Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Biblia Inasema Usiogope
Biblia Inasema Usiogope
Biblia Inasema Usiogope
Ebook130 pages1 hour

Biblia Inasema Usiogope

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Kwa sababu ya woga watu wanapoteza fursa nyingi sana maishani. Wengine wamepoteza nafasi ya kupata mchumba mzuri kwa sababu ya woga, wengine kwa woga siku ya interview wakakosa kazi na bado wengine fursa za biashara zikawapita. Lakini Neno la Mungu liko wazi kwamba huna haja ya kuogopa yeyote wala chochote ila Mungu Mwenyezi. Katika kitabu hiki, Biblia Inasema Usiogope, mistari mbalimbali katika Maandiko Matakatifu inachambuliwa kumpitisha msomaji kuanzia kuona kwamba woga ni dhambi hadi namna za kuishinda hofu na kutembea jasiri kama impasavyo mtu mwenye imani.

Hiki ni kitabu cha mafundisho ya Biblia yanayomfaa kila mtu lakini zaidi yule aliyebanwa na changamoto za kimaisha zinazomfanya ajawe na hofu kwa sababu ya kutoona uchochoro wa kutokea. Soma kitabu hiki na hutabaki mdhaifu tena.

LanguageKiswahili
Release dateFeb 25, 2023
ISBN9798215077429
Biblia Inasema Usiogope
Author

Msafiri J. Mwaikusa

MSAFIRI J. MWAIKUSA is an assistant pastor at a local Assemblies of God church in Dar es Salaam, Tanzania, where he lives with his wife, Tracy, and their children. He also hosts a weekly podcast named Biblia Inasema Usiogope which can be listened to through Radio Public, Google Podcast, Apple Podcast and other platforms. He holds a bachelor degree in Bible and Theology from the Global University of Springfield MO, U.S.A; Msafiri has an MBA and business experience in food industry and publication. He also has a teaching experience from the University of Dar es Salaam where he obtained his Bachelor of Science in Molecular Biology and Biotechnology.

Read more from Msafiri J. Mwaikusa

Related to Biblia Inasema Usiogope

Related ebooks

Related categories

Reviews for Biblia Inasema Usiogope

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Biblia Inasema Usiogope - Msafiri J. Mwaikusa

    UTANGULIZI

    Moja ya matokeo ya anguko, yaani dhambi ya Adamu kula tunda aliloagizwa asile, ni woga. Katika Mwanzo 3:10 Adamu na mkewe wakiwa wamejificha kati ya miti ya bustani, Adamu alimwambia Mungu kwamba "Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa..." Tangu wakati huo woga umekuwa ukiharibu maisha ya wanadamu kwa kuvuruga uhusiano wao na Mungu, uhusiano wa wao kwa wao, na uhusiano wao na mazingira na viumbe vingine vilivyoko duniani. Kuanzia binadamu kuanza kuchoma na kufyeka misitu na hata kugundua silaha za kumuua binadamu mwenzie kwa haraka vinaweza kuelezewa kwa msukumo utakanao na woga.

    Vilevile ukitathmini maisha yako au ya watu wa karibu wanaokuzunguka unaweza kuona ni namna gani woga umewazuia wengi kupiga hatua kimaisha na kuweza kufika katika viwango ambavyo Mungu aliwakusudia au kutokana na uwezo unaoonekana ndani yao pengine wangeweza kufikia. Fuatilia kuanzia woga wa somo la hisabati, woga wa mitihani, woga siku ya usaili, woga wa kusimama mbele za watu na kutoa hoja, woga wa kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea cheo fulani, woga wa kuwekeza mtaji katika wazo fulani la biashara n.k. utagundua kwamba woga ni tatizo kubwa.

    Kitabu hiki Biblia Inasema Usiogope kimekusanya masomo machache kutoka kwenye podcast yenye jina hilo hilo ambayo iko mtandaoni tangu mwaka 2021 ikiongezeka somo moja walau kila wiki. Masomo yaliyomo kwenye kitabu hiki yamechaguliwa kwa namna ambayo itamfanya msomaji ajenge msingi mzuri kutoka kwenye Biblia kuonyesha kwamba woga ni dhambi, madhara ya woga na namna ambavyo unaweza kushinda woga. Kimeandikwa katika lugha rahisi kueleweka na mifano kutoka kwenye maisha yetu ya kila siku. Lengo la mafundisho haya ni kujenga imani yako kwa Mungu katika Kristo Yesu ili kukufanya uishi kama jasiri katikati ya kundi kubwa la maadui na upinzani. Barikiwa.

    Sura ya Kwanza

    WOGA NI DHAMBI

    Hivi unajua kuna mtu alipata fursa ya kuongea na binti mzuri sana ambaye angemfaa kabisa kuwa mchumba wake na pengine baadaye waoane na kuwa na familia nzuri tu lakini aliogopa, binti akaenda na yeye akabaki anapigika? Na fursa kama hiyo hata kama imerudi inawezekana siyo binti yule tena. Kuna watu wengi tu wameshawahi kupoteza nafasi nzuri sana za kazi maishani mwao kwa sababu ya woga siku ya usaili. Na wapo watu wengi ambao wanaendelea kupoteza fursa za kibiashara ambazo zingewatoa na kuwabadilisha maisha yao kabisa wao na wapendwa wao, lakini kinachowakwamisha ni woga. Na kibaya zaidi katika watu hao wanaoogopa utakuta ni Wakristo.

    Tena wapo Wakristo wengi tu ambao wanasoma Biblia lakini hawafungui kusoma kitabu cha Ufunuo wa Yohana kwa sababu wanaogopa. Wanadai kwamba kitabu hicho kinachohusu siku za mwisho kinatisha. Lakini ili tupige hatua maishani tunapaswa kuacha woga. Hebu fikiria mtoto angeamua kutojaribu kupiga zile hatua za kwanza na kudondoka kwa sababu ya kuogopa angewezaje kutembea? Biblia inaonyesha kwamba mwoga na mzinzi wote sawa. Woga ni dhambi.

    Ufunuo wa Yohana 21:6-8

    6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima bure.

    7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.

    8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

    Wataalamu wa mambo wanasema inafaa kuanzia mwisho wakati unaanza. Ndiyo maana mjenzi anapaswa awe na picha ya jengo analolijenga ili ajue anajenga vipi na hata msafiri anaanza safari yake akijua anapoenda, au mwisho wa safari yake. Na hapa katika mistari hii ya kitabu cha mwisho kabisa katika Biblia inayoelezea mwisho wa mambo utakavyokuwa tunapata picha ya mambo yalivyo hata sasa. Unaona kwamba adhabu ya mwoga ni sawa na ya mzinzi, na ya mwongo na muabudu sanamu. Utaona kuna makundi mawili hapo yakiwekwa wazi kwa lugha ya kiagano ambayo Mungu amekuwa akiitumia tangu zamani katika Agano la Kale. Kundi la kwanza ni la wale walioshinda, au washindi. Hao wanapewa urithi na kuwa wana wa Mungu (mstari wa 7). Kundi la pili ni la waliobaki au wadhambi ambao sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto na kiberiti (mstari wa 8). Na katika makundi haya mtu mwoga yupo kundi la waliobaki, yaani wadhambi. Haya makundi ni yaki-agano tangu kale kwa sababu mara zote Mungu alikuwa akisema wapo watu wake na wasio wake, yaani wanaomkubali na kuambatana naye na wanaomkataa.

    Kutoka 19:4-5

    4 Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi.

    5 Sasa basi ikiwa mtatii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

    6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.

    Mungu amewachagua hao watu na kuwatoa Misri kwa mkono hodari ulionyooshwa lakini ili kuwapa nafasi ya kusikia sauti Yake na kulishika agano lake, hapo ndipo wanakuwa tunu Kwake. Kwa hiyo yapo mambo ambayo Yeye anategemea watu hao wafanye ili wawe wake kweli kweli, ufalme wa makuhani na taifa takatifu. Lakini hakuishia hapo tu, bado Mungu alitoa tamko la siku ile kuu iliyopaswa kuja...

    Yeremia 31:31-33

    31 Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuds.

    32 Si kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa mume kwao, asema Bwana.

    33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

    Kwenye Kutoka 19 Mungu alikuwa anaongea na taifa la Israeli kimwili, watu aliokuwa amewatoa Misri ambao ni wana wa Yakobo, uzao wa Ibrahimu. Kwenye Yeremia 31 anaongea na mabaki ya taifa la Israeli kimwili, lakini pia ni zaidi ya kimwili kwa sababu maneno hayo ya kiagano yalipambanuliwa na Yohana Mbatizaji aliposema "katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto (Luka 3:8). Na pia Wagalatia 3:29 inasema nanyi mkiwa mali ya Kristo, basi ninyi ni wa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ile ahadi." Kwa hiyo ni suala la kiroho na Agano Jipya linafanya kila aaminiye kuwa kwenye Agano na Mungu -Yeye atakuwa Mungu wetu na sisi watu wake kama 1 Petro inavyosema.

    1 Petro 2:7-10

    7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

    8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha, Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.

    9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliwaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

    10 ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

    Kwa hiyo mambo haya ya kiagano yataenda kukamilika katika kipindi hicho ambapo waovu watatupwa kwenye ziwa liwakalo moto na kiberiti na walioshinda kurithi mema na kuwa wana wa Mungu kweli kweli. Hivyo basi ili kuwa washindi na warithi inatupasa kuwa tofauti na wale watakaotupwa kwenye ziwa liwakalo moto na kiberiti. Yaani hatupaswi kuwa tusioamini, hatupaswi kuwa wachukizao, hatupaswi kuwa wauaji, hatupaswi kuwa wazinzi, hatupaswi kuwa wachawi, na hatupaswi kuwa waabudu sanamu wala

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1