Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Kushindwa Sasa Basi
Kushindwa Sasa Basi
Kushindwa Sasa Basi
Ebook159 pages1 hour

Kushindwa Sasa Basi

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Ulimwengu tunaoishi ni ulimwengu wa mapambano kati ya nguvu za giza na ufalme wa nuru. kadiri ule mwisho unavyokaribia ndivyo vita kati ya giza na nuru vinavyopamba moto. Watu wa Mungu wanahitaji kuvaa silaha zote za Mungu ili kupambana na nguvu za giza na kushinda na kumrudishia Mungu utukufu. Kushindwa sasa basi kitakufungua kutoka katika maisha ya kushindwa na kushambuliwa na adui shetani hadi kufikia maisha ya ushindi. Karibu sana upokee ushindi wako.

LanguageKiswahili
Release dateNov 12, 2016
ISBN9781370936038
Kushindwa Sasa Basi
Author

Charles Nakembetwa

Charles Nakembetwa Shamsulla a author and preacher of Gospel of Jesus Christ. He is also the author of BWANA OKOA NDOA YANGU, YOU CAN EASILY KILL FEAR [CONQUERING FEAR FACTOR] and KUSHINDWA SASA BASI. He holds Masters Degree in Public Administration specializing in Human Resources Management.

Related to Kushindwa Sasa Basi

Related ebooks

Reviews for Kushindwa Sasa Basi

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Kushindwa Sasa Basi - Charles Nakembetwa

    Kushindwa Sasa Basi

    Na

    Charles Nakembetwa

    Shamsulla

    Haki zote zimehifadhiwa@Charles Nakembetwa Shamsulla

    Kushindwa Sasa Basi

    ISBN 978-9976-9976-2-0

    Kimetolewa 2016

    Kimechapishwa Tanzania na

    Charles Nakembetwa Shamsulla

    Hakuna sehemu ya kitabu hiki inaweza kutolewa, kutunzwa au kunakiliwa kwa muundo au kwa namna yoyote, iwe kwa elektroniki, kimakanika, kufotokopi, ku-rekodi au vinginevyo pasipo ruhusa ya maandishi ya mchapishaji.

    Kwa taarifa zaidi unaweza kuwaasiliana na mwandishi kwa simu na email ifuatayo:

    +255-762-811-278

    Email:tmitigo@gmail.com

    UTANGULIZI

    Makusudi ya Mungu kukuleta dunia sio kwa bahati mbaya wala kukufanya kuwa muhanga wa mateso ya shetani na mawakala wake.

    Uumbaji wako ni wa kipekee na umepangiliwa na umekuja dunia kwa kusudi maalumu. Hatatokea mtu mwingine kama wewe milele yote. Kazi ya kukuumba iligharimiwa na umekuja duniani kukamilisha kusudi maalumu la Mungu. Bahati mbaya wengi wetu hatujitambui au hatujui kusudi la Mungu katika maisha yetu.

    Tunafikiri tumekuja kujaza dunia hii na kuishi kadiri maumbile ya kiasili yatakavyoongoza na wengine wanadhani walikuja duniani kutawaliwa na kupewa maelekezo na wengine.

    Utasikia wengine wanapopitia katika matatizo ya maisha na changamoto wanasema Mungu kapenda nipitie haya, au Mungu hakupenda nipate kitu hiki, wengine wanasema haikuwa riziki yangu.

    Hayo ni baadhi ya maneno yanayodhihirisha kuwa watu wengi wanaishi kwa kubahatisha na kufuata mkumbo wa dunia invyokwenda. Kumbuka biblia inasema kabla hujazaliwa nakujua na nimekuleta duniani kwa kusudi maalumu.Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa . Yeremia 1:5

    Wakati wako wa kuishi maishi ya ushindi umefika. Kitabu hiki ni majibu yako uliyoyasubiri kwa muda mrefu. Utasimama dhidi ya mashambulizi yote ya adui na mawakala wake. Mwisho wa muda wako wa kulia umefika.

    Bwana amekuandalia mlango wa kutokea na kukupa faraja katika Nyanja zako zote za maisha.

    Siri za ufalme wa Mungu wetu zimefunuliwa kwa ajili yetu ili tuweze kuishi maisha ya kukanyaga maadui wote na kutawala. Biblia inasema katika siku za mwisho kumjua Bwana kutakuwa kwingi kama maji ya bahari na watu watakula.

    Kushiba na kumshukuru Mungu wao. Kwa maana dunia itajazwa maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yafunikavyo bahari. 1wakoritho 14:14

    Usikae nyuma ya benchi, huu sio wakati wa kukaa nyuma na kusubiri, bali ni wakati wa kushiriki na kufaidi nguvu za milele za Mungu wetu. Kushindwa na kulia sio fungu letu, tumewekewa kuishi na kutawala katika ulimwengu wa sasa na ule ujao.

    Kumbuka kazi hii sio ya mwanadamu wala ya watu maarufu bali ni kazi ya Mungu wetu na Bwana wetu Yesu Kristo. Anauonyesha ukuu wake katika maisha yetu na tunatawala pamoja nae katika majira haya ya siku za mwisho.

    Wakati dunia inalia na kukosa majibu ya maisha, watu wake wataogolea katika maisha ya ushindi na kumshukuru na kumshangilia Mungu wetu. Dunia itakosa majibu ya maisha, bali wateule wataongoza katika nyanja zote za maisha. Jambo la kuzingatia ni kuwa ushindi wako hautakuja hivi hivi bali utakuja kwa kuzitii na kuzijua siri za ufalme wa Mungu wetu.

    Siri za ufalme ndio zitakuwa msingi ulioimara na ngao yetu katika mapambano haya. Wanyenyekevu na wenye njaa ya kweli ya mambo ya ufalme wa Mungu ndio watakaoziona kazi zake na kuufurahia wokovu katika siku za mwisho. Bali wenye upole watairithi nchi, watajifurahisha kwa wingi wa Amani. Zaburi 37:11

    Napenda nikuhakikishie ndugu yangu kuwa huu sio muda wa kukimbia huko na huko na kuabudu wanadamu na mungu watu, bali ni muda wa kumjua na kumtegemea Mungu katika kila jambo. Muda uliotumia kuwanyenyekea wanadamu watosha.

    Bwana wa mabwana anakuita na kafungua mikono yake akupokee na kukupa pumziko la kweli. Hata kama bahari ingetibuka kiasi gani, bado Bwana anamajibu ya kukufikisha ng’ambo.

    Kushindwa sasabasi, kinakupa funguo za kuweza kusimama katika changamoto yoyote utakayokutana nayo katika maisha yako. Utakuwa na uwezo wa kusimama peke yako na kuyaangusha majeshi ya adui yako hata kama mashambulizi yatakuwa na nguvu kiasi gani.

    Biblia inasema kuwa mmoja kati yenu atafukuza maelfu na wawili watafukuza makumi elfu. Mmoja angefukuzaje watu elfu, wawili wangefukuzaje elfu kumi, kama mwamba wao asingaliwauza, kama Bwana asingaliwatoa? Kumbukumbu la Torati 32:30

    Soma kitabu hiki kwa maombi na matarajio ili uweze kupata mtaji wa kukufanya kusimama dhidi ya vita vilivyopo na vitakavyokuja katika maisha yako. Kumbuka vita katika maisha ya wateule ni lazima na huwezi kukimbia. Unachotakiwa kufanya ni kuvaa silaha zote za Mungu ili uweze kushindana wakati wa uovu. Ibilisi hatakukimbia kwa sababu umesema wewe ni mtumishi wa Mungu au una hudhuria sana kanisani bali shetani atakuogopa na kukuheshimu kwa sababu ya kiwango cha kweli na nuru ya Mungu katika maisha yako.

    Amini usiamini, tumepewa kushinda na zaidi ya kushinda katika nyanja zote za maisha, haijalishi aina ya vita tutakayojihusha katika maisha yetu.

    Ukiona kuna eneo katika maisha yako bado unasumbuliwa na adui, ujue bado hujaingiza nuru ya kutosha kufukuza giza katika sehemu hiyo ya maisha yako. Uhuru hauwezi kuja hadi utakapoingiza nuru katika eneo hilo. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. Yohana 1:5

    Kitakachokutenganisha wewe na ushindi kwa sasa ni uvivu wa kusoma kitabu hiki na kiburi kukufanya ushindwe kupokea mafundisho yako katika kitabu hiki.

    Karibu pamoja tutembee pamoja katika mafundisho ya Mfalme wa wafalme ili tujifunze mbinu na mapenzi yake katika maisha yetu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za maisha. Kila mlima utasawazishwa na kila eneo lililopotoka katika maisha yako litawekwa sana, kumbuka tena vita sio vya kwetu bali vita ni vya Bwana.

    Kazi yetu sisi ni kukaa mkao ambao Bwana atakapokuwa akipita tukutane naye na kuuona mkono wake. Haijalishi umeshindwa mara ngapi na kukatishwa tamaa na maisha na mashambulizi ya adui, sasa wakati wako wa kutawala umefika.

    Kumbuka Bwana hatachelewa wala hatakawia. Siku elfu kwake ni sawa na siku moja na ahadi zake ni hakika na yakini. Lakini, wapenzi, msisahau neno hili, kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Yohana 1:5 Maana miaka elfu machoni pako ni kama siku ya jana ikisha kupita, na kama kasha la usiku. Zaburi 90:4

    Mwandishi wa kitabu hiki ameandika kwa lugha nyepesi ili kuwawezesha wasomaji wa aina zote kuupata ujumbe katika njia ya urahisi na ufasaha zaidi. Msomaji wa kiwango chochote cha elimu anaweza kusoma na kuelewa mafundisho ya kitabu hiki.

    Hata wale walio katika huduma na wanaotaka kukua katika huduma, kitabu hiki kitakuwa msaada mkubwa wa kuzijua siri na ufunuo mkubwa ulio katika kibabu hiki. Kumbuka Bwana anatuma watumishi wake katika siku za mwisho ili kutufungua macho na kutuwezesha kuzijua siri za ufalme na kuchukua nafasi zetu katika mwili wa Kristo.

    Kama utakuta sehemu yoyote katika kitabu hiki unashindwa kuelewa, omba Roho Mtakatifu na tumia biblia na kuchumguza maandiko kama watu wa Beroya walivyofanya.

    Walichunguza maandiko ili kuona kama mambo yale yaliyohubiriwa na mitume yaliendana na neno la Mungu. Neno la Mungu ndio kipimo chetu cha kweli na uhakika kutumia kuchunguza na kupata uhakika wa mapenzi ya Mungu katika kila jambo na mafundisho tunayokutana nayo katika maisha yetu.

    Nakuhakikishia msomaji wangu utakaposoma na kumaliza kitabu hiki maisha yako hayatakuwa kama yalivyokuwa hapo kwanza. Ninaamini Bwana atainua huduma yako ili uweze kusaidia wengine pia.

    Napenda nikupe siri moja kubwa katika maisha mtu wa Mungu kuwa, zawadi nzuri kuliko zote utakazoweza kumpa ndugu na jamaa katika maisha yake ni zawadi ya maarifa na ufahamu wa siri za Mungu.

    Nimekiandika kiabu hiki ili kuwashirikisha ndugu zangu wasomaji wa kiswahili siri za Mungu alizonifunulia. Nikaona ni vyema nikashirikiana na ndugu zangu katika hali ya upendo na kushirikiana karama za ufalme wa Mungu wetu, maana ni heri kutoa kuliko kupokea.

    Ni imani yangu kuwa hakuna mtumishi wa Mungu hata mmoja anayeweza kujua siri zote za ufalme wa Mungu, bali tumepewa karama za Mungu kwa kufaidiana. Mmoja anaweza kupewa karama ya unabii, karama ya kufundisha, kupambanua roho, upendo, kuhudumiana na nyingine nyingi kwa ajili ya kulijenga kanisa la Mungu na mwili wa Kristo upate kujengwa na kufikia kimo cha Kristo.

    Kuweka mafunuo na maono katika maandishi ni faida kubwa kwa wasomaji na mwili wa Kristo kwa lengo la kufaidiana na kujenga mwili wa Kristo ili uweze kufikia kimo cha Kristo hata ajapo mara ya pili, ambapo atalikuta kanisa lake likiwa kamilifu lisilokuwa na mawaa wala doa. Kumbuka Paulo alisema heri yeye anayehutubu na kulijenga kanisa kuliko yeye anaye nena kwa lugha.

    Ni imani yangu kuwa kwa njia ya kitabu hiki kitahutubu kwa watu wengi na kuwajenga wengi. Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, kwa maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa .1 Wakoritho 14:5

    Nakukaribisha ndugu msomaji ili uweze kupata chakula cha kukusaidia katika safari, maana safari bado ni ndefu na neema ya Bwana wetu Yesu Kristo itatuwezesha na kutusaidia kusimama na kuzipinga nguvu zote na mishale yote ya adui.

    Kumbuka tumepewa mamlaka kukanyaga nyoka, ng’e na kila aina ya pingamiza za adui shetani. Mwombe Bwana Yesu afungue macho yako ya rohoni unaposoma kitabu hiki ili upate kuziona siri za ufalme.

    SURA YA KWANZA

    UWEZA NA NGUVU ZA AGANO JIPYA

    Maisha ya wateule ni maisha ya mapambano dhidi ya nguvu za giza na wafalme wa anga. Ufalme wa Mungu wetu ni hakika na yakini vilevile ufalme wa giza ni dhahiri. Biblia inasema.

    Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Waefeso 6:12

    Jambo la kushukuru ni kuwa Bwana Yesu alishamaliza vita na kukabidhi mamlaka kwetu tuliompokea Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yetu.

    Ukombozi wetu sio njia tu ya kutorokea mbinguni pekee, bali ni njia ya kupokea nguvu zake za milele na kuishi kama watawala na washindi katika nyanja zote za maisha kuanzia katika ulimwengu wa sasa hata ule ujao.

    Unaweza kuwa huru kabisa mwili nafsi na roho. Kwa mpendwa wangu mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli. Mpendwa naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako inavyofanikiwa. 3 Yohana 1:1, 2.

    Kama Yohana mbatizaji angejua kuwa alikuwa anatembea katika nguvu na upako wa Elia asingekubali kukatwa kichwa kama

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1