Discover millions of ebooks, audiobooks, and so much more with a free trial

Only $11.99/month after trial. Cancel anytime.

Machozi Yamenishiya
Machozi Yamenishiya
Machozi Yamenishiya
Ebook135 pages54 minutes

Machozi Yamenishiya

Rating: 0 out of 5 stars

()

Read preview

About this ebook

Mateso, maumivu na siasa ni mambo yaliyojaa uchochezi mkali unaomsukuma mshairi kuzungumza waziwazi na kinagaubaga na hatimaye kumfanya mwandishi apandwe na jazba zinazofanya kazi fulani itoke nje ya kingo za ulingo wa kisanaa. Katika hali kama hii mshairi lazima atunge wimbo unaoimbika ndani ya nafsi yake mwenyewe kwanza, wimbo utakaomwezesha kunyanyuka kitandani asubuhi huku akijua hayuko pweke, ana wenzake wenye maumivu kama au kuliko yake. Mohammed Khelef Ghassani ana weledi huu wa kubaki ndani ya kingo za ulingo wa kisanaa, weledi wa kuichenga siasa kwa namna ya kuipa nguvu kubwa zinazoficha na kuzimua unagaubaga na hata ukali wake.
LanguageKiswahili
Release dateDec 20, 2019
ISBN9789987449156
Machozi Yamenishiya

Related to Machozi Yamenishiya

Related ebooks

Related categories

Reviews for Machozi Yamenishiya

Rating: 0 out of 5 stars
0 ratings

0 ratings0 reviews

What did you think?

Tap to rate

Review must be at least 10 words

    Book preview

    Machozi Yamenishiya - Khelef Ghassani

    NENO LA SHUKRANI

    Wakati fulani mnamo mwanzoni mwa miaka ya 2000, kaka yangu, Maalim Said Suleiman, aliniuliza ikiwa tungo nilizokuwa nimeshaziandika hadi wakati huo, zilikuwa zimeshapata mchapishaji. Wakati huo ilikuwa miaka kama mitano hivi tangu alipokuwa amenitembelea nyumbani kwetu kisiwani Pemba, akiwa ndio kwanza ametokea masomoni Uhispania, na nikamkabidhi baadhi ya mashairi ambayo hadi hapo nilikuwa nimeshayaandika.

    Kwenye mazungumzo hayo, nilimueleza jitihada ambazo nilikuwa nimechukuwa bila mafanikio. Nilimuambia ugunduzi wangu kuwa niliwaona wachapishaji wengi niliokuwa nimewasiliana wakiwa hawana imani na sanaa ya ushairi kwa kuwa haikuwa na wanunuzi. Mchapishaji ni mfanyabiashara na anaogopa kuwekeza kwa kisichokuwa na soko la uhakika. Tangu hapo, utamaduni wa kujisomea ni wa chini kwenye jamii zetu, na linapokuja suala la ushairi ndipo hali inazidi kuwa mbaya. Ukiwacha wanafunzi wa skuli na vyuo, ambao wanalazimishwa na mitaala yao kusoma ushairi, na ambao ni soko lililokwishamilikiwa na washairi maalum wenye majina na au ushawishi kwa watunga mitaala, mchapishaji hawezi kuwekeza kwenye kazi ya mshairi mdogo kama mimi, akikhofia kucheza pesa zake pata-potea.

    Ndipo akanishauri nimtafute Profesa Said Ahmed Mohamed kumtaka ushauri. Hilo lilikuwa ni jina kubwa sana kwangu. Sikuwa nimewahi kumuona kwa sura wala hata kufikiria kuwa kuna siku pangekuja kuwa na njia au sababu ya kukutana naye. Nikamuambia hiyo kazi angenifanyia yeye, maana sikuwahi hata kuwaza kuwa ningemfika Profesa Said wa Asali Chungu, wa Kivuli Kinaishi, wa Dunia Mti Mkavu, wa Tata za Asumini, wa Si Shetani Si Wazimu... na wa... Alimradi utetezi wangu ulikuwa ni mwingi sana, nikimuonesha kaka yangu kuwa sikuwa na pa kuanzia kumvaa Profesa Said.

    Lakini kadiri nilivyoonesha ugumu niliouhisi upo, ndivyo kaka yangu naye aliponionesha hoja na haja ya mimi mwenyewe kumtafuta mtu wa kunisaidia. Akanipa anwani yake ya barua-pepe na kuniwachia mwenyewe kufanya ninachopaswa kufanya. Naam, nikamtafuta kweli Prof. Said na nikamuomba mambo mawili: kwanza, awe mhariri wa kazi zangu za fasihi (zikiwemo hadithi fupi fupi) na, pili, atumie uzoefu wake kwenye uwanja huu kunitafutia wachapishaji.

    Ajabu ni kuwa sio tu kwamba alizichukuwa kazi hizo moja kwa moja, bali pia alianza kuzitangaza kwa kila aliyemuona kuwa anaweza kusikiliza na, matokeo yake, tangu wakati huo akaniweka kwenye orodha ya waandishi na washairi wanaoinukia. Hadithi zangu fupi fupi zimekuwa zikichapishwa kwenye mikusanyiko mbalimbali inayochangiwa na waandishi wengine wachanga na wakongwe, akiwemo yeye mwenyewe, Marehemu Mohamed Said Abdullah (Bwana Msa), Prof. Ken Walibora na Marehemu Omar Babu (Abu Marjan), nikiwataja wachache. Si hilo tu, bali pia akawa ananishajiisha kila mara niandike nyengine.

    Kwa diwani hii ya Machozi Yamenishiya, ambayo aliihariri na kuikamilishia kazi zake zote tangu mwaka 2007, alinifanyia la ziada jengine. Alimpa na kumuomba gwiji mwengine wa lugha na fasihi, Bwana Abdilatif Abdalla, aiwekee neno la awali. Ilikuwa sadfa yenye maana kubwa kwangu, maana hakika mimi mwenyewe ni mmoja wa wengi walioinukia kuipenda diwani ya Sauti ya Dhiki iliyoandikwa na Bwana Abdilatif na ambayo ilikuja kuniathiri sana kwenye uandishi wangu. Ni bahati mbaya kuwa Machozi Yamenishiya hayakuweza kupata mchapishaji kwa muda wote huo kutokana na sababu zile zile ambazo nimezitaja awali. Lakini ukweli ni kuwa wote wawili, Prof. Said na Bwana Abdilatif, waliihangaikia sana, hata ikafika mahala mimi – ambaye ni yangu – nikawa nawaonea huruma na kuwaambia bora waiwache tu. Haijawa riziki yangu! Tusemavyo kikwetu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba, hatimaye, muda wa kuchapishwa umewadia baada ya zaidi ya takribani muongo mmoja wa kusubiri.

    Kwa hivyo, kwa uzito wao watatu hawa niliowataja – kaka yangu, Maalim Said, Prof. Said na Bwana Abdilatif– neno hili la shukrani ni kwao. Nawashukuru kwa kujitolea kwao kwangu tangu nikiwa na umri mdogo kabisa wa kuweza kutambulika na kutambuliwa kuwa mshairi (wakati namkabidhi Maalim Said mashairi yangu kisiwani Pemba, nilikuwa na umri wa miaka 17 tu). Kikwetu, ningeliweza kusema kuwa waliniona na kunigotoa, kwani walikuwa na jicho la ndani la kuweza kuona kuwa ndani yangu mulikuwa na kipaji kinachopaswa kuendelezwa na kupewa nafasi.

    Mohammed K. Ghassani,

    Agosti 2016, Bonn - Ujerumani

    UTANGULIZI

    MSHAIRI NA DIWANI YAKE

    Linapokuja suala la kutaja mafanikio ya mshairi fulani, inatubidi kwanza tulikabili suala gumu la ki-ontolojia: ‘shairi ni nini’? Kwa vile suala hili hukosa jibu mwafaka, mimi hulipa fasili rahisi tu – yaani shairi ni umbo la sanaa-lugha linalojitofautisha na maumbo mengine ya sanaa-lugha kwa jinsi linavyosikika likisomwa kimoyomoyo au kwa kinywa kipana. Shairi, kwa hivyo, huvutia kwa utamu wake kimasikizi au kimaandishi kwa namna maneno ya kawaida yalivyoteuliwa na kupangwa kujenga hisia na kutoa taathira ya kiujumi na ujumbe.

    Kwa fasili hii, shairi huwa shairi tunapokutana nalo uso kwa macho au mdomo kwa sikio, bila ya kufikiria kanuni kandamizi zinazowekwa na washairi wenyewe au wahakiki wao. Tunapolisikia au kulisoma shairi na kulifahamu bila ya kuteswa na maneno au picha

    Enjoying the preview?
    Page 1 of 1