali walilia kwa sababu ya kuwasiliana, kwa kuwa hawakudhani mnawaelewa wanapozungumza lugha zao za kitoto. Hadi walipolia ndio mliwajali.

    Tazama, mwanao wa miezi chini ya sita. Akizungumza na wewe humwelewi. Bali unadhani anacheza,  bila kujua nawe unamchekea. Humtekelezei haja yake. Pengine anakwambia nataka kulala lakini sina usingizi, au nasikia njaa nataka kunyonya. Au mkojo umejaa kwenye nepi unanichubua.

    Ila akilia; haraka unamrukia. Utambembeleza kumpa faraja au utamtekelezea haja yake kulingana na aina ya kilio.

    Walezi wanajua. Mtoto hulia akiwa na njaa, akiwa mpweke, akisikia usingizi, akiwa na hofu atalia, pia hulia akimwona mtu mbaya au kwa kudeka tu, mlezi mzuri atavitofautisha vilio vyote hivyo kwa ufanisi wa kipekee.

    Kwa kuwa hili tumekua nalo basi limetuganda. Hata ukubwani tunalia kwa mengi. Hata furaha ikizidi tunalia, tunalia kwa hofu na kwa kuumizwa au kujeruhiwa. Kilio kinaleta faraja kama uchawi. Ni ajabu sana ukilia hata mtu mwenye umri mkubwa unajihisi umelivua zigo lililokuelemea.

    Unaweza kujisemea rohoni kuwa uliwahi kupatwa na mtihani, au mitihani mingi tu. Ila ukajipa ujasiri wa kutolia ovyo. Husemwa mwanadamu anapasa alie ili atoe dukuduku.

    Hivi ndivyo Mwenyezimungu anavyoweka mambo yake kwa siri kubwa. Unahitaji kujisumbua ili upate majibu. Usome uzingatie. Hatuna budi kulia, tulie kwa kiasi tunachoweza pale yanapotufika. Tusikithirishe na wala tusijibane.

    Ewe uliye na maya, furahi sihuzunike

    Tabia kama deraya, hifadhi uheshimike

    Maisha ni haya haya, kikujiacho kishike

    Bure sijione goya, kikosa sihamanike

    Kuku amepewa ngoya, baridi ahifadhike

    Kondoo kapewa haya, vitali anusurike

    Hata wakikusengenya, simama urukeruke

    Hako wa kukupokonya, heshima yako ishike

    Wale wamejikusanya, kuomba ufedheheke

    Katika mambo makubwa ambayo pengine si wengi wenye majibu sahihi ni namna ambavyo  tunabaki hai iwe kwa kupenda au kutopenda, hivi tumeshawahi kujiuliza sababu ya kuendelea kupumua na kuishi?

    Pengine linaonekana swali la mzaha. Halina maana wala faida kwa muulizaji na muulizwaji. Lakini hii ni habari kubwa iliyotawala maisha yetu. Ni sehemu kubwa ya sababu za kuumbwa.

    Haikutokea tu kwa bahati tukaumbwa. Tubebwe matumboni mwa mama zetu, tuwe wachanga, tuanze kusoma, tufanye kazi nasi tuoe au kuolewa, tuzae kisha ufike wakati tuondoke duniani.

    Basi tu huu ndio uwe mwisho wa kila kitu. Tumeumbwa kwa mchezo tu. Hapana. Tumeumbwa ili kumwabudu Mungu mmoja aliye hai. Hilo ndilo kusudi la uhai wetu. Ingawa wapo wenye mawazo kinzani, haki yao kuamua wanachoona kinafaa.

    Tafsiri yake; kwa muda wote wa uhai tulionao tunatakiwa kumuabudu Mungu. Kila tunachofanya, kusema au kutazama kiwe ni ibada.

    Wapo wanaodhani ibada ni kwenda msikitini au kanisani tu. Hapana. Ibada ni mfumo mzima wa maisha yetu ya kila siku.

    Kutoleana salamu, kula, kulala, kutembea kwa adabu, kuvaa kwa nidhamu, kufanya kazi, biashara, kuoa/kuolewa, kubeba mimba na kuzaa, kusameheana na kukanyana mabaya na kuamrishana mema. Vyote hivi ni ibada.

    Tena hii ndiyo ibada iliyopigiwa kelele na Mungu. Kwa sababu muda tunaoutumia kwa ibada ya kusali ni mdogo kuliko tunaoishi na wengine.

    Hivyo, uhai wetu usiwe balaa kwa wengine. Tusifanye watu watamani tuwahi kuondoka duniani.

    Tujitahidi uhai wetu uache athari kwa jamii. Watu waendelee kukutaja kwa wema kwa sababu ukishafariki kila kitu unakiacha. Utarudi kama ulivyokuja, mpweke, mnyonge usiye na msaada wowote ila uliyoyatanguliza kwa mikono na mdomo wako.

    Kitakachokusaidia ni dua za watoto wako uliowaandaa vema, sadaka yenye manufaa uliyoiacha au elimu njema uliyoipandikiza kwenye vifua vya wanadamu wenzio.

    Kinyume cha tafakuri hii ya kubaki hai, ipo tafakuri nyingine ya kuogopa kifo; Mwenyezi Mungu katika Quran Surat Al Muminun aya ya 12-15 anasema: "Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo.

    "Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama.

    "Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1