Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania
Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania
Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania
Ebook233 pages35 minutes

Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Omari Rashid Nundu, alizaliwa Tanga, Tanzania mwaka 1948 na huko ndiko alikopata elimu yake ya shule kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Glasgow, Scotland mwaka 1971 kusomea uhandisi na sayansi ya vyombo vya anga (Aeronautical Engineering); na baadaye kuendelea na shahada za juu na utafiti vyuo vikuu vya Cranfield, England na Concordia, Canada.

Omari amebahatika kufanya kazi kwenye taasisi mbalimbali duniani katika kuitendea haki taaluma hiyo aliyoisomea na anayoipenda. Kwa nyakati mbalimbali alikuwa mhandisi na mkurugenzi kwenye mashirika ya ndege, alikuwa mshauri na mhadhiri kwenye vyuo vya kimataifa, na pia alikuwa mkuu wa vitengo vya usafiri wa anga katika jumuia za kimataifa. Kabla ya kurejea Tanzania na kuwa mbunge wa Tanga na pia Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa Rais wa jopo la kimataifa la magwiji wa taaluma ya Usafiri wa Anga Duniani (Air Navigation Commission) kwa miaka miwili mfululizo.

Ingawa ni mhandisi na mwana sayansi aliyebobea, Omari anapenda kuongea lugha mbalimbali lakini ana mapenzi ya dhati kwa lugha ya Kiswahili ambayo ndiyo iliyomkuza. Hivyo basi kuwa yeye ni malenga wa mashairi halishangazi.

Utenzi uliomo mwenye kitabu hiki unajaribu kusimulia maisha na mwenendo wa Dunia kwa kadri alivyoyashuhudia mhandisi huyu hadi mwaka 2015.

LanguageKiswahili
Release dateJun 13, 2017
ISBN9781370045075
Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania

Related to Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania

Related ebooks

Reviews for Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Simulizi Ya Dunia Kwa Kugeza Tanzania - Omari Rashid Nundu

    Simulizi ya Dunia

    Kwa Kugeza Tanzania

    Simulizi ya Dunia

    Kwa Kugeza Tanzania

    Omari Rashid Nundu

    Dibaji

    Dunia ni kubwa na kuivinjari ni muhimu kwa atakayejaliwa uwezo wa kufanya hivyo. Somo la Jiografia linatowa mwanga huo mashuleni; pia uelewa wa mtu kuhusu Dunia unaimarishwa na utafiti wake mwenyewe kwa mambo anayoyaona na vitu anavyochezea akiwa mdogo. Udogoni nilibahatika kuishi mjini na vijijini nikicheza nchi kavu na hata mitoni na baharini. Maajabu yaliyoko huku ni mengi. Masomo ya shuleni na vyuo vikuu ndiyo hasa yanayafunua macho ya mweledi akayaelewa yale aliyoamua kuyasomea. Nilipenda sana kurusha tiara nilizozitengeneza mwenyewe. Kuunda na kuchezea tiara havikunitosha. Nilinuwia na nikajaaliwa kusomea fani ya uhandisi wa vyombo virukavyo angani. Hakuna jambo ambalo liliburudisha akili na mawazo yangu kama kujifunza, kudadisi na kutafiti kwa kina maswala haya. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kuniongoza huko. Maisha yangu yote ya udogoni na ukubwani yalitumika kwenye nyanja zihusuzo mambo hayo.

    Kila mtu ana ulevi wake ndivyo Waswahili tusemavyo nao wangu ulikuwa ni kusoma na kutunga mashairi. Sikuhitaji kufundishwa kufanya hivyo. Ni wazi kuwa mapenzi ya nyimbo za taarab yalinirahisishia kukitiza akilini mwangu vina na mizani kwa sentenso nizisemazo kila nilipotaka kufanya hivyo, na ndio maana niliweza kutunga mashairi na kuyatuma kwenye magazeti ya Ngurumo na Mwangaza nikiwa mdogo sana, mara tu baada ya kuanza kwenda shule. Katika harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika, mwanasiasa mmoja alipopinga ushiriki wa ubunge uliotaka kuwepo wabunge watatu kila jimbo kwa kuzingatia rangi yaani Mwafrika, Mhindi na Mzungu nilijikuta kukubaliana na wale walioafiki mfumo huo na nikatunga na kutuma shairi gazetini kumlaumu yule aliyepinga. Mtu huyu ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha siasa cha TANU ilimbidi aanzishe chama chake. Wakati mwengine najiuliza kwanini nilifanya hivyo bali sipati jibu la kuniridhisha. Hadi leo bado nashangaa kwanini nilifanya hivyo. Siamini kuwa upeo wa kisiasa wa umri wangu mdogo ule ulikuwa mkubwa kuliko wa ukubwani huu. Hata hivyo apangae na aongozaye ni Mwenyezi Mungu; basi naiwe hivyo.

    Hadi ukubwani nilipotamani kufanya jambo la kuniburudisha kutunga shairi kulijitokeza. Nilifanya hivyo sana nilipokuwa kwenye Jeshi la Kujenga Taifa, Ruvu, Disemba 1970 ambako nilitunga ngonjera kwa mashindano ya Wilaya ya Bagamoyo hadi Jimbo la Mashariki la wakati huo. Ngonjera yangu ndiyo iliyotumika kumsomea Mwalim Julius Nyerere wakati wa kutufungia mafunzo. Sikuisoma mimi.

    Mimi ni Muhandisi aliyebobea kwenye vyombo vya anga. Hivyo nilitumia miaka mingi ya maisha yangu ndani na nje ya Tanzania kwenye taasisi na mashirika ya usafiri wa anga. Baada ya kujishughulisha na mambo mengi ya kuendeleza nchi yangu, nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC), Afrika na Dunia nzima kwa jumla, shughuli ambazo ziliniwezesha kutembelea na pia kujifunza na kufanya kazi nchi nyingi duniani, mwaka 2010 nilirejea nyumbani kwetu Tanzania nikiwa na nia ya kupata nafasi ya kuwa mwakilishi wa wilaya yangu ya Tanga bungeni na hivyo basi kuweza kuchangia kwa dhati katika maendeleo ya nchi yangu kwa kutumia kikamilifu elimu na uzoefu nilioupata ndani na nje ya nchi yangu. Nilibahatika kuwa mbunge

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1