Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
Ebook158 pages2 hours

Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?

Rating: 4 out of 5 stars

4/5

()

Read preview

About this ebook

Kitabu hiki adimu kinaelezea kwa kina kuhusu fani nyeti ya Uafisa Usalama wa Taifa (ushushushu). Maelezo hayo yanahusu maana ya Uafisa Usalama wa Taifa, watu wanaojihusisha na fani hiyo, jinsi wanavyopatikana, mafunzo yao, maisha yao kazini, na changamoto mbalimbali kitaifa na kimataifa. Mtiririko wa maelezo unamfanya msomaji awe kama yupo katika safari ya 'ushushushu' tangu mwanzo hadi kazini. Maelezo hayo ni kuhusu taaluma hiyo popote pale duniani na si kwa nchi moja tu.

LanguageKiswahili
Release dateOct 15, 2017
ISBN9781370131747
Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?
Author

Evarist Chahali

Founder&CEO AdelPhilConsult | Ex-Intelligence Officer | Consultant | Social Entrepreneur |Swahili Teacher | Author | Blogger | Tech junkie |

Related to Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?

Related ebooks

Reviews for Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini?

Rating: 4 out of 5 stars
4/5

24 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Afisa Usalama Wa Taifa Ni Mtu Wa Aina Gani? Na Anafanya Nini? - Evarist Chahali

    Kuhusu mwandishi

    Mwandishi wa kitabu hiki, Evarist Chahali, ni Mtanzania mwenye makazi yake jijini Glasgow, Uskochi. Ni mhitimu wa Shahada ya kwanza katika Sosholojia (BA in Sociology) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, Shahada ya Uzamili katika Stadi za Vita (Master of Letters in War Studies) na Shahada ya Uzamili katika Utafiti wa Siasa (Master of Research in Political Research) alizopata katika Chuo Kikuu cha Aberdeen, Uskochi, ambapo bado anaendelea na Shahada ya Uzamifu katika Stadi za Siasa (PhD in Political Studies – Part-Time).

    Kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali nchini Tanzania, ambapo huko nyuma aliandikia magazeti ya ‘Kulikoni’ na ‘Mtanzania,’ na kwa sasa ni mwandishi wa makala katika gazeti la kila wiki linaloongoza nchini Tanzania, la ‘Raia Mwema. Kadhalika, mwandishi anamiliki blogu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ iliyoanzishwa mwaka 2006.

    Awali, mwandishi alikuwa mwalimu katika Shule ya Sekondari ya Ecknforde, Tanga, Tanzania kabla ya kujiunga na utumishi serikalini katika Ofisi ya Rais wa Jamhuri wa Munngano wa Tanzania. Hivi sasa, licha ya kuendelea na masomo yake ya Shahada ya Uzamifu (part-time) anajihusisha ushauri wa kitaalamu katika masuala ya intelijensia na usalama (intelligence and security consulting), mikakati ya siasa (political strategy consulting) na mahusiano na mawasiliano ya kimkakati (International PR and strategic communications), akiwa mwanzilishi na mmiliki wa kampuni ya ushauri wa kitaalam ya AdelPhil Consultancy iliyopo Glasgow, Uskochi.

    Shukrani

    Kitabu hiki ni toleo la kielektroniki la matokeo ya mfululizo wa makala (series) nilizozichapisha katika blogu yangu ya ‘Kulikoni Ughaibuni’ kuhusu fani ya Uafisa Usalama wa Taifa. Kutokana na makala hizo kuonekana kuwavutia wasomaji wengi, niliona kuwa kuna umuhimu wa kuzikusanya pamoja na kutengeneza kitabu hiki.

    Kadhalika, binafsi niliwahi kuwa Afisa Usalama wa Taifa huko Tanzania, kazi niliyoifanya kwa miaka 13. Na kwa vile ni maafisa usalama wachache mno, walio kazini au nje ya kazi, wenye fursa ya kuelezea kuhusu fani hiyo nyeti, wazo la kuandika kitabu hiki linakidhi haja hiyo.

    Kama ilivyokuwa kwa vitabu vyangu viwili vilivyopita, ninatunuku (dedicate) kitabu hiki kwa baba yangu mpendwa, Marehemu Mzee Philemon Chahali, ambaye pamoja na mkewe, mama yangu mpendwa, marehemu Adelina Mapango, ambao japo hawapo nasi kimwili, ninaamini kiroho wanafurahishwa na kazi hii yangu mtoto wao.

    Ninamshukuru dada yangu Mary, na wadogo zangu, Sr Maria-Solana na mapacha Peter na Paul (Kulwa na Doto) kwa upendo wao ulionisaidia mno kuandika kitabu hiki. Pamoja nao ni binamu zangu Gordian Mapango, George Mapango na Dignatus Mapango.

    Pia, ninawashukuru wasomaji wa blogu ya Kulikoni Ughaibuni, na watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, hususan Twitter na Facebook, kwa kulipokea vema wazo langu la uandishi wa vitabu.

    Mapungufu yoyote yaliyomo katika kitabu hiki ni yangu mwenyewe na ninabeba lawama zote. Kama nilivyotanabaisha hapo juu, mimi si mwandishi kitaaluma. Na pia ninakichukulia kitabu hiki kama maongezi (conversation) niliyoamua kuyaweka katika maandishi.

    Ni matumaini yangu makubwa kuwa kitabu hiki kitawahamasisha Watanzania wenzangu kuhusu haja ya kuweka uelewa na uzoefu wetu katika maandishi, sambamba na kuendeleza filosofia isiyo rasmi ya ‘sharing is caring.’

    Ninawatakia usomaji mwema.

    Evarist Chahali.

    Glasgow, Uskochi.

    Oktoba 2017.

    Utangulizi

    Kuna ukweli mmoja usiofichika wala kupingika kwamba watu wengi sana wanapenda kazi ya ushushushu, yaani Uafisa Usalama wa Taifa. Hiyo sio kwa Tanzania pekee bali sehemu nyingi duniani. Ukiingia mtandaoni utakutana na watu wengi wanaozungumzia taaluma ya intelijensia au/na wahusika katika hali ya kutamani kuifahamu taaluma hiyo nyeti au kuwa mhusika.

    Hata hivyo, pamoja na kiu hiyo kubwa ya ufahamu kuhusu taaluma ya ushushushu, imekuwa vigumu mno kuifahamu kwa undani kwa maelezo sahihi kutoka kwa wahusika. Kanuni na sheria zinawazuwia maofisa usalama wa taifa kuzungumzia lolote kuhusu taaluma hiyo. Hali ni ngumu zaidi kwa sehemu kama huko nyumbani Tanzania ambapo suala la uandishi tu ni tatizo sugu.

    Kimsingi, kinachokatazwa kisheria na kikanuni kuhusu kuzungumzia ushushushu ni kutoa siri au masuala yanayoweza kuhatarisha usalama wa taifa. Hakuna dhambi wala kosa kuelezea kwa ujumla, kwa mfano ushushushu ni kitu gani au shushushu ni mtu wa aina gani. Ukosefu wa machapisho kuhusu taaluma hiyo nyeti kumechangia sana mkanganyiko katika jamii kuhusu ushushushu na mashushushu huku baadhi wakiamini kwa dhati kabisa kuwa taaluma hiyo inahusika na ‘mambo mbaya tu,’ kama vile kuua watu wasio na hatia, umumiani (kunyonya damu kama ‘vampires,’ na hisia potofu kama hizo.

    Kwahiyo kitabu hiki, bila kukiuka kanuni na sheria za usiri zinazotawala taaluma hiyo, kinajaribu kufungua ukurasa mpya, angalau kwa huko nyumbani, kutoa picha ya jumla kuhusu taaluma hiyo muhimu mno kwa usalama na ustawi wa taifa letu, sambamba na kuelezea kwa undani mchango muhimu wa mashushushu kwa usalama wa taifa letu, ikiwa ni pamoja na kubainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili, na kutoa mapendekezo ya kuzikabili.

    Kwa ‘nchi za wenzetu,’ mashushushu wastaafu wamekuwa vyanzo vikuu vya uelewa kuhusu fani hiyo nyeti ambapo wamekuwa wakiandika vitabu mbalimbali, ilhali wengine wakishirikiana na sekta ya filamu katika utengenezaji wa filamu zinazohusu ushushushu. Kwa bahati mbaya (au pengine kwa makusudi tu), kwetu ile kuzungumzia tu jambo lolote linalohusu ushushushu ni kitu adimu mno. Kasumba hiyo imeawaathiri hata wanataaluma ambao hawajawahi kujihusisha kufanya tafiti au kuandika machapisho ya kitaaluma kuhusu fani hiyo. Uhaba wa ‘references’ unatoa kisingizio kizuri kwa wasomi wetu ‘kupuuzia’ mada hiyo muhimu.

    Kitabu hiki ni matokeo ya mlolongo (series) wa makala kuhusu taaluma hiyo adimu ambao niliufanya katika blogu yangu ya Kulikoni Ughaibuni lakini sikuweza kuukamilisha. Hata hivyo ni vema nikatoa tahadhari mapema kwamba nitakachoandika ni kile tu kinachoruhusiwa kuandikwa hadharani. Kimsingi, taaluma ya ushushushu inatawaliwa na usiri, na mengi ya yanayohusiana na taaluma hayo yanabaki kuwa siri. Hata hivyo, kuna maelezo ambayo yapo wazi japo inahitaji uelewa wa aina flani kuchora mstari kati ya kipi ni siri na kipi ni ruksa kuwa hadharani.

    Sura ya kwanza

    Uofisa Usalama wa Taifa (ushushushu) ni kitu gani?

    Kwa tafsiri rahisi, ushushushu ni taaluma inayohusu ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji (kwa mamlaka husika) wa taarifa za kiusalama kwa njia za siri (clandestine methods). Japo kwa Kiswahili ushushushu ni intelijensia, kiundani kuna tofauti kati ya ushushushu unaofanyika ndani ya nchi na unaofanyika nje ya nchi. Kwa hapa Uingereza, idara ya ushushushu inayoshughulika na masuala ya ndani inajulikana kama MI5 na ile inayohusiska na ushushushu nje ya nchi ni MI6. Kwa nchi kama Marekani, licha ya Shirika la ushushushu wa ndani, FBI, na lile la ushushushu wa nje, CIA, kuna mashirika mengine kadhaa yanayohusika na fani hiyo ndani na nje ya nchi hiyo.

    Hata kwa hapa Uingereza, licha ya M5 na MI6, kuna taasisi nyingine ya ushushushu ijulikanayo kama GHQC inayojihusisha na kunasa mawasiliano ndani na nje ya nchi hii. Taasisi kama hiyo ipo pia nchini Marekani, na inafahamika kama NSA.

    Kwa huko nyumbani, tofauti hizo zipo ndani ya muundo wa Idara yetu ya Usalama wa Taifa, kwa maana kwamba kuna taasisi moja tu lakini ndani yake kuna mgawanyo wa kimajukumu ya ndani na ya nje ya nchi.

    Kadhalika, japo mashushushu wamekuwa wakifahamika kwa kimombo kama pia kama ‘spies,’ ukweli ni kwamba ‘spy’ ni shushushu anayefanya kazi nje ya nchi yake, kitu kinachojulikana kiusalama kama ujasusi au espionage kwa Kiingireza.

    Japo mataifa mbalimbali yana miundo tofauti ya Idara zao za Usalama wa Taifa, lengo na kazi kuu ni ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishaji wa taarifa za kiusalama kwa mamlaka husika.

    Kwa minajili ya kitabu hiki, nitazungumzia zaidi mazingira ya huko nyumbani Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, Idara yetu ya Usalama wa Taifa ni idara ya serikali iliyo chini ya Ofisi ya Rais, ambayo ina jukumu la kukusanya na kuchambua taarifa za usalama na kuziwasilisha 'mahala kunakohusika' katika namna ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo ataona inafaa.

    Kimsingi, mkuu 'halisi' wa Idara hiyo ni Rais mwenyewe, ambaye kwa lugha ya kiusalama anafahamika kama 'sponsor.' Wakuu wa Idara za Usalama wa Taifa hufahamika kama spymasters.

    Maeneo makuu ya kazi za Idara ya Usalama wa Taifa ni kukusanya na kuchambua habari za kiusalama zinazohusiana na ujasusi (espionage), uzandiki (subversion), uhujumu (sabotage) na ugaidi (terrorism). Lakini jukumu la Idara hiyo si kukusanya taarifa hizo na kuzichambua tu bali pia kuzuwia matukio hayo yanayofahamika kama matishio ya usalama wa taifa.

    Kuna umuhimu wa kuelezea maana halisi za maeneo hayo manne. Ujasusi ni kitendo cha Idara ya Usalama wa Taifa wa nchi mmoja kukusanya taarifa za kiusalama kutoka nchi nyingine. Wakati kimsingi ujasusi kwa asili yake ulihusisha taarifa za kiusalama kati ya nchi na nchi, hususan masuala ya usalama na kijeshi, mazingira ya hivi sasa yamebadilika kwa kiasi fulani, hususan katika mataifa yaliyoendelea, ambapo ujasusi sasa wahusisha pia utafutaji wa taarifa za teknolojia za mawasiliano, utafiti wa kisayansi, usafiri wa anga, ulinzi, elektroniki, na maeneo mengine. Hii imepelekea walengwa wa ujasusi kuwa zaidi ya nchi au serikali za kigeni pekee bali pia hata taasisi nyingine za kigeni.

    Moja ya sifa kuu za masuala ya ujasusi ni kwamba ‘hakuna urafiki.’ Hii inamaanisha kila nchi inafanya jitihada za kijasusi kuhusu nchi nyingine. Mara nyingi, walengwa wakuu wa Operesheni za kijasusi ni nchi jirani, au kwa kiasi kikubwa zaidi, nchi maadui. Kwa nchi majirani, ujasusi ni muhimu kuhakikisha kuwa nchi husika ipo salama. Kwahiyo, kwa mfano, Tanzania ikifanya ujasusi kwa nchi jirani kama Rwanda, Burundi, DRC, na kadhalika, lengo sio kuzihujumu bali kuhakikisha usalama wa nchi yetu.

    Mbinu zinazotumika kufanya ujasusi hazina tofauti kubwa na zile zinazotumika kufanya ushushushu ndani ya nchi. Tofauti za msingi ni ukweli kuwa ushushushu huo unafanyika nje ya nchi, na hivyo kutengeneza mazingira ya hatari kwa maafisa wanaohusika, wanaofahamika kama majasusi.

    Japo majasusi kama walivyo mashushushu hutumia mbinu mbalimbali kukusanya taarifa za kiusalama, vyanzo vikuu vya taarifa hizo ni pamoja na kile kinachofahamika kama ‘open sources,’ au kwa kifupi OSINT yaani vyanzo vya wazi, kama vile magazeti, Intaneti, mkataba, na kadhalika. Vyanzo vingine ni vya mawasiliano (communication intelligence), kwa kifupi COMMINT, ambapo kwa kiasi kikubwa, mashushushu wenye jukumu hilo hunasa mawasiliano ya walengwa, kama vile simu, barua-pepe, fax, na kadhalika. Mbinu muhimu hapa ni ‘eavesdropping, ’yaani kusikiliza maongezi binafsi ya watu pasipo watu hao kufahamu. Mbinu nyingine ni kuweka kitu cha kunasa mawasiliano, kitu kinachofahamika kama ‘wiretapping.’ Eneo hili hujumuisha pia kunasa mawimbi ya sauti, kile kinachojulikana kama ‘signal intelligence,’ kwa kifupi SIGINT, na kunasa mawasiliano ya kielektroniki, kwa kifupi ELINT.

    Mbinu nyingine ni kunasa picha au taswira, mara nyingi kwa kutumia ndege au ‘drones,’ kitu kinachofahamika kama IMINT, yaani ‘imagery intelligence.’ Mbinu nyingine ni ukusanyaji taarifa

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1