Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Mirathi na Wosia: Utaratibu wa Kufungua, Kusikiliza na Kusimamia Mirathi na Wosia Kisheria Mahakamani: Legal, #1
Mirathi na Wosia: Utaratibu wa Kufungua, Kusikiliza na Kusimamia Mirathi na Wosia Kisheria Mahakamani: Legal, #1
Mirathi na Wosia: Utaratibu wa Kufungua, Kusikiliza na Kusimamia Mirathi na Wosia Kisheria Mahakamani: Legal, #1
Ebook548 pages5 hours

Mirathi na Wosia: Utaratibu wa Kufungua, Kusikiliza na Kusimamia Mirathi na Wosia Kisheria Mahakamani: Legal, #1

Rating: 5 out of 5 stars

5/5

()

Read preview

About this ebook

Elimu kuhusu utaratibu wa kufungua, kusikiliza na kusimamia mirathi na wosia Tanzania ni muhimu. Umuhimu unaongezwa na migongano katika sheria. Sheria zinaratibu aina tatu za mirathi: ya kimila, kiislamu na ya kiserikali. Sheria na taratibu kwa mfano za mirathi ya kimila au ya kiislamu inaweza kukamilisha mirathi mahakamani lakini ikapingwa kwa kutumia sheria nyingine zinazolinda haki za makundi mbalimbali. Mapungufu haya yamechochea umuhimu wa elimu ya utaratibu wa kisheria wa mirathi na wosia kwa makundi mbalimbali Tanzania.

Kitabu hiki kimebainisha sheria zinazohusiana na haki za warithi, taratibu za kupata urithi stahiki, wakfu, haki katika wosia, migongano katika sheria za kimila, kiislamu na za nchi na taratibu za mahakama zinazoweza kurekebisha mapungufu yaliyopo. Kitabu kinatoa mwanga wa namna haki za wahusika mbalimbali katika jamii zinavyolindwa na sheria mbalimbali, taratibu za kudai haki zao, vikwazo wanavyopaswa kuvitarajia, na namna ya kukabiliana na vikwazo hivyo kisheria mahakamani. Kimejengwa kuwa msaada katika kuelezea sheria na taratibu za mirathi na pia katika kubainisha misimamo tofauti ya sheria mbalimbali kuhusu haki za mirathi kwa makundi mbalimbali.

Jumla ya sheria 26, kanuni mbalimbali 11 na kesi 40 zimenukuliwa kuwezesha welewa mpana na kamili. Sehemu ya yaliyomo imebeba mada zote muhimu kumrahisishia msomaji kupata haraka kile anachokitafuta. Mazingira tata na migogoro inayojitokeza mara kwa mara vimeongezwa na kuwasilishwa kwa mpangilio sahili kuwezesha msomaji kupata mwanga wa mambo mbalimbali haraka zaidi.

Kitabu hiki ni msaada mkubwa kwa  wanazuoni, wataalamu wa sheria, waheshimiwa mahakimu na majaji katika ngazi zote, na wananchi wa kawaida. Kitabu, pia, kitaongeza mwanga kwa watunga sera na watunga sheria katika maeneo yanayohitaji maboresho kwa ajili ya kujenga mfumo, sheria na taratibu kamilifu na rafiki zaidi za mirathi na wosia Tanzania.

LanguageKiswahili
Release dateDec 23, 2020
ISBN9789987452439
Mirathi na Wosia: Utaratibu wa Kufungua, Kusikiliza na Kusimamia Mirathi na Wosia Kisheria Mahakamani: Legal, #1

Related to Mirathi na Wosia

Titles in the series (4)

View More

Related ebooks

Reviews for Mirathi na Wosia

Rating: 5 out of 5 stars
5/5

2 ratings1 review

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

  • Rating: 5 out of 5 stars
    5/5
    Greatest probate book for Tanzania. The content, high placed reviewers and carefully selected real life questions and answers makes the book excellent in its genre.

Book preview

Mirathi na Wosia - Mgongoro Ernest Jonathan

Mgongoro Ernest Jonathan

GDY PUBLICATIONS COMPANY LTD

S.L.P. 32172

Simu: +255 717326061, 752882235

www.gdypublications.com

info@gdypublications.com

Dar es Salaam

TANZANIA

––––––––

Matini © Mgongoro Ernest Jonathan

Upangaji kurasa © GDY Publications Company Ltd.

Usanifu jalada © GDY Publications Company Ltd.

––––––––

Toleo la Kwanza 2020

––––––––

ISBN  978-9987-452-43-9

––––––––

Haki zote zimehifadhiwa.  Hairuhusiwi kuiga, kunakili, kutafsiri au kukitoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote ile bila idhini ya GDY Publications Company Limited.  Kitabu hiki hakitaazimishwa, kuuzwa kikiwa kimetumika au kukodishwa kibiashara kwa namna yoyote ile zaidi ya makusudi ya uchapwaji wake bila idhini ya GDY Publications Company Limited.

––––––––

Mwandishi: Mgongoro Ernest Jonathan

Mpanga kurasa: GDY Publications Company Ltd.

Aliye sanifu jalada: GDY Publications Company Ltd.

Wahariri: Gabriel D. Kitua, Wigayu Kissandu

Yaliyomo

Shukrani...................................................xii

Virefu vya maneno yaliyofupishwa............................xiv

Sehemu ya kwanza: Mirathi

Utangulizi ..................................................2

Mahakama zinazoshughulikia mashauri ya mirathi...............4

Mahakama za Mwanzo......................................4

Mahakama ya Wilaya (inayokaliwa na Mahakimu Wakazi Wateule wa Wilaya)......5

Mahakama ya Wilaya........................................6

Mahakama Kuu.............................................7

Mali ya ubia..............................................9

Sheria zinazohusu mgawanyo wa mali za marehemu...........10

Msingi wa sheria za mirathi..................................10

Sheria ya Uthibitisho wa Wosia na Usimamizi wa Mirathi....10

Sheria ya Madaraka na Wajibu wa Mtawala Mkuu...........10

Sheria ya Udhamini wa Umma............................11

Sheria ya Watu wenye Asili ya Kiasia wasio Wakristo........12

Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai................12

Sheria ya Mirathi ya Kiserikali ya India.....................12

Sheria ya Mtoto.........................................13

Sheria ya Usimamizi wa Haki na Matumizi ya Sheria Mbalimbali ......13

Sheria ya Mahakama za Mahakimu........................13

Sheria zinazohusu mgawanyo wa mali kimila...................13

Kanuni za urithi kimila...................................14

Aina mbili za urithi wa kimila.............................14

Mkondo unaofuata ukoo wa baba ..........................14

Mkondo unaofuata ukoo wa mama..........................16

Watoto waliozaliwa nje ya ndoa...........................17

Sheria ya Mtoto na Haki za Mtoto wa Nje ya Ndoa .............19

Mirathi na watoto wa jinsia ya kike na wajane..............20

Haki ya kurithi ardhi.....................................20

Haki ya mjane mgumba kurithi mali za marehemu mume wake21

Wanapokosekana warithi halali wa marehemu.............22

Sheria zinazohusu mgawanyo wa mali kiislamu..................23

Mgawanyo wa mali kwa njia ya sheria ya Kiislamu ..........24

Daraja la kurithi..........................................25

Wanaostahiki kurithi.....................................26

Viwango vya mgawanyo..................................27

Warithi hawaruhusiwi kurithi kama marehemu anadaiwa ....33

Kuchelewa kugawa mirathi ya kiislamu.....................33

Mali ya wakfu..............................................34

Masharti yanayofanya wakfu uwe sahihi....................35

Msimamizi wa wakfu......................................35

Jinsi ya kuweka wakfu.....................................35

Wanufaika wa wakfu......................................36

Familia.................................................37

Jamii...................................................37

Familia na Jamii..........................................37

Uhusiano na tofauti kati ya wakfu na wosia.................38

Mali ya wakfu Tanzania Bara na Zanzibar...................39

Upande wa Tanzania Bara.................................39

Uandaaji wa wakfu........................................39

Kuanzishwa kwa tume ya wakfu............................40

Maelekezo ya mtoa wakfu lazima yafuatwe....................41

Usajili wa mali iliyo chini ya wakfu...........................43

Nini ufanye mali ya wakfu inapotumika vibaya.................44

Usimamizi wa mali ya wakfu Zanzibar......................45

Utaratibu wa uwekaji wakfu................................45

Masharti ya kukubalika wakfu...............................49

Usajili wa mali za wakfu....................................49

Uendeshaji wa mali za wakfu..............................50

Ukodishwaji wa mali ya wakfu.............................50

Kifo cha mpangaji........................................52

Utaratibu wa kubadili kitu kilichowekwa wakfu.................52

Mambo yanayoathiri uendelezaji wa wakfu....................54

Kufunga wakfu wa familia..................................54

Kumwondoa msimamizi wa wakfu...........................55

Sheria zinazohusu mgawanyo wa mali kiserikali .................55

Sheria ya Urithi ya India...................................55

Sheria ya Uthibitisho wa Wosia na Usimamizi wa Mirathi.....56

Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai.................56

Sheria ya Watu Wenye Asili ya Kiasia Wasio Wakristo .......56

Sheria ya Mtoto..........................................56

Mirathi ni haki ya kikatiba.................................57

Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 na Sheria ya Ardhi....58

Mirathi kwa Wakristo.....................................60

Sheria ya mirathi ya Kiislamu na Sheria ya Serikali ..............60

Waislamu wanaohoji sheria ya mirathi ya Kiislamu..........60

Wasiokuwa Waislamu wanaohoji sheria ya mirathi ya Kiislamu61

Utaratibu wa kufungua mashauri ya madai ya mirathi kisheria mahakamani.......63

Taratibu za kufungua maswala ya mirathi Mahakama ya Mwanzo..63

Watu wanaoweza kuwa wasimamizi wa mirathi.............70

Wajibu wa msimamizi wa mirathi.........................71

Utendaji wa msimamizi wa mirathi.........................76

Haki ya msimamizi wa mirathi.............................77

Idadi ya wasimamizi wa mirathi............................78

Wajibu wa mahakama katika kuthibitisha msimamizi wa mirathi.......79

Haki ya warithi dhidi ya msimamizi wa mirathi.............80

Ufafanuzi kuhusu muingiliano kati ya Mahakama ya Mwanzo na ya

Wilaya na Kuu............................................82

Taratibu za kufungua maswala ya mirathi Mahakama ya Wilaya na Mahakama Kuu......83

Utaratibu wa kutoa uthibitisho wa mirathi na hati za usimamizi83

Barua ya maombi ya usimamizi............................85

Utaratibu utumikao katika kuomba barua ya usimamizi .........88

Usimamizi katika mali chache............................91

Uchaguzi wa usimamizi katika mali chache................91

Maombi ya uthibitishwaji wa usimamizi katika mali chache.......92

Uteuzi wa msimamizi wa mirathi katika mali chache ............93

Ukomo wa kufungua mashauri ya mirathi.......................95

Mahakama ya Mwanzo......................................95

Ukomo wa kufungua mirathi katika Mahakamani ya Wilaya na

Mahakama Kuu.............................................97

Ukomo wa madai ya mali isiyohamishika ya marehemu..........97

Uhuru wa kujichagulia sheria ya mirathi ........................98

Pingamizi la taratibu za mirathi..............................100

Mrithi kunyimwa urithi na muusia...........................100

Pingamizi kwa wasii na msimamizi wa mirathi.................101

Mahakama ya Mwanzo..................................101

Mahakama za juu ya Mahakama ya Mwanzo .................102

Utaratibu wa kuweka pingamizi .............................103

Mahakama inaweza kubatilisha au kukataa uteuzi wa msimamizi wa

mirathi .................................................108

Ukomo wa pingamizi (zuio)..................................109

Haki ya mjane kugawiwa nusu ya thamani ya mali aliyoacha marehemu mume wake......111

Utaratibu unaotakiwa kufuata ili mjane apate nusu ya thamani

ya mali ya marehemu mume wake.............................111

Njia za kujenga hoja ya kupata nusu ya thamani ya mali ya

marehemu mume wake ....................................112

Kujenga hoja kutumia sheria ya ndoa......................112

Kutumia sheria za kimila na kanuni za haki za Uingereza....114

Ulinzi wa warithi wanawake kuhusu urithi wao.................116

Hitimisho la sehemu ya kwanza...............................120

Sehemu ya pili: Wosia

Utangulizi..................................................124

Wosia katika sheria mbalimbali...............................126

Wosia katika sheria za kimila................................126

Wosia wa mdomo.......................................126

Wosia wa maandishi.....................................129

Wosia wa Kiislamu..........................................130

Wosia wa mdomo au maandishi............................131

Muusia ana mamlaka ya kutoa zawadi mali yake...........132

Wosia wa kiserikali ........................................134

Wosia wa maandishi.....................................134

Wosia wa mdomo.......................................135

Taratibu za kuandika wosia katika sheria za mirathi.............135

Wosia ..................................................135

Kubadilisha wosia..........................................137

Sehemu salama ya kutunzia wosia............................139

Fomu ya kutunzia wosia ..................................140

Fomu ya kuchukua wosia ................................142

Jinsi ya kutekeleza wosia  ..................................143

Uthibitisho wa wosia Mahakama Kuu na Mteule wa Wilaya.......145

Taratibu muhimu za awali ..................................145

Utaratibu wa wosia na barua za usimamizi katika Mahakama Kuu na

Mteule wa Wilaya........................................145

Maombi ya uthibitisho wa wosia Mahakama Kuu na

Mteule wa Wilaya.........................................146

Ombi la kuthibitishwa kwa wosia..........................146

Kuthibitishwa kwa wosia wa mdomo ......................147

Kuthibitishwa kwa nakala ya wosia........................149

Kiapo cha usimamizi wa mirathi..........................149

Kiapo cha mtekelezaji wa wosia ....................................   150

Wosia ulioambatanishwa na barua ya usimamizi wa mirathi..151

Muombaji anapokuwa hajafikisha umri wa mtu mzima.......151

Wosia wa mirathi kwa ajili ya mtu aliyepungukiwa akili......153

Hitimisho la sehemu ya pili...................................155

Sehemu ya tatu: Mifuko ya hifadhi ya jamii

Utangulizi .................................................158

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi Wa Umma (PSSSF).....160

Aina za malipo..............................................160

Masharti ya malipo..........................................160

Taratibu za kufuatilia malipo..................................161

Maombi ya mafao ya kifo .................................161

Mafao ya Mirathi..........................................164

Pensheni ya urithi.......................................164

Kipindi cha malipo ya pensheni kwa wategemezi...........164

Maombi ya mafao ya mirathi ................................165

Nyaraka zinazotakiwa kuwasilishwa kwa ajili ya kuwezesha mirathi kulipwa......167

Mstaafu aliyefariki akipokea pensheni........................176

Kuchelewa kufungua maombi ya mafao ya mirathi .............177

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)......................179

Mafao ya mirathi...........................................180

Pensheni ya urithi ........................................180

Kiwango cha malipo ya pensheni kwa wategemezi..............180

Kipindi cha malipo ya pensheni kwa wategemezi...............180

Sifa zinazotakiwa.........................................181

Aina ya mafao ya pensheni yanayotolewa ..................181

Maombi ya mafao ya mirathi.............................182

Uthibitisho wa mlipwaji akiba (NSSF)......................184

Hitimisho sehemu ya tatu....................................186

Sehemu ya nne: Maswali yanayotatiza na majibu yake

Msimamizi / wasimamizi wa mirathi ..........................188

Uwezo marehemu kuchagua msimamizi......................188

Hivi mume wangu anaweza kuchagua msimamizi wa mirathi yake kabla

hajafa? Msimamizi huyo ni lazima awe kwa maana ya binadamu?......188

Hivi msimamizi wa mirathi ya marehemu lazima awe ndugu wa

marehemu?.............................................189

Tunaweza kuichagua RITA kuwa Msimamizi wa mirathi yetu? .190

Kuteuliwa moja kwa moja na mahakama......................190

Mahakama kuchagua msimamizi.........................190

Mahakama ikimchagua msimamizi wa mirathi ndiyo kazi ya mahakama

imekamilika?.............................................190

Mahakama ikiteua msimamizi wa mirathi, imempa kustahili kurithi mali

yote? ...................................................191

Hivi sheria haisemi kuwa kabla msimamizi wa mirathi hajateuliwa na

Mahakama ya Mwanzo, lazima Mahakama itoe tangazo kwenye magazeti

kuwa anayetaka kupinga uteuzi huo alete pingamzi yake katika miezi mitatu?

Kwa nini wakati mwingine muda wa pingamizi hutolewa mfupi kama wiki

mbili au tatu hivi tu?......................................191

Hivi sheria ya mirathi, inasema msimamizi wa mirathi awe mmoja tu?

Maana nimeona mahakama za mwanzo zinateua msimamizi mmoja tu kila

shauri..................................................193

Je ni sababu zipi zinazoweza kusababisha mahakama ikamuondoa msimamizi

wa mirathi?.............................................193

Sifa za msimamizi wa mirathi ................................194

Sheria imetaja watu wa aina gani ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa

mirathi?................................................194

Kuna namna ngapi za utoaji wa mamlaka ya usimamizi wa mirathi?......195

Wosia uliombatanishwa na barua ya usimamizi wa mirathi......196

Kama hakuna wosia .....................................196

Usimamizi wa mirathi kwa mambo maalumu..................197

Utaratibu wa kuomba usimamizi wa mirathi mahakamani........198

Ni Utaratibu gani utumikao katika kuomba usimamizi wa mirathi

mahakamani?...........................................198

Kama kuna wosia wa marehemu ...........................198

Kama hakuna wosia wa marehemu.........................199

Wajibu wa wasimamizi na haki za warithi......................199

Sheria imewapa wajibu upi wasimamizi wa mirathi?........199

Je watu wanaotarajia kufaidika na mirathi wana haki zipi za kisheria

kufuatilia usimamizi wa mirathi?..........................201

Haki ya kumtaka msimamizi asimamie mirathi au ajiondoe.....201

Haki ya kuweka pingamizi.................................202

Haki ya kukagua maendeleo ya kazi ya usimamizi wa mirathi....202

Sheria ipi itumike kwa mirathi ipi? ............................203

Mahakama huamuaje itumie sheria gani kwa mashauri tofauti

ya mirathi.................................................203

Mambo gani huangaliwa kabla ya mahakama kuamua kuchagua kutumia

aina mojawapo ya sheria za mirathi?......................203

Sheria ya mirathi ya kiserikali imetoa utaratibu gani wa kugawa mali?.......203

Urithi wa kimila umegawanywa katika madaraja mangapi? ..204

Daraja la kwanza........................................204

Daraja la pili............................................204

Daraja la tatu...........................................204

Mahakama ipi itumike kwa shauri lipi la mirathi? ...............205

Mashauri yapi ya mirathi yafunguliwe mahakama ipi?...........205

Mahakama zipi zina mamlaka ya kusikiliza masuala ya mirathi205

Mahakama ipi yenye mamlaka ya kufunguliwa mashauri ya mirathi

na katika mazingira yapi?................................206

Mahakama ya Mwanzo ina mamlaka ya kufunguliwa mirathi ya

mabilioni ya fedha? .....................................207

Sheria ya uthibitisho wa wosia na usimamizi wa mirathi inashughulika

na mambo yapi na ina lengo gani hasa?...................208

Haki za wajane na watoto wa kambo..........................209

Kuhusu haki za wajane.....................................209

Kama msimamizi wa mirathi akininyima haki yangu au kupendelea

warithi wengine, nifanye nini?............................209

Mahakama ikiamua kuwa nina haki ya kupata nusu ya mali aliyoacha

marehemu mume wangu, nifanye nini?....................209

Kama marehemu mume wangu alikuwa na kimada na amezaa naye

mtoto au watoto je, naye huyo kimada na watoto wake wanastahili

kurithi sehemu ya mali ya marehemu?....................209

Katika sheria za kimila mjane ana haki ya kurithi?...........211

Haki za watoto wa nje ya ndoa...............................211

Je watoto wa nje ya ndoa wanarithi?........................211

Maswali kuhusu mirathi za kiislamu..........................213

Mirathi panapokuwa na mke aliyepewa talaka na wategemezi wengine.......213

Pale wasii anapogawa mali kwa upendeleo na wengine kutopata marehemu anapoacha mke na watoto......213

Pale marehemu anapoacha hisa ya mali, mama, watoto 3 wa kike

na wa kiume na ndugu...................................213

Watoto wa mke wa kwanza wanapoona mirathi baada ya miaka 12, ili

hali marehemu aliwaandikia nyumba watoto wa mke wake wa mwisho......214

Pale mama anapoacha mali akiwa na watoto wanne, lakini kabla ya umauti aliolewa na mme mwingine ambaye hakubahatika kupata mtoto........214

Kama marehemu aliacha watoto wa kiume na wakike wa wake zake wawili wa ndoa na mke mkubwa alimuacha marehemu kabla ya umauti, je

watoto wake wanayo haki?...............................215

Ikitokea mume ameamua kuoa bila cheti cha ndoa kinachotambulika

kisheria, akafariki, je mke (mjane) anaweza kuwa mrithi halali?215

Ikiwa baba na mama wanaweza kurithiana, na mtoto anaweza

kumwandikia mama yake mali kabla ya kufa kwake kama zawadi?.......216

Je, inafaa kurithi wazazi wasio Waislamu?..................216

Je Uislamu unakubali mgao wa mali nyingine na theluthi ya mali kumpa mtoto wa kurithi (adopted)?.......217

Sehemu ya tano: Fomu mbalimbali za kisheria kuhusu mirathi na wosia

Fomu zinazotumika katika utaratibu wa kuendesha mashauri ya mirathi katika Mahakama Kuu, Wilaya Na Mahakama Ya Mwanzo.......219

Mahakama ya Mwanzo.....................................219

Chini ya Sheria ya Mahakama za Mahakimu 1963 Nyongeza ya 5, 1984........219

Fomu zinazotumika katika uthibitisho wa wosia na

usimamizi wa mirathi (barua ya usimamizi katika

Mahakama Kuu, Wilaya, Mahakama ya Wilaya

na Mahakama ya Hakimu Mkazi.)..............................220

Sheria ya uthibitisho wa wosia na usimamizi wa mirathi katika

kanuni ya uendeshaji mirathi, Jedwali la kwanza chini ya kifungu

cha 9 cha sheria ya Uthibitisho wa Wosia na Usimamizi wa Mirathi

sura ya 352 ya toleo la 2002...............................220

Fomu za wosia na wakfu.....................................268

Sheria ya usajili wa Nyaraka Sura ya 117 toleo la 2002..........268

Fomu zinazotumika katika usimamizi wa mali ya

wakfu na amana Zanzibar...................................268

Fomu za mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii.................269

Mfuko wa Penshion kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).........269

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)......................276

Mashauri yaliyo nukuliwa....................................278

Sheria na kanuni zilizo nukuliwa...............................281

Faharasa..................................................284

Marejeo ya ziada...........................................286

Kutabaruku

Kwa mke wangu mpendwa Getrude Vedastus Mahendeka na watoto wangu wapendwa Jovin Ernest Mgongoro na Ivynna Ernest Mgongoro

Shukrani

Kwanza kabisa, namshukuru Mwenyezi Mungu Kwa kuniwezesha na kunifungua akili nikaandika kitabu hiki.

Pia namshukuru Mh. Dickson Augustino Mmasi Hakimu Mkazi, Mh. Shija Mdadila Hakimu Mkazi, Mh. Nicosemu Mwakibibi Hakimu Mkazi, Mh. George Kazi Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Mh. Jaji John Samwel Mgetta Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa michango na mawazo yao ya kuboresha kitabu hiki.

Vile vile namshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Tunduru – Masasi, marehemu Mhashamu Baba Askofu Castor Paul Msemwa kwa kunipa nafasi kutoa mada inayohusu Sheria ya Mirathi na haki za mjane kurithi nusu ya mali waliyochuma pamoja na mume wake, katika kongamano la Umoja wa Wanawake Katoliki Kanda ya Kusini. Namshukuru Sheikh wa mkoa wa Rukwa, Sheikh Rashid Akilimali kwa kunipa muongozo wa Sheria za Mirathi kwa upande wa sheria ya kiislam. Pale palipopunguka Imam Athuman Hemid Fumo, Imam wa Masjd Annas Mtonga, Korogwe alipajazia vyema.  Nicodemus. N. N. Nditi (Jr) mkufunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kisheria kwa Vitendo (LST) na Msemo Mavale – wakili na mkufunzi wa muda wa Taasisi ya Mafunzo ya Kisheria kwa Vitendo (LST) kwa michango yao mizuri katika rasimu ya mwisho.

Uongozi wa NSSF na wa PSSSF kwa pamoja wametoa mchango mkubwa katika kukamilisha sehemu ya tatu ya kitabu - mifuko ya jamii.

Kwa namna ya pekee sana, ningependa kuwashukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Kabidhi Wasii Mkuu. Mamlaka hizi mbili zilipitia kwa kina rasimu ya kitabu hiki na kuwasilisha mapendekezo yao ya maboresho.

Wizara ya Katiba na Sheria walikuwa wa kwanza kukamilisha upitiaji  wa rasimu. Katika barua yao ya tarehe 21 May 2020, kumbukumbu namba AB.75/297/01/22, Wizara ilimpongeza mwandishi kwa kazi nzuri ikisema  kitabu kitakuwa msaada mkubwa na kwa watu wengi. Barua pia ilisema kuwa kitabu kinagusa maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida. Zaidi ya pongezi, Wizara ilitoa mapendekezo ya maboresho ambayo yote yalizingatiwa kwa umakini katika kukamilisha kitabu hiki.  Baada ya maboresho na uwasilishaji wa maelezo ya jinsi mapendekezo ya maboresho yalivyoingizwa, Wizara ilitoa pongezi tena kwa mwandishi na mchapishaji kwa kazi nzuri. Pongezi hizi za pili ziliwasilishwa kupitia barua ya tarehe 24 Agosti 2020 iliyokuwa na kumbukumbu namba AB.75/297/01/48.

Katika barua ya kumbukumbu namba BC.206/272/01/55 ya tarehe 28 Juni 2020, ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu ilitoa maoni kuwa kitabu kitakuwa msaada kwa jamii kwa sababu kinaelezea maswala ambayo ni chanzo cha migogoro katika jamii za Tanzania. Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu pia iliwasilisha mapendekezo ya maboresho ambayo yote yazingatiwa kwa umakini wakati wa kukamilisha toleo hili la kitabu.

Timu nzima ya jopo la uhariri likiongozwa na Bw. Gabriel D. Kitua, Afisa Mtendaji Mkuu wa GDY Publications Ltd. pamoja na Bi. Wigayu Kissandu, mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) walifanya kazi kubwa katika kuhakikisha kuwa kitabu kinakamilika kilivyostahili. Ni kwa kupitia mapitio kadhaa na utekelezwaji wa maboresho mengi ndipo tukaweza kuwa na kitabu unachokifurahia sasa mkononi mwako.

Mwisho lakini sio kwa umuhimu, nawashukuru Rose Silvester Matofali na Astrida kwa kuchapa kurasa nyingi za kitabu hiki.

Virefu vya Maneno Yaliyofupishwa

AC – Appeal Cases

BK –  Baada ya Kristo

EA – East Africa

EALR – East African Law Report

FN – Namba ya Fomu

FLR – Federation Law Report (US)

GN –  Government Notice

HCD – High Court Digest (Tanzania)

H.J. – Hijiria

L&R – Law and Report.

LRT – Law Reports of Tanzania. 

LAPF – Local Authorities Pension Fund (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Serikali za Mitaa)

Mh. – Mheshimiwa

Na. –  Namba

n.k. – na kadhalika

NPF – National Provident Fund

NSSF – National Social Security Fund (Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii)

PSSSF – Public Service Social Security Fund (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma)

RITA – Registration Insolvency and Trusteeship Agency (Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini)

Shs – Shilingi.

T – Tanzania

TLS – Tanzania Law School

TRL – Tanzania Law Report

Uk. – ukurasa

U.S – United State of America

WLAC – Women’s Legal Aid Centr

Sehemu ya Kwanza

Mirathi

Utangulizi

Tanzania ni nchi inayotambua uwepo wa taratibu tofauti za kufungua mirathi kwa kuzingatia maisha ya watu, mila, desturi na dini wanazoabudu. Uzoefu umeonesha kuwepo kwa matatizo mengi katika familia au ukoo pale mtu anapofariki, matatizo hayo hutokana na maswali ya msingi ambayo yatajibiwa katika sura hii.  Maswali hayo ni kama yafuatayo:

a)  Warithi halali wa mali za marehemu ni akina nani?

b)  Nani mwenye haki ya kusimamia mirathi ya marehemu?

c)  Je mjane/mgane aliyeachwa ana haki ya kurithi au kupata chochote katika mirathi hiyo?

d)  Ni sheria zipi zitatumika katika masuala ya mirathi?

e)  Nini wajibu wa msimamizi wa mirathi katika kusimamia mali za marehemu?

f)  Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika kushughulikia mirathi ya mwananchama wake ni upi?

Pamoja na kuwepo na sheria za kimila, sheria ya Kiislamu na sheria ya Kiserikali, nchi yoyote pia husimamiwa na kuongozwa na katiba. Mirathi ni haki ya kikatiba kama ilivyoainishwa katika ibara mbalimbali ndani ya katiba na hakuna mtu, taasisi au serikali yenye mamlaka ya kuzipora haki hizo. Ibara ya 13 (1), (2)[1] inatamka kuwa:

13(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

Mirathi maana yake ni kuondoa umiliki kutoka kwa mtu aliyekufa kwenda kwa warithi walio hai, kama kilichoachwa ni mali au haki miongoni mwa haki za kisheria[2] Mirathi ni mali inayohamishika (mfano: fedha na gari) na isiyohamishika (mfano: nyumba na shamba) vinavyoachwa na marehemu ambavyo hupewa warithi wake kwa kufuata taratibu zilizopo kisheria. Aidha, mirathi inajumuisha mafao ya mtumishi aliyefariki ambayo hulipwa kwa familia yake au ndugu zake marehemu kwa kuzingatia Sheria ya Mirathi.  Sura hii itajadili sheria ya mirathi zinazotumika Tanzania bara, utaratibu wa kufungua mirathi, kusikiliza na kusimamia mirathi kisheria mahakamani.

Sura hii itajadili sheria za mirathi zinazotumika Tanzania bara na pia itagusia baadhi ya sheria za mirathi zinazotumika Tanzania visiwani haswa upande wa mali za wakfu zinazosimamiwa na Sheria ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana namba 2 ya 2007 inayohusu Zanzibar pekee. Lengo ni kuonesha jinsi gani sheria hizi zinafanya kazi kwa ukaribu haswa upande wa mali za wakfu zinazowalenga Waislamu.

Sura ya 1:  Mahakama Zinazoshughulikia Mashauri ya Mirathi

1.1.  Mahakama za Mwanzo

Mahakama ya Mwanzo inayo mamlaka katika masuala yote yanayohusu usimamizi wa mirathi inayotokana na wosia na ile isiyotokana na wosia yenye asili ya sheria ya kimila na kiislam[3].

Sheria za mirathi zinazotumika katika Mahakama za Mwanzo ni sheria za Kimila na Kiislam pamoja na kanuni mbalimbali za uendeshaji mirathi.

Kanuni za utaratibu wa kufungua mashauri ya mirathi katika Mahakama za Mwanzo zilizotungwa chini ya Sheria ya Mahakama za Mahakimu[4], ndio zinazotumika katika kuendesha mashauri ya mirathi. Pia Mahakama za Mwanzo ni lazima zifuate utaratibu uliooneshwa katika Tangazo la Serikali Na. 49 la 1971. Mashauri ya Fanuel M. Ng’unda dhidi ya Herman M. Ngund’a na wengine[5], Richard J. Rukambura dhidi ya Isack N. Mwakajila na wengine[6] na Shomvi Uliza dhidi Mwajabu Rajabu[7] yanaainisha kanuni ifuatayo: 

Mahakama ya Mwanzo inayo mamlaka katika masuala yote yanayohusu usimamizi wa mirathi yenye asili ya sheria ya kimila na Kiislamu. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha sheria ya Mahakama ya Mahikimu na utaratibu wa kusikiliza mashauri ya mirathi umeainishwa katika jedwali la 5 la sheria ya Mahakama ya Mahikimu.

Mahakama ya Mwanzo inayo mamlaka ya kusikiliza shauri la usimamizi wa mali chache endapo mali ya mtu wa kabila fulani zitasimamiwa kutokana na sheria za kabila hilo isipokuwa kama marehemu katika muda wowote alikuwa ni mfuasi wa dini ya kiislam[8]. Vifungu vya sheria hii ya uthibitisho wa wosia na usimamizi wa mirathi[9] havitumiki katika usimamizi wa mali ambazo Mahakama ya Mwanzo haina mamlaka isipokuwa kama mwenendo kuhusiana na urithi wa usimamizi wa mali chache umeanza katika Mahakama ya Mwanzo, Mahakama Kuu inaweza kutoa maelekezo kuwa iendelee kusikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo au kuhamisha kwa kutumia kifungu cha 47[10]

Ikiwa agizo la kusimamia mali limefanywa na, au mwenendo kuhusiana na mirathi umeanzishwa katika Mahakama ya Mwanzo, Mahakama Kuu haitatoa agizo lolote, isipokuwa kama ikiona ni sawa katika maslahi ya haki au kwa ulinzi wa mnufaishwaji yeyote au mdai mali hiyo isimamiwe kwa kutumia sheria hii[11].

1.2.  Mahakama ya Wilaya (inayokaliwa na Mahakimu Wakazi Wateule wa Wilaya)

Jaji Mkuu anaweza kuteua Mahakimu Wakazi wa Mahakama ya Wilaya kusikiliza mashauri ya mirathi kama Mahakimu Wateule[12]. Mahakimu Wateule watakuwa na mamlaka katika mashauri yote yanayohusu mirathi na usimamizi wa mirathi huku wakiwa na mamlaka ya kuteua msimamizi wa mirathi na kutoa hati ya usimamizi wa mirathi ikiwa kama marehemu katika kipindi cha kifo chake alikuwa akiishi katika eneo ambalo hakimu huyo aliteuliwa. Pia watakuwa na mamlaka kurekebisha au kutengua mirathi hiyo[13]. Kama ilivyoamuliwa kwenye shauri la Shomari Abdallah dhidi ya Abdallah HusseinnaHassani Ramadhani[14],

"Shauri hili kwanza lilifunguliwa katika Mahakama ya Mwanzo lakini baada ya kugundulika kuwa Mahakama haina mamlaka, kumbukumbu zilitumwa Mahakama ya Wilaya ikasikilizwa na Hakimu Mkazi. Mrufani hakuridhika na maamuzi ya Hakimu Mkazi hivyo alikata rufaa Mahakama Kuu. Mahakama Kuu iliamua kuwa:

Ili Hakimu Mkazi aweze kusikiliza mashauri ya Wosia inabidi akae kama Hakimu Mkazi Mteule wa Wilaya aliyeteuliwa na Mh. Jaji Mkuu kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Uthibitisho wa Wosia na Usimamizi wa Mirathi Sura ya 352 Chapisho la 2002.

Pasipo kifungu cha 5 cha sheria hii, sura ya 352, iwapo Hakimu Mkazi atasikiliza shauri la Wosia na Mirathi kwa mujibu wa sheria hii sura ya 352 chapisho la 2002 na hajateuliwa maamuzi yake yatakuwa batili."

Mahakama ya Wilaya inayokaliwa na Hakimu Mkazi Mteule wa Wilaya inayo mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mirathi yasiyozidi thamani ya Sh shilingi elfu kumi na tano (15,000/=), zaidi ya thamani hiyo basi Mahakama ya Wilaya inayokaliwa na Hakimu Mkazi Mteule wa Wilaya italazimika kutoa taarifa Mahakama Kuu ya Tanzania ili itoe maelekezo mengine aidha kutoa kibali kwa mahakama ya Wilaya inayokaliwa na Hakimu Mkazi Mteule wa Wilaya kuendelea kusikiliza shauri hilo[15].

1.3.  Mahakama ya Wilaya

Mahakama ya wilaya, itakuwa na mamlaka katika usimamizi wa mirathi ya mali chache, pale ambapo marehemu amefia katika sehemu ambayo Mahakama ina mamlaka[16]. Mahakama ya Wilaya ina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya usimamizi wa mali chache zenye thamani isiyozidi shilingi za kitanzania milioni mia moja (Tshs. 100,000,000/=)[17]. Katika shauri la Ashura M. Masoud dhidi ya Salma Ahmad[18], Mahakama Kuu iliamua kuwa,

"Mamlaka ya Mahakama ya wilaya katika suala la mirathi na usimamizi imeelezwa

Enjoying the preview?
Page 1 of 1