Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
Ebook128 pages2 hours

Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?

Rating: 1 out of 5 stars

1/5

()

Read preview

About this ebook

Kitabu hiki kinafanya tathmini ya kina ya urais wa Dokta John Pombe Magufuli, Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tangu alipoingia madarakani Novemba 5, 2015 hadi Novemba 5, 2017. Kitabu kinaangalia maeneo ambayo Rais Magufuli amefanya vizuri na yale aliyofanya vibaya. Ni uchambuzi makini usioelemea upande wowote isipokuwa kwenye ukweli.

LanguageKiswahili
Release dateDec 8, 2017
ISBN9781370257492
Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli: Safari Ya Matumaini Au Nyota Iliyofifia?
Author

Evarist Chahali

Founder&CEO AdelPhilConsult | Ex-Intelligence Officer | Consultant | Social Entrepreneur |Swahili Teacher | Author | Blogger | Tech junkie |

Related to Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli

Related ebooks

Reviews for Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli

Rating: 1 out of 5 stars
1/5

1 rating0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Miaka Miwili Ya Urais Wa Magufuli - Evarist Chahali

    Shukrani

    Kitabu hiki kinachofanya tathmini ya kina ya miaka miwili ya utawala wa Rais Dokta John Magufuli ni mwendelezo wa uchambuzi wa siasa za Tanzania kwa mfumo wa vitabu. Kitabu cha kwanza ‘Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015: Magufuli vs Lowassa,’ kilichotoka Oktoba 2015 kilijadili kwa kina kuhusu uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani nchini Tanzania, uliofanyika mwezi huo. Kitabu cha pili, ‘Dokta John Magufuli: Safari ya Urais, Mafanikio na Changamoto Katika Urais Wake,’ kilijadili kipindi cha awali cha utawala wa Dokta Magufuli. Kilichonisukuma kuandikia kitabu hicho cha pili ni pamoja na ukweli kwamba kile cha kwanza kilichapishwa takriban wiki mbili tu kabla ya Uchaguzi Mkuu na hivyo kuwanyima fursa wasomaji wengi watarajiwa. Vilevile, kulionekana kuna haja ya kufanya tathmini ya uchaguzi huo ulioshuhudia mgombea wa chama tawala, Dokta Magufuli akiibuka mshindi.

    Kadhalika, mimi ni mwanafunzi wa stadi za siasa, na mara zote nimekuwa nikiamini kwamba njia mwafaka zaidi ya kuitumia elimu yangu ipasavyo ni kuitumikia nchi yangu kwa njia ya maongezi, aidha kupitia maandishi ya kwenye makala gazetini au bloguni au kwa makala za sauti ninazozitoa mara kwa mara. Ninasema ‘maongezi’ kwa vile mimi si mwandishi kitaaluma, na ninajitambulisha kama mfanya-maongezi (conversationalist) kuliko mwandishi. Kwahiyo, kitabu hiki ni sehemu na mwendelezo wa maongezi hayo.

    Licha ya kuwa mwanafunzi wa stadi za siasa, kitabu hiki, kama zilivyo makala zangu gazetini na bloguni, sio cha kitaaluma. Ni maongezi kati yangu na Mtanzania wa kawaida, awe mwenye shahada ya uzamifu kutoka chuo kikuu au mhitimu wa elimu ya msingi. Hii isitafsiriwe kama kukosa imani katika kujadili masuala mbalimbali kitaaluma bali nimeonelea kuwa ndio njia mwafaka ya kuongea na watu wengi pasi kuwepo kwa vikwazo vinavyoweza kuwanyima fursa wenzetu ambao hawakubahatika kielimu. Kitabu hili ni kwa ajili ya kila Mtanzania wa rika lolote, jinsia yoyote na wa kada yoyote – mwanasiasa au raia anayeichukia siasa, ‘mama ntilie’ au mwanasheria, mwanafunzi au mwalimu, nk.

    Kama ilivyokuwa kwa toleo la kwanza, ninatunuku (dedicate) kitabu hiki kwa baba yangu mpendwa, Marehemu Mzee Philemon Chahali, ambaye pamoja na mkewe, mama yangu mpendwa, marehemu Adelina Mapango, ambao japo hawapo nasi kimwili, ninaamini kiroho wanafurahishwa na kazi hii yangu mtoto wao.

    Ninamshukuru dada yangu Mary, na wadogo zangu, Sr Maria-Solana na mapacha Peter na Paul (Kulwa na Doto) kwa upendo wao ulionisaidia mno kuandika kitabu hiki.

    Pia, ninawashukuru watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, hususan Twitter na Facebook, kwa kulipokea vema wazo langu la uandishi wa vitabu.

    Mapungufu yoyote yaliyomo katika kitabu hiki ni yangu mwenyewe na ninabeba lawama zote. Kama nilivyotanabaisha hapo juu, mimi si mwandishi kitaaluma. Na pia ninakichukulia kitabu hiki kama maongezi (conversation) niliyoamua kuyaweka katika maandishi.

    Ni matumaini yangu makubwa kuwa licha ya faida tarajiwa ya mjadala wa undani kuhusu uchaguzi huo mkuu, kitabu hiki kitawahamasisha Watanzania wenzangu kuhusu haja ya kuweka fikra au mitizamo yetu katika maandishi, sambamba na kuendeleza filosofia isiyo rasmi ya ‘sharing is caring.’

    Ninawatakia usomaji mwema.

    Evarist Chahali.

    Glasgow, Uskochi.

    Desemba 9, 2017.

    Kuhusu Mwandishi

    Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).

    Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.

    Awali, mwandishi alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Munngano wa Tanzania. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) anajihusisha ushauri wa kitaalamu katika masuala ya intelijensia na usalama (intelligence and security consulting), mikakati ya siasa (political strategy consulting) na mahusiano na mawasiliano ya kimkakati (International PR and strategic communications), akiwa mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya ushauri wa kitaalam ya AdelPhil Consultancy iliyopo Glasgow, Uskochi.

    Utangulizi

    Oktoba 5 mwaka juzi – 2015 – Dokta John Magufuli aliapishwa kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla yake nchi hiyo iliongozwa na Marehemu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.

    Kitabu hiki ni mwendelezo wa vitabu vingine viwili vinavyozungumzia siasa za Tanzania hasa kuhusu uchaguzi na uongozi. Kitabu cha kwanza kilizungumzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kabla hakujafanyika, tathmini ya fursa kwa kila mgombea na chama chake.

    Kitabu cha pili kilihusu safari ya Dokta Magufuli kutoka kwenye mchakato wa kupitishwa kuwa mgombea wa chama chake hadi kushinda uchaguzi huo. Kadhalika, kilichambua mafanikio na changamoto kwa urais wake.

    Kitabu hiki kinaendelea vilipoishia vitabu hivyo viwili, kwa kufanya tathmini ya kina ya miaka miwli tangu Dokta Magufuli aingie madarakani.

    Sura Ya Kwanza

    Tarehe 25 Oktoba mwaka 2015, Watanzania walipiga kura ya kumchagua Rais mpya Dokta John Magufuli aliyemrithi mtangulizi wake, Rais wa Nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Japo uchaguzi mkuu haukuwa wa kwanza katika historia ya nchi yetu, mazingira yaliyouzunguka na hali halisi ya Tanzania wakati unafanyika, yaliufanya uwe na umuhimu wa kipekee.

    Kisiasa, angalau kwa chama tawala, CCM, yayumkinika kuhitimisha kuwa uchaguzi mkuu huo ulikuwa wa kwanza kufanyika ambapo ‘nguvu za Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere, hazikuwepo moja kwa moja (directly).’ Mara baada ya kung’atua, Nyerere ‘alimteua’ Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais, akitumia nafasi yake kama mwanasiasa mwenye nguvu zaidi nchini Tanzania. Baada ya Rais Mwinyi kumaliza mihula yake mawili mwaka 1995, Nyerere alitumia tena nguvu zake kisiasa na kuwezesha msaidizi wake wa zamani, Benjamin Mkapa kupitishwa na CCM, na hatimaye kushinda urais, madaraka aliyoshikilia kwa mihula mawili, kama mtangulizi wake, yaani Rais Mwinyi.

    Hata hivyo, duru za kisiasa zinaelezwa kuwa nguvu ya kisiasa aliyotumia Nyerere kumpitisha Mkapa iliwaathiri wanasiasa wawili vijana, Jakaya Kikwete na Edward Lowassa, ambao miaka 10 baadaye, walifanikiwa kmwingiza mmoja wao Ikulu.

    Kwahiyo japo Nyerere hakuwa hai wakati Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005, safari yake ya kuingiza Ikulu ilicheleweshwa kwa miaka 10 na nguvu za kisiasa za Nyerere. Kadhalika, kushinda urais kwa Kikwete akisaidiwa na rafiki yake Lowassa mwaka huo kulitazamwa kama ‘manufaa’ ya kutokuwepo Nyerere.

    Mwaka 2010, Kikwete alishinda tena urais, kama ilivyo kanuni isiyo rasmi ndani ya chama tawala CCM kwa rais aliye madarakani ‘kuruhusiwa’ kumaliza mihula miwili. Kwahiyo, hata kama ‘nguvu za Nyerere’ zilikuwepo wakati huo bado zisingemzuwia Kikwete kushinda tena.

    Katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu huu hali ilikuwa tofauti kabisa. ‘Nguvu za Nyerere’ zilionekana bayana kuondoka kabisa. Hata wanasiasa waliokuwa waamini wa itikadi zake, kwa mfano mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru, sio tu walionekana wenye mtizamo tofauti lakini baadhi yao, ikiwa ni pamoja na Kingunge mwenyewe, waliohama CCM na kujiunga na upinzani. Jina la Nyerere limebaki kama heshima tu lakini lisilo na uwezo wa kubadili chochote ndani ya CCM.

    Lakini, tukiacha kumhusisha Nyerere, kinyang’anyiro cha kumpata mgombea wa CCM wake ambapo hatimaye Dkt Magufuli ‘aliibuka kidedea’ kiliweka historia mpya, ambapo makada zaidi ya 40 walijitokeza kuwania kuteuliwa. Kuna waliotafsiri iwngi huo ya idadi ya ‘watangaza nia’ kama kukua kwa demokrasia ndani ya chama hicho, huku wengine wakieleza kuwa wingi huo ni ishara ya uchu wa madaraka, na wengine wakienda mbali zaidi na kudai kuwa Rais Kikwete aliishusha hadhi ya urais kiasi kwamba ‘kila Dick, Tom na Harry’ alidhani anaweza kuwa Rais.

    Kwa mara ya kwanza, CCM na Watanzania walishuhudia kampeni zisizo rasmi za makada waliotangaza nia za kuomba kupitishwa na chama hicho hata kabla kutangazwa rasmi kuanza kwa mchakato huo. Kampeni hizo zilikuwa kali, kana kwamba ni kampeni rasmi za kuwania urais. Awali, kuna waliohoji iwapo ukali wa mchuano huo ungepelekea chama hicho kupata mgombea bora au la, lakini hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Dkt Magufuli tangu aanze rasmi urais wake zinaweza kutoa jibu kuwa wingi wa waliojitokeza kuwania nafasi hiyo umeisaidia sana CCM kumpata mgombea, na hatimaye rais, bora.

    Jingine kisiasa, ni athari za mchakato wa chama hicho tawala kupata mgombea wake, ambapo jina la Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa halikupitishwa, na hatimaye

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1